NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe: 23/10/2026
SOMO: MUHESHIMU MUNGU ILI AKUHESHIMISHE
Mithali 8:18- 21 "Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao."
Neno linasema UTAJIRI na HESHIMA viko Kwake. Ukiona watu wanaheshimika unapaswa kutambua kuwa ni Mungu amewapa huko kuheshimika, vyote unavyohangaikia huku duniani Mungu anavyo na Yeye humpa yule amtakaye. Ukitaka kutambua hilo soma habari za mfalme Nebukadreza; yeye alikuwa mfalme aliyebarikiwa sana lakini hakumuheshimu Mungu, vyote alivyokuwa navyo alijua amevipata kwa nguvu zake, Mungu akampeleka porini kwa miaka 7 akala majani na matunda kama mnyama, mvua na jua vikampiga baada ya miaka 7 Mungu akamrudishia ufahamu wake.
Kwa muda wa miaka 7 aliyokaa porini hakuna aliyechukua mali zake wala hapakuwa na Mfalme mwingine aliyechukua nafasi yake. Ukishindwa kumuheshimu Mungu na YEYE kamwe hatakuheshimisha, usifikiri kila ulichonacho leo hii ni kwa nguvu na uweza wako, la! Acha kiburi, ukila na kushiba acha kunyanyua mabega na kusema bila wewe hakuna kinachowezekana, muheshimu Mungu aliyekupa vyote na YEYE atakuheshimisha.
PAROLE DU JOUR
Par lâApĂŽtre et ProphĂšte JosĂ©phat Ălias Mwingira- d'Ăglise Ephata
Date : 23/10/2026
THĂME : HONOREZ DIEU AFIN QUâIL VOUS FAIS ĂTRE HONORER
Proverbes 8:17-21 : "Jâaime ceux qui mâaiment, et ceux qui me cherchent avec diligence me trouveront. Avec moi sont la richesse et lâhonneur, les biens durables et la justice. Mon fruit est meilleur que lâor, oui, que lâor fin, et mon produit est prĂ©fĂ©rable Ă lâargent de choix. Je marche dans la voie de la justice, dans les sentiers de lâĂ©quitĂ©, pour faire hĂ©riter des biens Ă ceux qui mâaiment et pour remplir leurs trĂ©sors."
La Parole dit que la RICHESSE et lâHONNEUR sont auprĂšs de Lui. Lorsque vous voyez des personnes qui jouissent dâune grande considĂ©ration, sachez que câest Dieu qui leur a accordĂ© cet honneur. Tout ce que vous recherchez ici-bas appartient Ă Dieu, et Il lâaccorde Ă qui Il veut. Pour bien comprendre cela, pensez Ă lâhistoire du roi Nebucadnetsar. CâĂ©tait un roi richement bĂ©ni, mais il a manquĂ© dâhonorer Dieu ; il croyait que tout ce quâil possĂ©dait Ă©tait le fruit de sa propre force. En consĂ©quence, Dieu lâa envoyĂ© dans le dĂ©sert pendant sept ans, oĂč il a vĂ©cu comme une bĂȘte se nourrissant dâherbe et de fruits, exposĂ© aux intempĂ©ries jusquâĂ ce que, aprĂšs ces sept annĂ©es, Dieu lui rende la raison.
Durant ces sept annĂ©es passĂ©es dans le dĂ©sert, personne nâa pris ses richesses, et aucun autre roi nâa usurpĂ© sa place. Si vous ne parvenez pas Ă honorer Dieu, Il ne vous honorera jamais. Ne vous imaginez pas que tout ce que vous possĂ©dez aujourdâhui est le rĂ©sultat de votre propre force ou de votre puissance â certainement pas ! DĂ©barrassez-vous de votre arrogance ; lorsque vous ĂȘtes rassasiĂ©s, ne faites pas preuve dâorgueil et ne prĂ©tendez pas que rien ne serait possible sans vous. Honorez Dieu, qui vous a tout donnĂ©, et Il vous honorera en retour.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI IJUMAA YANGU.
YESU ameniweka HURU; adui zangu wote wamewekwa chini ya Miguu YANGU. Mimi ni Mshindi, Mimi Nimebarikiwa na BWANA.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe 22/10/2026
SOMO: UPONYAJI KUTOKA MAWAZO MABAYA
Warumi 1:28 "Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa."
