Joined May 2024
Sucha retweeted
Mapenzi yana tabia ya kukusogeza karibu na mtu kiasi cha kukufumbua macho uuone upande wake mwingine ambao si wengi wamewahi kuufikiria. Kwa kawaida, unapompenda mtu, unalazimika kujifunua na kumruhusu kuuona utoto wako, kuiona historia ya tabia zako, aibu zako, maumivu unayojiuguza, hofu usizozikiri kwa watu, hatia za makosa mengi uliyowahi kuyafanya na hata mazimwi unayojaribu kuyadhibiti yasiharibu taswira yako mbele za kadamnasi. Unapoanza mahusiano na mtu, unakutana na sura nzuri ambayo aghalabu huonekana na wengi wetu—busara, hekima, matumaini, furaha, ujasiri, uzuri wa sura na mengine mengi yanayokufanya umpende. Hata hivyo, kadri kina cha kuaminiana kwenu kinavyoongezeka ndivyo unavyopata ruhusa ya kukutana na tabia za faragha zisizofahamika na wengi. Hapa ndipo unapokutana na ile tofauti ya matarajio na kivuli kinene cha uhalisia wa mtu, hali inayoweza kuzalisha ugomvi mkubwa ambao kimsingi ni mtihani wa kukipokea kivuli cha tabia za mtu kisichoruhusiwa kukutana na watu. Ukiweza kupata mtu anayetambua kuwa mapenzi ni pamoja na kuelewa kuwa wewe ni ‘mradi wa ujenzi’ unaoendelea kushughulikia kivuli chako ambacho wakati mwingine wewe mwenyewe hukitambui; ukimpata mtu anayeelewa kuwa tabia hizo hizo zinazomkera huenda ndizo hizo hizo zilizowahi kukusaidia kukabiliana na utoto wenye upweke, unyonge na maumivu ya kukataliwa na watu uliowahitaji, na kwamba mkidhamiria mnaweza kusaidiana kukua pamoja bila kuzodoana, kuumizana na kulaumiana na hata pale kazi hiyo inapokuwa ngumu visasi na chuki havichukui nafasi, utakuwa mmoja wa watu wanaoishi maisha yenye uhuru na amani.
5
14
28
770
Sucha retweeted
“Kama huwezi kuwa na furaha ukiwa peke yako, huwezi kuipata ukiwa na mtu mwingine. Omba omba wawili hawawezi kusaidiana zaidi ya kuongezeana majanga.” —Osho
4
31
2
80
2,638
Mwenye akili, zile akili zenyewe, anatumia akili zake kutatua matatizo yanayoikabili jamii yake halafu matokeo yake anapata hela. Utajiri hauwi lengo kuu la maisha yake bali marupurupu ya kuzitumia akili zake vizuri kupata ufumbuzi wa matatizo yanayowasumbua watu. Mjinga, tatizo lake linakuwa kupambana kutafuta hela—kwa njia yoyote ikiwemo uhalifu—ili azibe ombwe la kutokuwa na akili na kuwathibitishia watu (hasa wenye akili) kuwa anaweza kuzitafuta na kuzipata.
2
15
26
689
Huwezi kutoa kisichokuwepo. Unatoa kile kilichokujaa. Ukiwa na furaha, kwa mfano, tutaona uso wako unakunjuka kuambukiza tabasamu kwa wanaokusogelea. Ukiwa na furaha maneno yako yatabeba furaha kutia moyo wengine. Ukiikosa furaha utaitafuta, aghalabu kwa kukosoa, kushambulia au kuumiza. Saa nyingine tunaumizwa na tabia za watu tukiamini tunatendewa tunachostahili. Kwamba hatupendwi na watu fulani kwa vile tumepungua. Tukichukiwa basi kuna kitu tunakikosa. Ukweli ni kwamba mtu anachokutendea, mara nyingi, huakisi kinachoendelea kwenye maisha yake. Hawezi kutoa kile asichonacho.
1
15
39
1,093
Gumu zaidi kusema katika haya manne ni lipi? 1️⃣ ‘Naomba msamaha. Naomba unisamehe.’ 2️⃣ ‘Nimeshindwa. Ninahitaji msaada.’ 3️⃣ ‘Nilipotoka. Sikuwa sahihi.’ 4️⃣ ‘Ninakupenda.’ Ugumu unaoupata katika moja wapo ya hayo manne hubeba hofu inayokwamisha eneo fulani la maisha yako: ✳️ Hofu ya kuonekana mnyonge. Kiburi. ✳️ Hofu ya kuonekana huwezi. Ujuaji. ✳️ Hofu ya kukosea. Ukamilifu. ✳️ Hofu ya kukataliwa. Upweke.
