umojadigital (@umoja_digital) header
umojadigital (@umoja_digital) profile picture

🌍 Umoja Digital | Tunakuletea Habari kutoka nyanja zote za maisha 🌟 Utamaduni | Biashara | Siasa | Sanaa | Habari za Sasa | Michezo | Afya na Zaidi

Joined November 2023
Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)Photo by umojadigital (@umoja_digital)
Wamumini wamiminika kutendewa miujiza ya kujaziwa gesi kwa mtumishi Pastor Tony #Umojadigital
1
18
UPOTOSHAJI Mke wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, amekanusha vikali barua inayosambaa mitandaoni ikidai amejiuzulu. Amesema barua hiyo haina ukweli wowote na siyo yeye aliyeiandika.
1
32
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla. #UmojaDigital
21
KAMATI KUU CCM YAMALIZA KIKAO MUDA HUU Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Wajumbe wa Kamati Kuu wakitoka kikaoni, baada ya kikao hicho kumalizika usiku huu.
29
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, iliyoketi leo Jumatatu, July 28, 2025, Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakitoka kikaoni baada ya kikao hicho kumalizika usiku huu.
36
Kwenye picha ni waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiendelea kusubiri Mkutano wa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla
34
Simba SC imetangaza kuachana na kiungo wake Debora Mavambo baada ya kuhudumu katika viunga vya Msimbazi kwa msimu mmoja. Mavambo anakuwa mchezaji wa 7 kuachwa katika dirisha hili la usajili baada ya Fabrice Ngoma, Nouma, Okejepha, Kijili, Manula na Hussein #umojaDigital
47
Kaptain wa Simba Zimbwe Jr baada ya kukaa Simba miaka 11 sasa aipa thank you na kuamua kutafuta changamoto nyingine nje ya Simba #UmojaDigital
21
Tanzania yapanda viwango FIFA kwa nafasi 4 juu, kutoka 107 hadi 103 #umojadigital #UmojaUpdates
1
17
Miili ya watu 42 walipoteza maisha katika ajali ya Same, iliyohusisha basi kubwa la abiria la channel one na basi ndogo coaster ya abiria kuagwa leo katika viwanjwa vya hospitali ya rufaa ya kanda KCMC. #umojadigital
1
28
#TANZIA Nyota wa Liverpool Mreno Diogo Jose da Silver ‘Diogo Jota’ amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 28 katika ajali ya gari aliyoipata akiwa Zamora nchini Spain. Taarifa kutoka nchini Spain zinasema mshambuliaji huyo amefariki akiwa sambamba na kakaake Andre Silva Nyota huyo chini ya Arne Slot ameisaidia Liverpool kubeba EPL msimu wa 2024-2025 akicheza michezo 26 huku akihusika katika mabao 9. #umojaDigital
1
219
Wakati Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda anaaihirisha mkutano na waandishi wa habari amesema , wamefanya jitihada za kuwapigia Simu Simba SC lakini katika hali isiyo ya kawaida Simu zao hazipatikani. "Simba walitakiwa kuwa hapa saa 5:30 asubuhi lakini hawajafika, kwa bahati mbaya hata kwenye simu hawapatikani na sisi hatuwezi kukaa hapa hadi saa 10 kwa sababu ratiba zingine zinatakiwa kuendelea"
49
Kihongosi achukua nafasi ya Makonda Arusha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuhamisha Kenan Laban Kihongosi kutoka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Paul Makonda. Taarifa za mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na Viongozi wengine wa ngazi mbalimbali nchini zimekuja siku chache tangu Rais Samia alipowataka Viongozi wanaotaka kwenda kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 waandike barua za kuachia nafasi za uongozi wanazozishikilia kwa sasa.
