clickHabari (@clickHabari) header
clickHabari (@clickHabari) profile picture

Chanzo chako namba moja cha habari Tanzania mtandaoni, kwa lugha ya Kiswahili.

Dar es Salaam
Joined November 2015
Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)Photo by clickHabari (@clickHabari)
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) unaofanyika Antalya, Uturuki.
1
34
President Samia Suluhu Hassan poses for a group photo with various leaders attending the 31st Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on Climate Change (COP31) at the Antalya Expo Center in Türkiye.
1
275
Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali wanaoshiriki katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), Antalya Expo Center nchini Uturuki.
1
38
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa tuzo za msimu wa 2025/2026 zinatarajiwa kutolewa Desemba 12, 2026, jijini Arusha. Kwa mujibu wa TFF, tuzo hizo zitahusisha makundi matano ambayo ni Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, ligi nyingine pamoja na tuzo za utawala.
2
329
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo haina nia ya kumkomoa aliyekuwa Kocha Mkuu wake, Fadlu Davids, bali inachofanya ni kudai haki yake kutokana na kuchelewa kwa kocha huyo kukamilisha malipo anayodaiwa. Ahmed amesema Davids anatambua wajibu huo na tayari alikuwa ameanza kufanya malipo, lakini kutokana na kuchelewa kukamilisha, Simba imelazimika kuwasilisha suala hilo katika mamlaka za juu ili kudai stahiki zake.
3
28
1,683
Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Antalya nchini Uturuki, leo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
187
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema hakuna mbuga ya wanyama iliyouzwa, bali kinachofanyika katika hifadhi hizo ni uwekezaji unaolenga kuimarisha shughuli za uhifadhi na kuboresha huduma. Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana Mwishawa, aliyefafanua kuwa hakuna mbuga iliyouzwa, iwe ni zile zinazosimamiwa na TANAPA au zinazomilikiwa na taasisi nyingine.
1
1
4
506
Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31). Akiwa nchini humo, Rais atahutubia mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali na kushiriki kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika pamoja na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan.
1
1
2
693
Rais Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kuhusu Maridhiano ya Zanzibar, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
3
475
Waziri Mkuu: Msichangishe wagonjwa fedha za mafuta ya ‘ambulance’ clickhabari.com/waziri-mkuu-…
1
343
Wanasayansi wameonya kuwa mwaka 2026 huenda ukawa mwaka wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa duniani, kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na hali ya El Niño. Taasisi huru ya utafiti ya Berkeley Earth ya Marekani imesema ina uhakika wa asilimia 95 kuwa mwaka 2026 utavunja rekodi ya joto iliyowekwa mwaka 2024, licha ya mwaka huo kuwa unakaribia kumalizika.
2
2
154
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa China, Xi Jinping, pamoja na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuhusu namna ya kumaliza vita dhidi ya Iran pamoja na kudhibiti na kupunguza silaha za nyuklia. Trump amesema anatarajia kukutana na viongozi hao katika mkutano wa kilele wa Asia-Pasifiki (APEC), utakaofanyika jijini Shenzhen, China, Novemba 18–19 mwaka huu.
136
Wakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Paul Kisabo, amesema wameanza maandalizi na mchakato wa kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya mteja wake. Kisabo amesema wamejipanga kuhakikisha wanatafuta haki ya Lissu, akisisitiza kuwa wanaamini hana hatia.
1
2
104
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza Simba SC faini TZS milioni 5 kwa kosa la waokota mipira wa timu hiyo kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC. TPLB imesema wakati wa mchezo huo, watoto hao walionekana wakimwaga maji nyuma ya goli la timu ya Namungo, kitendo kinachoashiria imani za kishirikina.
3
285
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza faini ya TZS milioni 5 klabu ya Azam FC kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City. TPLB imesema kabla ya kuingia uwanjani kwa ajili mazoezi mepesi (warm up) aliingia mtu aliyevaa jezi ya Azam na kuanza kumwaga vimiminika kwenye mstari wa uwanja karibu na benchi la ufundi la Azam, kisha akafanya ishara ya kuita ndipo wachezaji wakaingia uwanjani.
1
288
Isaya Yunge na Charlene Ruto wamefunga ndoa leo jijini Mwanza, katika hafla iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Rais wa Kenya, William Ruto, Mama Rachel Ruto, viongozi wa serikali na wageni mbalimbali.
1
7
796
Mahakama Kuu ya Tanzania imemhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uchochezi. Hukumu hiyo imetolewa leo, Novemba 6, 2026, na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Hata hivyo, mahakama imemweleza Lissu kuwa ana haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
2
217
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imesema ushahidi wa Jamhuri haujathibitisha kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ametenda kosa la uhaini, kwamba kauli zake hazijathibitika kuwa zililenga kuitisha serikali. Hata hivyo, mahakama imemtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi.
280
Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na familia ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, wakiwa mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili.
2
448