Peter Madeleka retweeted
Wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo wakisoma Gazeti la Nipashe wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho,Wakili Peter Madeleka.Uzinduzi wa kampeni hizo umefanyika leo Septemba 5,2025 katika eneo la Kivule, baadhi ya vipaumbele vya mgombea huyo akishida ubunge ni....
✍🏿Elimu: Kupanua na kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari, kujenga madarasa na vyoo, kuhakikisha upatikanaji wa madawati na vitabu bure kwa wanafunzi.
✍🏿Afya: Kuboresha vituo vya afya vilivyopo, kujenga vipya kwenye maeneo yenye uhitaji, kusimamia upatikanaji wa dawa na kuhakikisha akina mama na watoto wanapata huduma bora bila vikwazo.
✍🏿Ajira: Kuanzisha programu za ujasiriamali kwa vijana na wanawake kupitia vikundi vya kijamii, kuwezesha mikopo midogo na kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi (VETA).
✍🏿Miundombinu: Kuboresha barabara za ndani ya Kivule ziweze kupitika mwaka mzima, kusimamia upatikanaji wa maji safi na umeme, pamoja na kufuatilia miradi ya maendeleo kwa uwazi.
Tembelea epaper.ippmedia.com kusoma gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi.
#NipasheDigital #NipasheMwangaWaJamii #miaka30yakupashahabari
Peter Madeleka retweeted
‼️This time I’m very serious SULUHU MUST GO‼️🚨🇹🇿
Why settle for a copy when we can have an original? @SuluhuSamia playbook seems straight out of @realDonaldTrump White House. Time for change! #SamiaMustGo
From 'Make Tanzania Great Again' to 'I alone can fix it' - sounds familiar? We need leadership, not echoes of Trump. #SamiaMustGo
Samia Suluhu Hassan's latest: 'I know words, I have the best words.' No, thanks, we've heard it before. #SamiaMustGo
If Samia keeps borrowing Trump's lines, maybe she should borrow his 'You're fired!' too. #SamiaMustGo I’m very serious.
Peter Madeleka retweeted
Kwa MAELEKEZO ya Mteja wangu ERICK MOSHI, ninakusudia KUMSHITAKI katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar Es Salaam,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa KINONDONI, CHRISTIAN NYAKIZEE, kwa KUSHIKILIA MALI za Mteja wangu KINYUME CHA SHERIA, akimtuhumu KUIBA TZS 6 BILIONI za BENKI YA CRDB.
Peter Madeleka retweeted
Mwandiko wa Adv: @PMadeleka unasomeka vizuri kwenye ubao ✍️
Peter Madeleka retweeted
Ili uwe Mpiga Kura wa TLS lazima uwe na sifa kama za Adv @PMadeleka na Kura ya Peter inaenda kwa Adv @Mwabuk2Boniface ameshaweka waz ✔️
Sasa nyie Mawakili wa S/R mnaotaka kuja kupiga kura kwa mlango wa nyuma na mkitambua fika hamna Lesen kitaumana.
#KataaBaolaMkonoTLSSiyoNetball
Peter Madeleka retweeted
ALIPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.
Jina: Enock John Zakaria Chambala.
Kabila : Muha.
Mzaliwa: Kigoma Bitare
Urefu : Kati ya ft 5.7 na Ft 6
Rangi: Mweusi
Kazi: Mfanyabiashara wa Mkonge
Makazi: Tanga, Kange, Karibu na Kituo kipya Cha Mabasi
Elimu: Shahada ya Maendeleo ya jamii Tumaini university Iringa.
Mara ya mwisho alipatikana kwa njia ya simu siku ya Juma mosi tarehe 6 Julai 2024.
Lakini mpaka sasa simu yake haipatikani kabisa, tumejaribu kumtafuta kupitia Rafiki zake wa Karibu hata wao wanasema hawajui.
Tunaomba yeyote mwenye taarifa yake atusaidie atoe taarifa kituo Cha polisi au ofisi yoyote ya serikali.
Mtoa taarifa hii ni mdogo wake Enock John naitwa Baraka John Chambala. (0767 219 312)
kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo.
