Mlima Sayuni retweeted
TAL!
Baada ya kukutwa na hatia aliomba kuongea na mawakili wake, tukamzunguka kila mtu akawa anampa mitigation facts,
akasema kwani hamjui wana hukumu?, tukamjibu tunajua!,
akasema nikifanya mitigation itabadili hukumu yao?, tukajibu hapana!
Akasema let me speak my mind!
Mlima Sayuni retweeted
“Mimi ni raia mwema na mzalendo wa nchi hii. Nimekuwa Mbunge mara mbili. Nimekwenda jeshini. Nimekuwa Rais wa Mawakili. Mimi sio mpiga kelele na wala mchochezi. I am a SOLID PATRIOT.” - Tundu Lissu.
Mlima Sayuni retweeted
“Today the High Court has confirmed what we have said from day one: the treason charge was a political fabrication. The prosecution failed to prove any intention to intimidate the government.
Instead of ordering my release after 577 days in detention, the court has convicted me of an offence I was never charged with and never given a chance to defend.
This is not justice. This is damage control.
History will record how the court searched for a lesser charge simply to keep me in prison.” Tundu Antipas Lissu
November 6, 2027
—Admin.
Mlima Sayuni retweeted
Huyu ndo Jaji Ndunguru ambae kamfunga Mhe. Lissu kwa agizo la Nduli Idd Amin Mama.
Incase kimuona huko kanisa au mtaani maana najua kuna watu ni jirani yenu.
Mlima Sayuni retweeted
Congratulations, comrade @TunduALissu, for defeating the trumped-up treason charges.
The conviction for “incitement” is meant to give tyrant @SuluhuSamia a pyrrhic solace.
Today is a triumph of fearlessness, focus and the truth over the culture of impunity and institutional lies.
The struggle continues.
Telling the truth is a revolutionary act.
#SocialismIsTheSolution
#RevolutionNow
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 501
Wakili wa Serikali kimsingi anasema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba 2025 yalitokana na kauli zangu kama nimemuelewa sawa sawa.
Kwenye kesi hii sina hakika kama mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Chande wala yeye hajaja kutoa ushahidi hapa kuthibitisha hizo vurugu zilisababishwa na vurugu za wanasiasa gani.
Mnaambiwa mnitolee adhabu kali kwa kosa ambalo kama lipo limefanyika kwazaidi ya miezi 6 limefanyika baadae mimi nikiwa gerezani, mkikubaliana na hoja hiyo huu utakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo.
Watu kicheko😂😂😂😂😂
Wakili wa Serikali Mkuu anataka muamini projo za mitandaoni, mkikubali utakuwa ni uthibitisho kuwa ni maagizo.
Wakili wa Serikali Mkuu amewaambia vile vile kwasasa hawana taarifa zozote kama hili ni kosa langu la kwanza, maana yake anaashiria kwamba kuna previous conviction, sasa kwavile hana uhakika mimi nitawaambia ukweli, sijawahi kutiwa hatiani na kosa lolote la jinai, wamenishtaki kwa zaidi ya miaka 24 tangu 2002 hawajawahi kunipata, I have never ever been convicted for a criminal offence, kwahiyo mnapofikiria adhabu lazima mjue kwamba mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia.
Mhe. Lissu anaendelea
Waheshimiwa majaji nafaham mnajua kwamba nina msiba mkubwa sana wa mtu aliyenilea, amenifanya mimi kuwa mwanasheria, kwasabu sikupata nafasi ya kumuuguza, nilikuwa natumaini kuwa Mahakama itaniacha niende nikamzike Mzee Alutte, I was hoping that, inaelekea kuwa hiyo haipo kwenye mahesabu yenu, mnapokuwa mnafikiria adhabu mfikirie na hilo, family obligationdls is a factor kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, Dunia nzima inajua, magazeti everywhere, I was hoping that nitapata nafasi ya kwenda kumzika huyu aliyenilea.
