Pinned Tweet
A year ago, on the 26/10 I ran the marathon and dedicated it to praying for a better Tanzania as we were approaching election season.This year, I dedicated my run to all the victims of the massacre that happened on 29/10 to TL and to everyone who has been abducted and tortured🇹🇿
This man has fought so many battles in his life, hii ni nothing kwake wanachoshindwa kuelewa ni kuwa wanazidi kuwapa watanzania more reasons za kuendelea kumuunga mkono Lissu katika mapambano yake. Justice will prevail 🙏🏾
Kama kuna one of the very few politicians wa Kenya wametumia voices zao kucall against the injustices happening in TZ and UG ni Sifuna since he was in ODM hadi leo kaform chama chake cha Linda Mwananchi jamaa bado anamsupport Lissu na waTZ. He deserves to be the 6th 🫡
Dee. retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 499
Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025
Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu.
Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka
Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence.
Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani.
Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi.
Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi.
Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa.
Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande.
Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo.
Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria.
Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini.
Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema?
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza.
Jaji Ndunguru:Sawa
Part 500 itaendea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost.
Dee. retweeted
Whatever happens today.
TALs ideas will live beyond prison walls.
For that i am certain.
Such infectious ideas of a free society cant be jailed.
Dee. retweeted
#Updates Katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu, Mahakama haijamkuta na hatia ya kosa la uhaini. Hata hivyo, Mahakama imemtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi ndani ya shtaka hilo.
Dee. retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 498
Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic.
Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice.
Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo.
Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm.
Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger.
Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa.
Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently.
Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana.
Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi.
Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Dee. retweeted
Baada ya kutamka kuwa Tundu Lissu hakufanya kosa la UHAINI, sasa Mahakama imemtafutia kosa lingine, UCHOCHEZI.
Mind you, kesi ya Uchochezi iko Kisutu.
Sasa hii ni practice ya wapi?
All said and done, Lissu sio Mhaini.
Uchochezi? Come on!
Dee. retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Dee. retweeted
As the High Court of Tanzania delivers its judgment today in the legally bankrupt treason trial of CHADEMA Party Leader Tundu Lissu, I stand in unwavering solidarity with him and the people of Tanzania.
The future of our Jumuia does not belong to neocolonial puppets, corrupt elites, or captured states. It belongs to deep structural reforms, constitutionalism (Ukatiba), and Pan-African solidarity anchored firmly in democratic values and human dignity.
The march towards true Reform–Mageuzi is unstoppable.
Kumekucha!
@TunduALissu @ChademaTZ2 @MariaSTsehai @judiciarytz @TitoMagoti @HecheJohn
My leader #FreeTunduLissuNow
From Ukonga Maximum Security Prison to the world by @TunduALissu
I want to comment on SA politics so bad but naogopa kuambiwa concentrate on fighting the dictatorship in your home country
You guys really think these are the kind of men we dream of getting married to 😆
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zimekuwa zikibainisha ubadhilifu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma, lakini wahusika hawachukuliwi hatua za kisheria, hali inayochangia kuendelea kwa upotevu wa fedha za Serikali.
Amesema Bunge lina wajibu wa kufuatilia na kuhakikisha watu wanaotajwa katika ripoti hizo wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria, badala ya kuendelea kuzichukulia hoja za CAG kama jambo la kawaida (business as usual).
Ametoa kauli hiyo wakati akichangia hoja za kamati mbalimbali za Bunge la 13, Mkutano wa Tano, akieleza kuwa kutokuwapo kwa uwajibikaji kwa waliohusika na ubadhilifu wa fedha katika miradi mbalimbali ya Serikali kunatoa nafasi kwa vitendo hivyo kuendelea.
Ado ameshauri Bunge kutumia mamlaka yake kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua, akirejelea sakata la ESCROW kama mfano unaoonesha umuhimu wa Bunge kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.
Dee. retweeted
CHADEMA yafanya kumbukumbu ya kitaifa ya waliopoteza maisha matukio ya Oktoba 29
Leo Novemba 03, 2026, CHADEMA imefanya tukio la kitaifa la kuwakumbuka walipoteza maisha matukio ya Oktoba 29, ambapo viongozi, wanachama na wageni wengine waliwasha mishumaa na kuweka mashada ya maua kuwakumbuka Watanzania waliopoteza maisha mwaka jana.
Chama hicho kimeeleza kuwa kumbukumbu hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka.

