0787 887 901(Bruno John Chambala)
0767 669 854 (Baba yake)
@ExMayorUbungo tupate njia kukomesha mambo haya
Peter Madeleka retweeted
Rais wa Gabon aliyepinduliwa, Ali Bongo pamoja na wanawe wawili wamegoma kula wakilalamikia vitendo vya ukatili na mateso wanayofanyiwa wakiwa kizuizini.
Mawakili wao wamedai mke wa Bongo, Sylvia na mwanawe mkubwa, Noureddin walipigwa na kunyongwa wakiwa kizuizini huku wakidai Noureddin aliteswa na hata kupigwa kwa shoti ya umeme.
Jeshi lilimuondoa Bongo madarakani kwa madai ya kutowajibika kwa Serikali pamoja na uongozi mbaya ambao ungeweza kupelekea nchi kwenye machafuko.
Peter Madeleka retweeted
Wewe unayebisha unamjua Mungu?
Una namna yoyote ya kubatilisha maneno yake?😂
“Mambo ya kiimani haya😎”
Peter Madeleka retweeted
Wakili wa kujitegema nchini Wakili Peter Madeleka ametoa maoni yake juu ya ujio wa mkuu wa mkoa mpya wa Arusha Paul makonda katika mkoa huo.
Wakili Madeleka kuptia ukurasa wake wa mtandao wa X amesema ni fursa muhimu kwake kutumia taaluma yake kumfundisha Katiba na Sheria hasa katika eneo la haki za Binadamu na Uhuru.
“ Ni FURSA MUHIMU ya kumfundisha KATIBA na SHERIA, hasa UHURU na HAKI ZA BINADAMU. Nitaifanya KAZI hiyo Kwa MOYO wangu wote kwa kuwa PAUL MAKONDA ANAFUNDISHIKA” ameandika Wakili Madeleka.
Awali kupitia mahojiano na kituo kimoja cha televisheni Wakili Madeleka alisema wanaohitaji kupewa elimu ya katiba ni viongozi wa CCM na viongozi wa serikali kwakuwa wao ndio waendeshaji wa shughuli za serikali na za kisiasa za kila siku akisema hawaijui Katiba akimtolea mfano Paul Makonda kutoa maagizo kwa Mawaziri.
Wakili Madeleka baada ya uteuzi huo wa Makonda amesisitiza kwa kusema anao wajibu wa kumfundisha Katiba.
“ Ninao WAJIBU wa KUMFUNDISHA Paul Makonda SOMO la KATIBA na SHERIA, na hasa kuhusu HAKI ZA BINADAMU. Nadhani, ATAFAULU tu” ameongeza.
Usiku wa kuamkia 31 March 2024 kumetoka taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan kufanya teuzi na mabadiliko kadhaa yaliyohusisha wizara na wakuu wa mikoa na wilaya ambapo katika teuzi hizo Makonda ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.
Peter Madeleka retweeted
#TANZANIA: Wakili @PMadeleka aingilia kati sakata la kutekwa kwa Mfanyabiashara wa Madini na kupotea kwa zaidi ya miezi mitatu huku jeshi la Polisi likituhumiwa kuhusika kwenye utekaji huo.
Zaidi: youtu.be/ZJUJMqQE4Aw
Peter Madeleka retweeted
Feleshi katafuta UGOMVI na Peter.
Sasa anafundishwa SHERIA ya GN na Peter.
Wacha nicheke mie.
AMA kweli kila mbuyu una SHETANI wake.
😂😂
Peter Madeleka retweeted
GAZETI LA SERIKALI & UPOTOSHAJI TOKA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:
Gazeti la Serikali (GAZETTE) lilianzishwa na "General Orders" ya 1957. Sheria hii imefanyiwa marejeo mara kadhaa ikiwemo; mwaka 1971, 1994 & 2009. Kwa mujibu wa kifungu C.28 (a), GAZETI la Serikali linatakiwa kutolewa (published) kila siku ya IJUMAA ya Wiki tu. Hili ni sharti la LAZIMA na halina mjadala & haijawahi kutokea GAZETI likatoka siku tofauti na Ijumaa.