Waheshimiwa majaji leo ni mwaka na miezi 7 niko gerezani, mnapofikiria adhabu kali muitoe msije mkasahau kwamba huyu mtu ameshakaa gerezani kwa kosa ambalo mmelisema wenyewe kuwa sio kosa, halijathibitishwa na wala msije mkasau walichokisema jopo la Majaji watatu wenzenu: Jaji Mruma, Dkt. Longopa na Jaji Rumisha kuhusiana na niliyotendewa gerezani.
Wamesema nimenyimwa fursa ya kuwasiliana na mawakili wangu, Viongozi wenzangu wa chama halali cha Chadema, nimenyimwa fursa hata ya kuomba Mungu. Majaji wenzenu wamesema hayo yaliyotendeka nilinyimwa fursa na haki ya kujitetea, msije mkasau hayo mnapofikiria adhabu kali.
Waheshimiwa Majaji mimi ni raia mwema wa nchi hii, mzalendo wa nchi hii, nimetumikia nchi hii kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi mara 2 nimekwenda Jeshini, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hii, mimi sio mpiga kelele, I am a patriotic, ndio maana nimeona na mabalozi wako Mahakamani, wanajua mimi ni patriotic hivyo mnapofikiria adhabu msije mkasahau hoja hii.
Waheshimiwa Majaji gerezani sio mahali pazuri sana, nasema hivyo kwasababu nimeishi kwa siku 577, nakaa kwenye chumba cha sita kwa sita, sio sheraton hotel, unaweza ukasema tu funga kama hujui Gereza ni nini?
Nasema haya kwasababu mimi sio mzima sana, kwenye huu mwili wangu nina operesheni 25, visu vya madaktari, ninatembea na risasi mwilini.
Katika risasi 16 zilizoingia mwilini moja walishindwa kuitoa, ninatakiwa niwe naenda Hospital Ubeligiji, Hospital ya chuo kikuu cha Luven nilikotibiwa baada ya yaliyonikuta miaka 9 iliyopita, nimeshamiss appointment 4 kwasababu ya kesi hii, juu ya yote hayo Majaji nina kisukari huu mwaka wa 6 sasa, kwahiyo mtakapokuwa mnatafakari hiyo adhabu kali, mkumbuke hilo kwamba hali yangu ya kiafya sio nzuri sana.
Waheshimiwa majaji kosa la uchochezi mara ya mwisho nilipoangalia ni kosa lenye dhamana, kama itawapendeza Kwa vile hili kosa lina dhamana, mnipe dhamana ili nikatie uamuzi wenu huu rufaa nikiwa nje kwa dhamana lakini muhimu zaidi pia ili nikamzike huyu aliyelala (Mzee Alute), nilisema sina mpango wa kuomba ila dhamana naomba.
Part 502 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 500
Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini.
Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’ing’inia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini????
Maana yake ni nini waheshimiwa majaji?
Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini.
Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo.
Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji.
Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu,
Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili.
Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza.
Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham.
Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.
Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 498
Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic.
Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice.
Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo.
Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm.
Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger.
Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa.
Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently.
Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana.
Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi.
Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 497
Jaji Nduguru anasema, pia tunasukumwa hivyo na kifungu cha 10 cha Kanuni ya adhabu kuwa nia ya mtu lazima iambatane na matendo ya dhahiri ya mshtakiwa na sio maneno tu.
Kwa mtazamo wetu dai kwamba upande wa utetezi walifanya kwa lengo la kushinikiza Serikali kufanya mabadiliko haimaanishi ni kuwa ni kuitishia Serikali ni msimamo wetu kuwa kesi ya upande wa mashtaka imeegemea zaidi katika maoni kuwa maneno ya mshtakiwa yalilenga kuitishia serikali.
Mahakama inaamua kuwa sio lazima provocative speeches zinaweza to constitute kosa kwa maana zinalenga kuhamasiha mabadiliko hivyo sio lazima ziwe kosa la jinai.
Hatujapata ushahidi wa moja kwa moja ukiachia ushahidi wa namba 1,2 na 16 ambao ni tafsiri zao, sisi tunaona kutokuwa na ushahidi tunasema kwamba maneno hayo sio kwamba yanapelekea uhaini.
