Updates from the United Republic of Tanzania #URTUpdates

Dar es Salaam, Tanzania
Joined September 2023
URT Updates retweeted
visitngorongoro
@visitngorongoroOct 18
4
3
109
URT Updates retweeted
visitngorongoro
@visitngorongoroOct 6
WAANDISHI WA KIMATAIFA WAKOSHWA NA UZURI WA NGORONGORO Waandishi nguli wa habari za michezo na burudani kutoka sehemu mbalimbali duniani, walioko nchini Tanzania kwa ziara ya kiutalii na kufuatilia maandalizi ya AFCON 2027, Oktoba 5, 2026 wamefika katika Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia utajiri wa vivutio vya utalii nchini. Katika ziara hiyo, waandishi hao wamejionea wanyamapori mbalimbali wakiwemo simba, faru, twiga na wengine, huku wakipata fursa ya kutembelea pia Makumbusho ya Binadamu wa Kale na kujifunza historia ya mwanadamu. Waandishi hao wamesema ziara hiyo imewapa picha halisi ya Tanzania, wakisisitiza kuwa wageni watakaokuja nchini kwa ajili ya AFCON 2027 hawatapata fursa ya kufurahia mpira pekee, bali pia watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali na kujionea uzuri, historia na utamaduni wa Tanzania. “Hii ndiyo Tanzania! Ukija kwa AFCON 2027, hutafurahia mpira tu - utapata pia nafasi ya kugundua maajabu ya Tanzania kama Ngorongoro.”
4
8
350
The AI era must expand the ability of nations to shape their own future, not create new forms of technological dependency. That requires stronger cooperation to build the infrastructure, skills, research and governance capabilities that no country can secure alone. For Africa, the priority is to capture more of the value created by AI through harnessing our energy, resources, data and talent to build our own capabilities, enterprises and solutions. Kenya is pursuing this through our National Artificial Intelligence Strategy, with investments in digital infrastructure, data and AI governance, research, innovation and commercialisation to strengthen local capability, improve public services, raise productivity, and create new enterprises and jobs. Co-chaired the High-Level AI Middle Powers Coalition meeting with Finland’s President Alexander Stubb on the sidelines of the United Nations General Assembly in New York.
39
96
7
430
36,036
Leo, Septemba 22,2026 nimetoa taarifa kwa umma kuhusu tukio lililosababisha vifo na majeruhi katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ipole, mkoani Tabora, pamoja na vifo vya wanyamapori katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, mkoani Arusha. Tukio la Tabora lilitokea Septemba 18, 2026, katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Ipole, wilayani Sikonge, wakati watumishi wa uhifadhi walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kulinda maliasili na rasilimali za Taifa. Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu sita na wengine watano kujeruhiwa. Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo, mazingira na wahusika wa tukio hilo. Hadi sasa, watu 34 wanashikiliwa kwa ajili ya kusaidia uchunguzi. Kuhusu tukio la Ngorongoro, lililotokea pia Septemba 18, 2026, vifo vya simba 11 na fisi wawili vimethibitishwa. Uchunguzi wa awali umebaini kuwapo kwa majeraha katika mizoga ya baadhi ya wanyamapori hao. Uchunguzi wa kitaalamu unaendelea ili kubaini chanzo kamili cha vifo hivyo na kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria. Ninawahakikishia wananchi na wadau wote wa uhifadhi kuwa Serikali itaendelea kusimamia uchunguzi wa matukio haya kwa umakini, weledi na kwa kuzingatia sheria za nchi. Tutaendelea kuimarisha usalama na mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi wanaotekeleza majukumu ya kulinda maliasili na rasilimali za Taifa. Vilevile, tutaongeza juhudi za kuzuia migogoro na kujenga mahusiano endelevu kati ya mamlaka za uhifadhi na jamii zinazozunguka maeneo yaliyohifadhiwa. Serikali inatambua na kuthamini nafasi muhimu ya wananchi katika usimamizi endelevu wa maliasili. Kwa msingi huo, tutaendelea kuweka mkazo katika mawasiliano, ushirikishwaji wa jamii na utatuzi wa changamoto kwa njia za amani, mazungumzo na kwa mujibu wa sheria. Ninatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu, kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyoendesha uchunguzi na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa wakati taratibu rasmi za uchunguzi zikiendelea. @SuluhuSamia @mwigulunchemba1 @visitngorongoro @ccm_tanzania – at Dar es Salaam, Tanzania
1
1
66
URT Updates retweeted
visitngorongoro
@visitngorongoroAug 26
Sometimes, the closest you can get to nature is to simply walk with it. No traffic. No engine. No rush. Just the wild. Your footsteps, the whisper of nature, and the feeling of being completely present in Destination Ngorongoro. Walk slowly. Feel deeply. Experience the Wonders. #wondersarecalling #experiencethewonders #destinationngorongoro #visitngorongoro #karibunyumbani
1
3
1
4
184
URT Updates retweeted
Nimekuwa na wasaa mzuri wa kuzungumza na kushiriki burudani na michezo pamoja na wananchi mjini Zanzibar leo jioni, mara tu baada ya kuwasili kutokea Dodoma. Ahsanteni sana kwa mapokezi mazuri na kwa upendo wenu. Pamoja na mambo mengine, nikiwa Zanzibar nitaungana na wananchi katika Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival), jukwaa muhimu linaloendelea kuwakutanisha wananchi na wadau mbalimbali katika kuenzi utamaduni, michezo, sanaa na kuimarisha mshikamano wetu.
