Christian Bwaya retweeted
Mahojiano kama haya yanayofanywa na Waziri wa Elimu mwenyewe Prof Mkenda, kwa kiasi kikubwa, yanachangia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu elimu, wasomi na nafasi ya sayansi na tafiti katika kutatua matatizo yanayowagusa watu.
Tunahitaji juhudi kama hizi kuondoa mawazo yanayopandikizwa kwa vijana kuwa kama ‘ujanja ujanja’ unalipa basi hatuhitaji elimu. Hongera kwa Waziri Mkenda na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Christian Bwaya retweeted
Replying to @brayansilayo_ @bwaya
"....Tukiifupisha matokeo yake ni watu kufikiri uchuuzi na uchawa unatosha....." - @bwaya.
Replying to @bwaya
Christian Bwaya retweeted
Finally, mzigo umenifikia. Alhamdullilah
xitter.cf/mayengodr/status/21103…
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya
Waziri Mkenda anafanya kazi nzuri, ila tunaomba pia ajira kwa wasomi zizidi kuhakikishwa, vijana wakiona wasomi wanaajiriwa watapenda elimu zaidi
Christian Bwaya retweeted
Replying to @97Yamungu @bwaya
Sidhani kana wengi tunatumia hizi vitu kujifunza. Angalia maudhui yanayizalishwa yepi ni elimu yepi ni burudani. Pia angalia jamii namna inashiriki kwenye mijadala muhimu
Mahojiano kama haya yanayofanywa na Waziri wa Elimu mwenyewe Prof Mkenda, kwa kiasi kikubwa, yanachangia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu elimu, wasomi na nafasi ya sayansi na tafiti katika kutatua matatizo yanayowagusa watu.
Tunahitaji juhudi kama hizi kuondoa mawazo yanayopandikizwa kwa vijana kuwa kama ‘ujanja ujanja’ unalipa basi hatuhitaji elimu. Hongera kwa Waziri Mkenda na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Christian Bwaya retweeted
Walter Mischel, mshunuzi maarufu aliyepata kuwa pia mwalimu wa Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani anaweza kuwa na mawili matatu kwako unapotafakari namna utakavyoianza safari yako ya 2025 wiki ijayo.
Miaka ya 1970, Walter Mischel alifanya utafiti unaoendelea kuthibitika duniani kote kuonesha kuwa siri ya mafanikio ya mtu ni subira —uwezo wa kudhibiti mihemuko (tamaa ya macho, hisia) kama gharama ya kufikia małengo. Gugo kitu kinaitwa Marshmallow experiment, au delayed gratification kujifunza zaidi.
Mischel aliwatumia watoto wa miaka minne, wengi wakiwa watoto wa walimu wa chuo hicho. Kawagawia wale watoto, mmoja mmoja kwa wakati tofauti Marshmallow, mfano wa keki ya kimarekani. Mischel anawapa agizo rahisi, “Kaa hapa na Marshmallow naondoka kidogo. Ukiweza kusubiri nikirudi ukawa hujaila nikaikuta, basi nitakupa ya keki ya pili.”
Marshmallow ya pili ilikusudiwa kuwa ‘zawadi ya ushindi’ kwa maana ya kuutambua uvumilivu wa mtoto. Hata hivyo, ikiwa mtoto angeila, haidhuru, lakini mtoto asingepata zawadi ya keki (marshmallow) ya pili. Mischel anaondoka baada ya kuhakikisha mtoto ameelewa maelezo hayo, anarudi baada ya dakika kumi na tano.
Christian Bwaya retweeted
“Ukiwa na akili nyingi na unajua unazo, na unazitumia vizuri kutatua matatizo yanayoikabili jamii, kwa kawaida, huhangaishwi tena na mashindano ya kujikusanyia vitu vinavyoonekana. Dalili ya kwanza kuwa huna akili ni kufikiri lengo la maisha haya ni kujitajirisha, kufanya anasa na kuwatambia watu kuwa unawazidi starehe.”
Mwenye akili, zile akili zenyewe, anatumia akili zake kutatua matatizo yanayoikabili jamii yake halafu matokeo yake anapata hela. Utajiri hauwi lengo kuu la maisha yake bali marupurupu ya kuzitumia akili zake vizuri kupata ufumbuzi wa matatizo yanayowasumbua watu.
Mjinga, tatizo lake linakuwa kupambana kutafuta hela—kwa njia yoyote ikiwemo uhalifu—ili azibe ombwe la kutokuwa na akili na kuwathibitishia watu (hasa wenye akili) kuwa anaweza kuzitafuta na kuzipata.
Tatizo ni kutafuta utajiri kufidia tatizo la kukosa akili—unautafuta utajiri kama lengo kuu la maisha.
Replying to @bwaya
Sidhani kama kutafuta utajiri na kutumia akili kutatua matatizo ya jamii ni vitu vinavyopingana. Mtu anaweza kufanya yote mawili. Swali ni, je, tatizo ni kutafuta utajiri au kuufanya utajiri kuwa kipimo cha mafanikio ya maisha?
Kwa mwenye akili anayezitumia vizuri kutatua matatizo ya jamii, pesa inakuwa matokeo sio lengo kuu—reward system. Lakini pia anapozipata hazimtesi na kumtumbukiza kwenye anasa na majigambo.
