
Medical doctor (MD)❣💉🏥|SJUIT-ALUMNI||#GetVaccinated|ProtectOthers. #YourLifeIsWealth|#YourHealthMatters. #SimbaSCTanzania|#ManUtd|#RealMadrid Democracy
Dar es Salaam, Tanzania
Joined April 2021
- Tweets9.8K
- Following808
- Followers483
- Likes9.2K
Don't ask about my income/salary, ask me how many nights I've stayed awake, how many meals I've skipped, and how many moments with my beloved family I've missed. #LifeOfMedicine 🙏🙏
36
Behind every recovery is a team that refused to quit, but serving with heart. Honoring the hands, eyes and the hearts that never give up🙏🙏.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
“KATI YA RISASI NA MIUJIZA: Simulizi ya Profesa Dr Mpoki na Kupona kwa Tundu Lissu"
Na Emily Mwakilembe
Kwa Tundu Lissu, Prof. Mpoki Ulisubisya ni kama Musa aliyeshuhudia mkono wa Mungu ukiwakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri.
Naam!👇
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kama alivyoshuhudia Bahari ya Shamu ikipasuka mara mbili na njia ikafunguka katikati ya maji.
Ni kama Yoshua alivyoyaona kwa macho yake kuta za Yeriko zikianguka kwa sauti ya tarumbeta.
Ni kama Eliya alivyoshuhudia mtoto wa mjane wa Sarepta akirejea katika pumzi ya uhai.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Ni kama Yohana alivyolikuta kaburi tupu, ushuhuda wa muujiza ulio hai.
Sikiliza, nikupe kwanza historia ya daktari huyu ni nani hasa?.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Tanzania tulibahatika kupata mmoja wa madaktari bingwa wa kwanza wazawa waliobobea katika taaluma ya Anesthesiolojia tiba ya usingizi na uangalizi wa wagonjwa mahututi.
Si mwingine bali ni Dkt. na Profesa Mpoki Ulisubisya, gwiji, kipaji adimu, kutoka Rungwe, Tukuyu, Mbeya
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Rais wa TLS, Adv. Boniface Mwabukusi, huiita ardhi ile ya kinabii.
Wapo watakaodhani ni kwa sababu ilimtoa daktari wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere Dkt. David Mwakyusa, bingwa wa magonjwa ya figo (Nephrologist)
La hasha! Leo ninazungumzia jabali lingine Prof. Mpoki Ulisubisya
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Mwanaume huyu ameshiba vitabu, aliyekunywa elimu mpaka ikamvika joho la Uprofesa; daktari bingwa wa usingizi na tiba za wagonjwa walio katika hali hatarishi.
Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI).
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Pia Dk. Mpoki alikuwa mhadhiri wa chuo cha tiba Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), akifundisha kizazi cha madaktari chipukizi.
Si hilo tu aliwahi pia kulitumikia taifa kama Balozi wa Tanzania nchini Cuba.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Huyu si mtu wa kawaida; ni hazina ya akili, nidhamu na hofu ya Mungu.
Akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati ule wa tukio zito la kushambuliwa kwa risasi kwa Tundu Lissu, Mpoki alisimama imara kuongoza kikosi cha madaktari kama nahodha wa jahazi lililokumbwa na dhoruba kali
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Aliongoza mapambano ya sekunde kwa sekunde kuhakikisha kuwa Lissu anabaki hai.
Kwa umakini, utaalamu na utulivu wa hali ya juu, alihakikisha anapatiwa huduma ya kwanza kwa weledi wa kiwango cha kimataifa na hatimaye kuhamishiwa salama katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kulizuka tetesi kwamba punde tu baada ya kufanikisha operesheni hiyo ya uhai, aliondolewa katika nafasi yake.
Hili libaki kuwa tetesi; historia italihukumu.
Lakini ukweli ni kwamba mabadiliko yalionekana wazi mbele ya macho ya umma.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Miaka saba na miezi sita baadaye, Profesa Mpoki alipokutana tena uso kwa uso na Tundu Lissu katika msiba wa Prof. Philemon Mikol Sarungi machozi yalimtoka.
Si machozi ya udhaifu, bali ya mshangao mtakatifu.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Kwa uzoefu wake wa kitabibu na umri wake katika taaluma, hakuwahi kushuhudia mwili uliosambaratishwa kwa risasi nyingi kiasi kile ukirejea katika hali ya kusimama, kuzungumza na kutembea tena.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Ilikuwa kama kuiona historia ikiandika ukurasa wa muujiza mbele ya macho yake mwenyewe.
Leo hii, kama angeulizwa kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili Lissu, huenda angesema: “Futeni kesi hiyo.” Kwa sababu kwa macho yake ya kitabibu, alishuhudia kile ambacho si cha kawaida.
Dr. Fadhili (MD) retweeted
Aliona roho isiyokubali kuzimwa.
Aliona mwili uliokataa kushindwa.
Aliona maono yanayolindwa na mkono usioonekana.
Tundu Lissu si kiumbe wa kawaida.
Kila jaribio la kumzima limegeuka kuwa moto unaowachoma wanaouasha.
Kila risasi ilimpa sauti kubwa zaidi.




















