TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW) header
TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW) profile picture

Afrika kama ilivyo

Joined August 2022
Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)Photo by TRT Afrika Swahili (@trtafrikaSW)
Akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya askari na maafisa wenye kuchafua taswira ya jeshi hilo.
1
121
Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran: - Kila mtoto ana haki ya kukua kwa usawa na katika mazingira salama - Ni lazima kulinda haki za mtoto za kupata elimu, huduma ya afya, usalama na haki ya kutoa maoni - Tunapoadhimisha Siku ya Watoto Ulimwenguni, tunaomba kukomeshwa kwa mateso kwa watoto walio vitani , hasa wa Gaza
109
Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imerejea kwa kishindo kwenye Ligi Kuu ya NBC, baada ya kuifunga Polisi Tanzania, katika mchezo uliofanyika Novemba 20, kwenye uwanja wa Ushirika, mkoani Kilimanjaro. Mabao ya Yanga yalipatikana katika dakika ya 31 ya mchezo, kupitia kwa Cheikh Touré, kabla ya mshambuliaji Peter Shalulile ‘Shashaman’ kuongeza la pili, katika dakika ya 75. Ushindi wa Yanga unadhihirisha mwanzo mpya wa kocha wa Fadlu Davids ndani ya kikosi cha ‘Wananchi’, mara baada ya kuachana na Manqoba Mngqithi, mwezi uliopita.
1
2
159
Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran: - Meli ya kitafiti ya Kituruki ya Oruc Reis imewasili Pakistan kwa ajili ya shughuli yake ya pili, baada ya kukamilisha ile ya Somalia - Chombo hicho, kitakusanya taarifa za 2D na 3D kutoka maeneo mawili yaliyotengwa nchini Pakistan - Shughuli hii, inadhihirisha uwezo wa kihandisi wa Uturuki katika kukuza ushirikiano katika sekta ya nishati
145
Akizungumza Novemba 20, 2026 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi la Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, serikali yake ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kurejesha mshikamano, kuimarisha umoja wa taifa na kuweka msingi wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
55
Serikali ya Kenya televisheni kubwa nje ya uwanja wa Talanta, maarufu kama Uwanja wa Raila Odinga, ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya fainali za AFCON 2027. ‘Skrini’ hizo, zimewekwa ili kuwawezesha mashabiki wengine kutazama mechi wakiwa nje ya uwanja, inapotokea wamekosa nafasi ya kuingia ndani ya uwanja huo wa kisasa. Uwanja wa Talanta, una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 na ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika wakati wa michuano ya AFCON 2027.
98
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, amesema kuwa nchi hiyo inaongoza kwa ukuaji wa uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kulingana na Rais Samia, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa kati ya asilimia 6.3 na 6.5 mwaka 2026. Kiongozi huyo, alikuwa akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026 wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania.
1
105
Waziri wa Nishati wa Uturuki, Alparslan Bayraktar, amesema ushirikiano wa nishati kati ya Uturuki na Islamabad umeingia katika hatua mpya, huku shughuli za utafiti wa mafuta na gesi zikitarajiwa kufanyika katika vitalu vitano, viwili katika nchi kavu, na vitatu baharini. Waziri huyo alisema meli ya Oruc Reis iliwasili Pakistan baada ya safari ya siku 19 na imepewa jukumu la kufanya utafiti katika mabonde ya Indus na Makran ili kubaini uwezekano wa kuwepo kwa akiba ya mafuta na gesi. Shughuli hizo zinatarajiwa kuchukua takribani miezi miwili.
1
89
Ndugu wa wahamiaji waliopotea katika ajali ya boti karibu na pwani ya Yenne, nchini Senegal, wanaendelea kuwatafuta wapendwa wao. Boti hiyo iliyokuwa imebeba wahamiaji wanaoelekea Visiwa vya Canary vya Hispania ilizama Novemba 18, 2026, ambapo watu wanne wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa mpaka sasa hawajulikani walipo. Taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda boti hiyo ilikuwa na abiria kati ya 50 na 100. Timu za uokoaji zinaendelea na utafutaji huku mamlaka ikichunguza chanzo cha ajali hiyo. Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema takriban watu 600 wamepoteza maisha wakijaribu kwenda Visiwa vya Canary kutoka Afrika Magharibi mwaka huu,
100
Kocha wa timu ya Aston Villa Unai Emery, amekuwepo Villa Park tangu Oktoba 2022. Kufikia mwezi Machi 2026 alifanikiwa kushinda mechi yake ya 100 na klabu hiyo, licha ya msimu huu kuonekana kusuausa. Ataweza kuendeleza mikakati yake ya kuipaisha zaidi timu hiyo?
1
218
Vita vya Marekani dhidi ya Iran vimeigharimu Marekani kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola bilioni 48.3 tangu vilipoanza mwishoni mwa mwezi Februari. Hayo yalielezwa na afisa wa bajeti wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Arthur Miller, alipokuwa akitoa ushahidi mbele ya wabunge tarehe 19 Novemba. Kiasi hicho kinajumuisha gharama za operesheni za kijeshi, silaha na risasi zilizotumika, pamoja na vifaa vya kijeshi vilivyohitaji kubadilishwa. Hata hivyo, kiasi hicho hakijumuishi gharama za ukarabati wa kambi na miundombinu ya kijeshi ya Marekani katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati iliyoharibiwa na mashambulizi ya Iran.