29
MUSEVENI KUWANIA TENA KITI CHA URAIS 2026 Rais wa muda mrefu wa Uganda, Yoweri Museveni, atawania tena urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka 2026, chama chake tawala kimethibitisha Museveni mwenye umri wa miaka 80, ambaye amekuwa madarakani kwa karibu miongo minne, alitarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwania muhula mwingine wa uongozi wa taifa hilo la Afrika Mashariki. Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya chama cha National Resistance Movement (NRM), chama hicho kilisema kuwa Museveni "amewasilisha nia ya kutetea nafasi ya Mwenyekiti wa NRM na kuwa mgombea urais wa chama katika uchaguzi wa 2026." Museveni, ambaye hapo awali alisifiwa kwa msimamo wake wa utawala bora baada ya kuingia madarakani kama kiongozi wa waasi mwaka 1986, ameendelea kukandamiza wapinzani kwa miaka ya karibuni na kubadilisha katiba mara kadhaa ili kujiruhusu kuendelea kugombea. Taarifa ya chama hicho imekuja wakati ambapo wapinzani wake wakuu, akiwemo mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa maarufu, Bobi Wine (jina halisi Robert Kyagulanyi), naye ametangaza rasmi nia ya kugombea urais mwaka 2026. Bobi Wine alishindwa na Museveni katika uchaguzi wa 2021, uchaguzi ambao ulighubikwa na tuhuma za udanganyifu mkubwa na matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola. Wine amekamatwa mara kadhaa, huku mwana wa Museveni na anayechukuliwa kama mrithi wake wa kisiasa, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, akitoa vitisho vya wazi dhidi yake kupitia mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kutishia kumkata kichwa. Mpinzani mwingine wa muda mrefu wa Museveni, Kizza Besigye, alitekwa mwaka jana akiwa nchini Kenya na kurejeshwa kwa nguvu Uganda, ambako sasa anakabiliwa na hukumu ya kifo kwa kosa la uhaini. Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu duniani yamepinga vikali mashtaka hayo, yakisema ni ya kisiasa. Mke wa Besigye, Winnie Byanyima, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, alisema kuwa mumewe anashikiliwa "kwa sababu za kisiasa". Aliongeza: “Anahukumiwa kwa sababu ameamua kuwania nafasi ya uongozi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia.”
1
15
Mwaka 2002, watu 281 walifariki katika ajali ya treni iliyotokea kilomita 388 kati ya stesheni za Igandu na Msagali mkoani Dodoma. Ajali hiyo ni miongoni mwa ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea barani Afrika.
19
📢 Nyota wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Pedri yupo nchini Tanzania katika hifadhi ya Tarangire inayopatikana mkoani Arusha kwa ajili ya mapumziko ya msimu uliopita. Nyota huyo hivi sasa anafanya vizuri zaidi barani ulaya kwani msimu huu ameisaidia klabu yake ya Barcelona kuchukua ubingwa wa La liga, Copa dey rey pamoja na Supercopa huku akiifikisha timu yake ya taifa ya Hispania fainali ya UEFA Nations League. Zlatan Ibrahimovic pia yupo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwaajili ya kutalii. #umojadigital
1
2
137
📢 Klabu ya Simba imepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo ya kuruhusiwa kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kufanya mazoezi ya mwisho siku ya Jumamosi Juni 14. Kikosi cha Simba kitafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Mkapa kwa ajili ya Dabi ya Juni 15 #umojadigital
1
15
🖊️ Imeandikwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, @ahmedally_ “Ni kweli kwamba Bodi ya Ligi inasimamia timu 32 za madaraja tofauti, lakini inashangaza kuona watu wakitaka ivunjwe kwa sababu ya timu moja tu! Ina maana timu 31 zifarakishwe kwa sababu ya maslahi ya timu moja? Kwa nini Bodi ya Ligi iwe na upendeleo kwa timu moja kati ya timu 32 ambazo inazisimamia? Acheni utoto. Acheni dhana ya kwamba nyie ni bora kuliko wengine. Mnaamua kucheza mpira lakini hamheshimu mamlaka wala kufuata kanuni zilizowekwa. Tunaelewa kuwa mnaungwa mkono na viongozi kutoka kada mbalimbali, lakini katika hili, ni nguvu ya soka na sheria zake zitakazoshinda. Tarehe 15 Juni ni siku ya mageuzi ya mpira wa miguu Tanzania. Hiyo ndiyo siku ambayo kila mmoja atajifunza umuhimu wa kuheshimu mamlaka za soka. Ndiyo siku tutakayomaliza utoto katika masuala ya msingi." #umojadigital
3
50