5
15
41
1,799
Kama kuna kiashiria kimoja kizuri cha ukomavu wako kihisia ni uwezo wa kumsikiliza mtu hasa yule usiyejua hulazimiki kumsikiliza. Ukomavu huo unakuchochea kutamani kuelewa ‘ulimwengu’ wa mwenzako—anafikiri nini, anaona nini, anaamini nini, anataka kufanya nini—bila kuteka uzoefu wake wala simulizi lake na kulipima kwa mizania ya misimamo na matarajio yako. Usikivu wako unapimika vizuri kwa namna unavyoweza kusikia kisichoweza kusemwa kwa maneno. Unasikiliza sauti inayobeba hisia zilizo nyuma ya maneno anayochagua mwenzako. Unasikiliza ujumbe unaobebwa na uso wa mtu. Unasikiliza kuelewa maana ya kimya cha mtu bila kumhukumu na kumshinikiza kukuamini. Unasikiliza kuelewa kinachomgusa zaidi, kinachobeba matumaini yake, kinachomtia ujasiri, kinachobeba fahari yake na kumfanya ajione muhimu miongoni mwa binadamu wenzake. Kadhalika, usikivu wako huambatana na ule upendo wa dhati unaojaribu kuuelewa woga wa mwenzako, kuelewa ilikojificha aibu yake, ukurasa upi wa maisha yake asingependa kuusoma kwa sauti na kubaini swali lipi asingependa uulize maana linaweza kutibua unyonge na hisia za kushindwa. Unasikiliza kinachomkera, kinachotishia heshima yake, kinachotishia kesho yake na hata kuchochochea hasira yake. Unapokuwa na ukomavu wa kihisia, kwa hakika humsikilizi mwenzako kama mtu anayemsoma mwenzake ili kubaini mapungufu yake, wala humsikilizi ili umshauri, umrekebishe, umkosoe na kumfundisha cha kufanya bali kumuelewa yeye kama binadamu timamu, mwenye uhuru mwenye na utashi anayeishi kwenye dunia yake bila kuiingilia. Usikivu, kwa ufupi, ni kumsikiliza mwenzako kwa lengo la kujifunza maana, kwa hakika, unaheshimu uelewa wake hata kama huuelewi.
3
16
25
1,115
Tunatamani kusoma. Tukishasoma tunaanza kubeza elimu. Tunatamani kupendwa. Tukishapendwa tunawachukulia poa wanaotupenda. Tunaanza kuwapenda wasiotupenda. Tunatafuta kazi. Tukishazipata tunaanza kufanya yasiyohusiana na kazi. Tunatamani tusichonacho. Hatuthamini tulichonacho.
6
39
2
104
2,439
#TajiriLaKihaya Hoja yako ina sehemu muhimu, Haki inaweza kucheleweshwa na momentum ya kisiasa inaweza kubadilika. Lkn hapa ndipo nadhani hoja yako inahitaji kujengwa upya. Siku zote kucheleweshwa kwa haki si ushahidi kwamba mapambano yameshindwa. Nakujibu kwa mifano 👇 1/7
#TajiriLaKihaya Kama unaamini Tanzania kuna HAKI, basi unaweza kuwa unajiandaa kwa “shock” kubwa. Kwanza, Tundu Lissu amekuwa mahabusu tangu Aprili 2025 akishtakiwa kwa uhaini kesi ambayo bado inaendelea… Lakini swali langu si tu Lissu atahukumiwa au ataachiwa? Swali ni,ikiwa mchakato utaendelea kucheleweshwa mpaka muda ambao uchaguzi mwingine umepita, nani atakuwa ameshinda? Kwa sababu haki iliyocheleweshwa inaweza kupoteza maana yake kisiasa, hata kama mwisho wa siku hukumu itatolewa. Na tusijidanganye kuhusu kelele za mitandaoni… Tumewahi kuona watu wakipotea, wakikamatwa au kuuawa; mitandao ikajaa hasira kwa siku kadhaa, hashtags zikapanda, watu wakaomba likes na reposts 200 ili post iende mbali halafu kimya. Mdude Nyagali, ali kibao, soka,Tesha,Polepole…nk Hivyo tusije tukajipa faraja kwamba “Lissu akihukumiwa, nchi haitakaa kimya.” Really? What exactly will happen? Raia wataandamana? CHADEMA itachukua hatua gani? Jamii ya kimataifa itafanya nini zaidi ya statements? Na sisi kwenye mitandao tutafanya nini zaidi ya kupost mara mbili tatu kuomba watu wa-repost na kusema tufanye hii post ifike mbali? 