Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga) header
Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga) profile picture

Medical doctor (MD)❣💉🏥|SJUIT-ALUMNI||#GetVaccinated|ProtectOthers. #YourLifeIsWealth|#YourHealthMatters. #SimbaSCTanzania|#ManUtd|#RealMadrid Democracy

Dar es Salaam, Tanzania
Joined April 2021
Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)Photo by Dr. Fadhili (MD) (@JrFadiga)
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Tanzania Vision 2050: The Healthcare We Want.
1
53
6
35
2,454
Dr. Fadhili (MD) retweeted
“KATI YA RISASI NA MIUJIZA: Simulizi ya Profesa Dr Mpoki na Kupona kwa Tundu Lissu" Na Emily Mwakilembe Kwa Tundu Lissu, Prof. Mpoki Ulisubisya ni kama Musa aliyeshuhudia mkono wa Mungu ukiwakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri. Naam!👇
18
153
3
631
56,516
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kama alivyoshuhudia Bahari ya Shamu ikipasuka mara mbili na njia ikafunguka katikati ya maji. Ni kama Yoshua alivyoyaona kwa macho yake kuta za Yeriko zikianguka kwa sauti ya tarumbeta. Ni kama Eliya alivyoshuhudia mtoto wa mjane wa Sarepta akirejea katika pumzi ya uhai.
1
8
83
8,450
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Ni kama Yohana alivyolikuta kaburi tupu, ushuhuda wa muujiza ulio hai. Sikiliza, nikupe kwanza historia ya daktari huyu ni nani hasa?.
1
8
75
8,208
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Tanzania tulibahatika kupata mmoja wa madaktari bingwa wa kwanza wazawa waliobobea katika taaluma ya Anesthesiolojia tiba ya usingizi na uangalizi wa wagonjwa mahututi. Si mwingine bali ni Dkt. na Profesa Mpoki Ulisubisya, gwiji, kipaji adimu, kutoka Rungwe, Tukuyu, Mbeya
1
11
99
6,816
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Rais wa TLS, Adv. Boniface Mwabukusi, huiita ardhi ile ya kinabii. Wapo watakaodhani ni kwa sababu ilimtoa daktari wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere Dkt. David Mwakyusa, bingwa wa magonjwa ya figo (Nephrologist) La hasha! Leo ninazungumzia jabali lingine Prof. Mpoki Ulisubisya
1
10
75
5,914
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Mwanaume huyu ameshiba vitabu, aliyekunywa elimu mpaka ikamvika joho la Uprofesa; daktari bingwa wa usingizi na tiba za wagonjwa walio katika hali hatarishi. Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI).
2
11
1
81
5,986
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Pia Dk. Mpoki alikuwa mhadhiri wa chuo cha tiba Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), akifundisha kizazi cha madaktari chipukizi. Si hilo tu aliwahi pia kulitumikia taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Cuba.
1
11
80
5,505
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Huyu si mtu wa kawaida; ni hazina ya akili, nidhamu na hofu ya Mungu. Akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati ule wa tukio zito la kushambuliwa kwa risasi kwa Tundu Lissu, Mpoki alisimama imara kuongoza kikosi cha madaktari kama nahodha wa jahazi lililokumbwa na dhoruba kali
2
14
87
5,609
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Aliongoza mapambano ya sekunde kwa sekunde kuhakikisha kuwa Lissu anabaki hai. Kwa umakini, utaalamu na utulivu wa hali ya juu, alihakikisha anapatiwa huduma ya kwanza kwa weledi wa kiwango cha kimataifa na hatimaye kuhamishiwa salama katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.
1
14
101
5,709
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kulizuka tetesi kwamba punde tu baada ya kufanikisha operesheni hiyo ya uhai, aliondolewa katika nafasi yake. Hili libaki kuwa tetesi; historia italihukumu. Lakini ukweli ni kwamba mabadiliko yalionekana wazi mbele ya macho ya umma.
1
9
89
5,431
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Miaka saba na miezi sita baadaye, Profesa Mpoki alipokutana tena uso kwa uso na Tundu Lissu katika msiba wa Prof. Philemon Mikol Sarungi machozi yalimtoka. Si machozi ya udhaifu, bali ya mshangao mtakatifu.
2
18
122
5,745
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kwa uzoefu wake wa kitabibu na umri wake katika taaluma, hakuwahi kushuhudia mwili uliosambaratishwa kwa risasi nyingi kiasi kile ukirejea katika hali ya kusimama, kuzungumza na kutembea tena.
1
16
109
5,286
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Ilikuwa kama kuiona historia ikiandika ukurasa wa muujiza mbele ya macho yake mwenyewe. Leo hii, kama angeulizwa kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili Lissu, huenda angesema: “Futeni kesi hiyo.” Kwa sababu kwa macho yake ya kitabibu, alishuhudia kile ambacho si cha kawaida.
1
12
103
5,222
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Aliona roho isiyokubali kuzimwa. Aliona mwili uliokataa kushindwa. Aliona maono yanayolindwa na mkono usioonekana. Tundu Lissu si kiumbe wa kawaida. Kila jaribio la kumzima limegeuka kuwa moto unaowachoma wanaouasha. Kila risasi ilimpa sauti kubwa zaidi.
1
23
151
5,561
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kila dhoruba ilimpa mabawa mapana zaidi. Yeye ni mbeba maono; ni alama hai ya mapambano yasiyokubali kunyamazishwa. Na Profesa Mpoki shahidi wa kwanza wa mapambano yale ya uhai anabaki kuwa Musa aliyeliona bahari likipasuka.
