| Philosophy | Theology | Roman Catholic |Ps 20:7| Pray, Hope And Don't Worry |God wins in the end| Uncouth & Impolite get BLOCKED🚫

East Africa
Joined April 2018
Pray the Rosary. Keep the beads rolling.
3
14
259
MITAGUSO MIKUU 21 YA KANISA KATOLIKI. Mtaguso ni Mkutano mkuu wa Maaskofu WOTE duniani, unaoitishwa na kuongozwa na Papa (au kwa idhini yake), ili kujadili na kuchukua maamuzi mazito kuhusu imani, maadili, nidhamu, au uongozi wa Kanisa zima ulimwenguni. Kwa kawaida Maamuzi na Mafundisho yanayotolewa na Mtaguso Mkuu (hasa yanapothibitishwa na Papa) huwa na mamlaka ya juu sana ya kiroho na kisheria ndani ya Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki limekuwa na Mitaguso Mikuu 21 ya Kiekumene, kuanzia Mtaguso wa Nisea mwaka 325 hadi Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikano (1962–1965). Hii ndiyo orodha ya Mitaguso hiyo na umuhimu wake kwa ufupi: 1. Nisea I (325): Ulitetea uungu wa Yesu Kristo dhidi ya mafundisho ya Arius. 2. Konstantinopoli I (381): Ulifafanua imani kuhusu Utatu Mtakatifu, hasa uungu wa Roho Mtakatifu. 3. Efeso (431): Ulithibitisha cheo cha Bikira Maria kama Mama wa Mungu (Theotokos). 4. Chalcedon (451): Ulifafanua kwamba Kristo ni Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli, katika nafsi moja. 5. Konstantinopoli II (553): Ulithibitisha mafundisho kuhusu umoja wa nafsi ya Kristo. 6. Konstantinopoli III (680–681): Ulifundisha kwamba Kristo ana mapenzi ya kimungu na ya kibinadamu. 7. Nisea II (787): Ulithibitisha uhalali wa kuheshimu picha takatifu, ukitofautisha heshima na ibada inayomstahili Mungu pekee. 8. Konstantinopoli IV (869–870): Ulishughulikia migogoro ya uongozi na nidhamu ya Kanisa. 9. Laterano I (1123): Ulishughulikia uhusiano kati ya Kanisa na mamlaka za kisiasa. 10. Laterano II (1139): Ulilenga kurejesha umoja na kuimarisha nidhamu ya Kanisa. 11. Laterano III (1179): Ulisisitiza kwamba uchaguzi wa Papa unahitaji theluthi mbili ya kura za makardinali wapiga kura. 12. Laterano IV (1215): Ulifafanua mafundisho na kuimarisha maisha ya sakramenti. 13. Lyons I (1245): Ulishughulikia migogoro kati ya mamlaka ya kipapa na watawala wa kisiasa. 14. Lyons II (1274): Ulijaribu kurejesha umoja kati ya Kanisa la Roma na Kanisa la Mashariki. 15. Vienne (1311–1312): Ulishughulikia mageuzi ya Kanisa na suala la Shirika la Knights Templar. 16. Konstanz (1414–1418): Ulisaidia kumaliza mgawanyiko wa uongozi wa kipapa uliojulikana kama Western Schism. 17. Basel–Ferrara–Florence (1431–1445): Ulifanya juhudi za kuunganisha Makanisa ya Mashariki na Magharibi. 18. Laterano V (1512–1517): Ulijadili mageuzi ya Kanisa kabla ya Matengenezo ya Kiprotestanti. 19. Trento (1545–1563): Ulifafanua mafundisho ya Kikatoliki katika kipindi cha Matengenezo ya Kiprotestanti na kuimarisha malezi ya makasisi. 20. Vatikano I (1869–1870): Ulifafanua mamlaka ya Papa na fundisho la kutokukosea kwa Papa katika mazingira maalumu ya kufafanua rasmi imani au maadili. 21. Vatikano II (1962–1965): Ulileta mafundisho na maelekezo muhimu kuhusu liturujia, utume wa Kanisa, umoja wa Wakristo, uhuru wa dini na uhusiano na ulimwengu wa kisasa. 📌 JAMBO LA KUZINGATIA: Vatican II ndio Mtaguso Mkuu wa mwisho wa Kiekumene katika historia ya Kanisa Katoliki hadi sasa. Hata hivyo, haukufuta mitaguso iliyotangulia; mafundisho yake yanaeleweka katika mwendelezo wa imani na Mapokeo ya Kanisa. Mitaguso hii inaonyesha jinsi Kanisa, katika historia yake ya karibu miaka 2,000, lilivyokabiliana na changamoto za mafundisho, nidhamu, umoja na utume wake duniani. Tumsifu Yesu Kristo.
