BecaTZA (@BecaTZA) header
BecaTZA (@BecaTZA) profile picture

AWARD WINNING| JOURNALIST|SOCIAL MEDIA CONSULTANT| ASST. EDITOR| @millardayo | https://xitter.cf/t.co/hHJOhHirpG & AyoTV| MR.HABARI CHAPCHAP📲 IG,FB &TWITTER @becatza

Dar es Salaam, Tanzania
Joined June 2013
Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)Photo by BecaTZA (@BecaTZA)
BecaTZA retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es salaam, leo Novemba 13, 2026, akitokea Antalya nchini Uturuki, ambako alishiriki Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31). Rais Samia amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi. Akiwa Jijini Antalya, Rais Samia alishiriki mikutano mbalimbali ya ngazi za juu, ikiwemo iliyojadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Tanzania za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda mazingira. Aidha, Novemba 12, 2026, Rais Samia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini humo. #MillardAyoUPDATES
12
5
115
19,051
BecaTZA retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuhutubia leo, Novemba 11, 2026, Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaofanyika Antalya, Uturuki. Rais Samia yupo Antalya kushiriki mkutano huo unaofanyika kuanzia Novemba 9 hadi 20, 2026, ukiwakutanisha Viongozi wa Nchi na Serikali kutoka sehemu mbalimbali duniani kujadili na kuendeleza hatua za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa ajenda kuu za COP31 ni kuongeza upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha ustahimilivu wa sekta muhimu za kiuchumi, kuendeleza matumizi ya nishati safi, hususan nishati safi ya kupikia, pamoja na kuharakisha utekelezaji wa Mkataba wa Paris kwa kushirikisha Nchi zote, ikiwemo kuendeleza biashara ya kaboni. Katika mkutano huo, Tanzania na Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) zinatarajiwa kusaini makubaliano yatakayoweka msingi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mikutano mbalimbali ya UNFCCC itakayofanyika barani Afrika. #MillardAyoUPDATES
7
6
1
44
8,700
BecaTZA retweeted
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili leo, Novemba 10, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Antalya nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31). Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Rais Samia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Antalya kesho, Novemba 11, 2026, kabla ya kufungua kikao cha Viongozi wa Afrika kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Novemba 12, 2026. Kikao hicho kimeandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na Uturuki, Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) na Clean Cooking Alliance, kikilenga kuimarisha ushirikiano na uwekezaji katika matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika. Katika mkutano huo, Tanzania inalenga kuhamasisha upatikanaji wa fedha za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo mafuriko na ukame, huku takribani Dola za Marekani milioni 20 zikielezwa kutengwa kwa Tanzania kupitia Mfuko wa Hasara na Uharibifu. #MillardAyoUPDATES
1
3
46
10,531
a canary trap
24
17
99
15,757
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameanza ziara maalum ya siku nne katika Klabu ya FC Barcelona nchini Hispania kwa mwaliko wa Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta. Makonda ameanza ziara hiyo tarehe 14 Septemba 2026 kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka nchini Tanzania. Mazungumzo hayo yalijikita katika maeneo ya kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi, uendeshaji wa timu ya taifa, pamoja na namna uzoefu wa Barcelona unavyoweza kusaidia maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Barcelona inatambulika duniani kwa mfumo wake wa kukuza na kuendeleza vipaji vya wachezaji, jambo linaloifanya kuwa miongoni mwa klabu zinazotumika kama mfano katika maendeleo ya soka la kisasa. Aidha, sehemu kubwa ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania iliyotwaa Kombe la Dunia 2026 wametokea FC Barcelona. Katika ziara hiyo, Rais Laporta pia amempatia Makonda salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea tarehe 7 Septemba 2026. Laporta amemkabidhi Makonda barua maalum ya rambirambi kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia, akimtaka aendelee kuwa na moyo wa subira na ujasiri katika kipindi hicho cha majonzi. Makonda akiwa ameambatana na Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), anatarajiwa kushuhudia mchezo kati ya Barcelona na Racing Santander utakaochezwa tarehe 16 Septemba 2026 katika Uwanja wa Camp Nou, jijini Barcelona, akiwa na mwenyeji wake Joan Laporta, Rais wa FC Barcelona.