GAZETI lilianzishwa kwa lengo la kutoa matangazo ya taarifa muhimu za Serikali ikiwemo; taarifa za utunzi wa sheria za Bunge, Kanuni, teuzi za maafisa wa Serikali, ufutwaji wa nyaraka kama vile hati za viwanja na taarifa nyingine muhimu. GAZETI pia hutumika kama chombo cha kufanya MAREJEO.
SHARTI LA KISHERIA KUTANGAZWA KWA MAWAKILI WA SERIKALI:
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) amepewa mamlaka ya kuteua Mawakili wa Serikali (State Attorneys) na baada ya uteuzi huo, majina ya wateule yanatakiwa kutangazwa kwenye GAZETI LA SERIKALI. Hili sio OMBI bali ni SHARTI LA LAZIMA.
UPOTOSHAJI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU:
Tafadhali rejea hapo chini kuna nyaraka mbili; moja ni "HATI" ya uteuzi wa Mawakili wa Serikali na nyingine ni GAZETI LA SERIKALI ambalo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inadai ilichapisha majina ya Mawakili wote walioteuliwa!
Ukisoma kwa umakini kwenye "HATI" ya uteuzi & pia ukisoma kwenye GAZETI utagundua nyaraka zote zina namba 103 & 38. Lakini, tofauti ni tarehe ambapo, HATI ina tarehe 26 Septemba 2022, wakati GAZETI lina tarehe 23 Septemba 2022.
Hilo GAZETI limetoka siku ya Ijumaa kama sheria inavyoelekeza. Hati ya uteuzi imetoka siku ya tarehe 26 Septemba 2022, ambayo ni Jumatatu. Hii ina maana kwamba, HATI ilitoka wiki iliyofuata BAADA ya GAZETI kuchapishwa. Pia, kila GAZETI lina namba yake peke (unique number) ambayo haijirudii kamwe.
Namba 103 inamaanisha mwaka, kwahiyo magazeti yote ya mwaka mzima yatakuwa na (VOLUME NO.) inayofanana. Isipokuwa, toleo namba za GAZETI hutofautiana. Mfano, kama GAZETI la Ijumaa hii ni Vol. 103, Toleo Na. 38, la Ijumaa ijayo litakuwa Vol. 103, Toleo Na. 39 na kuendelea.
Nataka Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajue kwamba, siku ya JUMATATU ambayo anasema kuna HATI imechapishwa, hakuna GAZETI limetoka siku hiyo. Kisheria, chini ya kifungu C.28(a) Jumatatu ni siku ya mwisho ya kuwasilisha (kabla ya saa SITA MCHANA), taarifa zote kwa Mpiga Chapa wa Serikali ili taarifa hizo ziweze kuchapishwa na kutangazwa siku ya IJUMAA.
Hivyo, GAZETI la tarehe 26 Septemba 2022 halipo & GAZETI la tarehe 23 Septemba 2022 lenye kurasa 92, halina GN. 583B wala orodha ya Mawakili. Kutokana na dosari hii, Mawakili wote wa Serikali hawana MAMLAKA ya kisheria kusimamia kesi yoyote ile mahakamani au kutekeleza majukumu mengine.
Kwa msimamo huu wa kisheria, sio tu kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ivunja MIIKO & MAADILI ya Uwakili, bali pia Mawakili wametoa taarifa potofu mbele ya mahakama na hili ni kosa la kutoa USHAHIDI WA UONGO chini ya kifungu 104 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code, Cap. 16), kosa lenye adhabu ya MIAKA SABA (7) gerezani.
Rais SSH, nikuombe utumie hekima & busara katika hili kwa kuzingatia maslahi ya umma.
Nawasilisha.
#BabaMwita ⚖️
Peter Madeleka retweeted
UJUMBE WA WAZI KWA MHE. RAIS SSH KUHUSU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (AG) & NAIBU WAKE
Mhe. Rais SSH, naomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe kwa sababu kuu moja; IMESHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE (UZEMBE).