😂 Hili si suala la Lissu pekee. CHADEMA, kama kuna njia yoyote ya kisheria, kisiasa na kidiplomasia ya kuhakikisha Lissu anapata haki na uhuru wake kwa wakati, itumike sasa. Tusisubiri hukumu ndipo tuanze kujiuliza tulipaswa kufanya nini. Let’s save Lissu kwa njia halali, yenye mkakati na yenye matokeo. Swali la mwisho… Unadhani Lissu akihukumiwa kifungo cha maisha au adhabu ya kifo, nini hasa kitafanyika? Je, tutasimama na kuchukua hatua? Au tutapiga kelele mitandaoni kwa siku chache, halafu maisha yataendelea kama kawaida kama ilivyotokea kwa wengine? Hili ni swali ambalo CHADEMA, wapinzani, wanaharakati na kila Mtanzania anayejali haki anapaswa kujiuliza sasa, si baada ya hukumu. Maana huko mahakamani kutegemea Lissu atapata Haki ni kujidanganya waziwazi…
17
28
1
100
6,032
Mtu ni Anonymous, DP yake katuni, Then anawaambia Wanaharakati KEYBOARD WARRIOR 😁 Wazee siku moja moja twendeni front
6
5
67
1,498
So tuache kuwaamini WANAHARAKATI tukuwmini wewe (Anonymous). Mkuu, Ulishawahi hata kuwekwa mkononi mwa Mamlaka dhalimu, Ulowahi hata kuwekwa lockup sababu ya kuoambana na unyanyasaji wa Dola? Umuhimu wa Wanaharakati upo sababu wao ndio wako Front na Wanajulikana Sura mpaka majina wakipambana, Sisi wengine ni Keyboard Warrior kuandika ujinga ujinga tuko kitandani.
Baada ya yote haya yaliyotokea ktk nchi iliyolaaniwa, bado kuna watu wanaamini kwamba wanaharakati ni watu wa muhimu na wanawajali. Sad enough hata watu wasomi ambao tungetegemea wawe na uelewa zaid nao wanafikiria hivo. Hapo ndo utagundua si suala la elimu, IQ ya mbongo ni zero.
8
13
67
2,367
#TajiriLaKihaya Juzi nilimuona Baba Levo akimuomba msaada Waziri wa Kenya, Ali Hassan Joho. Kwa muda mrefu pia tumekuwa tukijadili namna Rais William Ruto alivyo msikivu, mpaka kufikia hatua ya kuandaa majadiliano ya wazi na vijana kupitia X. Ukiangalia kwa ujumla, kuna kitu Watanzania wengi tunatamani kujifunza kutoka Kenya: uhuru mpana wa wananchi, utawala wa sheria, kuheshimu Katiba, taasisi kuwa na nguvu, na viongozi kuwa tayari kusikiliza hata sauti zinazowakosoa. Na tunapozungumzia historia ya mageuzi ya kisiasa Kenya, hatuwezi kupuuza mchango wa Hayati Raila Odinga na wengine waliopigania mabadiliko hayo. Lakini kuna sehemu moja ya historia yao ambayo sisi Watanzania tunapaswa kuitazama kwa umakini sana. Kenya haikufika hapo kwa sababu Wakenya hawakuchukiana. Walifikia hapo kwa sababu, wakati fulani, viongozi wao walitambua kwamba chuki na kisasi haviwezi kujenga taifa. Baada ya uchaguzi wa 2007, Kenya ililipuka. Kulikuwa na ghasia kubwa, watu waliuawa, familia zikavunjika, wengine wakalazimika kuyakimbia makazi yao, na mgawanyiko wa kisiasa ukachukua sura ya kikabila. Na watu wengi waliokuwa pande tofauti za siasa walikuwa mahasimu wakubwa. Lakini mwisho wa siku walikaa mezani. Wakazungumza,Wakafanya compromises,Wakameza baadhi ya ego zao Na wakajaribu kuiokoa nchi kwanza. Mchakato huo ukasaidia kufungua ukurasa wa mageuzi makubwa yaliyofikia Katiba mpya ya Kenya ya 2010. Leo hii, ukiangalia siasa za Kenya, utaona watu waliokuwa mahasimu wakubwa miaka iliyopita wamewahi kukaa upande mmoja wa meza, kufanya kazi serikalini, bungeni au kushirikiana kwenye masuala ya kitaifa. Hii ndiyo point ambayo tunapaswa kuielewa Tanzania. Mpinzani wako wa leo si lazima awe adui yako wa milele. Siasa zinabadilika,Marafiki wanabadilika,Maadui