Unahitaji uponyaji katika mawazo yako; uponyaji huu unahusu mtu aliyepitia maisha mabaya ya uovu ambayo yamesababisha akili yake iharibiwe na mawazo hayo. Siku zote mtu wa aina hii huwaza mawazo mabaya na hali hii huvuta ghadhabu ya Mungu juu yake.
Maisha ya mtu mwenye mawazo mabaya na aliyekataa kuwa na Mungu katika fahamu zake, huwa mabaya kwa sababu hutembea katika hasira ya Mungu wakati wote na anapatwa na majanga mbalimbali na huwa hafikii mwisho mwema. Watu wa aina hii wamejaa husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya, husengenya na husingizizia.
Mwanangu unahitaji Neno la Mungu likuponye ili utoke kunako mawazo mabaya, ruhusu Neno la Mungu lijae ndani yako kwa wingi na wakati wote tafakari Ukuu wa Mungu ili kuruhusu mawazo mazuri katika akili yako ili kuweza kuiponya akili yako kutoka katika mawazo mabaya.
Zaburi 107:19-21 "Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya na shida zao. Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu."
WORD OF THE DAY
By Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church
Date: 22/10/2026
MESSAGE: HEALING FROM EVIL THOUGHTS
Romans 1:28
âAnd even as they did not like to retain God in their knowledge, God gave them over to a reprobate mind, to do those things which are not convenient.â
You need healing in your thoughts. This healing concerns a person who has gone through a sinful and evil lifestyle that has caused their mind to be corrupted by those thoughts. Such a person constantly thinks evil thoughts, and this condition brings the wrath of God upon them.
The life of a person who has evil thoughts and has rejected God in their knowledge becomes miserable because they live under the wrath of God at all times. They experience various calamities and do not come to a good end. Such people are full of envy, murder, strife, deceit, malicious intentions, gossip, and slander.
My child, you need the Word of God to heal you so that you can come out of evil thoughts. Allow the Word of God to dwell richly within you, and continually meditate on the greatness of God. This will allow good thoughts to fill your mind and enable you to heal your mind from evil thoughts.
Psalm 107:19â21
âThen they cry unto the LORD in their trouble, and he saveth them out of their distresses. He sent his word, and healed them, and delivered them from their destructions. Oh that men would praise the LORD for his goodness, and for his wonderful works to the children of men!â
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.
YESU ameniweka HURU; Mimi Nimebarikiwa. Kwangu hakutapungua Kicheko, Sherehe, Furaha, Tafrija, Karamu na Utele.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe 21/10/2026
SOMO: IMANI INAKUPA KUPOKEA
Marko 5:25-34 âNa mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitaponaâŠâŠâŠ..â
Huyu mwanamke aliyetokwa na damu hakuwa na msaada wowote kutoka kwa marafiki zake, mume wala watoto, alikuwa hana tumaini, alikuwa mpweke kwa muda wa miaka kumi na mbili; madaktari walifanya udaktari wao lakini hakupona.
Mwanamke huyu alikuwa katika uhitaji mkubwa kwa sababu alitumia fedha zake zote kwa ajili ya kujitibia, kwake hakukuwa na kilichosalia bali Imani yake kwa Mungu pekee. Lakini siku moja alisikia kelele ndipo akauliza ni kelele za nini? Akaambiwa Yesu anapita huyu mwanamke alijadili katika nafsi yake, akajiambia âlazima uamke maana hii ni nafasi pekee uliyonayo na ukiikosa utakufa na ukiipata utaishi.â
Ndipo mwanamke huyu aliamua kuchukua hatua ya kumwendea Yesu kwa sababu alikuwa amechoshwa na hali yake, akijiambia âkama nikifa basi nitakufa nikiwa najaribu kuishiâ ndipo akachukua hatua ya kumwendea Yesu na kwa kupitia Imani yake akaponywa, Yesu hakumwombea yule mwanamke bali kwa Imani na neno la yule mwanamke lilimfanya yeye apokee uponyaji wake.
Inatosha kusema kuwa una Imani, sasa ni wakati wako wa kutendea kazi Imani yako, maneno yoyote unayotamka katika Imani mara zote yanawezeshwa na Mungu ili yapate kutimia kwa sababu Imani inatoka juu kwa maana hiyo unapotamka kwa imani unaiamrisha mbingu ishuke na kutendea kazi lile neno ulilolitamka.
