Symon Goodluck retweeted
SINEMA INAENDELEA : Mwanaharakati Maria Sarungi, Hilda Newtown na Twaha, walivyokutwa kwenye kikao cha siri huko Nairobi cha kutengeneza sinema ya kupotea kwa kijana msaidizi wa Tundu Lissu ambaye hafahamiki hata na familia ya Tundu Lissu.
CHADEMA wala waje na kitu kingine ila hili la kujiteka, ni sinema kama sinema nyingine na Watanzania washazishtukia.
Symon Goodluck retweeted
Huyu jamaa mlinzi @daviddjumbe alivyoona boss wake @TunduALissu hatoboi na kesi ya uhaini akaamua akimbie zake Kenya kama watesi wenzake wakina Maria na Hilda waliopewa ufadhili na kulipwa dola 700 kwa mwezi kuleta machafuko nchini
Symon Goodluck retweeted
Huyu dada yukogo smart sana kwenye masuala ya uchambuzi wa siasa π₯π₯
Anaongea fact tupuπ₯π₯
Symon Goodluck retweeted
CHAUMA πͺ
Hiki sasa ndo Chama Kikuu cha upinzani nchini kikifuatiwa na ACTπ₯π₯π₯π₯ β at Tanzania
Symon Goodluck retweeted
Ni matusi kwa Waafrika kumfananisha Tata Madiba (Nelson Mandela) na Kibaka @TunduALissu
1.Mandela hakuficha watoto wa mke nje ya nchi wakati akiwa jela, Lissu ameficha mke na watoto Marekani akisingizia sababu za kiusalama. Wakati wa Mandela, SA ilikuwa hatari zaidi lakini waliamua kubaki nchini.
2. Mandela alitanguliza maridhiano badala ya visasi. Baada ya kutoka gerezani - Mandela hakulipiza kisasi kwa waliomtesa, alihubiri msamaha na umoja wa kitaifa. Lissu mara zote huzungumza kwa lugha kali ya mgawanyiko dhidi ya walioko madarakani.
Lissu na chama chake hawazitaki 4R za Rais Samia Suluhu zinazolenga kuleta amani, ustawi wa uchumi na maisha ya watu, wanataka visasi, vita na umwagaji wa damu, tofauti kabisa na alivyo Mandela.
3. Mandela alijenga chama chake (ANC) badala ya kukigawa β Alileta mshikamano ndani ya chama chake katika kipindi kigumu. Lissu amekuwa akihusishwa na migogoro ya ndani ya chama chake (CHADEMA), ikiwemo kutofautiana na viongozi wenzake hadi kupelekea viongozi wengi wa chama hicho kujivua uwanachama.
4. Mandela alikuwa na uaminifu mkubwa kwa wananchi wake - Alirudi nyumbani na kuishi pamoja na raia wake baada ya ukombozi. Lissu ameendelea kuishi ughaibuni kwa muda mrefu hata baada ya kupata nafasi ya kurejea.
Symon Goodluck retweeted
Ndani ya Bunge la Ulaya lina jumla ya wabunge 720 kati ya hao kuna wabunge 102 ambao ni mashoga na ndio wanaomuunga mkono Lissu.
Symon Goodluck retweeted
Sababu ya Pili kwa nini tunashiriki uchaguzi
ππΏUkweli wa kihistoria kuwa, kote duniani ambapo mpinzani alisusa, mtawala alipita kirahisi na alitumia fursa hiyo kujiimarisha na kuongeza ukandamizaji. @ACTwazalendo hatutaki kumpa mtawala fursa hiyo.
#OperesheniLindaDemokrasia
Symon Goodluck retweeted
MBOWE : NIMEKUWA MTAZAMAJI
"Nikiwa Mwenyekiti niliona madhara ya kususia Uchaguzi sikutamani sasa Chama chetu kisusie tena uchaguzi, ila kwa kua siko kwenye nafasi nabaki kuwa mtazamaji maamuzi ya viongozi" - Freeman Mbowe - Aliyekua Mwenyekiti CHADEMA
Chanzo : Boma Hai FM 89.3
Symon Goodluck retweeted
Mwandishi mwandamizi wa habari za siasa wa Mwananchi, Peter Elias amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kisiposhiriki uchaguzi Mkuu wa 2025, kitapoteza nguvu ya ushawishi wake kwa umma kilioujenga kwa muda mrefu.
Amesema uhai wa chama chochote cha siasa ni pamoja na kushiriki chaguzi zinazofanyika na kutimiza malengo ya kushika dola, lakini ukiwa nje ya mchezo huwezi kupata ushawishi huo.
Elias ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 16, 2025 wakati akichokoza mjadala wa Mwananchi X Space wenye mada isemayo: Kanuni za maadili ya uchaguzi 2025 na mustakabali wa siasa za Chadema, ulioandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL).
Msingi wa hoja imejikita katika kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Marais, Wabunge na Madiwani, kinachovitaka vyama vya siasa, Serikali na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kusaini kanuni hizo.
Aprili 12, 2025 Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima alisema Chadema hakitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba na chaguzi ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano baada ya chama hicho, kususia kusaini kanuni, hivyo kukosa sifa ya kushiriki mchakato huo.
βFursa pekee ilivyonavyo vyama vya siasa ni kujijenga kupitia uchaguzi na vikishinda vikapata viti vinakuwa na sauti bungeni katika kuwakilisha wananchi,βamesema Elias.
Katika maelezo yake amekishauri Chadema kuona haja ya kufanya mazungumzo ya maridhiano kama ilivyoshauriwa na baadhi ya viongozi wastaafu kwa kuwa ni jambo linalozungumzika katika kutafuta mustakabali wao.
