Manka 🌹 retweeted
Mwenyezi Mungu akapate kubariki haso zetu hii leo zikapate kuzaa matunda🙏.
Gm wakuu🤝
Manka 🌹 retweeted
Gari ya kwanza Ile inasepa. Ya pili Mali ni shindili😂. KILIMO kwetu ni kama mpira kwa aucho ni kugusa TU. Tunajitafuta 💪
Manka 🌹 retweeted
NIA NJEMA.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia
Utakalo hutimia
Kwa utii navumilia
Teso na matata pia
Nipe bwana Neema zako
Niongeze sifa yako
Amina
Manka 🌹 retweeted
Ee Baba yetu Mungu Mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.
Manka 🌹 retweeted
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
Manka 🌹 retweeted
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Manka 🌹 retweeted
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALAIKA WA BWANA
•Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
•Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu.
~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Manka 🌹 retweeted
Walee watoto wako katika njia njema. Wapende na uwajali. Wasikilize, lakini USIWADEKEZE!
Manka 🌹 retweeted
Fanya wakati wao bado wanafikiria,amka wakiwa wamelala,jiwekee akiba wao wakiwa wanamwagilia moyo💪
Manka 🌹 retweeted
KWARESMA: OMBA FURAHA KATIKA MAISHA YA KIROHO.
"Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema, Furahini." (Wafilipi 4:4)
Furaha ya Bwana ni nguvu yako. Usiruhusu huzuni itawale moyo wako.
•Mungu akupe furaha ya kweli katika kumtumikia.
•Mungu akupe kibali cha kuombea wale waliokata tamaa wapate furaha mpya katika Kristo.
•Mungu akubariki kila unapopitia huzuni na mkato wa tamaa.
Uwe na siku njema!
Manka 🌹 retweeted
"Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu." (Isaya 1:18)
Manka 🌹 retweeted
Ee Masiha tunakuabudu tunakushukuru; kwani umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu!
Manka 🌹 retweeted
SALA YA USIKU - JUMATANO
K. Ee Mungu, uje kutusaidia.
W. Ee Bwana, utusaidie hima.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele. Amina. Aleluya
Tuwaze katika moyo makosa tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo kwa maneno, kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu: (kimya kifupi)
Namwungamia Mungu mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo, na kwa kutotimiza wajibu: nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana namwomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
K. Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele.
UTENZI
Sote twamshukuru Mungu wetu,
Kwa mioyo, mikono na sauti,
Kafanya maajabu Yeye huyo,
Vyake viumbe vinashangilia;
Tangu mwa mama zetu mikononi
Za kwetu njia kazibarikia
Tuna vipawa vya upendo tele,
Hata leo bado ni Mungu wetu.
Uwe karibu Mungu Mkarimu
Kwa siku zote za maisha yetu,
Mioyo yetu iwe mikunjufu
Kwa amani yako tuchangamshwe;
Katika neema yako tuweke,
Mashakani njia utuoneshe,
Utuepushe na maovu yote
Ya ulimwengu huu na ujao.
Sifa na shukrani kwako Mungu
Kwako Baba sasa na zitolewe,
Kwa Mwana, na kwa anayetawala
Pamoja na ninyi juu mbinguni,
Ewe Mungu Mmoja wa milele
Mbingu na dunia zakuabudu;
Vile ilivyokuwa ndo ilivyo,
Na hivyo itakuwa kwa milele.
M. Rinkart 1586-1649
Ant. 1: Ee Mungu, uwe mlinzi wangu na kimbilio langu.
Zab.31:1-5
Kwako, Ee Mungu, nakimbilia usalama,/
usikubali niaibike kamwe;*
wewe ni mwadilifu, uniokoe.
Unitegee sikio, uniokoe haraka:/
Uwe kwangu mwamba wa usalama,*
ngome imara ya kunisalimisha.
Wewe ni mwamba wa usalama wangu na kinga yangu;*
kwa hisani yako uniongoze na kunielekeza.
Unitoe katika mtego walionitegea;*
unisalimishe katika hatari.
Mikononi mwako naiweka roho yangu;*
uniokoe, Ee Mungu, Mungu mwaminifu.