wanabadilika. Lakini taifa linabaki. Ndiyo maana hata kwenye sheria, mahakama huangalia precedents,maamuzi ya nyuma ili kusaidia kuelewa na kuamua mambo yanayofanana. Kwa nini basi sisi tusifanye hivyo kwenye siasa? Kwa nini tusiiangalie Kenya kama case study? Si kwa sababu Kenya imekamilika. La hasha!Wao pia wana matatizo yao. Lakini wamepitia baadhi ya machungu tunayoyaona leo, na kuna mambo wamejifunza kwa gharama kubwa sana. Sisi hatupaswi kusubiri kulipa gharama ileile ili tujifunze. Na hapa ndipo ninapowaambia wanasiasa wetu wote: CCM, CHADEMA na vyama vingine. Serikali na upinzani. Viongozi na wanaharakati. Msiweke ego zenu juu ya mustakabali wa nchi. Msiweke chuki juu ya maridhiano. Na kwa CHADEMA hasa: Msikubali harakati ziwe mbadala wa siasa. Mwanaharakati anaweza kupaza sauti. Mwanasiasa anatakiwa pia kujua wakati wa kukaa mezani, kujadiliana na kutafuta suluhu. Kukaa mezani hakumaanishi umesaliti msimamo wako. Kufanya negotiation hakumaanishi umeshindwa. Compromise haimaanishi umeuza nchi. Wakati mwingine compromise ndiyo njia pekee ya kuokoa nchi. Na kwa Serikali: Kusikiliza upinzani si udhaifu. Kuruhusu ukosoaji si kushindwa. Kuheshimu Katiba si hisani. Kuheshimu haki za raia si zawadi kutoka serikalini,ni wajibu wa dola. MWACHIENI LISSU… Tunapaswa kujenga Tanzania ambayo hata mtu anayekupinga leo anaamini kwamba kesho, akibadilisha msimamo au akishinda uchaguzi, naye atalindwa na mfumo huohuo. Kwa sababu kama tunajenga mfumo wa kumlinda mshindi leo na kumuadhibu mshindwa, kesho mfumo huo unaweza kutugeukia sisi wenyewe. Tusijenge Tanzania ya kulipizana. Tujenge Tanzania ya taasisi. Tusisubiri mpaka taifa ligawanyike ndipo tuanze kutafuta maridhiano. Tusisubiri kizazi kijacho kiulize: “Mlikuwa mnaona haya yote yakija, kwa nini hamkukaa mezani mapema?” Tujifunze kutoka kwa majirani zetu. Kenya haikuwa perfect. Lakini walijifunza kutokana na makosa yao. Na Tanzania pia inaweza kujifunza bila kupitia maumivu yote waliyopitia wao. Mwisho wa siku, CCM inaweza kushinda uchaguzi. CHADEMA inaweza kushinda uchaguzi. Chama kingine kinaweza kushinda uchaguzi. Lakini hakuna chama kitakachoshinda kama Tanzania yenyewe itapoteza. 🇹🇿 TAIFA KWANZA✌️
89
65
9
244
17,906
Andiko la Lema linaweza kuwa sahihi au lisiwe sahihi na kama amekosea akosolewe. Lakini hii ya baadhi ya influencers, wanaharakati na watu maarufu kwenda deep kumshambulia kwa maneno makali, kuchafua jina lake na kuhusisha mambo mengine yasiyohusiana na kosa lenyewe haiwezi kujenga chama Kama amekosea, mkosoe kama mkosaji msimjengee taswira ya kuwa mtu mbaya kwa sababu ya andiko moja Maana huyu huyu Lema mnayemchafua leo, kesho mtamhitaji kwenye mikutano ya hadhara aeneze sera za chama. Lakini huku mtandaoni mnawafanya watu waamini kuwa Lema ni mtu mbaya kwa kumtupia maneno Hapa tunajenga chama kweli au tunabomoa? Humu ni mtu mhimu kwenye chama chetu na nimoja ya ngome yetu mhimu yakimkakati. Hata nyie huwa mnakosea vingi tu so tubakishe maneno
93
55
24
276
50,322
