A Man of Wisdom retweeted
Kwako Mh Freeman Mbowe.
Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu. Tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya ulipokuwa Mkti wetu.
Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku mwenyekiti wetu, Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na Chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.
Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbali mbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki. Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.
“Mungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”
Wagalatia 6:7
Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi? Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?
Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20. Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani. Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano .
Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.
“Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.” Mwanzo 4:10
Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwanini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki , maana hata Kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu. Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako Mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ?
Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa. Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma ?
“Dhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.”
Nelson Mandela
Kwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba , usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini.
Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko.Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.
Huu si mwaliko wa ugomvi. Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.
“Haki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.”
Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali.
Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya haki.
A Man of Wisdom retweeted
No one has a better collection of pictures than Late Muhammadu Buhari (RIP), his memory is going to live on till eternity through colourful lenses.
A thread of some of his legendary, as well as immortal photos 🧵
1.
A Man of Wisdom retweeted
Dira (vision):
“Tazania iwe nchi yeneye demokrasia ya kweli
na maendeleo ya watu wake wote”
Dhima (Mission):
“Kutoa uongozi bora, sera sahihi,
mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo
endelevu ya Tanzania”
Tunu za Chama (Values):
Uadilifu, Ubora, Uwajibikaji,
Uzalendo na Utu.
Hii ndio Chadema na ndio maana tunasimama hapa tulipo. Wale wanaosema lengo la chama ni kushika dola, unashika hiyo dola kwa kufuata misimamo hii ya chama sio nje ya haya.
A Man of Wisdom retweeted
Ndugu Watanzania,
Kwa heshima na taadhima, ninawaandikia barua hii nikiwa mwenye uchungu wa kweli juu ya hatima ya nchi yetu. Sauti yangu ni sauti ya mamilioni ya Watanzania waliokata tamaa. Ni kilio cha taifa lililonyimwa haki, likakandamizwa kisiasa, na sasa likielea bila dira.Leo tunashuhudia kilele cha udanganyifu wa kitaifa unaoitwa uchaguzi. Kinachoendelea mbele ya macho yetu si uchaguzi, bali ni maonyesho ya kisiasa yaliyotengenezwa na CCM kwa ajili ya kudumisha utawala wake wa mabavu. Mfumo wetu wa uchaguzi umepoteza uhalali. Tume ya uchaguzi haijitegemei. Sheria zimejaa upendeleo. Na uhuru wa wapinzani unadhibitiwa kwa vitisho, vifungo, na masharti ya hovyo.
Katika hali hii ya giza, chama kikuu cha upinzani CHADEMA tumechukua msimamo wa kishujaa na wa kizalendo: “No Reforms, No Elections.”
Hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi.
Hakuna tume huru, hakuna ushiriki.
Hakuna sheria ya haki, hakuna maana ya kura.Msimamo huu wa CHADEMA si wa ukaidi. Ni msimamo wa kulinda heshima ya wananchi, wa kupigania demokrasia ya kweli, na wa kusema ukweli kwa ujasiri wakati ambapo wengine wanaogopa.
Lakini kinachouma zaidi ni hiki: wakati CHADEMA wanasimama imara kwa ajili ya taifa, wimbi kubwa la watu — hasa vijana — linakimbilia kuchukua fomu za kugombea. Wengi wao hawana sera, hawana maadili, wala hawana dira ya taifa. Wanaona kutokuwepo kwa CHADEMA kama fursa ya kupenya bila ushindani. Wanadhani kuwa uchaguzi bila chama kikuu cha upinzani ni “mteremko wa kisiasa.” Hawajui kwamba wanashiriki katika kufunika kaburi la demokrasia. Na kilicho cha aibu zaidi ni kuwepo kwa baadhi ya vyama vinavyojiita vya upinzani vinavyoshiriki uchaguzi huu huku wakijua fika kuwa hakuna usawa, hakuna haki, na hakuna matumaini. Hawa si wapinzani — ni wasindikizaji wa watawala. Wamesahau wajibu wao wa kupigania haki ya wananchi. Wameamua kuuza heshima ya siasa kwa tiketi ya kugombea.
Sisi ndio tulipaswa kuwa mstari wa mbele kulinda msingi wa “No Reforms, No Elections.” Sisi ndio tungepaswa kulia na kudai tume huru. Tungepaswa kuandika, kuandamana, kuhamasisha na kushinikiza mageuzi ya kweli ya kisiasa. Lakini badala yake, tumekuwa mashabiki wa mfumo huu wa hovyo. Tumeingia kwenye siasa bila kusoma historia ya taifa letu. Tumejitosa kwenye uchaguzi wa aibu tukidhani kuwa siasa ni jukwaa la sifa na Fedha badala ya uwanja wa majukumu.
Nawauliza leo:
Je, ni ujasiri au ni ujinga kugombea uchaguzi ambao tayari umepangwa?
Ni uadilifu au ni tamaa kugombea pasipo haki wala sheria ya haki?