Atukuzwe Baba...
*Ant. 2: Kutoka ndani ya moyo wangu nakulilia, Ee Bwana.*
Zab.130
Katika unyonge wangu, nakulilia, Ee Mungu./
Ee Bwana, sikiliza sauti yangu,*
uitegee sikio sauti ya ombi langu.
Kama, Ee Mungu, ungeweka kumbukumbu ya madhambi yetu,*
ni nani, Ee Bwana, angeweza kusimama mbele yako?
Lakini wewe watusamehe dhambi,*
ili tukutumikie kwa uchaji.
Naweka tumaini langu lote kwa Mungu;*
nina imani sana na neno lake.
Namngojea Mungu kwa hamu kubwa,/
kuliko mlinzi usiku anavyongojea pambazuko;*
kuliko walinzi wanavyongojea kupambazuke.
Ee Israeli, umtumainie Mungu,/
maana yeye ni mwenye upendo mkuu;*
daima yuko tayari kutuokoa.
Naam, atawaokoa watu wa Israeli,*
katika maovu yao yote.
Atukuzwe Baba....
Ant. 2: Kutoka ndani ya moyo wangu nakulilia, Ee Bwana.
SOMO: Ef.4:26-27
Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima. Msimpe Shetani nafasi.
KIITIKIZANO
K. Mikononi mwako, Ee Bwana, naiweka roho yangu.
Ant. Utuokoe, Ee Bwana, wakati tukiwa macho; utulinde tukiwa usingizini; ili tukeshe pamoja na Kristo, na tupumzike naye kwa amani.
WIMBO WA SIMEONI: Lk.2:29-32
Sasa, Bwana, umetimiza ahadi yako,/
waweza kumruhusu mtumishi wako,*
aende kwa amani.
Maana kwa macho yangu/
nimeuona wokovu utokao kwako,*
ambao umeutayarisha mbele ya watu wote:
Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa,*
na utukufu kwa watu wako Israeli.
Atukuzwe Baba na Mwana...
SALA
Tuombe: Bwana Yesu Kristo, mpole na mnyenyekevu wa moyo, unawapatia wale wanaokufuata nira laini na mzigo ulio mwepesi kuuchukua. Twakuomba uzipokee sala na kazi zetu za leo, na utujalie pumziko tunalohitaji, ili tuwe daima tayari kukutumikia, Wewe, unayeishi na kutawala daima na milele, Amina.
BARAKA
K. Bwana atujalie usiku mtulivu, na mwisho mkamilifu, Amina.
WIMBO KWA BIKIRA MARIA
Ewe Mama wa Kristo, sikia kilio chetu,
Ewe nyota ya bahari, ewe Mlango wa mbingu,
Mama wa yeye mwenyewe, ambaye alikuumba,
Tunapozama topeni, msaada twakuomba;
Kwa furaha ile ile, Gabrieli alokupa,
E Bikira wa pekee, wa kwanza na mwisho pia,
Twakuomba tujalie, tupewe yako huruma.
Manka 🌹 retweeted
SALA YA JIONI.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
UNGAMO LA DHAMBI.
Na tuwaze katika moyo makoda yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo(………………………)
Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenyeheri, Bikira daima, malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
+Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina.
Ee Mungu mwenye huruma, uwashushie baraka zako, Baba Mtakatifu wetu Francis na maaskofu, na mapadre, na mashemasi, wakulima, wafanyakazi wote, wanafunzi na jamii yote unaowafanya kuwa watu wako . Uwaokoe wale wasiokujua bado, uwafariji wagonjwa, waelekee wanaozimia waweze kuona mwanga wa milel, Amina.
ANGELUS.
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria,naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Ndimi mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyosema.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Neno wa Mungu akatwaa mwili,akakaa kwetu.
~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu,tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu,ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika,kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu;kwa mateso na msalaba wake,tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Bikira Maria Malkia wa amani~Utuombee!
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina🙏
Manka 🌹 retweeted
Tunawatakia Jumatano njema ya Majivu na mfungo mwema wa Kwaresma Wananchi.
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko






