Tunajua kuwa Serikali ina wajibu wa kusimamia uchaguzi, sheria na hivyo maneno yanayo desrupt election yanaconstitute kosa la uhaini.
Hoja ya tatu na ya mwisho ambayo ni ambayo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo ya kuchochea umma kuvuruga uchaguzo kwa lengo la kuitishia serikali.
Tukiangalia ushahdi wa Jamhuri hasa namba 1,2 na 16 ambao waliegemea kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na walisema kusambazwa kwa maneno hayo kulifanywa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mshtakiwa na watu waliokuwepo kwenye mkutano huo, shahidi namba 17 alieleza kwamba matukio hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma kuhusiana na msimamo wa No reforms, No election.
Upande wa mashtaka wanaeleza kuwa kwa kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na mshtakiwa kukiri kuwa aliongea maneno hayo basi mahakama ione kuwa upande wa mashtaka umethibitisha publication hata kama hakuna picha mjongeo.
Upande wa utetezi ulieleza kuwa sio Lissu aliyesambaza maneno hayo, na kukosekana kwa video hakuna uthibitisho kuwa Lissu alichapisha.
Tunakubaliana na Lissu kuwa hakuna ushahidi kuwa yeye ndio alichapisha na kusambaza hayo maneno kwenye YouTube ya Jambo TV.
Kitendo cha kuonekana tu kwenye Jambo TV sio lazima kuwa Tundu Lissu ndiye aliyepandisha kwenye Jambo TV.
Tumeona kwamba upande wa mashtaka wamethibitisha kwamba kauli hiyo ilitolewa na mshtakiwa, na kuwa ilisambazwa na mshtakiwa alitoa hotuba hiyo katika umma sio kwa kificho hivyo kauli za mshtakiwa hazikuwa kauli za siri.
Mahakama hii inaona kwamba kauli hizo kupandishwa kwenye mtandao wa Jambo TV haimaanishi kuwa Lissu ndiyo aliyepandisha.
Hivyo basi kutothibitisha uhusika wa Lissu kuchapisha maneno hayo kwenye Jambo TV upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha element za kosa. Kwa kitendo cha kutokutolewa video clip does not defeat ushahidi wa mdomo ambao ulitolewa na shahidi wa 17 ambaye alikuwepo na mshtakuwa hapingi maneno hayo.
Kutokana na ushahidi uliopo, upande wa mashtaka hawajatupa ushahid kuwa Lissu alilenga kutenda kosa la uhaini.
Failure kuleta ushahidi hoja ya tatu inakuwa pia haina mashiko, treason per see kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) haijathibitishwa na kifungu hiki hakina minor offence lakini ni jukumu la ku evaluate ushahidi na kuona kama kuna kosa dogo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 319(1-2) cha CPA kinaelekeza mahakama kwamba inaweza to substitute kosa pale ushahidi unapoonyesha kwamba kunaweza kuwa na kosa dogo.
Part 498 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 495
Suala la uhalali wa hati ya mashtaka liliwahi kulalamikiwa mwanzoni mwa shauri hili na Mshtakiwa na katika uamuzi wake wa Sept 2025 ilieleza kuwa hati ya mashtaka ilikuwa sahihi.
Mshtakiwa alisema kuwa Kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji kushawishi kikundi cha watu na sio umma kama ilivyoandikwa hivyo alisema hati hiyo inakinzana na Ibara ya 13 ya Katiba ya Tanzania inayohusu uhalali wa kisheria (principal of legality)
Katika pingamizi la pili alisema upande wa mashtaka haukueleza taasisi ya serikali ambayo anadaiwa kuitishia na katika hoja ya tatu mshtakiwa alisema haijasema nia au lengo la kufanya huo uhaini kwasababu pia maneno ambayo hayajatumika katika sheria hivyo alisema mahakama ione hati ina mapungufu
Upande wa mashtaka walikiri kuwa ni kweli hati ya mashtaka imetumia neno public lakini tafsiri ya neno public kinajumuisha mtu yeyote au kikundi cha watu hivyo walikidhi matakwa ya sheria, katika hoja ya pili walisema hati ya mashtaka imetumia neno executive.