1
4
17
474
Weka juhudi katika kile unachofanya. Ndoto bila juhudi hubaki kuwa mawazo. Hata hivyo, juhudi zinapaswa kwenda pamoja na maarifa, nidhamu na utayari wa kubadilisha mbinu pale mambo yanaposhindikana.
3
25
739
ROZARI TAKATIFU, MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi) 1. Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu. 2. Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani. 3. Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara. 4. Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo. 5. Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
1
6
1
33
626
Mwanakondoo aliyetolewa sadaka ndiye Kristo aliyefufuka kwa ushindi. Katika sadaka yake tunapata Msamaha, na katika ufufuko wake tunapata tumaini.
6
30
660
SALA YA ASUBUHI +Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni. Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. KANUNI YA IMANI. Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina. AMRI ZA MUNGU. 1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine. 2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. 3. Shika kitakatifu siku ya Mungu. 4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani. 5. Usiue. 6. Usizini. 7. Usiibe. 8. Usiseme uongo. 9. Usitamani mwanamke asiye mke wako. 10. Usitamani mali ya mtu mwingine. AMRI ZA KANISA. 1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa. 2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu. 3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka. 4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka. 5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka. 6. Shika sheria katoliki za ndoa. Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina. MALAIKA WA BWANA •Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. •Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. •Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina. SALA KWA MALAIKA MLINZI Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina. Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani. +Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
3
8
41
657
Stella Matutina, ora pro nobis. Stella del Mattino, prega per noi. Morning Star, pray for us. Nyota ya asubuhi, utuombee.
17
473
Tunaukimbilia, ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe kila siku tuingiapo hatarini, Ee Bikira Mtukufu mwenye baraka, Amina.🙏 Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama Mwanzo na sasa na siku zote na milele amina.
4
5
64
1,047
Pray the Rosary. Keep the beads rolling.
19
485
"Twaeni mnywe nyote. Hiki ndicho kikombe cha Damu yangu. Damu ya Agano jipya na la milele. Itakayomwagika kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wengi kwa maondoleo ya dhambi. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu"
2
43
694
Sala yangu ipae mbele yako Bwana, kama moshi wa ubani altareni; na kuinuliwa kwa mikono yangu kuwe kama sadaka ya jioni🙏
1
2
73
990
SALA YA JIONI. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina. Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina. SALA YA MATUMAINI. Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina. SALA YA MAPENDO. Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina. UNGAMO LA DHAMBI. Na tuwaze katika moyo makoda yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo(………………………) Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenyeheri, Bikira daima, malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu. +Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina. SALA YA KUTUBU. Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina. Ee Mungu mwenye huruma, uwashushie baraka zako, Baba Mtakatifu wetu Francis na maaskofu, na mapadre, na mashemasi, wakulima, wafanyakazi wote, wanafunzi na jamii yote unaowafanya kuwa watu wako . Uwaokoe wale wasiokujua bado, uwafariji wagonjwa, waelekee wanaozimia waweze kuona mwanga wa milel, Amina. ANGELUS. Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria,naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. ~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Ndimi mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyosema. ~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Neno wa Mungu akatwaa mwili,akakaa kwetu. ~Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu,tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu,ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika,kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu;kwa mateso na msalaba wake, tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina. Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu ~ Utuombee! SALA KWA MALAIKA MLINZI. Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina. Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele, Amina. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina🙏
5
1
29
612
"Twaeni Mle nyote, huu ndio Mwili wangu, utakaotolewa kwa ajili yenu"
2
63
699
Haijalishi unapitia nini au changamoto gani kwenye maisha yako, jitahidi sana usiuze roho yako kwa shetani. Faida yake inaweza kuonekana nzuri machoni, lakini gharama yake ni kubwa mno moyoni.
