Nimefurahishwa kushuhudia majaribio ya teknolojia ya ndege nyuki (drones) kutoka Mati Technologies kampuni ya kizalendo ya Babati, Manyara.
Hii ni faida ya kuweka mazingira rafiki na wezeshe kwa wawekezaji wetu hasa wa ndani kunapoleta matokeo chanya na ubunifu zaidi.
Teknolojia hii itasaidia kilimo chetu kwa kunyunyiza dawa na mbolea kwa haraka na ufanisi mkubwa, na pia kutoa huduma nyingine nyingi za kijamii.
Hongera sana David Mulokozi na timu yako nzima ya Mati kwa hatua hii muhimu.
Karibuni Manyara kwa uwekezaji na maendeleo bora ya mkoa na nchi yetu!
Uwajibikaji rafiki wa maendeleo πΉπΏ
7
252
ZIARA MAALUM β LANGO LA KUINGILIA HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE (MAMIRE)
Leo tarehe 17 Septemba 2025, nikiwa na Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, nimetembelea na kukagua ujenzi wa lango jipya la kuingilia Hifadhi ya Taifa Tarangire kupitia barabara ya Mamire.
Mradi huu wa thamani ya Tsh Bilioni 3.9, unaotekelezwa na Elerai Construction Ltd.chini ya usimamizi wa TANAPA, umefikia hatua za mwisho za umaliziaji.
Lango hili litakuwa chachu kubwa ya kuimarisha utalii , kurahisisha safari za watalii kutoka Babati , Dodoma, Singida na mikoa jirani, na kukuza shughuli za kiuchumi zinazohusiana na utalii katika eneo letu.
Nimeagiza mkandarasi kuhakikisha mradi unakamilika na kukabidhiwa mwanzoni mwa Oktoba 2025 kama ilivyopangwa.
Wakazi wa Babati na maeneo jirani, nawahimiza kuchangamkia fursa hii wekezeni katika hoteli za kitalii, maduka makubwa, na huduma nyingine zinazosaidia sekta ya utalii.
Uwajibikaji rafiki wa maendeleo πΉπΏ
#Tarangire #UtaliiManyara #TANAPA #Babati #InvestInTourism
Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Dar es salaam Leo Agosti 28,2025.
ππππππππ
Leo Julai 24, 2025 nimeongoza hafla ya kukabidhi rasmi mkandarasi kutoka kampuni ya Wesons Engineers kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi mpya ya mabasi (Makatanini), barabara za lami kilomita 4.7 na mitaro ya kupitisha maji kilomita 8.15 katika mji wa Babati.
Mradi huu unagharimu Shilingi Bilioni 19.996 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 15. Nimeelekeza mkandarasi kuhakikisha ubora wa kazi na muda wa utekelezaji vinafuatwa kikamilifu, sambamba na kuwapa kipaumbele wananchi wa eneo hili kwa ajira za ujenzi.
Ujenzi wa stendi hii ni hatua muhimu katika kukuza uchumi wa Babati na Mkoa wa Manyara kwa ujumla.
Wana Manyara tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupatia fedha hizi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi wetu moja kwa moja.
Nawaomba wananchi waendelee kuitunza miradi hii na kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu.
Uwajibikaji rafiki wa maendeleo πΉπΏ
Queen Sendiga retweeted
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. @queen_sendiga, Julai 12, 2025 amepokea Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa @ccm_tanzania Mirerani, Wilayani Simanjiro, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi , Katika Mkoa wa Manyara, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika
Queen Sendiga retweeted
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. @queen_sendiga, Julai 12, 2025 amepokea Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa @ccm_tanzania Mirerani, Wilayani Simanjiro, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi , Katika Mkoa wa Manyara, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Mamlaka za Serikali za mitaa saba (7) ambazo ni Simanjiro, Kiteto, Babati Wilaya, Babati Mji, Mbulu Mji, Mbulu Wilaya na Hanangβ. Mwenge wa Uhuru utakimbizwa mkoani Manyara kwa mzunguko wa kilometa 1,197.10 na utatembelea miradi 51 yenye thamani ya shilingi bilion 71.3. β at Tanzania
The Fourth China-Africa Economic and Trade Expo, Changsha, China
Theme: China and Africa β Towards Modernization
Manyara to the World, Proudly Represented πΉπΏππΎ
Nimeshiriki hafla maalum ya utoaji wa Tuzo ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, leo tarehe 31 Mei 2025.
Tuzo hiyo ya heshima imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa Rais Samia katika kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidiplomasia nchini, pamoja na uongozi wake mahiri wa kuleta mshikamano Kitaifa.
Leo tumefunga rasmi Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mafanikio makubwa. Katika siku hii muhimu, tumesikiliza na kupokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025β2030, ilani inayogusa kwa kina uhalisia wa maisha ya Mtanzania mmoja mmoja, pamoja na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Aidha, tumepokea maelekezo na maagizo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani mwaka 2025. Chama chetu kipo imara, kimejipanga, na sisi sote tupo tayari kwa mwaka huu wa uchaguzi.
Mitano tena kwa Samia!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Asante sana Dodoma.
@CCMTanzania
1
6
250
Leo nimepata heshima ya kuhudhuria Bunge Jijini Dodoma kufuatia mwaliko maalum wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Innocent Bashungwa. Nimefuatilia kwa karibu uwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Ni jambo la faraja kuona mipango inayolenga kuimarisha usalama na ustawi wa wananchi wetu ikiwekwa mezani kwa ajili ya mustakabali wa Taifa letu.
Hongera sana Mhe Innocent Bashungwa kwa uwasilishaji mzuri wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 -uliowasilishwa kwa umahiri, dira na dhamira ya dhati kwa maendeleo ya Taifa letu.






















































