Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1) profile picture
Dar es Salaam, Tanzania
Joined January 2023
Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)Photo by Sixbert Mmanda (@SixbertMmanda1)
PUMZIKA KWA AMANI, BINTI. Kwa masikitiko makubwa na huzuni isiyoelezeka, tunakuaga wewe uliyeondoka duniani kabla ya wakati wako. Uhai wako umekatishwa kikatili na watu wazima waliopoteza utu, huruma na thamani ya uhai wa binadamu. Inasikitisha zaidi kusikia kwamba, licha ya vifo na maumivu ya wahanga, bado kuna wanaokimbilia kuendeleza kile wanachokiita MARIDHIANO, kana kwamba wamesahau kwamba UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIO MSINGI WA MARIDHIANO YA KWELI NA YA KUDUMU. Binti, kifo chako hakitakuwa sababu ya sisi kunyamaza. Tutaendelea kudai na kupigania haki yako na haki ya wahanga wengine wote. Hatutakubali damu iliyomwagika, maisha yaliyopotea na machozi ya familia zilizofikwa na majonzi vifunikwe kwa pazia la maridhiano yasiyo na ukweli, haki wala uwajibikaji. MARIDHIANO SIYO KICHaka CHA KUJIFICHA KUKWEPA UWAJIBIKAJI. Hatuwezi kujenga amani ya kweli kwa kusahau waliopoteza maisha yao wala kwa kuwanyima wahanga haki wanayostahili. Pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu mzito. Hakuna maneno yanayoweza kufuta maumivu yenu. Tunawaombea nguvu, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. PUMZIKA KWA AMANI, BINTI. HAKI YAKO TUTAENDELEA KUIDAI. KUMBUKUMBU YAKO HAITAFUTIKA. ××××××××××××××××××××× REST IN ETERNAL PEACE, DEAR DAUGHTER. With profound sorrow and indescribable grief, we mourn your untimely departure from this world. Your life was cruelly cut short by adults who appear to have lost their humanity, compassion and respect for the sanctity of human life. What makes this tragedy even more heartbreaking is hearing that, despite the deaths, suffering and anguish of victims and their families, some are still determined to proceed with what they call RECONCILIATION, as though they have forgotten that TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY ARE THE VERY FOUNDATION OF GENUINE AND LASTING RECONCILIATION. Our beloved daughter, your death will not silence our voices. We shall continue to demand and fight for justice for you and all other victims. We shall not allow the blood that has been shed, the lives that have been lost and the tears of grieving families to be buried beneath a false veil of reconciliation that has neither truth, justice nor accountability. RECONCILIATION MUST NEVER BECOME A SANCTUARY FOR THOSE SEEKING TO EVADE ACCOUNTABILITY. There can be no genuine and lasting peace built upon forgotten lives, suppressed truths and denied justice. My deepest condolences go to your family, relatives, loved ones and everyone affected by this heartbreaking loss. REST IN ETERNAL PEACE. WE SHALL CONTINUE TO DEMAND JUSTICE FOR YOU. YOUR MEMORY SHALL NEVER BE ERASED. BAK MWABUKUSI
43
315
2
1,249
18,493
Sixbert Mmanda retweeted
SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.