1
5
41
1,068
TUKIO LA KUSIKITISHA Padre afariki dunia baada ya kuangukiwa na MSALABA katikati ya adhimisho la Misa Takatifu. Jana Oktoba 17, 2026 huko Guayaquil, Ecuador (Kanisa la Our Lady of Perpetual Help), Padre Patricio Sánchez alipoteza maisha ghafla baada ya Msalaba mkubwa wa mbao uliokuwa ukutani Altareni kuachia na kumwangukia kichwani wakati akiwa anaadhimisha Misa iliyokuwa ikirushwa mubashara (Live Broadcast). Tukio hili limeacha sintofahamu na simanzi kubwa kwa waumini wa Parokia hiyo na Kanisa Katoliki duniani kote. Padre ameaga dunia akiwa katikati ya huduma takatifu aliyoitiwa kuifanya hapa duniani. Baada ya ajali hiyo kutokea, Jimbo Kuu la Guayaquil (Arquidiócesis de Guayaquil) pamoja na Kardinali ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Mwadhama Luis Gerardo Cabrera Kadinali Herrera walitoa taarifa rasmi kupitia kurasa zao za kijamii na vyombo vya habari. Kardinali Cabrera alieleza masikitiko yake makubwa na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Padre Patricio Sánchez Molinari, ndugu, marafiki, na shirika lake la kitawa. Kwenye taarifa hiyo walieleza kuwa Padre Sánchez "amekwenda kwenye Nyumba ya Baba yake wa milele ili kufurahia uwepo na utukufu wake." Raha ya milele umpe ee Bwana, na Mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani, amina 🙏🏽
14
12
103
9,160
ALAMA ZA KIKRISTO (1): CHI-RHO (☧) 1. JINA LA ALAMA Chi-Rho (☧) ni alama ya Kristo. Pia huitwa Christogram, yaani alama inayotumia herufi kuwakilisha jina la Yesu Kristo. 2. ASILI YA ALAMA Alama hii inatokana na alfabeti ya Kigiriki. Ina herufi mbili zilizounganishwa: Χ (Chi): Herufi ya 22 katika alfabeti ya Kigiriki na Ρ (Rho): Herufi ya 17 katika alfabeti ya Kigiriki. Herufi hizi ni za mwanzo za neno la Kigiriki "ΧΡΙΣΤΟΣ — CHRISTOS". Maana yake ni Kristo, yaani Mpakwa Mafuta. Herufi hizo huunganishwa na kutengeneza alama ☧. Hivyo, alama hii humwakilisha Kristo. 3. HISTORIA YA ALAMA HII Chi-Rho ni mojawapo ya alama za kale za Kikristo. Alama hii ilipata umaarufu mkubwa katika karne ya nne, wakati wa Mfalme Konstantino Mkuu (Constantine the Great). Kabla ya vita vya Milvian Bridge mwaka 312 BK, Konstantino anahusishwa katika mapokeo ya kihistoria na tukio la maono ya alama ya Kikristo. Katika kipindi kilichofuata, alama ya Chi-Rho ilitumika kwenye bendera ya kijeshi iliyojulikana kama Labarum. Ni muhimu kufahamu kwamba Konstantino hakubuni alama hii; ilikuwa tayari inajulikana kabla ya utawala wake, lakini matumizi yake yaliongezeka sana wakati wa utawala wake. 4. MAANA YAKE KATIKA BIBLIA Ingawa alama yenyewe haijaamriwa katika Biblia, maana yake inahusiana moja kwa moja na jina la Kristo. Rejea ya kwanza: Mathayo 16:16 Mtume Petro anamkiri Yesu kuwa Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Rejea ya pili: Wafilipi 2:9–11 Mtume Paulo anaeleza jinsi Mungu alivyomtukuza Yesu na kwamba kila ulimi utakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana. Rejea ya tatu: Ufunuo 1:8 na Ufu 22:13 Kristo anajitambulisha kama Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Aya hizi zinasaidia kuelewa maana ya kiimani ya Chi-Rho, ingawa hakuna mojawapo inayotaja alama hiyo moja kwa moja. 5. MAANA YAKE KATIKA KANISA KATOLIKI Alama Chi-Rho inatukumbusha mambo makuu manne: A. Utambulisho wa Kristo Alama hii inamtangaza Yesu kuwa Kristo, Mpakwa Mafuta wa Mungu. B. Ushindi wa Kristo Katika sanaa ya kale ya Kikristo, Chi-Rho ilihusishwa na ushindi wa Kristo na ushindi wa imani ya Kikristo. C. Kristo kuwa kiini cha maisha ya Kanisa Inatukumbusha kwamba Kanisa halijikusanyi kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Kristo. D. Kumkiri Kristo hadharani Alama hii imekuwa njia ya kuonyesha utambulisho wa Kikristo katika sanaa, maandishi na mapambo ya makanisa. 