Upande wa mashtaka walieleza kuwa majukumu ya Executive ni kutekeleza sheria hivyo mshtakiwa alikuwa anaelewa maana ya neno Serikali na hivyo aliweza kuelewa na kutoa utetezi wake.
Mahakama inaona kwamba mapingamizi ya mshtakiwa kuhusu hati ya mashtaka hayana mashiko kwasababu ilishatolea uamuzi huko nyuma na inamaelezo ya kutosha.
Neno public katika tafsiri ya kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu kinazumzia mtu yeyote au kikundi cha watu, tumeangalia pia kwa umakini ushahidi na utetezi hivyo mshtakiwa alielewa hati ya mashtaka.
Maelezo katika hati ya mashtaka yanajitisheleza kabisa na kwa mujibu wa shauri la Nasibu Mahakama inatakiwa kutumia neno kama lilivyo hivyo neno executive linaeleweka kama lilivyotajwa kwenye hati ya mashtaka.
Katika hoja ya tatu tunakubaliana kuwa upande wa mashtaka lazima waeleze nia mahususi kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), hivyo tunaona kwamba mapingamizi yote hayana mashiko kwasababu tulishayatolea uamuzi.
Kinachofuata sasa ni kuangalia viini vitatu, viini hivyo ni-;
1. Endapo mshtakiwa yuko chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d).
Ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha hili, pande zote mbili wanakubaliana kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT.
Hata katika usikilizwaji wa hoja za awali mshtakiwa alikubali kuwa alikuwa na utii wa JMT ni mzaliwa wa Tanzania, ana pasipoti ya Tanzania na 3/4/2025 alitoa maneno hayo akiwa ndani ya JMT, Mahakama inaona kwamba mshtakiwa alikuwa na utii wa JMT.
2. Kiini cha pili ni endapo mshtakiwa alitenegeneza nia ya kuhamasisha umma kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali kinyume na kifungu cha 39(2)(d).
Upande wa mashataka wana wajibu wa kuthibitisha nia hiyo tofauti na political criticism, nia ni internal state of mind na lazima kifafanuliwe na ushahidi, matendo ya mshtakiwa.
Upande wa mashtaka waliegemea kwenye hoja kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alisema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, tutauvuruga uchaguzi, upande wa mashtaka waliegemea kuwa mshtakiwa alikuwa na nia ya kuitishia Serikali na waliegemea kwa upande wa ushahidi wa mashahidi wao kuwa mshtakiwa ni mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya Tanzania.
Upande wa Jamhuri waliegemea upande wa ushahidi wa shahidi wa kwanza ambaye aliona maneno hayo yanaviashiriia vya uhaini.
Shahidi alieleza kuwa mshtakiwa kutoa maneno hayo mbele ya waandishi wa habari na kusambazwa maneno hayo, mshtakiwa alikusudia kuitishia serikali.
Shahidi wa 16 upande wa mashtaka alieleza kuwa alipoona hayo maneno walipanga kuwapiga mawe wapiga kura, shahidi wa 17 alisema alikuwepo kwenye mkutano na kuwa ulirushwa live kwenye mitandao ya kijamii, alisena maneno aliyotamka Lissu hakuona kama yanashida yoyote ile.
Part 496 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 6, 2026
Last time tuliishia part 493 so leo tunaendelea na -;
Part 494.
Karani amewasha kipaza sauti kutoa Tangazo kuwa watu wakae kwenye viti vyao na simu zao wahakikishe zinatolewa sauti na milio ya aina yote.
Waandishi wa Habari na wao wako wakutosha sijawahi kuwaona Mahakamani kwenye kesi yoyote wakiwa wa idadi hii ni wengi sana sana.
Hata waandishi ambao huwa hawajagi kabisa naona wamekuja, namuona yule Charles William wa Wasafi nae leo yupo kuna mtiti hapa unataka kutokea, wanataka kumnyayua Mzee Mpoki alienda kukaa viti vya Mawakili wa Serikali 😂😂😂
Wale watoto wa serikali ambao huwa wanakaa kwenye benchi la nyuma ya akina Katuga, leo wamekaa mawakili wa Mhe. wabishi hatari wamegoma kusimama.