NATOA UFAFANUZI
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi, ibara 59(3), ikisomwa sambamba na vifungu 16B, 24(3) & (4) vya Sheria inaitwa "The Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act. Cap 268, sambamba na aya 7 ya "The Office of the Attorney General (Re-structure) Order", GN. No. 48 ya 2018, Mwanasheria Mkuu wa Serikali AMEKIUKA masharti ya sheria hizi ili kuwapa MAMLAKA Mawakili wa Serikali (State Attorneys) UHALALI wa kufanya kazi zao.
Vifungu vilivyoorodheshwa hapo juu vinaelekeza kwamba, baada ya Mwanasheria Mkuu (AG) kuteuliwa na kushika madaraka, anatakiwa KUTEUA Mawakili wa Serikali na majina yao yote ni LAZIMA yatangazwe kwenye GAZETI LA SERIKALI kwa kuzingatia aya 3(1) ya AG (Appointment of Law Officers & State Attorneys).
HOJA YA OFISI YA AG
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (kupitia mjadala wa mahakamani), tayari utaratibu huo wa kisheria wa uteuzi & utambuzi wa Mawakili wa Serikali umeshafanyika kupitia GN. No. 583B ya tarehe 26 Septemba 2022, ambayo kwa msimamo wa kisheria, kifungu 9 cha GN. hii mpya KIMEFUTA GN. iliyotangulia ya 2020.
UHALALI WA KISHERIA WA TANGAZO LA SERIKALI JIPYA
Tatizo la Ofisi ya AG, ni kutofautisha kati ya "TANGAZO LA SERIKALI" & "TANGAZO KUWA GAZETTED!"
GN. No. 583B ya 26 Septemba 2022 (yenye kurasa 3 tu) haikidhi VIGEZO vya kisheria kwa sababu zifuatazo; moja, haina ORODHA ya Mawakili wote wa Serikali walioteuliwa na AG, pili GN. hii haikutangazwa kwenye GAZETI LA SERIKALI kama sheria inavyomwelekeza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya kifungu 24(4) tajwa hapo juu.
Hii ina maana kwamba, GN. hii mpya haina UHALALI na HAIPO (ni muswada tu na sio sheria). Lakini pia, maana nyingine ni kwamba AG hakuteua Mawakili wa Serikali kama alivyoelekezwa na sheria, na maana nyingine ni kwamba, Mawakili WOTE wa Serikali wa sasa wanatekeleza majukumu yao kinyume cha sheria. Ni BATILI.
UKWELI
Tangazo la mwisho lililofuata utaratibu wa kisheria la Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni la GN. No. 1011 ya 27 Novemba 2020 ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Prof. Adelardus L. Kilangi aliorodhesha majina ya Mawakili wote wa Serikali 1763 & kuwatangaza kupitia GAZETTE.
Hapo chini 👇🏾 nimeweka "HATI" toka kwa AG wa sasa yenye MAPUNGUFU ya kisheria, lakini pia "mfano" wa namna majina ya Mawakili yanatakiwa kuorodheshwa ili kukidhi TAKWA LA KISHERIA – kitu ambacho hakikufanywa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa sasa & Naibu wake.
HITIMISHO
Nitoe pongezi kwa Adv. P. Madeleka kwa kuibua hoja hii, na baada ya majadiliano naye na kufanya utafiti wangu binafsi, nimegundua mapungufu tajwa hapo juu & naunga mkono hoja ya Adv. Madeleka.
Kwamba, utaratibu wa kuteua Mawakili wa Serikali (State Attorneys) UMEKOSEWA na naomba baada ya utafiti wako, Mhe. rais, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali IWAJIBISHWE kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa UZEMBE huu uliojitokeza.
Credit: @PMadeleka
Naomba kuwasilisha.
#BabaMwita
Peter Madeleka retweeted
Mtendahaki ni Mungu pekee, lakini duniani wasimamia haki ni mahakama, hivyo ni muhimu kuwa waadilifu.
#MamaYukoKazini
Peter Madeleka retweeted
Feleshi anampeleka Madeleka Kamati ya Nidhamu kwa kumkosoa Hakimu.
Swali kwa Feleshi:
Unaelewa kila tukikata rufaa tunamkosoa Hakimu au Jaji?