#TajiriLaKihaya CHADEMA lazima tujifunze kutofautisha UANAHARAKATI na SIASA. Tukifika mahali tunawaacha wanaharakati watupangie chama chetu kifanye nini, nani awe kiongozi, chama kisimame wapi na kiamue mambo gani, tutakuwa tunakipeleka chama kwenye hatari ya kukiua kwa mikono yetu wenyewe. Mwanaharakati na mwanasiasa wanaweza kuwa na malengo yanayofanana, lakini majukumu yao si lazima yawe sawa. Mwanasiasa anawajibika kwa chama, wanachama, sera, wapiga kura na taasisi za chama. Anaingia kwenye uchaguzi, anatafuta ridhaa ya wananchi na anapaswa kufanya maamuzi yanayoweza kubeba chama kizima. Mwanaharakati, kwa upande mwingine, anaweza kuingia na kutoka kwenye ajenda mbalimbali bila kuwa na wajibu wa moja kwa moja kwa taasisi ya chama. Leo anaweza kuunga mkono CHADEMA kwa sababu anaona chama kinasimamia jambo analoamini; kesho anaweza kukosoa CHADEMA au kuunga mkono nguvu nyingine ikiwa anaona ajenda yake inahitaji kufanya hivyo. Na hilo si kosa. Huo ndiyo uanaharakati. Tatizo linaanza pale chama kinapoacha kujenga msimamo wake wa ndani na kuanza kuongozwa na presha kutoka nje. CHADEMA ni taasisi ya kisiasa. Ina wanachama, katiba, viongozi, vikao, sera na wajibu kwa mamilioni ya Watanzania. Hivyo, maamuzi yake makubwa lazima yatokane na wanachama na mifumo halali ya chama, si kelele za mitandaoni au presha ya watu ambao hawabebi mzigo wa taasisi hiyo. Na tuwe wa kweli,anayekukosoa si lazima awe adui yako, na anayekusifia si lazima awe rafiki yako. Wanaharakati wana nafasi muhimu sana katika demokrasia. Wanaweza kuibua matatizo, kuhoji mamlaka, kutetea haki na kusukuma mijadala ambayo wanasiasa wakati mwingine wanaogopa kuigusa. Chama makini kinapaswa kuwasikiliza. Lakini kuwasikiliza si sawa na kuongozwa nao. CHADEMA inapaswa kuwa na uwezo wa kuchukua hoja nzuri kutoka kwa wanaharakati, kuzipima kwa sera na misingi ya chama, kisha kufanya uamuzi unaolinda maslahi mapana ya Watanzania. Pia tunapaswa kuwa waangalifu na ushawishi wa nje. Dunia ya leo ina nguvu kubwa za kiuchumi, kisiasa na kiitikadi zinazojaribu kuathiri mijadala katika nchi mbalimbali. Hii si sababu ya kumshuku kila mwanaharakati kuwa anatumiwa na mtu fulani,lakini ni sababu ya chama kuwa na uwezo wa kuchambua kila ajenda na kujiuliza: Nani anafaidika? Ajenda hii inamlinda nani? Inaendana na misingi yetu? Na mwisho wake ni nini kwa Tanzania? Hatupaswi pia kuingia kwenye siasa za kuamini kwamba kila anayekuja na fedha, taasisi, NGO au ajenda kutoka nje ana nia mbaya. Lakini vivyo hivyo, hatupaswi kuwa wajinga kiasi cha kuamini kwamba kila ushawishi wa nje hauna maslahi nyuma yake. CHADEMA inahitaji uhuru wa kimkakati. Tusijenge chama kinachotegemea personalities za mitandaoni, influencers au wanaharakati maarufu. Watu huja na kuondoka, lakini taasisi inabaki. Leo mtu anaweza kuwa karibu sana na CHADEMA kwa sababu anaona chama kina nguvu. Kesho akabadili msimamo. Kesho kutwa akahamia chama kingine. Hiyo ni sehemu ya uhuru wake. Lakini chama hakiwezi kubadili misingi yake kila mtu maarufu anapobadili msimamo. Chama lazima kiwe na dira yake. Tunataka CHADEMA iwe chama cha wanachama, sera, taasisi na misingi, si chama kinachoendeshwa na trend za X. MWITO WANGU KWA CHADEMA Sasa ni wakati wa kuchukua hatua, si kubishana tu mitandaoni. Kwanza, chama kiimarishe vikao na mifumo yake ya ndani ili maamuzi muhimu yafanywe kwa mujibu wa katiba, kanuni na misingi ya chama. Pili, CHADEMA ijenge utamaduni wa uwajibikaji na hoja, si utamaduni wa kufuata umaarufu wa mtu. Hakuna mwanachama, kiongozi, mwanaharakati au influencer anayepaswa kuwa juu ya taasisi. Tatu, viongozi wa chama wakumbuke kwamba nguvu yao ya msingi haitoki kwa wanaharakati, influencers wala watu maarufu mtandaoni. Nguvu ya chama inatoka kwa wanachama na wananchi wanaokipa ridhaa.
