Swala la vijana wa kiume kumuangalia mtoto wa kiume anapelekewa moto halijakaa ki code something is wrong with this generation
2
27
Hii kesi Wananchi wataiamua
UKISIKIA UTAFUNZWA NA DUNIA NDIYO HIVI SASA.
CHIBA amekuwa msumbufu kwa miaka mingi sana na amekuwa akichezea tawala nyingi sana zilizokuwa zinapita kwenye nchi hii na alijiaminisha kuwa yeye ni jasiri sana na hakuna anayeweza kumfanya kitu ka kauli zake,matendo yake na hata tabia zake ndiyo maana alikuwa ni mtu asiyejali anachosema na kutenda na madhara yake.
HAJAWAHI kuwa mtu makini kupima kauli zake na matendo yake kama mwanasiasa uchwara kwa muda mrefu sana na matokeo yake akajivika cheo cha kuwa mropokaji mashuhuri na akidhani ana kinga ya kutoshughulikiwa anapotoa kauli za uchochezi na za hovyo.. Alifika mahali alijiona ana kibali cha kufanya hivyo na asiguswe na yoyote. Amefanya hivyo sana wakati wa utawala wa Mkapa,JK na Kambale na akajiona yeye ni mropokaji mteule.
CHIBA hajaanza haya leo wala jana amekuwa anafanya haya kwa muda mrefu sana na alidhihirika kuwa ni mtu mshenzi na wa hovyo sana alipokuwa Rais wa TLS. Alipokuwa rais wa TLS ndipo alipoharibu kabisa taasisi ile na ikageuka kuwa jukwaa la wanasiasa pamoja na wanaharakati na toka kioindi kile TLS haijawahi kupona ulemavu ule mpaka leo na ndiyo maana ina watu kama Mwambukusi ambao ni waropokaji kwenye kila kitu badala ya kufanya majukumu yao ya kitaaluma kama wanasheria.
KITENDO cha DPP kukata rufaa ya hukumu ya miaka minne aliyopewa Chiba ni kielelezo kuwa CHIBA bado ana safari ndefu sana kuelekea kumaliza kesi hii kwa rufaa au kwa vyovyote vile na safari hii siyo nyepesi kama anavyofikiria na itamkalisha jela kwa muda mrefu sana ikiwa ni sehemu ya kumfundisha kwa kuwa alishindwa kufunzwa kwao sasa acha dunia isiyo na huruma imfunze sasa..
DPP amepinga hukumu ya miaka minne maana yake DPP ana uhakika Chiba alitenda kosa la ugaidi na ana uhakika alithibitisha kosa hilo na mahakama kuu imekosea kutomhukumu kunyongwa hadi kufa hivyo imeomba mahakama ya rufaa kurejea shauri lake na hukumu ile na kutoa hukumu stahiki kulingana na kosa la uhaini alilokuwa anakabiliwa nalo.
MAHAKAMA YA RUFAA ina jukumu la kuangalia mwendendo wa kesi na ushahidi kule mahakama kuu na kuipitia hukumu ile ya miaka minne na kuna kila dalili kuwa itafanya na kuamua yafuatayo;
1. Kuirudisha kesi mahakama kuu ikaanze upya na kupangiwa majaji wengine na kurekebisha makosa ya majaji wa mahakama kuu na kutoa hukumu stahiki ya kosa la uhaini ambalo ni kumnyongelea mbali Chiba mpaka kufa AU
2. Kuamua kufuta hukumu ya miaka minne ya Chiba na kumhukumu kwa kosa stahiki na kumnyongelea mbali
HAYA NDIYO matokeo mawili tu ya kesi ya Bwana Chiba na hakuna kitu kitaamuliwa na mahakama ya rufaa tofauti na haya mambo mawili hapo juu.
LAKINI kwa nini haya yanatokea ! Yanatokea kwa kuwa dola na vyombo vyake vimeamua kushughulika na wahalifu wa aina ya Chiba ambao kwa miaka mingi sana wamekuwa wanavunja sheria na kujificha kwenye siasa na kudhani wanaweza kuchoma moto na kuharibu hii nchi na wakaachwa tu huru kwa kuwa ni wanasiasa.
CHIBA ni miongoni mwa watu walioitumia vibaya sana nafasi ya kufanya siasa ndani ya Tanzania alikosea sana kupiga hesabu zake na kudhani awamu hii ni legelege na angeweza kutoboa na siasa zake za kitoto sasa kajikuta yuko jela na asipokuwa mwangalifu atazeekea jela au atafia jela..
TULIPOKUWA tunawasihi na kuwaonya kuwa msichezee dola chezeeni ndevu mlikuwa mnadhani tunawatania eeeh.. Haya sasa pambaneni na mikesi hiyo isiyoisha yaani..