Huwa tunasema:
The judge ERRED in law and fact.
Jaji na Hakimu ni binadamu wanakosea Kisheria, KiFACT na Kinidhamu. Hawako juu ya sheria
Peter Madeleka retweeted
TAFAKARI KUHUSU KAMATI YA MAADILI YA MAWAKILI:
Kamati ya Maadili ya Mawakili (Advocates Committee) imeanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mawakili (The Advocates Act, CAP. 341). Jukumu kubwa ni kusikiliza MALALAMIKO & UTETEZI baina ya wanasheria. Baada ya hoja kusikilizwa Kamati hutoa maamuzi, ikiwemo kutoa adhabu ya mtu KUSIMAMISHWA kwa muda (temporary suspension) au KUFUTWA uwakili kimoja (permanent removal) na adhabu nyingine kutokana na UZITO wa tuhuma.
Nafasi ya kushinda kesi mbele ya Kamati hii ni ndogo mno kutokana na MUUNDO wa Kamati. Kwa kifupi, Kamati inafanya kazi kwa mfumo wa kimahakama.
WAJUMBE WA KAMATI:
Kamati ina wajumbe wa KUDUMU wawili na wengine wasio wa kudumu ambapo wakudumu ni Jaji wa Mahakama Kuu (M/Kiti wa Kamati) ambaye hupendekezwa na Jaji Mkuu & Wakili wa kujitegemea ambaye huteuliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Naibu wake – ambao hawa ni wajumbe wasio wa kudumu na huingia kwenye Kamati pale tu wanaposhika nyadhifa zao. Mfano, Rais akiteua DPP mpya leo, DPP aliyeko sasa anapoteza ujumbe kwenye Kamati na huyu DPP mpya ndiye atashika nafasi hiyo ya ujumbe. Hivyo hivyo kwa AG & Naibu AG. Pia, Kamati imepewa uwezo wa kuteua mtumishi wa mmoja wa Serikali mwenye sifa za uwakili kuwa "Secretary" wa Kamati.
UBORA WA KAMATI KWENYE KUTOA HAKI:
Kwa mtazamo wangu, hii Kamati imeundwa KIMKAKATI & MAKUSUDI kabisa ili KUDHIBITI wanasheria wanaoikosoa Serikali. Utaelewa hili ukirudia listi ya wajumbe; JAJI WA MAHAKAMA KUU, DPP, AG, NAIBU AG & WAKILI TOKA TLS.
Ili maamuzi yawe halali unahitaji kura za wajumbe wawili (minimum). Je, kwa hao niliowataja unadhani hapa haki itaweza kutendeka ukizingatia MLALAMIKAJI kwenye kesi zote ni AG, ambaye ni MJUMBE wa Kamati ya KUHUKUMU? Hili nawaachia mjadili lakini binafsi sioni haki kutendeka.
Pia, niweke kumbukumbu sawa, unayemuona kwenye hiyo picha 👇🏾 ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wa sasa Jaji Eliezer Feleshi, ambaye ndiye amehusika kupeleka mawakili watatu mbele ya Kamati ya Maadili akiwemo Adv. Fatma Karume, Adv. Mwabukusi na sasa ni zamu ya Adv. Madeleka. Mtu huyo huyo mmoja!
KESI YA WAKILI FATMA KARUME:
Ndugu Ado Shaibu, Katibu Mkuu Taifa, ACT (wakati huo akiwa Katibu Uenezi) alifungua kesi ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Adelardus Kilangi uliofanywa na rais JPM (Hayati), kwa hoja kwamba uteuzi huo ulikuwa na makosa, kwamba Prof. Kilangi hakukidhi vigezo vya kuteuliwa.
Mwaka 2019, huyu AG wa sasa wakati huo akiwa Jaji Kiongozi (Jaji boss wa mahakama Kuu) alimsimamisha kwa muda (suspend) Adv. Karume kutokana na kilichoelezwa na Mawakili wa Serikali kwamba ni UTOVU WA NIDHAMU wa kiwakili (professional misconduct) uliofanywa na Adv. Karume kwenye wasilisho la kesi (submission).