98
53
16
218
60,972
Tatizo sio hawa jamaa wenye Podcast kufanya Podcast zao, wala kulipa watu ku-push # zao. Hiyo ni sehemu ya biashara na marketing. Tatizo ni pale wanapoanza kuzungumza mambo ambayo hayana uhalisia na maisha ya vijana wanaowasikiliza. Unaposema umenunua gari la milioni 170, wakati unasema unalipwa mshahara wa Sh 250,000, bila kutoa maelezo ya msingi ya hiyo tofauti imetoka wapi, ni jambo linaloshangaza. Sidhani kama hapo kuna jambo la msingi la kumfundisha kijana. Badala ya kumjenga, unaweza kumfundisha kwamba mafanikio makubwa yanapatikana kwa njia zisizoeleweka—na hata kuhalalisha au kuhamasisha fedha haramu. Podcast iwe sehemu ya kuelimisha, kujenga fikra na kuonyesha njia halali za kufanikiwa, si kutengeneza maisha ya kuigiza ambayo vijana watajaribu kuyaiga bila kujua gharama yake.
8
7
2
30
2,983
ni kujidanganya kudhani kwamba huduma za umma zinaweza kuboreshwa pale ambapo watu waliokabidhiwa jukumu la kuhakikisha hilo linatokea hata hawatumii huduma hizo. kama kitu hukitumii wewe, wala mtu yoyote unayemjali kama mtoto wako, hamasa ya kukiboresha unaitolea wapi?
13
108
5
451
9,892
Sucha retweeted
The Most Comprehensive Resource For Cisco GNS3 Labs! ✅ 🎓 📥 Download GNS3 Labs: ipcisco.com/cisco-gns3-confi… 👉Start to Learn TODAY: ipcisco.com/membership/ . Please ReTweet & Share! . #cisco #networkengineer #gns3
2
20
81
3,464
Jizungushe na watu wanaoongea kwa vitendo, si maneno. Watu wanaopanga maisha kwa miongo, si wiki. Wanaoona lengo na kulifuatilia bila kusita. Watu wanaosali zaidi, wanaokulazimisha ukue, utoe kilicho bora ndani yako, na wasikubali uishi chini ya uwezo wako. Hawa ndio watu wanaobadilisha dunia. Wanasukumana kila siku kuwa bora zaidi. Kwao kazi ni vita na sanaa kwa wakati mmoja, malengo ni haki yao, na biashara ni mchezo wanaoujua kushinda. Ukibarikiwa kuwapata, shikamana nao. Usipowapata… kuwa mmoja wao. 🔥
13
102
6
371
7,698
#TajiriLaKihaya Ufaham kwamba JAMBAZI wakitaka kukuvamia NYUMBANI kwako - watakuvamia tu… wakihitaji Milion zao watakuja tu kuzifata! Ila Tukijenga Nyumba , tunaweka milango, tunaweka Geti kubwa kwenye fence,Tunazungusha Ukuta… ikibidi tunaajiri na Masai kabisaaa hata kama Hana silaha… Ni kweli Mungu Anatulinda ila hatumuachii bila kufanya chochote- Vivyo hivyo Kwa wake zetu- Ni kweli kwamba mwanamke kama ni kahaba au Hakuheshimu na Akiamua kucheat kwenye ndoa atacheat tu! Ila Tunamtengenezea mazingira ya kumlinda na kumuepusha na vishawishi vya nje- Kwanza kabisaa ni kabla Haujao- unachagua Mke atakae Kua Mama Bora kwa watoto wako na Mlezi wa familia- awe BIKRA, ukishindwa basi Asiwe SINGLE MOTHER, na atoke kwenye familia nzuri- awe kalelewa na maadili mazuri- ikiwezekana na wazazi wake wawili Haswa BABA. Pili,Hakikisha anakua House wife- hata kama ni msomi- kazini kuna vishawishi vingi saana- unam Expose mke wako na threats nyingi saana kule kazini… Mke kazi yake kuu ni KUZAA KWA UCHUNGU na kulea familia… Mwanaume KATAFUTE RIZKI KWA JASHO… Mwanaume ukishakubali kwenda kinyume na maandiko na kufata Mila za kizungu za 50-50 tayari Ushapotea na Ndoa imeshakushinda! Wanaume tuyakubali majukumu na tuwalinde wake zetu kwa wivu mkubwa mno!