Kama unataka kuona miujiza kwa haraka tamka neno kwa imani utapata muujiza kwa haraka zaidi ya kuomba.
WORD OF THE DAY
By Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church
Date: 21/10/2026
MESSAGE: FAITH ENABLES YOU TO RECEIVE
Mark 5:25â34
âAnd a certain woman, which had an issue of blood twelve years, and had suffered many things of many physicians, and had spent all that she had, and was nothing bettered, but rather grew worse, when she had heard of Jesus, came in the press behind, and touched his garment. For she said, If I may touch but his clothes, I shall be wholeâŠâ
This woman who had been bleeding had no help whatsoever from her friends, husband, or children. She had no hope and had been lonely for twelve years. The doctors had done what they could as medical practitioners, but she was not healed.
This woman was in great need because she had spent all her money trying to treat herself. Nothing was left for her except her faith in God alone. But one day, she heard a commotion and asked what the noise was about. She was told that Jesus was passing by. This woman reasoned within herself and said, âYou must get up, because this is the only opportunity you have. If you miss it, you will die, but if you seize it, you will live.â
Then this woman decided to take action and go to Jesus because she was tired of her condition. She told herself, âIf I die, then I will die while trying to live.â So, she took the step of going to Jesus, and through her faith, she was healed. Jesus did not pray for the woman; rather, the faith and words of the woman enabled her to receive her healing.
It is enough to say that you have faith; now it is time for you to put your faith into action. Whatever words you speak in faith are always empowered by God so that they may come to pass, because faith comes from above. Therefore, when you speak in faith, you command Heaven to come down and act upon the word you have spoken.
If you want to see miracles quickly, speak a word in faith, and you will receive your miracle more quickly than through prayer.
PAROLE DU JOUR
Par lâApĂŽtre et ProphĂšte JosĂ©phat Ălias Mwingira- d'Ăglise Ephata
Date : 21/10/2026
THĂME : LA FOI VOUS PERMET DE RECEVOIR
Marc 5:25-34
« Or, il y avait une femme atteinte dâune perte de sang depuis douze ans. Elle avait beaucoup
souffert entre les mains de plusieurs médecins, avait
dĂ©pensĂ© tout ce quâelle possĂ©dait sans aucun soulagement, son Ă©tat ayant mĂȘme empirĂ©. Ayant entendu parler de JĂ©sus, elle sâapprocha par derriĂšre, au milieu de la foule, et toucha son vĂȘtement. Car elle se disait : âSi je peux seulement toucher ses vĂȘtements, je serai guĂ©rieââŠâŠâŠ.. »
Cette femme, qui souffrait dâune perte de sang, ne bĂ©nĂ©ficiait dâaucun soutien â ni de la part dâamis, ni dâun mari, ni dâenfants. Sans aucun espoir, elle a vĂ©cu dans lâisolement pendant douze ans. Les mĂ©decins ont fait tout leur possible, mais elle nâa pas Ă©tĂ© guĂ©rie.
Elle se trouvait dans un Ă©tat de profonde dĂ©tresse, ayant dĂ©pensĂ© tout son argent en traitements mĂ©dicaux ; il ne lui restait plus rien, si ce nâest sa foi en Dieu. Puis, un jour, entendant de lâagitation, elle a demandĂ© ce qui se passait. On lui a rĂ©pondu que JĂ©sus passait par lĂ . Elle sâest dit en elle-mĂȘme : « Il faut que tu te lĂšves, car câest ta seule chance ; si tu la laisses passer, tu mourras, mais si tu la saisis, tu vivras. » Cette femme a pris la dĂ©cision de sâapprocher de JĂ©sus, car elle Ă©tait Ă©puisĂ©e par sa situation, se disant : « Si je dois mourir, autant mourir en essayant de vivre. » Elle a pris lâinitiative dâaller vers JĂ©sus et, grĂące Ă sa foi, elle a Ă©tĂ© guĂ©rie. JĂ©sus nâa pas priĂ© pour elle ; câest sa propre foi â exprimĂ©e par ses paroles â qui lui a permis de recevoir sa guĂ©rison.