Jaji Kiongozi wakati huo, Eliezer Feleshi akamsimamisha kwa muda Adv. Karume kutofanya shughuli za uwakili na kuamuru malalamiko yapelekwe kwenye Kamati ya Maadili (Advocates Committee) ili tuhuma dhidi yake zichunguzwe na yeye (Fatma) apate nafasi ya kujitetea.
Lakini, kabla hata kesi haijafika kwenye Kamati (kwa utaratibu uliopangwa kisheria), tayari AG Kilangi (mlalamikiwa kwenye kesi ya msingi) akapeleka malalamiko mengine kwenye Kamati akilalamika KUCHAFULIWA na Fatma. Ndipo, Kamati pasipo kumsikiliza vyema Adv. Karume ikamfutia leseni yake ya uwakili, hivyo akapoteza uwakili wake.
RUFAA:
Kupitia Wakili Peter Kikatiba, Adv. Karume akakata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Mawakili kufutiwa uwakili wake. Mahakama IKABATILISHA maamuzi ya Kamati kwa hoja kwamba, Kamati ilikiuka AMRI ya Jaji Kiongozi (Feleshi). Kwa maamuzi haya ya Mahakama Kuu, Fatma alitakiwa arejeshewe uwakili wake, lakini mpaka sasa ni SIASA tu zinafanyika.
Ushauri wangu, Sheria ya Mawakili ifanyiwe marekebisho ili kuwe na USAWA linapokuja swala la utoaji haki. Vinginevyo, mtaendelea KUUMIZA wanasheria.
#BabaMwita ⚖️
Peter Madeleka retweeted
Asante Wasanii #TanzaniaAllStars kwa wimbo huu wa kumsindikiza mpendwa wetu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa.
#RIPLowassa tutaonana baadaye.
Peter Madeleka retweeted
Wakili wa kujitegemea nchini Wakili Peter Madeleka @PMadeleka amemshutumu Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika Wakili Harold Sungusia kwa kile anachodai kuwa anaendesha ofisi kwa upendeleo.
Wakili Madeleka amesema baadhi ya wanachama wa Chama hicho wamekuwa wakikumbwa na madhila mbalimbali ikiwemo kukamatwa na kutishiwa kuuawa huku Chama hicho kikiwa kimya bila kuchukua hatua katika wakati ambao wanachama wengine wakikumbwa na madhila kama hayo hujitokeza hadharani kwa haraka na kuchukua hatua.
"TLS chini ya Rais HAROLD SUNGUSIA imekuwa ikifanya kazi yake kwa UBAGUZI MKUBWA. Imekuwa ikichukua HATUA dhidi ya VITENDO vinavyofanywa kwa MAWAKILI anaowataka yeye. Sisi wengine hata TUKITISHIWA KUULIWA au KUWEKWA GEREZANI hakuna HATUA zinazochukuliwa na TLS. UBAGUZI ni SUMU TLS" ameandika Madeleka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.
" Licha ya kwamba nimepata MISUKOSUKO kama KUTISHIWA KUULIWA na KUWEKWA GEREZANI kinyume cha SHERIA, TLS chini ya MARAIS wote akiwemo huyo 👇(Rais Sungusia) HAIJAWAHI kuwa na MSAADA kwangu kama MWANACHAMA wake. Tuwe MAKINI na watu wanaoomba KUONGOZA TLS" ameongeza Madeleka.
Hadi hivi sasa bado Uongozi wa Chama hicho haujajibu lolote na tunaendelea kuufuatilia ili kupata majibu ya shutma hizo.
Peter Madeleka retweeted
HII IFIKE KWA DPP:
Maelezo ya DPP yanaonesha baada ya Ndg. HASHIM kupeleka malalamiko yake polisi, Bi. PAULINE GEKUL naye akapeleka malalamiko polisi, hii tunaita (counterclaim). DPP anasema huwenda akaruhusu ufunguaji wa "kesi dhidi/juu ya kesi" (counter lawsuit). Hii ina maana, upo UWEZEKANO kwa DPP kuleta kesi mbili mahakamani; moja dhidi ya Pauline (Hashim mlalamikaji) na nyingine dhidi ya Hashimu (Pauline akiwa mlalamikaji).