CHIBA amekuwa mtu toxic sana kwenye siasa za Tanzania na amekuwa ni mtu mwenye kujaza watanzania sumu sana mpaka amefika mahali anadhani anaweza kufanya mapinduzi na kuangusha serikali kwa maandamano na vurugu. Haya yalifanyika 29 Oktoba 2025 na mi mipango yao kwa muda mrefu sana na kilichotokea 29 Oktoba ilikuwa ni mipango yao ya muda mrefu sana. Chiba ni mhaini na anyongwe tu.
KUWAKUMBUSHA tu nikuwa mpaka rufaa hii itakaposikilizwa na kuamuliwa ndipo Chiba ataweza kutaka rufaa tena kwa ajili ya kupinga hukumu HALAFU jingine la muhimu ni kuwa mahakama inakwenda mapumziko kuanzia sasa mpaka Februari 2027 😁
#KigogoMediaUpdates
28
Zile takwimu zinazotolewa Mfano Wenye HIV ni 1.8 zinakubalika kwa sababu hakatajwa mtu,vivyo hivyo na alichosema Bwana Daktari no offence
Sharp-Man retweeted
Anaandika Askofu BAGONZA (PhD)
NAANIKA UJINGA WANGU NA KUFICHA HEKIMA YANGU!
Upo wito wa maridhiano kitaifa. Ya namna gani? Tunapishana. Wapo wanaotaka tugange yajayo na wapo wanaotaka tugange yaliyopita. Mimi nina haya. Nimeona bora nianike ujinga wangu ili nipate msaada:
1. Inaonekana maridhiano bila Chadema hayakubaliki. Washawishiwe; wasilazimishwe.
2. Chadema hawawezi kwenda kwenye maridhiano bila Mwenyekiti wao. Siasa ilimweka ndani. Siasa imwondoe. Sheria tunaisingizia.
3. Chadema hawamiliki tena upinzani. Upinzani umehamia mioyoni mwa wananchi katika vyama vyote. Hata CDM wakienda maridhiano bila kuzingatia UKWELI na UWAJIBIKAJI, upinzani utabaki mioyoni mwa wananchi.
4. Tume zimesema mengi kuhusu yaliyotokea 29/10/2025. Tunajichelewesha kukubali kuwa “washauri-machawa” ndio wanahujumu maridhiano. Ukihujumu maridhiano unamhujumu Mkuu wa nchi unayedai unamtetea. Agenda ya rais ajaye atoke Zanzibar ina mantiki gani wakati huu?
5. Yaliyotokea 29/10/2025 yamewapokonya viongozi wetu ujasiri wa kuongoza na kukemea uovu. Maridhiano ya KWELI yatarejesha ujasiri huo. Nani ajitokeze kukemea RUSHWA na kuhimiza watu “walinde migongo” yao?
6. Hivi sasa silaha ya wananchi ni kununa na kuomba dua la kuku. Silaha ya serikali ni “kuacha” utekaji uendelee na “kutohimiza” waliotekwa kuachiliwa. Sioni maridhiano bila hao watu kuonekana!
7. Katika kuteka watu tumeteka UHURU wa wananchi. Bila uhuru hakuna utawala wa sheria. Bila utawala wa sheria tunaongozwa na shuruti ya watawala. Tuirejeshee mahakama uhuru wake kabla mahakama haijaamua kuurejesha yenyewe na kusababisha maasi.
8. Kuhusu Uhuru wa mahakama ninaamini: kwamba, Ni vigumu kwa Rais aliyepo na waliopita kuuaminisha umma kuwa hawaingilii mahakama. Iwe wanaingilia au hawaingilii, umma unaamini kuwa wanaingilia. Hekima ni kutoingilia, lakini wanapolazimika waingilie kwa manufaa ya taifa na si manufaa ya urais, chama au kundi. Kwa sasa waache kujitetea kuwa hawaingilii kwa sababu hakuna atakayewaamini.
9. Ninaendelea kuamini kwamba
Urais siyo rais. Urais ni taasisi.
Utaasisi unaweza kuwa kokoro.
Ndani ya kokoro waweza kuwamo wanaoijumu taasisi ya urais na rais mwenyewe.
10. Wasiojulikana wana nguvu kuliko wanaojulikana. Matokeo yake, viongozi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa, wanawatumikia na kuwatii wasiojulikana kuliko wanavyowatumikia wananchi. Mabadiliko haya ni kikwazo cha maendeleo.
Jamanie! Weusi wa Mjaluo si kukosa sabuni. Siri anaijua kamongo.
😡😡😡😡😡
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 502
Mhe. Lissu anaendelea
Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana.
Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli.
Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi.
Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa.
Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave.
Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana.
Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha.
Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo.
Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu.
Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani.
Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini.
Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine.
Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa.
Majaji wanatoka.
Naomba Repost yako.
1
144
Sharp-Man retweeted
Hoja ya pili, kwamba Lissu alitengeneza 'nia ya kuzuia uchaguzi kwa lengo ya kuitisha serikali' - imepigwa chini.
It goes without saying that this flickering case was dead on arrival.
I see the light
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
103



















