Rahisi sana ongea na watu wa Mlilo wape 1M kaa pembeni show inaisha mapema sana..
Issue ya simu 100k wanakusaka mpaka wanakupata..
Sema dua ya aliyedhulumiwa inapokelewa haraka...
mKigoma ⚓ retweeted
الأَبناءُ علىٰ دينِ أُمَّهاتِهم فِي الغَالِب.
Mara nyingi Watoto wanakuwa katika Dini ya Mama zao...
فاظفر بذات الدين تربت يداك
Hivyo Chagua Mke mwenye Dini itapata baraka mikono yako.
mKigoma ⚓ retweeted
Chukia utakavyo, lakini Uislamu ni dini ya haki. ☝️🕌
Uislamu unatoa mwongozo katika maisha, unafundisha haki, uadilifu na heshima kwa binadamu. Unaweza kuuchukia Uislamu, lakini chuki yako haibadilishi usilamu ni dini ya haki
إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ☝️
mKigoma ⚓ retweeted
MIONGONI MWA ALAMA ZA KIYAMA
Mtume wa Allah ﷺ amesema:
“Miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa kwa elimu, kuenea kwa ujinga, kunywewa pombe, kuenea kwa uzinzi, kupungua kwa wanaume na kuongezeka kwa wanawake, mpaka itakapofikia kuwa mwanamume mmoja ndiye atakayesimamia wanawake hamsini.”
Mafunzo kutoka katika Hadithi..⏬
Hadithi hii inatufundisha kwamba miongoni mwa alama za Kiyama ni kuenea kwa mambo ambayo ni kinyume na maadili ya Kiislamu, kama vile ujinga wa dini, unywaji wa pombe na uzinzi.
Pia Mtume ﷺ ametaja kupungua kwa wanaume na kuongezeka kwa wanawake, mpaka idadi yao itakuwa kubwa sana ikilinganishwa na wanaume.
Jambo la muhimu: “Kuondolewa kwa elimu” hakumaanishi vitabu vya elimu kutoweka tu, bali pia kuondoka kwa elimu kupitia kufariki kwa wanazuoni, kisha ujinga ukaenea na watu wasiojua wakaanza kuzungumza na kutoa hukumu bila elimu.
Mtaani kugumu kinoma.
Buku 10 kuipata kipengele na ukiipata inasha faster yani..
Buku 10 ambayo hata kuku mzima hupati..
Pesa ipo wapi?.. 😤😤
Nikumbushe tena 😂😂... Boy gari limewakia kwenye mteremko asaivi..
mKigoma ⚓ retweeted
Do you say the full Tashahhud if you join the prayer in the last rak’ah?
- Sh. Sulayman Ar-Ruhayli
mKigoma ⚓ retweeted
HADITHI YA MTUME ﷺ ✅
Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini, ‘Aishah رضي الله عنها, kwamba Mtume ﷺ amesema:
رَكْعَتَا الفَجْرِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا
“Rakaa mbili za Swala ya Alfajiri ni bora kuliko dunia na vyote vilivyomo ndani yake.”
📚 Sahih Muslim, 752
🎓 Kauli ya Al-‘Allamah Ibn ‘Uthaymin رحمه الله
Amesema..
“Dunia tangu ilipoumbwa mpaka kisimame Kiyama, pamoja na mapambo yake yote; dhahabu na fedha, starehe, majumba, vyombo vya usafiri na mengineyo rakaa hizi mbili ni bora kuliko dunia na vyote vilivyomo ndani yake.”
📚 Sharh Zad al-Mustaqni‘, 4/70
Rakaa mbili zinazokusudiwa hapa ni Sunnah ya Alfajiri, yaani rakaa mbili zinazotangulia Swala ya faradhi ya Alfajiri.
Ni Sunnah yenye fadhila kubwa sana kiasi kwamba Mtume ﷺ ameilinganisha na kitu kilicho bora kuliko dunia nzima na yaliyomo ndani yake.
🌸 Usikose rakaa hizi mbili, hata kama ni kwa sababu ya uzito wa usingizi.
Allah atuwezeshe kuzihifadhi Sunnah hizi na kuzitekeleza kwa ikhlasi. Aamiin.
