Ameingia Mheshimiwa Lissu akiwa na vibe na kusema TUTAFIKA! TUTAFIKA! TUTAFIKA!
Wameingia Mawakili wa Serikali.
MAJAJI walikwisha ingia hata kabla Mawakili wa Serikali hawajaingia.
Muda huu wanawasha zile mic zao ili tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema karani tuendeleeee.
Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasoma namba ya shauri karani.
Anasimama Katuga anajitambulisha niko na wenzangu Job Mrema, Cathbert mbiringe ba Winniwa Kasala
Tunaiwakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri linakuja kwa ajili ya uamuzi na upande wa Jamhuri tuko tayari.
Mshitakiwa vipi wewe?
Mheshimiwa Lissu anasema niko tayari pia.
Majaji Wanateta pale kabla hawajaanza kuusoma huo uamuzi.
Jaji Ndunguru anasoma, naomba tusikilize Hukumu.
Katika shauri hili Mshitakiwa Tundu Lissu anashitakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)d kanuni ya Adhabu 2023.
Maelezo yanasema kwamba Tarehe 03/04/2025 Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam mshitakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Kudhihirisha nia hiyo kwa kitendo cha kutamka maneno ya wanasema kitu kimoja sahihi kwamba msimamo huu unaashiria uasi na tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kuleta mabadiliko na huu uchaguzi tutauvuruga.
Mshitakiwa alikana hati ya mashitaka na shauri likaanza kusikilizwa.
Kama ilivyo kawaida upande wa Mashitaka waliongozwa na Wakili Renatus Mkude na Ajuaye Zengeli na Nasoro Katuga na anawataja Mawakili wote wa Serikali.
Upande wa Mashitaka walileta mashahidi 17 na ambao kati yao 17 walikuwa ni mashahidi wanaolindwa.
Na mshitakiwa alijiwakilisha Mwenyewe na alileta Mashahidi wanne na yeye alikuwa watano na pia utetezi walitoa vielelezo anbavyo ni 16.
Baada ya upande wa mashitaka kutoa ushahidi na mshitakiwa alijitetea na walileta hoja za majumuisho walileta hoja hizo.
Mahakama hii iliongozwa na kanuni mbalimbali ni
1. Katika Mashauri ya Jinai mwenye jukumu la kuthibitisha ni Upande wa Mashitaka.
2. Kutiwa hatiani kwa mshitakiwa hakutazingatia udhaifu wa mshitakiwa.
3. Ushahidi utatazamwa kwa ujumla wake na sio vipande.
4. Mashaka yoyote hata kama yana uzito kiasi gani hayabadilishi burden ya kuthibitisha shitaka.
Mahakama hii imechunguza kwa umakini hati ya mashtaka, ushahidi na mawasilisho ya pande zote mbili na kuja viini vitatu vya kuthibitisha
Moja: Iwapo Mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT
Mbili: Iwapo Mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali.
Tatu: Iwapo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kusambaza maneno hayo.
Mahakama imeona ni vyema ifafanue kwanza katika hoja ambazo zinaonekana kama mapingamizi wakati wa hoja za majumuisho ya mshtakiwa.
Kwa kuwa hati ya mashtaka ndio inayoanzisha shauri la jinai ni vyema tuamue kwanza kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka. Mshtakiwa alisema hati ya mashtaka ina mapungufu katika maeneo matatu moja kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kinazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu, pili hati ya mashtaka haikutoa taarifa muhimu ambazo zilipelekea ashindwe kutoa utetezi kamili na tatu hakuna lengo lilioonyeshwa katika hati ya mashtaka.
Part 495 itaendele kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Mlima Sayuni retweeted
Wakoloni WEUSI mnajiona mpo salama sana sasa mnapopambwa na CHAWA wenu.
Kiuhalisia hamuwezi kuuwa watanzania kwa maelfu mkabaki SALAMA never.
Ni suala la muda tuu.