Na ni uzalendo au ni usaliti kushiriki uchaguzi ambao unawadhulumu mamilioni ya Watanzania kwa kimya?
Wito wa “No Reforms, No Elections” si wimbo wa CHADEMA peke yake. Ni wito wa kila Mtanzania anayejua tofauti kati ya haki na hila, kati ya uongozi na ulaji, kati ya siasa safi na siasa ya hovyo.
Watanzania wenzangu, huu si wakati wa vigeugeu. Si wakati wa kusubiri kufaidika kwenye mfumo uliopinda. Ni wakati wa kusema ukweli, hata kama ni kwa uchache.
Wito wangu, tuunge mkono kauli ya “No Reforms, No Elections” kwa vitendo, si maneno.
Tuwakemee vijana wanaogeuza siasa kuwa jukwaa la kutafuta umaarufu badala ya majukumu
Tuwalaani wapinzani bandia wanaosaidia CCM kudumisha mfumo huu wa mabavu.
Pasipo mageuzi, uchaguzi ni mzaha.
Pasipo uchaguzi huru, hatuna uhuru.
Pasipo ujasiri wa vijana, hatuna kesho.
A Man of Wisdom retweeted
Replying to @MarekaMalili
USA will never let you look north Korea if unatengeneza nuclear watakwambia ni hatari na tishio kwa dunia ukiback down watakuja kwenye missile then watakuja kwenye human rights yaani Wao NJIA zote hawaepukiki
Even now they won't leave you alone watch until the end
A Man of Wisdom retweeted
Kama miaka mitatu wamekopa trilioni 50.
Ukiangalia miradi yote mikubwa kama SGR imesimama wakandarasi wanadai na wameondoka site.
Nchi nzima napokea malalamiko ya wakandarasi kufirisika kwasababu ya kutolipwa madeni na serikali.
Hivi fedha zimekwenda wapi na itakuwaje hawa watu wakipata hata miezi sita mbele!!!!
A Man of Wisdom retweeted
Polisi, usalama, mahakama, msajili michezo..
Nini hawajatumia kujaribu kufifisha nguvu ya wananchi kudai mabadiliko kwa kutumia #NoReformsNoElection .
Nimezunguka mikoa karibia yote ya Tanzania, tumepata shida nyingi, majaribu na hata kuumizwa lakini tumeona kiu kubwa ya wananchi kutaka mabadiliko.
Tabora tulinyimwa uwanja, ukaruhusiwa kutumika saa tano, mkutano jioni saa nane, mkutano umetangazwa masaa mawili na uwanja ukatapika watu.
Tunawashukuru Watanzania kwa michango yenu tumeweza kusafiri, kula na kulala.
tutaongea na nyie mda sio mrefu.
Chama chenu kiko imara zaidi, tutaishida vita hii dhidi ya udhalimu, dhuluma, utekaji, uporaji wa mali za umma, umasikini na ufisadi. Tutashinda na tutashangilia pamoja.
A Man of Wisdom retweeted
Kikwete hata hajui dini yake inasema nini anaongea tu bora aendelee kutupiga kwenye vitaru vya carbon credit biashara ya Matrillion ambayo mwanae Miraji anafanya, Samia ni muoga sana , Siku Kikwete akifungua tu mdogo kuongelea haki, wanapita naye
A Man of Wisdom retweeted
This right here is what my family and I chose to listen to for Sunday Service. Yes with a Muslim Elder & Clergy! He has reminded us that we are first humans and that Ubuntu spirit binds & unites us beyond the little religious, ethnic,”national” class, gender or class differences
A Man of Wisdom retweeted
Sauti za kukemea UTEKAJI, UUAJI na KUUMIZA Watanganyika zinaongezeka kwa kasi kubwa sana.
Mtumishi hapa naye amepita alimo pita jasiri Josephat Gwajima.
Haya sasa, nendeni mkafungie na hili kanisa kama mlivyo fungia Ufufuo na Uzima.
A Man of Wisdom retweeted
Siku hizi Matombo hakukaliki yaani nikiona tu mambo kama haya napanda basi faster to Daslama 🔥🔥🙌🏾🙌🏾😋
A Man of Wisdom retweeted
Dakika zako 3:27 hazitaenda bure USIKU wa leo. Msikilize GWAJIMA.🧠
Watu kama hawa HAWATAKIWI (GWAJIMANAZATION).
REPOST 500
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
A Man of Wisdom retweeted
I will not be intimidated. I will not be silenced. My voice will be heard, and my vision will be realized.
I was born once, and I will die once. There is no dress rehearsal for life—everything I do, I do with intention. No one is coming to save us. You are the change you seek.
This country is ours. Lets all be ready to be counted among those who stood up, who fought to make our nation great again.
#strongertogether
#NoReformsNoElection
#FreeLissu