1
46
💪💪
Ladies and gentlemen, this is the President of Botswana who got irritated with his ministers. He calls a spade a spade without curtains. You can say let me hear the president is speaking...
63
BecaTZA retweeted
BARUA YA WAZI KWA JOKATE MWEGELO 🇹🇿 Dear @jokateM , Kuna nyakati ambazo mtu mmoja anapofanikiwa, tunapaswa kusimama kidogo na kusema: “Hii ni yetu.” Leo ni moja ya nyakati hizo. Kuwekwa kwako kwenye jalada la UncutXtra la Uingereza Toleo la 23 – Entrepreneurship Edition si tu habari ya wewe kuonekana kwenye cover ya jarida la kimataifa. Ni zaidi ya picha. Ni simulizi ya safari, uthubutu, nidhamu na maono ya mwanamke Mtanzania anayezidi kuvuka mipaka. Na jambo moja limevutia zaidi “Beyond the Crown.” Kwa sababu ukweli ni kwamba, Jokate, safari yako haiwezi kufupishwa kwenye taji la ulimbwende ulilowahi kuvaa. Taji lilikuwa mwanzo tu. Kilichokuja baada yake ni ujasiriamali, uongozi, ubunifu, utumishi wa umma, kujenga taasisi, kuhamasisha vijana na kuendelea kujitengenezea nafasi katika maeneo ambayo wengi hawakutarajia. Na sasa jina lako limewekwa pamoja na majina makubwa yaliyowahi kuangaziwa na UncutXtra. Hii ni hatua kubwa. Lakini zaidi ya yote, ni ukumbusho kwamba Tanzania ina watu wenye uwezo wa kubeba simulizi yetu mpaka kwenye majukwaa makubwa ya dunia. Jokate, tunakupa maua yako kabla ya siku moja isiyo na jina ukatangulia. 💐 Si kwa sababu kila kitu kwenye safari yako kilikuwa rahisi, bali kwa sababu uliendelea kusonga. Kutoka kwenye ulimwengu wa urembo, ukaingia kwenye biashara, ukaingia kwenye uongozi, ukagusa utumishi wa umma, na leo unaendelea kujenga simulizi ambayo kizazi kijacho kitaweza kuitazama na kusema: “Inawezekana.” Hongera sana Jokate Urban Mwegelo. Kutokea kwako kwenye jarida hili kwa namna fulani, imebeba pia bendera ya Tanzania. 🇹🇿 Endelea kuthubutu. Endelea kuvuka mipaka. Na zaidi ya yote, endelea kutukumbusha kwamba taji la ulimbwende linaweza kuwa mwanzo wa safari, lakini kinachomfanya mtu akumbukwe ni kile anachofanya baada ya kulivaa. Congratulations, Jokate. Beyond the Crown indeed. ❤️🇹🇿 Naitwa Chapo255 THE WALKING MEDIA
13
22
2
102
22,934
BecaTZA retweeted
If you look at the people in your circle and don't get inspired, then you don't have a circle, you have a cage….
2
2
287
If you look at the people in your circle and don't get inspired, then you don't have a circle, you have a cage….