153
197
14
1,108
60,353
Unaweza kuwa mtu mzima kimwili, miaka 30 kwa umri, miaka 40 kwa umri, lakini kihisia ukawa mtoto mdogo wa miaka minne. Hisia ni ile mihemuko yako, ule mwitikio wako kwa yanayotokea, mawasiliano yasiyotumia lugha kuelezea hali yako ya ndani, ikichochewa na matukio, mawazo, au uzoefu. Utoto wa kihisia, ni ile hali ya kushindwa kutafsiri hisia zako mwenyewe, kuendeshwa na hisia, na hivyo kuathiri namna unavyoelewa hisia za wengine wanaokuzunguka. Utoto wa kihisia hukufanya uwetegemee wengine kushughulikia hisia zako mwenyewe. Huwezi kuwajibikia hisia ulizonazo, ujue kwa hakika nini ufanye, mathalani unapokasirika na hivyo muda mwingi unakuwa mtu wa kuwalaumu wasiohusika. Unapokuwa mtoto, huwezi kusema unachohitaji kwa uwazi. Kumbukumbu za hisi zako kupuuzwa na kutafsirika vibaya zinakuzuia kufahamika unajisikiaje. Unazunguka kukwepa kile hasa unachotamani kifanyike ukiogopa kutokueleweka. Unategemea mtu aelewe mahitaji usiyo yasema na wakati huo huo ukilaumu kitu kisipofanyika kama ulivyotarajia. Hata pale unapofanikiwa kusema unachohitaji hujui kusema kwa adabu, heshima na staha ukitambua unaotaka wakusikie nao wana hisia. Unapozungumza una lugha inayoumiza, inayoshambulia, inayolalamika, inayoonesha dharau, kejeli, majivuno, kiburi na ujuaji. Ingawa mtu mwingine anaweza kulalamika, kwako haisikiki kama jambo la muhimu. Kadhalika, utoto wa kihisia huambatana na kukwepa mazungumzo magumu. Unaogopa kuambiwa umekosea, unatafsiri ukweli kama kulaumiwa, kusemwa, kusimangwa, na hivyo mara nyingi, unaacha mazungumzo muhimu hewani. Unapenda ‘amani’ inayofukia mazungumzo (mf basi bwana yaishe), huwezi kuomba msamaha moja kwa moja, una tabia ya kuzira, kumnyamazia mtu kama namna ya kumuadhibu na kumuonesha umuhimu wako. Nini kinachangia hali hii? Kwanza malezi. Unapolelewa kwenye mazingira ambayo kusema hisia inaonekana kuwa kosa, mazingira ambayo mazungumzo ya wazi kuhusu hisia ngumu yanatafsirika kwa udhaifu, ni rahisi kuchagua kuficha hisia kama njia salama ya kuishi. Lakini pia, majeraha ya kihisia. Kuna nyakati hatuwezi kusema hisia zetu tukiogopa kuchokoza kumbukumbu za maumivu tuliyowahi kukutana nayo. Mkusanyiko wa hisia zisizoshughulikia, hutengeneza kisuguu ya hisia zisizozungumzika, ambazo aghalabu huonekana kama haiba ya mtu—‘hivi ndivyo nilivyo,’ ‘jifunze kuishi na mimi,’ ambao ndio utoto wenyewe wa kihisia.
11
1
26
793