Hoja yangu haikuwa ubaya wa pesa bali hatari ya mtu kukosa akili na kufikiri anaishi kutafuta pesa kama lengo kuu. Umeelewa ndugu yangu? L
Replying to @bwaya
kama jamii tumejiwekea system ya rewards ili ku motivate human beings kusolve matatizo
kama una akili kweli,na una solve matatizo ya jamii kweli,kuna system ya rewards ambayo ni pesa which ukiishika vizuri eventually inakua wealth
sasa,huwezi kwepa hii system ya rewards and punishments tuliyojiwekea
kipimo kwamba una solve sana matatizo ya jamii tutayapima vipi ndugu?
tukuamini tu bwana wewe kwa mdomo tu eti "nasolve sana"?
tuwekee measuring metrics tujue bwana Bwaya amesolve matatizo magumu kiasi hiki kwenye jamiii tuone!
“Ukiwa na akili nyingi na unajua unazo, na unazitumia vizuri kutatua matatizo yanayoikabili jamii, kwa kawaida, huhangaishwi tena na mashindano ya kujikusanyia vitu vinavyoonekana. Dalili ya kwanza kuwa huna akili ni kufikiri lengo la maisha haya ni kujitajirisha, kufanya anasa na kuwatambia watu kuwa unawazidi starehe.”
Christian Bwaya retweeted
Hatia ni utu wa mwanadamu. Unapopoteza uwezo wa kujisikia hatia unaacha kuwa mtu. Unakuwa sawa na wanyama wengine wasio na dhamiri inayowakumbusha kuwajibika kwa wengind. Hatia, kimaumbile, huturudisha kwenye wajibu wa kuutafakari mstari unaotenganisha mema na mabaya. Unapojisikia hatia maana yake dhamira yako inakushtaki kwa kufanya maamuzi unayojua si sahihi—mf. umemwuumiza mwezako, hujatenda haki nk—na huu ndio msingi wa uadilifu wa mwanadamu.
Somo la hatia tunajifunza mapema kupitia mahusiano yetu na wazazi. Katika hali ya kawaida, mtoto hapendi kuwakosea wazazi/walezi wake. Ukiwa mtoto hujisikii salama bila upendo wa wazazi. Tunahitaji kuona nyuso za wazazi wetu zikitufurahia. Tunapokemewa kwa kukosea, kwa mfano, tunajisikia hatia, ambayo kimsingi ni woga wa kupoteza uhusiano wetu na watu muhimu kwenye maisha yetu. Woga huo ni kengele ya kurudi kwenye mstari. Tunajifunza kujisikia aibu kwa matendo yetu yasiyopendeza. Ukumbwani, hatia huendelea kuwa kengele ya kutukumbusha tunapowakosea wenzetu.
Hutokea mazingira ya kimalezi yanayoua dhamiri inayotukumbusha kujirudi. Chukulia wazazi wasiopatikana kihisia kwa watoto wao. Chukulia wazazi wakali wanaowafanya watoto waone hawana cha kupoteza. Chukulia wazazi wanaofikiri kumdhalilisha mtoto mbele za watu kunamsaidia kumuonya. Hawa, kwa ukali wao, hasira na ukatili huwafundisha watoto hisia nyingine inayoitwa fedheha.
Unapofedheheka, aghalabu unaanza kuwa na maswali mengi kuhusu utu wako. Unapoteza kujiamini kwamba wewe ni mtu anayestahili heshima. Unaanza kuhoji namna watu wanavyokuona. Unaanza kujidharau. Unagundua hakuna kitu utafanya kikakubalika. Unapoteza matumaini ya kumridhisha mzazi. Unaanza kukosa kitu cha kupoteza. Mawili yanaweza kutokea. Kwanza, uwe mpweke asiyeamini ana lolote la kuchangia kwenye jamii ingawa unapotelea kwenye sonona. Pili, uwe jitu katili lisilo na dhamiri tena. Hili la pili likitokea unakuwa sawa na watu walikosa ukaribu utotoni kuwafundisha haja ya kujisikia hatia.
Watu wakatili wasiojisikia hatia kuumiza wengine, aghalabu hawakupendwa utotoni, waliishi utoto wenye upweke na hawakuwa na watu waliowapenda na kuwafanya wajikie kuna kitu cha kupoteza wasipojirudi. Hawa, aghalabu, huishia kuwa watu wazima wasiojisikia hatia wala fedheha na hupoteza dira inayoamsha dhamiri. Hawa hugeuka kuwa watu wakatili wanaoweza kufanya uovu dhidi ya binadamu wenzao na hawajutii. Hawa, wakipata nafasi na madaraka, wana uwezo wa kukuumiza na bado wakategemea uombe msamaha kwa kuwachokoza.
Christian Bwaya retweeted
Mama zetu, enzi hizo, hawakulaza watoto kwenye matoroli. Mtoto alibebwa mgongoni au kifuani. Utamaduni huu umethibitika kusaidia kujenga ukaribu na watoto.
Tabia zetu nyingi zenye utu—kujali, kupenda, kuelewa hisia na kuumizwa na maumivu ya mwingine—zinaanza na hakikisho la uwepo mzazi kimwili kwa mtoto. Usiache kumbeba mtoto. Usiache kumkumbatia mtoto.
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya
Vik, Kari, et al. "Infancy and caring: Descriptions from motherless infants’ caregivers in an institution in rural Tanzania." Psychology and Developing Societies 30.1 (2018): 105-125.
Vik, K., Daudi, V. Z., Kajula, L. J., Rohde, R., Ubuguyu, O. S., & Saibulu, J. N. (2018).