Il ne suffit pas de dire que lâon a la foi ; le moment est venu de mettre cette foi en action. Toute parole prononcĂ©e dans la foi est investie par Dieu du pouvoir de sâaccomplir, car la foi vient dâen haut. Par consĂ©quent, lorsque vous parlez avec foi, vous ordonnez au ciel de descendre et dâagir en accord avec les paroles que vous avez prononcĂ©es. Si vous souhaitez voir des miracles rapidement, prononcez une parole dans la foi ; vous connaĂźtrez un miracle bien plus vite que par la priĂšre seule.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATANO YANGU.
YESU ameniweka HURU; Mimi ni Mmiliki, na Nitamiliki pamoja na Wamiliki. Mimi ni Mtawala.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMANNE YANGU.
YESU ameniweka HURU; Familia yangu itakuwa na Amani, kwetu kutakuwa Kwema, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo, wala ukata. YESU ameniweka HURU.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe 19/10/2026
SOMO: MAISHA YA WOKOVU
Wokovu ni Maisha yanayojumuisha mambo matatu muhimu ambayo ni UTAKATIFU, NENO na MAOMBI.
Maisha hayo huhitaji mtu kukagua matendo yake kama yanamwezesha kufanya mapenzi ya Mungu na kutimiza kusudi la kuumbwa kwake. Maisha hayo siyo ya lawama bali ni ya UTAKATIFU, TOBA na UTAKASO. Mara nyingi katika maisha yetu watu hutenda dhambi kwa kujua au kwa kutokujua. Kila siku kuna mambo tunayachukulia kiurahisi japokuwa yana madhara makubwa katika Wokovu wetu na ndio maana tunahitaji kufanya toba kila mara.
Mtu anaweza asitende dhambi lakini ni rahisi kujinajisi mwenyewe kupitia vyakula, vinywaji na maneno yake. Wana wa Israel walishindwa kuingia katika nchi ya ahadi kwa sababu walijinajisi kwa maneno yao wenyewe, watu wengi leo hii wameshindwa kupokea baraka zao kwa sababu ya kujinajisi wenyewe kwa kupitia mawazo, maneno na hata matendo yao wenyewe.
Hivyo basi, tunapaswa kuwa makini ili tusijinajisi na hatimaye kushindwa kutimiza kusudi la Mungu kwetu ambalo litapelekea kushindwa kupokea yale ambayo Mungu ametukusudia katika maisha yetu. Ukikubali kuokoka basi ukubali kuishi maisha ya Utakatifu, Toba na Maombi wakati wote ili kulinda wokovu wako.
WORD OF THE DAY
By Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira, Efatha Church
Date: 19/10/2026
MESSAGE: THE LIFE OF SALVATION
Salvation is a life that encompasses three important things, which are HOLINESS, THE WORD, and PRAYER.
This kind of life requires a person to examine their actions to determine whether they enable them to do the will of God and fulfill the purpose for which they were created. This life is not about condemnation, but rather about HOLINESS, REPENTANCE, and SANCTIFICATION. Often, in our lives, people commit sins knowingly or unknowingly. Every day, there are things we take lightly, even though they have serious consequences for our salvation. That is why we need to repent continually.
A person may not commit sin, yet it is easy to defile themselves through the foods they eat, the drinks they consume, and the words they speak. The children of Israel failed to enter the Promised Land because they defiled themselves through their own words. Many people today have failed to receive their blessings because they have defiled themselves through their own thoughts, words, and even actions.
Therefore, we must be careful not to defile ourselves and ultimately fail to fulfill God's purpose for us, which would lead to missing out on what God has destined for our lives. If you accept salvation, then you must also accept to live a life of Holiness, Repentance, and Prayer at all times in order to safeguard your salvation.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATATU YANGU.
YESU Ameniweka HURU; Mimi ni wa Mambo Makubwa. Nitafanya Mambo Makubwa Mjini, Nitafanya Mambo Makubwa Mashambani.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU.
YESU ameniweka HURU; Mimi ni Mzima, hakuna cha kunidhuru.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI IJUMAA YANGU.
YESU ameniweka HURU; maadui zangu wote wameshindwa, Mimi ni MSHINDI.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.
YESU ameniweka HURU; Sitapungukiwa na Kitu.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATANO YANGU.
YESU ameniweka HURU; Namiliki Mjini, Namiliki Vijijini.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMANNE YANGU.
Mimi na Familia Yangu TUKO HURU.
Haleluya.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.


















