5
80
1,017
Sixbert Mmanda retweeted
Wazazi wangu ni baraka kubwa sana!! Kuna muda wanahakikisha ndoto zangu zinatimia kupitia wao! Asanteni kwa kila jambo wazazi wangu, na sasa rasmi leo tunaondoka kwenye nyumba za kupanga. NI MUNGU NA WAZAZI!❤️🔥🙏🏽✅
2025, I will never forget you❤️ By Gods Grace........... 2026 in coming House 2/2
28
35
8
291
26,922
Sixbert Mmanda retweeted
Ee Mungu tuma malaika wako 😭😭🤲
5
83
537
16,369
Sixbert Mmanda retweeted
ROZARI TAKATIFU, MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi) 1. Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu. 2. Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani. 3. Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara. 4. Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo. 5. Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
8
50
716
Sixbert Mmanda retweeted
ROZARI TAKATIFU - MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa) 1. Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi. 2. Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu. 3. Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi. 4. Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu. 5. Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
13
54
897
Sixbert Mmanda retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 496 Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la! Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa. Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live. Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali. Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali. Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini. Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa. Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini. Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa. Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
167
634
28
1,737
149,108
Sixbert Mmanda retweeted
FREE TUNDU LISU
2
21
1
80
1,427
Sixbert Mmanda retweeted
Leo watu wana wasiwasi mkubwa kwani kuna mtu anasimama mbele ya mahakama kuhukumiwa. Lakini nyuma ya jina lake kuna binadamu, kuna familia, kuna mama, kuna ndugu, kuna marafiki na kuna watu ambao mioyo yao haitakuwa na amani mpaka watakapojua hatima ya siku hiyo. Kuna jambo moja ambalo tunapaswa kulikumbuka sote: kabla hatujawa wafuasi wa itikadi yoyote, sisi ni binadamu. Kabla hatujawa na tofauti za kisiasa, tulikuwa na utu mmoja. Na kabla hatujatofautiana kwa misimamo, tulikuwa na wajibu mmoja wa kuheshimiana. Huenda tukatofautiana kuhusu Tundu Lissu, tukatofautiana kuhusu siasa zake, kauli zake na misimamo yake. Lakini tusiruhusu tofauti hizo zitufanye tusahau kwamba hata mtu tunayepingana naye kisiasa anastahili haki, heshima na kutendewa kwa utu. Leo, tusitamani mtu ashindwe kwa sababu hatumpendi. Tusitamani mtu aumizwe kwa sababu hatuungi mkono mawazo yake. Tusifurahie machozi ya familia ya mwingine kwa sababu tu hatuko upande wake. Kuna ushindi unaoweza kuipatia nafsi furaha ya muda mfupi, lakini ukaacha taifa na jeraha la muda mrefu. Tanzania tunayoiota haitajengwa kwa kushangilia maumivu ya wengine, bali kwa kujifunza kuutambua utu hata pale tunapotofautiana. Mungu awape hekima watakaohusika, faraja wenye hofu, nguvu wenye maumivu na amani Watanzania wote. Tusisubiri siku ambayo tutakuwa tumempoteza mtu ndipo tujifunze thamani ya utu wake. Sote ni binadamu. Na hakuna itikadi inayopaswa kuwa kubwa kuliko ubinadamu wetu.
3
47
1
197
6,930
Sixbert Mmanda retweeted
Happy All Saints day. Herini kwa Sherehe ya Watakatifu wote.
1
6
46
717
Sixbert Mmanda retweeted
SALA YA KUTUBU. Mungu wangu, nimetubu sana, niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi, Amina.
4
9
50
837
Dainess mdogo wangu walikupiga risasi tabata na mwili wako haukuonekana tukafanya ibada ya picha kanisani 😞 baadae mwili ukapatikana kitunda ukiwa umeharibika sana na kubadilika Ni mwaka sasa tunakukumbuka sana ni ngumu kusamehe na kusahau 🙏🏻
75
448
12
1,568
25,647
Sixbert Mmanda retweeted
RAHA YA MILELE UWAPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UWANGAZIE ROHO ZA MAREHEMU WOTE WAPUMZIKE KWA AMANI 🕊️🕊️ – at Dar es Salaam, Tanzania
16
176
553
6,357
Sixbert Mmanda retweeted
TAARIFA KWA UMMA
2
46
169
2,737
Sixbert Mmanda retweeted