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Symon Goodluck retweeted
Kesi iliyofunguliwa na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Zanzibar, inatarajiwa kutajwa leo Alhamisi Aprili 17, 2025 kwenye Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam,ikisikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga ambapo pamoja na mambo mengine wanalalamikia upendeleo katika mgawanyo wa rasilimali za chama pamoja na stahiki nyinginezo.
Kesi hiyo ya madai imefunguliwa na Said Issa Mohamed, ambaye anajitambulisha kama mwanachama na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu, ambao wanajitambulisha kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.
Katika kesi hiyo kulingana na Tovuti ya gazeti la Mwananchi, walioeleza kupata nakala ya kesi hiyo, Walioifungua wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa wadaiwa wamekiuka sheria zinazohusiana na vyama vya siasa na Katiba ya chama hicho.
Wamechukua hatua hiyo na kuomba Mahakama iamuru na kutamka hivyo wakidai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.
Pia, wanadai kuwa kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia; pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa msingi huo, walalamikaji hao wanaomba Mahakama hiyo itoe hukumu na amri dhidi ya wadaiwa kwamba wamekiuka kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.
Pia wanaiomba Mahakama hiyo itamke kwamba ugawaji wa fedha, mali na rasilimali kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kiutawala kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar unaofanywa na wadaiwa ni kinyume cha sheria na ni batili.
Vilevile wanaiomba Mahakama itamke na kuwaelekeza wadaiwa kuzingatia kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.
Amri nyingine wanazoomba ni kusitishwa kwa muda kwa shughuli zote za kisiasa hadi hapo kutakapokuwepo na utekelezaji wa maagizo ya Mahakama.
Na wanaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio la kudumu dhidi ya matumizi ya mali, fedha na rasilimali za chama hadi wajibu maombi watakapotekeleza matakwa ya sheria husika.
Mbali na amri hizo, wanaiomba Mahakama iamuru, wadaiwa walipe gharama za kesi hiyo na itoe nafuu nyingine yoyote ambayo Mahakama itaona inafaa kuzitoa.
Tayari Mahakama imeshatoa wito kwa Chadema kupitia Katibu Mkuu kufika mahakamani wakati kesi hiyo itakapotajwa.
Symon Goodluck retweeted
Kwa wale Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, wasivunje madirisha wala nyumba! KARIBU @ACTwazalendo tufanye Siasa.
Tunaweza kuleta mageuzi tukiwa mchezoni. Uchaguzi ni jukwaa la kuelimisha na kuamsha umma (mobilization). Uchaguzi ni jukwaa la kuionyesha dunia tunachopigania (exposing the flaws).
Symon Goodluck retweeted
Quatro de Fevereiro Airport, Luanda, Angola
Mwanadiplomasia namba moja wa nchi yetu Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipowasili Angola kwa mwaliko wa Mhe. Rais JoΓ£o LourenΓ§o. Katika ziara hii Mhe. Rais pia amepata heshima ya kihistoria kuhutubia Bunge la Angola.
Symon Goodluck retweeted
Kibaha Shopping Mall, Kibaha, Mkoa wa Pwani
Haya ni moja ya matokeo ya kazi za Mama kwenye maisha ya Watanzania na hizi ni sauti za wananchi wa Kibaha na wanufaika wa mradi.
Symon Goodluck retweeted
Siku nzuri katika kazi nchini Angola, ikiwa ni siku ya pili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu, kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa JoΓ£o Manuel GonΓ§alves LourenΓ§o. Tanzania na Angola zimedumu katika ushirikiano wa kidugu kwa zaidi ya miaka arobaini sasa toka enzi za waasisi wetu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati AntΓ³nio Agostinho Neto.
Baada ya kukamilika kwa kazi ya kutafuta uhuru wetu iliyofanywa na waasisi wetu, ni jukumu letu sasa kuendelea na kazi ya kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya nchi zetu hizi, pamoja na kukuza ushirikiano wa kimkakati, wenye lengo la kuleta tija zaidi kwenye maendeleo na ustawi wa wananchi wetu.
Symon Goodluck retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza iliyosainiwa na Wachezaji wa Timu hiyo kutoka kwa Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025. Mmiliki wa Klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe ameeleza dhamira yake ya kuitumia Klabu yake kutangaza utalii nchini Tanzania. Rais Dkt. Samia pia amemkaribisha Mmiliki huyo wa Club ya Manchester kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini.
Symon Goodluck retweeted
Sehemu ya kazi siku ya leo nilipokutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, Ikulu, Dar es Salaam. Tumekuwa na mjadala mzuri kuhusu kushirikiana katika masuala ya uhifadhi pamoja na utafiti.
Sambamba na hayo, nimesikiliza dhamira ya Sir Jim Ratcliffe kuitumia Klabu ya Manchester United kutangaza utalii wa nchi yetu, ambapo pia nimemkaribisha kuanzisha Vituo vya Mafunzo ya Michezo (Sports Academy) hapa nchini. Nimepokea na kumshukuru kwa salamu za kheri toka kwa Kocha Ruben Amorim kwa niaba ya wachezaji wa Klabu ya Manchester United, na za Kocha Mstaafu, Sir Alex Ferguson.
Symon Goodluck retweeted
Asante kwa Mama kutoka kwa wananchi wa Fukayosi, Pwani na ahadi yao kwake kwa mwaka 2025.







