Thanks Denmark🙏
Mlima Sayuni retweeted
‼️UJUMBE KUTOKA GEREZA LA UKONGA‼️
Anaandika @Advocate_Kisabo
Nimetoka Ukonga kuzungumza na Mhe. Lissu, he is fine na anawasalimia wote, amesema
"I remain optimistic about tomorrow but am also prepared for the worst, so if the best comes, I will go straight to Arusha to take my brother home. If the worst happens, then the struggle will continue. It will not be the end of the world; it will just be a new chapter in the struggle for justice and democracy in this country" akaongezea kuwa I am sustained by the line of a famous Kenyan freedom fighter Koigi wa Wamwere who authored the autobiography I Refuse to Die: My Journey for Freedom na Mhe. Lissu amemalizia kuwa TL insoumiese "
Mlima Sayuni retweeted
‼️ALERT‼️
Nimejulishwa na mmoja wa Wanahabari kwamba kesho Waandishi wa habari wa Dar es salaam wameitwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kuahidiwa kupewa Tsh 100,000 kila mmoja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salam imetangaza kununua front page za magazeti ambayo yako willing kuwauzia na mpaka sasa kuna magazeti kadhaa tayari yamefikiwa so wanaendelea kunegotiate na magazeti mengine.
Lengo la kufanya haya yote ni ili Magazeti na Media zote nchini yasiipe uzito Hukumu ya kesi ya mchongo ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu ambayo itasomwa kesho asubuhi.
#FreeTunduLissu
Mlima Sayuni retweeted
Replying to @HildaNewton21
Magazeti yanasomwa na nani nchi hii, sisi wagalatia tunakusoma wewe, updates zako tunaziforward na zinapaa kama moshi wa ubani.
Mlima Sayuni retweeted
🚨 UJUMBE WA MHE LISSU LEO KUELEKEA HUKUMU YAKE KESHO.
Anaandika wakili KISABO.
Nimetoka Gereza la Ukonga kuzungumza na Mhe. Tundu Lissu. Yuko salama na anawasalimia wote.
Mhe. Lissu amesema:
"Bado nina matumaini makubwa kuhusu kitakachotokea kesho, lakini pia nimejiandaa kukabiliana na hali mbaya zaidi.
Ikiwa mambo yatakwenda vizuri, nitaelekea moja kwa moja Arusha kumchukua ndugu yangu na kumrudisha nyumbani.
Lakini ikiwa mambo yatakwenda vibaya, basi mapambano yataendelea.
Huo hautakuwa mwisho wa dunia. Itakuwa ni mwanzo wa sura mpya katika mapambano ya kudai haki na demokrasia katika nchi hii."
Akaongeza:
"Ninaendelea kupata nguvu na moyo wa kupambana kupitia kauli ya mpigania uhuru maarufu wa Kenya, Koigi wa Wamwere, ambaye aliandika kitabu cha historia ya maisha yake kinachoitwa I Refuse to Die: My Journey for Freedom, yaani Ninakataa Kufa: Safari Yangu ya Kupigania Uhuru."
Mhe. Lissu amemalizia kwa kusema:
"TL INSOUMIS" — TUNDU LISSU HASALIMU AMRI!
#FreeTunduLissu
Mlima Sayuni retweeted
Kesho Novemba 6 nchini Tanzania ni Siku ya Tundu Antipas Mughwai Lissu (TAL Day). Kwa jinsi Mahakama Kuu itakavyotoa uamuzi/hukumu juu ya mashitaka ya uhaini yanayomkabili Lissu, ndiko kutakavyochagiza uamuzi wa RAIA Ni SiSi kuadhimisha SIKU YA LISSU kila mwaka au la, miaka yote
Mlima Sayuni retweeted
Rule of law: @IG_NPS 🇰🇪 in court
Sasa ukija 🇹🇿Lissu alitaka IGP afike kama shahidi akagoma na mahakama inamkodelea tu mi macho 🚮
Ila mnaoendesha nchi kama kiosk ya kimama chenu zamu yenu inakuja na mtatamani kungekuwepo na rule of law
Eniwei #FreeTwahaMwaipaya
We need him safe and alive!

















