
ALT wa udhibiti na usimamizi wa taka za plastiki nchini, kilichofanyika Dodoma Januari 30,2025. Amesema inakadiriwa kuwa nchi yetu inazalisha taka ngumu kati ya tani milioni 14.4 hadi 20.7 kwa mwaka sawa na wastani wa Kilogram 241 – 347 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Aidha, maeneo ya mijini yanakadiriwa kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi wa taka ikilinganishwa na maeneo ya vijijini. “Takwimu za maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa taka ngumu nchini zinaonesha wastani wa mabaki ya bustani, mbao, na vyakula ni 63.4%; mchanganyiko wa taka za kielektroniki, vifaa vya nyumbani, majivu, na taka zisizo na kemikali ni 12.8%; taka za plastiki ni 12%; taka za karatasi ni 6.1%; taka za vioo ni 4.2%; na taka za metali ni 1.5%. Bw. Mitawi ameongeza asilimia 70 ya taka ngumu zinazozalishwa nchini zinaweza kurejelezwa. Hata hivyo, ni asilimia 5-10 pekee ya taka hizi hurejelezwa ambapo kiwango kikubwa cha urejelezaji kinatokana na taka za plastiki, karatasi, chuma chakavu, aluminium, glasi, taka za kielektroniki,

ALT Hata hivyo, amesema ushirikiano huu unalenga kukusanya na kurejeleza tani milioni 12.5 za taka za plastiki nchini kote kwa mwaka. Kiwango kikubwa cha taka zinazozalishwa hutupwa ovyo, ispokuwa katika Halmashauri saba zenye madampo ya kisasa. Kwa upande Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa amesema katika kukabiliana na udhibiti wa taka hususani taka za plastiki, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imechukua hatua mbalimbali katika kuimarisha usimamizi wa taka nchini ikiwemo Kutunga na kufanya marekebisho ya Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati na Miongozo mbalimbali. “Vile vile, Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vipindi vya redio, television, warsha na mikutano mbalimbali. Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa mradi wa mfano wa urejelezaji wa taka za plastiki uliopo Jijiji la Dodoma, Kata ya Chamwino ambao upo katika hatua za majaribio.

ALT Naye Mkurugenzi wa HUDEFO Bi. Sarah Pima amesema wamekuwa wakishirikiana na serikali katika kuhamasisha Uhifadhi wa Mazingira hasa katika mikoa ambayo imekuwa ikizalisha taka za plastiki kama vile Dar es Salaam. Ameongeza pia wamekuwa wakitoa elimu kwa makundi mbalimbali kama vile waandishi wa Habari ambao kupitia vyombo vya Habari elimu imekuwa ikiwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.

