6. KWANINI ALAMA HII INAWEKWA KWENYE MAVAZI YA KILITURUJIA? Alama hii inapowekwa kwenye vazi la kiliturujia, Chi-Rho huwaelekeza waamini kwa Kristo. Kwa mfano, inaweza kupatikana kwenye Kasula (Chasuble) ambalo ni vazi la padre wakati wa kuadhimisha Misa; Vitambaa vya altare na mapambo ya mahali pa ibada; Vitu vya sanaa ya Kikristo; Baadhi ya misalaba na mapambo ya makanisa. Hata hivyo, si lazima kila vazi la padre liwe na alama hii. Matumizi yake hutegemea muundo wa vazi na mapokeo ya kisanii ya watengenezaji wa vazi husika. 8. Muhtasari Jina: Chi-Rho Alama: ☧ Lugha ya asili: Kigiriki Herufi zinazounda alama: Chi (Χ) na Rho (Ρ) Neno linalowakilishwa: ΧΡΙΣΤΟΣ (Christos) Maana yake: Kristo, Mpakwa Mafuta Historia muhimu: Ilipata umaarufu mkubwa katika karne ya nne, hasa wakati wa Konstantino Mkuu. Maana ya kiimani: Utambulisho wa Kristo na ushindi wake. Chi-Rho inatukumbusha kwamba Kristo ndiye kiini cha maisha ya Kanisa. Kwa padre, ni ukumbusho kwamba huduma yake inapaswa kumwelekeza mwanadamu kwa Kristo, si kujitafutia utukufu wake mwenyewe. Tumsifu Yesu Kristu!
4
42
1,674
🌍 DOMINIKA YA MISIONI| 18 OKTOBA 2026 Leo Kanisa Katoliki linaadhimisha Dominika ya Misioni Duniani, ambayo mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1926, chini ya Papa Pius XI. Kaulimbiu ya mwaka huu, iliyochaguliwa na Papa Leo XIV ni: "One in Christ, United in Mission" — "Umoja katika Kristo, tumeungana katika utume." Upekee wa maadhimisho haya ni kutukumbusha kwamba uinjilishaji si jukumu la mapadre, watawa na wamisionari pekee. Kila Mkristo, kwa njia ya Ubatizo, anaitwa kuwa shahidi wa Kristo na kushiriki katika kueneza Injili. Unaweza kuwa mmisionari kwa sala zako, sadaka zako, matendo yako ya huruma/upendo na ushuhuda wa maisha yako. Huhitaji kwenda nchi za mbali ili kumtangaza Kristo; unaweza kuanza nyumbani, kazini, shuleni na katika jamii yako. Leo tuwaombee wamisionari wote wanaotangaza Injili katika mazingira mbalimbali, na kwa ukarimu tuunge mkono kazi ya Kanisa ya kuwafikishia watu wote Habari Njema ya wokovu. "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe." (Mk 16:15) Miaka 100 ya utume: Umoja katika Kristo, tumeungana katika kueneza Injili! 🌍✝️ Herini sana kwa Dominika ya Misioni.
1
19
475
"Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, utege sikio lako ulisikie neno langu." (Zab. 17:6)
5
68
1,027
Kama uko kwenye ndoa, sali bila kuacha, lakini kumbuka kwamba sala haiondoi wajibu wa kuchukua hatua zinazofaa. Kusamehe si sawa na kuhalalisha makosa, na kupigania ndoa hakumaanishi kuvumilia kila aina ya madhara bila mipaka. Lengo si kushinda mabishano dhidi ya mke/mume wako, bali kutafuta ukweli, kurejesha heshima na kuona kama nyote wawili mko tayari kuijenga upya ndoa yenu.
9
19
650
MFUMO WA ALAMA ZA KIKRISTO: TUNAZIELEWA KWELI? Umewahi kujiuliza maana ya alama kama ☧, IHS, ΑΩ au INRI unazoziona kwenye mavazi ya mapadre, Altare, Misalaba na Makanisa ya Katoliki? Tutaanza mfululizo wa kujifunza alama moja baada ya nyingine: asili yake, historia, maana yake ya kibiblia na umuhimu wake katika imani na liturujia ya Kanisa. Lengo si kuzitambua tu, bali kuelewa ujumbe wa Kristo unaowasilishwa kupitia alama hizo. Tumsifu Yesu Kristo.
5
9
75
3,091