Kesi za aina hii, mara nyingi hufungiliwa ili KUMLAZIMISHA mlalamikaji wa kwanza (ambapo huwa ndiye mwathirika wa kweli) kuondoa malalamiko yake mahakamani! Hili likitokea, maana yake Hashim huenda atalazimika "kuua" kesi dhidi ya Pauline ili kesi dhidi yake ifutwe. Mara nyingi makubaliano haya huwa yanafanyika nyuma ya pazia (ila sitegemei Hashim kukubali hili).
Jambo jingine, kwenye maelezo ya DPP kuna maeneo mengi amejieleza KISIASA (sio uhalisia wa sheria). Ametafsiri sheria kimakosa (labda kwa makusudi) ili tu KUHALALISHA (justify) alichokifanya.
MSIMAMO WA SHERIA:
Kwa faida ya wengi, mtu anapofungua kesi kupitia kifungu 128(2)&(4) CPA, Hakimu hutakiwa KUANDAA (yeye mwenyewe) au KUSABABISHA KUANDALIWA kwa hati ya mashtaka. Kwenye "kesi ya Hashim", Hakimu alijiridhisha pasipo na shaka kuwa taratibu zote za kisheria zilifuatwa na Wakili wa mlalamikaji, ndipo akaandaa hati ya mashtaka na kupanga siku ya kusikilizwa kwa kesi.
Hii ina maana, tayari Hakimu alisharuhusu Wakili Peter Madeleka aendeshe mashtaka kama mtu binafsi (private prosecutor), na katika hatua hii, tayari Hakimu alikuwa ameshatumia kifungu 99 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) kinachompa mamlaka ya kuamua kesi isimamiwe na MTU BINAFSI.
Ukweli ni kwamba, kama Hakimu angetaka ofisi ya DPP iendeshe mashtaka, basi ANGESABABISHA hati ya mashtaka kuundwa ya ofisi hiyo ili kuruhusu Mawakili wa Serikali kuendesha kesi. Hili halikufanyika kwa sababu Hakimu hakutaka uwepo wa moja kwa moja wa DPP kwenye kesi hii (labda kutokana na sababu kwamba mtuhumiwa ni kiongozi wa Serikali, tena ofisi ya DPP iko chini ya Wizara aloyokuwa anaongoza (mtuhumiwa)).
Ndiyo, Katiba ibara 59(B, Sheria ya Mashtaka 9(1)(c) & CPA 91(1) vinatoa mamlaka kwa DPP kuingilia na kuondoa kesi, lakini, baada ya kukusikiliza kwa MAKINI, nimebaini uondowaji wa kesi hii una walakini na hila. Tukirudi kwenye ibara 59B ya Katiba, nadhani DPP ametumia madaraka yake visivyo kwa sababu uamuzi wake haukuwa na MASLAHI YA UMMA.
Narudia tena, sababu alizozitoa DPP hazinifanyi niamini alileta NOLLE kwa nia njema.
Mwisho, nimkubushe DPP kuwa vifungu vya 131A & 225(4) vya CPA, vikisomwa sambamba na mwongozo wake wa mwezi Septemba ulioanza utekelezwaji Octoba 2022. Kisheria kosa analotuhumiwa Pauline upelelezi wake unatakiwa ukamilike ndani ya SIKU SITINI (60) kwa sababu ni kosa ambalo halisikilizwi mahakama kuu.
Unless, of course, atumie ile "LOOPHOLE" ya Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa kuomba KIBALI toka kwake (DPP) ili azidishe muda wa upelelezi – kitu ambacho kwenye macho ya sheria, na kwa sababu jambo hili linamuhusu DPP uamuzi huo utaleta MGONGANO WA KIMASLAHI (conflict of interest). Pia itapelekea MISCARRIAGE OF JUSTICE.
Nikiwa kama raia mwema, nataka kuona haki ikitendeka. Tusubiri hukumu ya rufaa.
#BabaMwita ⚖️



































