AyoTV (@ayotv_) header
AyoTV (@ayotv_) profile picture

Official Video Twitter page for @millardayo | We tell the best news and stories from East Africa | from the Most Subscribed to Journalist on YouTube in Africa.

Joined May 2014
Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)Photo by AyoTV (@ayotv_)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itafungua tena Ubalozi wake Nchini Angola ili kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kibiashara kati ya Mataifa hayo mawili. Akizungumza leo, Oktoba 29, 2026, Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es salaam, baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, Rais Samia amesema uamuzi huo unalenga kuendeleza ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Angola. “Kwenye mazungumzo yetu nimemuarifu Mheshimiwa Rais kwamba Tanzania imeamua kufungua tena Ubalozi wake Nchini Angola, ambapo hivi karibuni nitateua Balozi ili tuweze kufanya kazi kwa karibu zaidi,” amesema Rais Samia. #MillardAyoUPDATES
20
8
1
143
20,321
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu amesema Klabu hiyo haina nia ya kumfukuza Mwekezaji, huku akidai kuna baadhi ya Watu wanaotanguliza maslahi yao binafsi badala ya kusimamia maendeleo ya michezo na ustawi wa klabu, hali ambayo amesema imekuwa ikisababisha migogoro ndani ya Simba. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mangungu amesema baadhi ya Watu hao wamekuwa wakitumia fedha kwa ajili ya kumshambulia, kumtukana na kumdhalilisha, huku akidai kuwa fedha zinazotumika katika shughuli hizo zinaingia kwenye deni la mwekezaji wa klabu hiyo. “Kuna Kikundi cha Watu ambacho badala ya kusimamia maslahi yanayohusu ustawi wa michezo Nchini na maendeleo ya vilabu, wao wanaangalia maslahi wanayopata katika mifuko yao na matumbo yao, pesa hizo wanazozipata ndizo zinazotuletea shida,” amesema Mangungu. #MillardAyoUPDATES
6
2
50
6,074
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuingia ubia katika mradi wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Lobito (Lobito Refinery) nchini Angola. Akizungumza leo, Oktoba 29, 2026, Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es salaam, baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Angola, João Lourenço, Rais Samia amesema Tanzania imekaribishwa kushirikiana na Angola katika Sekta ya Mafuta, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Mataifa hayo mawili. Rais Samia amesema kwa muda mrefu Angola imekuwa ikisafirisha mafuta ghafi nje ya Nchi, lakini tangu Rais Lourenço alipoingia madarakani, Serikali ya Angola imechukua hatua za kuanzisha viwanda vya kusafisha mafuta ndani ya Nchi hiyo. #MillardAyoUPDATES
11
9
1
151
21,020
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, ameagiza kukamatwa kwa baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Lukonde, Kata ya Tomondo, Halmashauri ya Morogoro, wanaodaiwa kumtishia usalama Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ismail Mkimbu, kwa kutoridhishwa na maamuzi yake kuhusu masuala mbalimbali. Agizo hilo limetolewa wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa na Wananchi wa Kijiji hicho, ambacho kina mgogoro wa ardhi kati ya Wananchi na Mwekezaji, baadhi ya waliokamatwa wanadaiwa kutoridhishwa na maamuzi ya Serikali yaliyotolewa awali kuhusu eneo linalogombaniwa. Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ya kusikiliza kero za Wananchi na kutafuta suluhisho, Sendiga anatarajiwa kuzunguka Mkoa mzima kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.#MillardAyoUPDATES
4
4
1
167
20,976
Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaochezwa leo, Oktoba 29, 2026. Bao la Simba limefungwa na Rushine De Reuck dakika ya 42 na kuipa timu hiyo ushindi katika mchezo huo. #MillardAyoUPDATES
4
5
52
5,456
1
5
12
4,152
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameagiza Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, kutunzwa na kupambwa kwa kupanda miti na kuotesha misitu ili kuwa na mandhari nzuri na ya kuvutia. Rais Samia ametoa agizo hilo leo, Oktoba 30, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa miundombinu ya Mji wa Serikali Mtumba, akisisitiza umuhimu wa kutunza miundombinu iliyojengwa pamoja na mazingira yanayouzunguka Mji huo. “Nisisitize suala la kutunza miundombinu, tunataka Mji huu usimamiwe, uwe na mandhari nzuri ya kuvutia, ukiangalia ramani ya Mji wa Serikali, kuna maeneo yanaoneshwa ni ya kijani, ya kuotesha misitu,” amesema Rais Samia. Aidha, Rais Samia amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kuwa ya kijani katika ramani ya Mji wa Serikali yanatumika kama ilivyokusudiwa, ili misitu iliyopangwa kuoteshwa katika maeneo hayo iwepo. “Agizo langu kwako Katibu Mkuu Kiongozi, yale maeneo ya kijani yawe ya kijani kweli kweli, ili misitu iliyokusudiwa iwepo, iwe mvua ama jua,” amesisitiza Rais Samia. #MillardAyoUPDATES