2
2
287
Paris, France 📍
2
2
1
12
1,764
BecaTZA retweeted
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ametoa wito kwa Serikali kupitia kwa DPP kufuta kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, akisema kesi hiyo ni ya uongo huku akisema tayari kampeni za kupaza sauti ili Lissu aachiwe zimeanza ndani na nje ya nchi na endapo sauti yao haitosikilizwa wataenda kwenye hatua ya pili ya kuitisha maandamano. Heche amesema hayo mwenye mahojiano maalum na Waandishi wa @AyoTV_, Mika Ndaba na Bakari Chijumba ambapo amesema “Bado, na tunaendelea kusisitiza kwamba hii kesi ni ya kisiasa, ya uongo, haina ushahidi wowote wa maana hakuna itakapoenda ni kumpotezea muda, DPP afute hii kesi hiyo Mamlaka anayo, afute hii kesi kwasababu risk ya hiyo kesi, Watanzania wanajua Lissu ameshikwa kwa kesi ya uongo na alitakiwa awe anaenda kuhudhuria matibabu tangu apigwe risasi mwaka 2017 kila baada ya miezi mitatu anaenda check up na kuna risasi moja imebaki mwilini mwake ambayo hawawezi kuitoa kwasababu imekaa sehemu mbaya ikitolewa italeta damage” “Kuendelea kumshikilia na kumzuia kupata matibabu kwa mwaka mzima, chochote kikimpata kwenye mikono ya Serikali itakuwa balaa kubwa sana haitoeleweka, sisi hatotukubali, itakuwa ni jambo baya na litaleta shida kwenye nchi hii, wamuachie arudi mtaani afanye shughuli zake” “Hakuna aina yoyote ya mazungumzo, mawasiliano au chochote kitakachofanywa bila Mwenyekiti wetu kuwepo kwasabababu yeye ndiye anaweza kutuongoza kwenye jambo lolote, hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika bila yeye kuwepo” “Sisi kama Chama hatuwezi kwenda kwenye maridhiano ya ulaghai, ya kupotezeana muda,, Lissu alishapewa ofa aliambiwa tutakutoa gerezani uende nje ya nchi tutakupa walahu fedha uende ukakae usirudi hapa akakataa, tutaomba wawekewe hadi vikwazo vya kusafiri nje ya nchi, kunyimwa misaada ya Kimataifa hadi Lissu aachiwe, tutafanya kampeni ndani hadi nje ya nchi, Mimi nafikiri wanasumbuliwa na Ego wanaona aibu kwamba tutaonekana tumeshindwa, ustaarabu ukikosea ‘kasi haina maana ukiwa umepotea’ waelewe wamepotea, ukipotea Mtu Mstaarabu ukitoka ukakiri inakugharimu nini?, wakiendelea kumshikilia Lissu tutaenda hatua ya pili ambayo ni ngumu” #MillardAyoUPDATES
17
99
621
23,917
Smoke screen
120
red herring
8
7
37
10,095
BecaTZA retweeted
🚨🇺🇸 Full video of ICE agents EXECUTING an INNOCENT WOMAN! Welcome to Trump’s America…
653
2,767
283
10,304
652,416
📍 Sheikh Zayed Grand Mosque in Abu Dhabi, UAE.
162
Samia Suluhu atashinda kwa zaidi ya 83%. CHADEMA itaendelea kuzama zaidi katika mifarakano ya kimaslahi. ACT Wazalendo bado itasinyaa katika siasa za Bara. Vyama vya siasa vipya vitaanzishwa. Mbio za Urais 2030 ndani ya CCM zitaleta siasa mpya, zenye mengi ya kushangaza na mikakati ya aina yake kuanzia tarehe 1 Novemba 2025 hadi tarehe 30 Julai 2030.