25
78
3
229
27,640
🙏🙏 to @UNhumansecurity Trust Fund, @JapanAmb_TZ, @MofaJapan_en , @Ndc_tz , #Tanzania #Peacekeeping Training Center, @UNmigration, @IOMTanzania for partnership to enhance peace, security & prosperity for the people of 🇹🇿. @mfa_tanzania @UNDPAfrica @UnitedNationsTZ @urtupdates – at Dar es Salaam, Tanzania
Stronger partnerships = safer communities. 🇹🇿 Great meeting with 🇯🇵ese embassy, TPTC, @IOMTanzania , & the Immigration Dept to advance our Human Security Programme. Together, we're building better systems & using tech to support 🇹🇿's border communities. #Tanzania #Peacebuilding
1
2
1
6
343
URT Updates retweeted
President of the Republic of Uganda, His Excellency Yoweri Kaguta Museveni has arrived in Dar es Salaam for a two-day official visit at the invitation of the President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan. During the visit, the two Heads of State will hold bilateral talks aimed at further strengthening the longstanding relations and cooperation between Tanzania and Uganda. Their discussions will focus on key areas of mutual interest, including trade and investment, infrastructure and transport, energy, tourism, defence and security, as well as regional integration @UbaloziUganda @UGHighCommDAR @UgandaMFA
5
16
3
48
47,413
URT Updates retweeted
Leo jijini Dar es Salaam nimeungana na viongozi wengine wa Afrika kufungua Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 na Jukwaa la Miundombinu Afrika, ambapo Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji. Jukwaa hilo, linaloadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, limekuwa sehemu muhimu ya kuunganisha mitaji, miradi na wataalamu ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani Afrika. Katika mkutano huo nimeeleza kuwa, Tanzania inashirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha miundombinu, ikiwemo barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege. Hatua hii inachochea ukuaji endelevu wa uchumi kwa kupunguza gharama za usafirishaji, kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kutoa ajira na kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha usafirishaji. Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kimazingira duniani, nimesisitiza umuhimu wa Afrika kuimarisha miundombinu inayohimili mabadiliko hayo na kuunganisha nchi zetu ili kuendelea kukuza biashara, uwekezaji na uongezaji thamani wa rasilimali zetu.
31
78
2
203
20,909
URT Updates retweeted
Mapema leo Ikulu, jijini Dar es Salaam nimekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa mawasiliano, mashauriano na ushirikiano katika masuala muhimu yanayolihusu Taifa letu. Mazungumzo haya ni fursa ya kubadilishana mawazo na mitazamo mbalimbali kwa maslahi mapana ya Taifa, huku tukiendelea kujenga msingi wa kuheshimiana, kuelewana na kushirikiana. Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa kisiasa katika kulinda amani, kudumisha umoja wa kitaifa na kusukuma mbele maendeleo yenye manufaa kwa Watanzania wote.
87
85
12
246
33,385
TAARIFA KWA UMMA
3
3
63
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa, Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma.   Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
3
13
1
66
3,719
URT Updates retweeted
Julai 25 kila mwaka ni Siku ya Mashujaa; siku adhimu ya kuwakumbuka na kuwaenzi wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani ya nchi yetu. Kwa ujasiri, uzalendo na kujitolea kwao, walituachia msingi imara wa uhuru, amani, umoja na mshikamano tunaouenzi hadi leo. Tunapowakumbuka mashujaa wetu, tuendelee kulinda tunu walizotuachia kwa kudumisha amani, umoja na kufanya kazi kwa bidii katika kujenga Tanzania yenye maendeleo na ustawi, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mungu Ibariki Tanzania.
