Replying to @_zack255 @kigogo2014 @RashdaZunde @Getrude_mollel @Kipanga1986 @kwamekivaisi @MankindUwezo @dictatorbin @joharimshana @1ngadu1 @420Cousin
NYIE CHAWA NANI ANAWALIPA KUTWA NZIMA SAA 24 MPO KUTETEA WAOVU MITANDAONI¿¿¿😭😭😭
mobappdev retweeted
KISIWA CHA AMANI:
Hata kama kuna Kesi za “UHAINI” zinaendelea kufunguliwa MAHAKAMANI 👇, lakini Tanzania bado ni KISIWA CHA AMANI kwa kuwa ipo SALAMA. Kama AFCON na WATALII hawatakuja kwa sababu ya “UHAINI”, basi huo ni UWOGA wao tu. 🥲🥲
mobappdev retweeted
Tunalaani vikali kukamatwa kwa kiongozi wetu Zakaria Obadi huko Kahama.
Serikali na CCM wanapaswa kuelewa kuwa demokrasia haiwezi kufungwa pingu, na mawazo hayawezi kushindwa kwa vitisho.
Mnaweza kuwakamata watu, lakini hamwezi kukamata dhamiri za wananchi. Mnaweza kulazimisha ukimya, lakini ukimya wa hofu si ridhaa, na ukandamizaji si ushindi.
Historia imethibitisha, nguvu inaweza kuchelewesha mabadiliko, lakini haiwezi kuua kiu ya uhuru na haki.
Nguvu ya uongozi si kunyamazisha upinzani, bali ni kuwa na ujasiri wa kukabiliana na hoja.
mobappdev retweeted
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Rukwa,
Benjamin Mizengo amelitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu mahali walipo Coletta Ntidyicha na Ibrahim Myovela, akisisitiza kuwa vyombo vya usalama vina wajibu wa kulinda maisha ya raia na mali zao.
Replying to @ChademaTZ2 @HecheJohn
Nchi yenye madini ya kila aina,mbuga za wanyama kila mahali😭😭😭
mobappdev retweeted
Makamu Mwenyekiti Mhe. @HecheJohn akiwa njiani kuelekea Haydom kwenye Kongamano la Bawacha amekutana na wananchi wa kijiji cha Qaru, Kata ya Endabash, Wilaya Karatu wakiwa wanachota maji. Walipata wasaa wa kumweleza Mhe. @HecheJohn adha ya maji wanayopitia katika kijiji hicho.
Replying to @mshambuliaji
Naomba uulize watawala, jee Tungekua na mtu kama KABILA anachofanya huko DRC jee hapo Tanzania angefunguliwa mashtaka gani??very sad 😭😭😭
JEE WANA NIA YA DHATI KWELI YA MARIDHIANO au ni kupoteza muda 2030 ifike???
mobappdev retweeted
Gutted to learn that my brother, John Pambalu, has been charged with treason, joining a long list of those targeted for persecution by Samia Suluhu's bloody regime.
This nonsense must stop now.
Free John Pambalu Now.
Replying to @EsirEid
Wanaimba MARIDHIANO HUYU MIOYO YAO IMEJAA CHUKI😭😭😭 sasa sijui kina KABILA wangefunguliwa kesi gani hapo bongo.Maana kila raia mhaini gaidi😭😭😭 @lifeofmshaba @ccm_tanzania @godbless_lema @HecheJohn
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesikitishwa na taarifa ya Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya Uchaguzi wa chama hicho Makao Makuu, John Pambalu kufunguliwa mashtaka ya uhaini sawa na yale yanayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu huku akisisitiza kuwa hatakimbia nchi hata kama naye atafunguliwa mashtaka ya uhaini au ugaidi.
Heche ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika Kongamano la Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara lililofanyika Haydom, wilayani Mbulu.
Pambalu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la uhaini lililoainishwa chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyorekebishwa mwaka 2023. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa kuwa kati ya Septemba 1, 2025 na Oktoba 29, 2025, katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam, Pambalu alidhamiria kuwashawishi wananchi kukwamisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Hati hiyo inaeleza kuwa alionesha nia hiyo kwa kuendesha na kuratibu maandamano yasiyo na kikomo kote nchini kwa lengo la kuitisha na kuishinikiza Serikali.
“Najua na mimi wakati wowote watanipa kesi ya aina hiyo hiyo au nyingine wanayotaka iwe ya ugaidi iwe ya uhaini lakini mimi nimesema sitakimbia nchi yangu. Hii ni nchi yetu. Tutaipambania tukiwa humu. Tutapambana tukiwa humuhumu... Uhakika kama jua linavyochomoza asubuhi... Kitu nilicho na uhakika nacho ni kwamba tutashinda, hilo nina uhakika nalo”, ameeleza heche akibainisha kuwa Pambalu alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa zaidi ya siku 10 kabla ya kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka hayo.
mobappdev retweeted
..... Kuna siku watu wengi watainamisha vichwa vyao kwa aibu na fedheha,
Pale watakapogundua ukubwa wa uovu walioutetea na thamani ya mashujaa waliowadhihaki.
Pindi ukweli utakapofunua yale waliyoyafumbia macho, wengi watajuta kwa kusimama upande usio sahihi wa historia.
mobappdev retweeted
MUNGU Mbariki huyu kijana Japhate Manyama, Mratibu wa CHASO Mkoa wa Mwanza.
Hakika nchi yetu ipo mikono salama chini ya vijana wenye akili timamu.
Nasikiliza hii clip huku natokwa na machozi ya FURAHA kuwa katika nyakati ngumu kama hizi kuna watu kama JAPHATE wamegoma kuwa MISUKULE.
Tumpe dogo REPOST 200.