1
11
90
5,101
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Daktari aliyeshika mkono wa historia, akasimama katikati ya kifo na uhai, akachagua uhai ushinde. Huu si hadithi ya mtu mmoja. Ni simulizi ya taifa. Ni kumbukumbu ya siku ambayo sayansi, imani na ujasiri vilikutana katika chumba cha upasuaji na uhai ukashinda.
1
14
110
10,937
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Profesa Mpoki, shahidi wa meza ya upasuaji, anabaki na simulizi moyoni simulizi ya mtu aliyepaswa kuondoka, lakini akaamua kubaki. Tutafakari sote unaweza Ku-share
6
41
188
10,295
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Ni mategemeo ya kila mgonjwa anayefika hospitali kupata huduma, huduma iwe salama, bora, na yenye kuzingatia taaluma. Hata hivyo, katika baadhi ya mazingira, mgonjwa anaweza kupata madhara kutokana na uzembe wa kitabibu (medical negligence au medical malpractice). Ni muhimu kufahamu kuwa kuna sheria zinazomlinda mgonjwa, na kuna mifumo rasmi ya kitaaluma ya kushughulikia malalamiko hayo. 1. Sheria ya Makosa ya Madai (Law of Tort) - Hii ndiyo sheria kuu inayotumika pale mgonjwa anapopata madhara kutokana na uzembe wa daktari au mtoa huduma za afya. Ili kuthibitisha uwajibikaji wa daktari au hospitali, vipengele vitatu muhimu lazima vithibitishwe: i. Wajibu wa Huduma (Duty of Care) - Daktari ana wajibu wa kutoa huduma za matibabu kwa umakini, uangalifu, na kwa kufuata viwango vya kitaaluma vinavyokubalika. ii. Uvunjifu wa Wajibu (Breach of Duty) - Hii hutokea pale daktari anaposhindwa kufuata viwango vya taaluma yake, kwa mfano: - Kutoa dawa isiyo sahihi - Kufanya upasuaji bila kufuata taratibu - Kusahau kifaa cha upasuaji tumboni mwa mgonjwa - Kushindwa kufanya uchunguzi unaotakiwa kabla ya matibabu iii. Madhara (Causation/Damage) - Ni lazima ithibitike kuwa kosa la daktari ndilo lililosababisha moja kwa moja madhara aliyoyapata mgonjwa, kama vile maumivu makali, ulemavu, au gharama za ziada za matibabu. 2. Baraza la Madaktari (Medical Council of Tanganyika – MCT) - Chini ya Medical Practitioners and Dentists Act, Tanzania ina Baraza la Madaktari linalosimamia maadili, nidhamu, na viwango vya taaluma ya udaktari. Wewe kama mgonjwa, una haki ya: - Kuwasilisha malalamiko rasmi dhidi ya daktari - Kuomba uchunguzi wa kitabibu au kimaadili Endapo uzembe au ukiukwaji wa maadili utathibitika, Baraza linaweza: - Kumsimamisha daktari kazi - Kumfuta daktari na kuchukua leseni yake - Kutoa onyo kali au adhabu nyingine za kinidhamu Hatua hizi zinalenga kulinda wagonjwa na kulinda heshima ya taaluma ya udaktari. 3. Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) - Iwapo uzembe wa daktari ni mkubwa kupita kiasi (gross negligence) na: i. Umesababisha kifo cha mgonjwa, au ii. Umesababisha ulemavu wa kudumu Daktari anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai, na adhabu inaweza kujumuisha: i. Faini ii. Kifungo cha gerezani Hii hutumika pale ambapo uzembe unaonekana kuwa wa wazi, wa hatari, na wa kupuuza maisha ya mgonjwa. 4. Sheria ya Afya ya Jamii (Public Health Act) - Sheria hii inaweka masharti na viwango vya Utoaji wa huduma za afya, Usalama wa wagonjwa an Uwajibikaji wa hospitali na vituo vya huduma za afya. Hospitali au kituo cha huduma za afya kinachokiuka viwango hivi kinaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Hatua za Kuchukua Kama Mgonjwa Umepata Madhara Ikiwa mgonjwa au ndugu amepata madhara, hatua zifuatazo zinaweza kuchukuliwa: - Fungua Malalamiko Hospitalini - Anza kwa kutoa taarifa kwa Medical Officer In Charge (MOI) au uongozi wa hospitali husika. - Ripoti kwa Baraza la Madaktari (MCT) - Kwa ajili ya hatua za kinidhamu dhidi ya daktari aliyehusika. - Wasiliana na Mwanasheria, kama lengo ni kudai Fidia ya gharama za matibabu, Fidia ya maumivu na mateso (pain and suffering) au Fidia ya kupoteza uwezo wa kufanya kazi. 4. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - Mgonjwa anaweza pia kuwasilisha malalamiko kwa Tume hii ikiwa haki yake ya kupata huduma bora za afya imekiukwa. Jambo Muhimu la Kuzingatia Ushahidi ni nguzo muhimu katika kushughulikia madai ya uzembe wa kitabibu. Hakikisha unahifadhi: - Nyaraka zote za matibabu (medical records) - Risiti na stakabadhi za malipo - Ushahidi wa daktari mwingine anayethibitisha uwepo wa madhara hayo (second opinion) - Nyaraka au vielelezo vinavyothibitisha madhara Mgonjwa ana haki ya msingi ya kupata huduma salama, bora, na yenye heshima. Uzembe wa kitabibu sio jambo la kupuuzwa. Sheria, taasisi, na taratibu zipo ili kulinda maisha na haki za wagonjwa. Kadri jamii inavyoelimika kuhusu haki zake, ndivyo uwajibikaji na ubora wa huduma za afya unavyoimarika. Mshirikishe rafiki unayehisi anatakiwa kujua hili.
2
11
1
24
2,552