65
83
30
212
25,167
URT Updates retweeted
1
3
8
814
URT Updates retweeted
MAKONDA: KISWAHILI HAS REMAINED A PILLAR OF NATIONAL UNITY AND IDENTITY FOR OVER SIX DECADES The Minister for Information, Culture, Arts, and Sports, Hon. Paul Makonda, has said that the Kiswahili language has continued to serve as a key foundation for building unity, solidarity, and national identity in Tanzania since 1962, acting as a unifying force among Tanzanians from diverse ethnic and cultural backgrounds. Speaking on 7th July 2026 World Kiswahili Language Day celebrations held in Paris, France, Hon. Makonda said the Government will continue working with various stakeholders within and outside the country to ensure that Kiswahili is further promoted, strengthened and gains greater recognition in international platforms. He said Kiswahili is not merely a means of communication but a national heritage and an important instrument for promoting peace, social cohesion, and mutual understanding, and for advancing socio-economic development in Tanzania and across the world. Hon. Makonda emphasized that Tanzania’s history demonstrates the vital role Kiswahili has played in building a united nation, noting that the language has been an essential link in strengthening relations among citizens while preserving Tanzanian culture, values, and traditions. He also commended Tanzanians living abroad (Diaspora) for their significant contribution to promoting, showcasing, and safeguarding the Kiswahili language and Tanzania’s cultural heritage in different parts of the world. He noted that the efforts of the Diaspora have played a major role in enhancing the global recognition and appreciation of Kiswahili, further strengthening Tanzania’s position as an important centre for the promotion, teaching, and development of the language worldwide.
1
9
25
1,083
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilishaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia yaMtandao, leo tarehe 29 Juni 2026, Makamu wa Rais akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.   Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.
3
12
2
53
3,920
URT Updates retweeted
RAIS DKT. MWINYI AISHUKURU INDIA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO, APOKEA MWALIKO RASMI WA KUTEMBELEA INDIA Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Serikali ya India kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Juni 2026, alipokutana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey, pamoja na ujumbe wake, waliofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo. Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza uwekezaji unaofanywa na wawekezaji na taasisi binafsi za India nchini na kueleza utayari wa Zanzibar kuimarisha ushirikiano na India katika elimu ya ufundi na mafunzo ya amali. Aidha, amesifu mchango wa Taasisi ya Teknolojia ya India Madras, IIT Madras Zanzibar, katika utoaji wa elimu na mafunzo ya kitaalamu, pamoja na kuleta mageuzi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. IIT Madras Zanzibar ni kampasi ya kwanza ya kimataifa ya taasisi hiyo nje ya India. Kwa upande wake, Balozi Bishwadip Dey amemkabidhi Rais Dkt. Mwinyi mwaliko rasmi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya India, Mhe. C. P. Radhakrishnan, wa kutembelea India mwezi Julai 2026. Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi pia anatarajiwa kutembelea makao makuu ya IIT Madras yaliyopo Chennai. Vilevile, Balozi Dey ameihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa India itaendelea kuimarisha ushirikiano na Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo kwa manufaa ya pande zote mbili. – at Tanzania
1
1
5
251
URT Updates retweeted
Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki. Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.
70
123
10
728
31,710
Leo, Juni 30, 2026, nimekutana na wataalamu wa Idara ya Wanyamapori pamoja na Wakuu wa Taasisi za Uhifadhi zilizo chini ya Wizara kujadili mikakati ya kuimarisha uhifadhi wa maliasili na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa Taifa. @TzTawa @tzparks – at Dar es Salaam, Tanzania
1
3
46
URT Updates retweeted
Kheri ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika. Kutimia kwa ndoto ya kila mtoto kunategemea maamuzi na hatua tunazochukua leo. Tunapojiandaa kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, tumeazimia kujenga Taifa ambalo kila mtoto anapata malezi na makuzi bora, analindwa na anajengewa msingi imara wa maisha yake. Huu si wajibu wa serikali pekee, bali ni wa kila mwananchi, kwani uhai, ulinzi, usalama na maendeleo ya Taifa letu vinategemea ustawi wa watoto wetu.
43
96
1
239
10,854