FREE TWAHA MWAIPAYA 🚨 I am reading reports saying Tanzanian activist Mwaipaya was abducted in Nairobi, Kenya, on October 25, 2026. We demand immediate confirmation of his whereabouts, his safety, and his unconditional release. On my way to church this Sunday, I read yet another alarming report of an activist being abducted. Have those in power lost their minds? Every day, someone is reportedly targeted for their political views or for speaking out. I have listened to Twaha speak. His voice reflects concern for his people and the future of his country. SPEAKING OUT IS NOT A CRIME. As Tanzania approaches the painful anniversary of October 29, families are still searching for loved ones, grieving, and demanding answers. Yet the fear continues. Yet enforced disappearances continue. ENOUGH IS ENOUGH! No ONE has the right to treat human beings as if their lives have no value. Human dignity, freedom, and justice are not privileges. 🇹🇿 TANZANIA, STOP CROSS-BORDER REPRESSION! KENYA, PROTECT HIS RIGHTS! We demand urgent action from the Kenyan and Tanzanian authorities. Confirm Twaha’s whereabouts. Ensure his safety. Hold those responsible accountable. We appeal to the United States, the European Union, the European Parliament, the Commonwealth, the United Nations, the African Union, international human rights bodies, and the global media: Please do not look away. These keep happening- ENOUGH IS ENOUGH! FREE TWAHA MWAIPAYA NOW! Free @Twaha_Mwaipaya #FreeTwahaMwaipaya #EndAbductionsEA #EndTransnationalRepression #FreeAllPoliticalPrisoners @UNHumanRights @UN_SPExperts @Europarl_EN @EU_Commission @eu_eeas @kajakallas @EUCouncil @ECHR_CEDH @commonwealthsec @CommonwealthFdn @AfricanUnion @achpr_cadhp @amnesty @hrw @CPJAfrica @CIVICUSalliance @FrontLineHRD @fidh_en @article19org @ISHRglobal @OMCT_ @StateDept @SecRubio @DefendDefenders @Reuters @AP @BBCWorld @AJEnglish @CNN @dwnews @France24_en @VOANews @nytimes @AlJazeera @onefreepress @StateDeptSpox @usembassytz #FreeTwahaMwaipaya #EndAbductionsEA #PASNet #FreeAllPoliticalPrisoners #HumanRights #Kenya #Tanzania #EndTransnationalRepression
9
227
2
542
4,550
Sixbert Mmanda retweeted
SALA YA ASUBUHI +Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni. Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. KANUNI YA IMANI. Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina. AMRI ZA MUNGU. 1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine. 2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. 3. Shika kitakatifu siku ya Mungu. 4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani. 5. Usiue. 6. Usizini. 7. Usiibe. 8. Usiseme uongo. 9. Usitamani mwanamke asiye mke wako. 10. Usitamani mali ya mtu mwingine. AMRI ZA KANISA. 1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa. 2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu. 3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka. 4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka. 5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka. 6. Shika sheria katoliki za ndoa. Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina. MALAIKA WA BWANA •Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. •Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. •Neno wa Mungu akatwaa mwili, akakaa kwetu. ~Salamu Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu Amina. SALA KWA MALAIKA MLINZI Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina. Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani. +Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
5
6
76
1,142
Sixbert Mmanda retweeted
ROZARI TAKATIFU, MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi) 1. Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu. 2. Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani. 3. Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara. 4. Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo. 5. Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
11
46
827
Leo nilikuwa Kijiji cha Makiungu, Ikungi. Mwenyekiti wa Wilaya katika hotuba yake alizungumzia watu ambao wametekwa na kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hawajulikani walipo. Nafikiri tatizo kubwa la jamii yetu si mateso na uhuni pekee tunayopitia, bali ni jinsi tulivyojifunza kuishi navyo kana kwamba ni sehemu ya kawaida ya maisha. Tumefika mahali ambapo ukatili hautushangazi tena, dhuluma haitunyimi usingizi, na mambo ambayo yalipaswa kututikisa kama jamii yanapita mbele yetu kama habari za kawaida. The most dangerous stage of social decay is not when evil happens, but when society loses the ability to be shocked by it. Jamii inapofikia hatua ya kuzoea maumivu ya wengine, inakuwa imeanza kupoteza utu wake. Na pale tunapozoea uovu, ukimya wetu huanza kuupa uovu uhalali. Tatizo si kwamba hatuoni kinachoendelea. Tatizo ni kwamba tumeanza kukiona bila kuhisi wajibu wa kufanya chochote. Mateso yanapokuwa kawaida, haki huonekana kama ombi, na uovu unapokuwa utamaduni, utu hugeuka kuwa jambo la hiari.
5
53
1
294
14,512
KIMENUKAAAAAAAAA, naomba mniruhusu nilale, nikiamka na drop watoto shule then drop 💣 . Video itakuwa hewani saa 1 usiku ya Tanzania. Yani saa 1 usiku fanyeni ku refresh page….. ISHU NI DIPU!!!!!
105
292
8
2,414
135,013
Thamani yake ni sawa na gharama ya kununua Apartment Kariakoo au kununua nyumba Sinza Tsh 200,000,000/= Mabwege au vipera maziwa wanaopaka lotion za Tsh 10,000/= hawawezi kuvaa hii 💯 Kama una hela 📌 Tuwasiliane Kwa WhatsApp ☎️ +255719068333 Mudi in Dubai 🇦🇪
5
27
2
48
3,254