128
Wakimbizi wa Rohingya walikusanyika siku ya Alhamisi katika kambi huko Bangladesh kufuatilia uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa iwapo mauaji yaliyofanywa na Myanmar dhidi ya Waislamu wachache mwaka 2017 ni mauaji ya kimbari. Viongozi wa Rohingya waliweka televisheni kubwa katika maeneo ya wazi ndani ya kambi, ambapo zaidi ya wakimbizi 1, 000 walifuatilia na kufurahia hukumu hiyo. Sayed Ullah ambae ni kiongozi amesema wakati Warohingya wakifurahishwa na uamuzi huo bado hawajaweza kurudi nyumbani.
1
136
Viongozi wa eneo la kusini-magharibi mwa Uganda la Kanungu wameonesha wasiwasi wa uchimbaji haramu wa dhahabu unaoendelea katika eneo hilo. Tangu kugunduliwa kwa dhahabu katika eneo hilo mapema mwaka huu, video za hivi karibuni zinaonyesha mamia ya wachimba madini katika mashimo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kanungu Francis Byamukama amesema mashimo matano ya madini yaliendelea kufuliwa licha ya marufuku ya serikali, huku watu wawili wakipoteza maisha. Julai 2026, Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda ilisimamisha shughuli za uchimbaji madini, ikisema wachimbaji hawakuwa na leseni.
1
4
308
Ndege ndogo ilianguka katika barabara kuu ya Monterrey-Nuevo Laredo huko Apodaca, Mexico, Novemba 18 baada ya kupata hitilafu katika mfumo wa umeme. Watu wote sita waliokuwa katika ndege hiyo wamesalimika kwa kupata majeraha madogo.
1
241
Uganda imeweka utaratibu mpya wa usafiri kwa abiria wa anga, mashirika ya ndege, watoaji wa huduma za usafiri na watu wanaovuka mipaka kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa Ebola. Wizara ya Afya imetangaza Novemba 19 kwamba hatua za uchunguzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe zimeimarishwa kwa abiria wote wanaowasili na wanaotoka. Wasafiri sasa watatakiwa kujaza fomu zitakazotoa taarifa za mzunguko wa wasafiri. Uganda pia imeyaonya mashirika ya ndege na watoaji wa huduma za usafiri kwamba watakabiliwa na vikwazo iwapo watakiuka maelekezo hayo. Hatua hizi zinakuja wakati ambapo Uganda inaendelea kusalia bila maambukizi ya Ebola tangu Agosti 27, baada ya kukamilisha kipindi cha lazima cha ufuatiliaji cha siku 42 bila kuripoti maambukizi mapya.
118
Wanawake ambao ni sehemu ya timu iliyopangwa kwa ajili ya kuzika walioathirika na Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wanasema wanakabiliwa na unyanyapaa kutoka kwa jamii. Mpango wa Mazishi ya Heshima na Salama (DSB) umeunda timu zinazotoka ndani ya jamii ili kushughulikia vifo vinavyotokana na Ebola, kwa lengo la kupunguza maambukizi.
2
198
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amepitisha muswada wa bajeti kwa kutumia kura yake ya turufu, licha ya kukataliwa na bunge, hatua ambayo inaonekana kuwa muhimu katika kurejesha utulivu wa hali ya kifedha ya nchi hiyo, wakati Senegal ikiendelea na juhudi za kukidhi masharti ya mkopo kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Senegal, ambayo inakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni, imeingia katika mkwamo wa kisiasa na kibajeti ambao haujawahi kushuhudiwa. Rais Faye amekuwa katika mvutano na Bunge la Taifa, ambako chama cha upinzani cha Pastef chenye idadi kubwa ya wabunge kimekuwa kikikataa mapendekezo yake kuhusu bajeti. Kiongozi wa chama cha Pastef, Ousmane Sonko, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa kisiasa wa rais lakini baadaye akageuka kuwa mpinzani wake, anapinga hatua ya kurekebisha madeni ya nchi, ambayo inahitajika katika masharti ya mkopo wa IMF.
1
4
564
Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, alimwambia aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kwamba anamuheshimu na kumsifu kwa ujasiri wake, katika mazungumzo yao ya mwisho ya simu, kwa mujibu wa nakala ya mazungumzo hayo iliyochapishwa Jumatano usiku na gazeti la Israel la The Jerusalem Post. Mazungumzo hayo ya simu yalifanyika Januari 15, 2025, wakati Israel ikiendeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Yalitokea siku tano kabla ya Biden kuondoka madarakani. Kauli hizo za Biden zinatofautiana na maelezo aliyoyatoa katika kitabu chake cha kumbukumbu, Promise Me, America, kilichotolewa Jumanne. Katika kitabu hicho, Biden anamshutumu Netanyahu kwa kuwa na “tabia zinazofanana na za Donald Trump” na kwa “kuzipindisha taasisi za kidemokrasia ili zitumikie maslahi yake binafsi.”
1
128