147
202
545
309,402
Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Ackson, leo Novemba 07, 2025 ametangaza rasmi kujiondoa katika kugombea nafasi hiyo, @AyoTV_ imethibitisha taarifa hizi na inafuatilia zaidi kujua sababu za yeye kujiondoa. #MillardAyoUPDATES
158
42
15
1,063
136,181
TUSIWAHUKUMU MEDIA, NI WAHANGA WENZETU Kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa (Antonio Gutierres) “WHEN JOURNALISTS ARE SILENCED, WE ALL LOSE OUR VOICES” tafsiri yake ni kwamba “Wana Habari wakinyamazishwa, sote tunapoteza Sauti zetu” Sisi tunawalilia wao kwa kupoteza sauti zetu, ila tunajisahaulisha kuwa WAMENYAMAZISHWA!! Kama ambavyo Telecom Companies ambazo mmezilipia Bando, na bado INTERNET ikakatwa! Au kama ambavyo Unalipia LUKU na bado UMEME unakatwa! Wanahabari hawajawa kimya kwa kupenda, hivyo tuwape some Grace, na kujivisha viatu vyao. Wamenyamazishwa kwa njia nyingi, na pengine vitisho ambavyo kibinadamu walishindwa kujizuia. In Journalism wanasema “Hakuna Habari kubwa kuzidi Maisha yako” so when your life is on the line inabidi uwe mpole… na tumeshuhudia kuwa Maisha ya watu hayajathaminiwa. Na isitoshe, WAPO waliojaribu kufanya kazi katika mazingira haya magumu, na wengine wakapatwa madhila kama raia wengine yalivyowapata. Kuna Journalist amepigwa risasi (Azam Media), wengine wamefariki (Clouds Media), na pia wengine wamekamatwa (Ayo TV). Bongo Five walikuwa na Journalist Ubungo wakati maandamano yanaanza wakitoa ripoti, DW Swahili walitoa Tathmini ya kinachoendelea. KAZI YAO NI NGUMU, na mara nyingi wanaweka maisha yao on the line ili tu waweze kutuhabarisha. Wameuwawa watoto wa chini ya 18 yrs, Vijana wa under 30 na hata Wamama na Wazee, sasa unadhani Wengejali wewe umevaa Vest ya PRESS, wakati kuna WanaCCM AMBAO WAMEPIGA KURA ASUBUHI NAO WAMEULIWA? Imagine Millard Ayo ana reporter wake allegedly amekamatwa na polisi hadi sasa, ila haja ripoti (unadhani ana uhuru kiivyo kweli, maana UTU ANAO NAMJUA VIZURI) Kumbukeni KHALIFA SAID Aliwahi kufukuzwa kazi na Kampuni yake ya Media, Sababu Kauli zake ziliwaudhi Watawala. Na ingawa mimi napenda Media kuajiri watu wenye Weledi na Media Ethics, ila Issue ya ITHIBATI ililetwa kama njia ya kuzibana media pia. Na cha ziada ni kwamba, baadhi ya media Inamilikiwa na Chama (Uhuru, Magic, Channel 10), Serikali (TBC), viongozi na makada wa Chama na Serikali, na Wapambe na Chawa (Wasafi, Crown). Media Independent za Wafanyabiashara wao wanaogopa kuwa sanctioned. Na Kingine, Hata hizo DeutcheWelle, BBC na Aljazeera, Citizen Kenya, etc ambazo zimekuwa ziki ripoti, content wamezitoa kwa Our people on the ground ambao wao hawana uhuru wa kutoa kwenye outlet zao. Bora wao hata walikaribu, wengine nyie ambao ndio sasa mnajitokeza kusema PRAY FOR TANZANIA, Mlienda SHOPPERS PLAZA mkanunua vyakula, mkajifungia ndani HAMKUANDAMANA wala KUPIGA KURA… Alafu ndio wakwanza kuwanyooshea vidole MEDIA; Mtu yeyote mwenye kufuatilia yanayoendelea nchini atasikitika na kuwaonea huruma Media ila sio kuwa CONDEMN. The Leader
49
81
9
426
91,539
Abracadabra..
Samia Suluhu atashinda kwa zaidi ya 83%. CHADEMA itaendelea kuzama zaidi katika mifarakano ya kimaslahi. ACT Wazalendo bado itasinyaa katika siasa za Bara. Vyama vya siasa vipya vitaanzishwa. Mbio za Urais 2030 ndani ya CCM zitaleta siasa mpya, zenye mengi ya kushangaza na mikakati ya aina yake kuanzia tarehe 1 Novemba 2025 hadi tarehe 30 Julai 2030.
247