9
11
267
32,774
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma umegharamiwa kwa fedha za ndani za Serikali bila kutegemea mikopo. Rais Samia ameyasema hayo leo, Oktoba 30, 2026, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali Mtumba, akieleza kuwa Serikali imejibana na kukusanya fedha zake ili kufanikisha ujenzi wa majengo na miundombinu ya kisasa katika Mji huo. “Watumishi wa Umma, kama mnavyoona tumepata majengo na miundombinu mizuri, imara na ya kisasa tuliyojenga kwa fedha zetu wenyewe, hapa hakuna mkopo, tumejichunga, tumejichanga kujenga kwa fedha zetu wenyewe,” amesema Rais Samia. #MillardAyoUPDATES
1
3
65
7,455
1
7
4,476
Klabu ya Manchester United imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa miamba ya Darajani, Chelsea, katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa leo, Oktoba 31, 2026, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Morgan Rogers dakika ya 50 na Cole Palmer dakika ya 64 kwa mkwaju wa penalti, huku Manchester United ikilazimika kumalizia mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki Lisandro Martínez kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 63. #MillardAyoUPDATES
1
2
77
9,640
Bayern Munich na Borussia Dortmund zimetoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) uliochezwa leo, Oktoba 31, 2026, kwenye Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani. Mchezo huo maarufu kama Der Klassiker umezikutanisha miamba hiyo miwili ya soka Nchini Ujerumani, huku kila timu ikifanikiwa kufunga mabao mawili katika pambano lenye ushindani mkubwa. Matokeo hayo yamezifanya timu hizo kugawana pointi moja moja katika mbio za kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa Bundesliga. #MillardAyoUPDATES
5
134
16,521
1
16
4,789
Kampuni ya TotalEnergies (@totalenergies_tz ), imezindua kadi mpya inayolenga kurahisisha malipo ya huduma mbalimbali, kufuatilia matumizi na kudhibiti gharama za magari kwa kampuni na wamiliki wa magari Nchini Tanzania. Kadi hiyo iliyoboreshwa kutoka mfumo wa awali wa kadi ya mafuta sasa inawawezesha Wateja kupata huduma mbalimbali katika vituo vya TotalEnergies, zikiwemo ununuzi wa mafuta ya Excellium yenye viambata, gesi ya kupikia, huduma za maduka ya Bonjour, kuosha magari na kubadilisha oili. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano TotalEnergies Getrude Mpangile amesema kadi mpya imekuja na mifumo iliyoboreshwa ya usalama inayomwezesha mteja kupokea taarifa za kila muamala kupitia ujumbe wa simu au barua pepe, hatua inayosaidia kufuatilia mahali, muda na kiasi kilichotumika, unaziwezesha kampuni kufuatilia matumizi ya Madereva wao kwa urahisi zaidi. Aidha, Mteja anaweza kupata huduma hata akisahau kadi yake kwa kutumia OTP inayotumwa kwa namba ya simu au mobility pay App, Wateja pia wanaweza kuona ripoti za matumizi na kusimamia salio la kadi zao kwa njia ya kidijitali bila kufika ofisini. Hata hivyo, kadi hizo zinapatikana katika mfumo wa malipo ya kabla na malipo ya baada, huku Mteja akihitaji kitambulisho na namba ya simu ili kupata kadi hiyo.#MillardAyoUPDATES
5
6
135
17,814
4
11
3,424
Watu tisa wameripotiwa kufariki dunia baada ya ndege ndogo aina ya Learjet 60 kuanguka katika eneo la Makazi karibu na Cresthaven, Kaunti ya Palm Beach, Jimbo la Florida Nchini Marekani. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Uchukuzi wa Marekani, Sean Duffy, kupitia mtandao wa X, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 12 mchana kwa saa za Marekani, huku Watu wote tisa waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakidaiwa kupoteza maisha. Taarifa hiyo inaeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa imetokea Austin, Texas, ikielekea Bahamas kabla ya kupata ajali hiyo. Aidha, taarifa hiyo inasema Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) imetuma timu eneo la tukio kusaidia uchunguzi unaofanywa na Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafiri (NTSB), huku Duffy akitoa pole kwa Familia na Ndugu wa waliopoteza maisha. #MillardAyoUPDATES
6
8
149
11,183
Mfanyabiashara kutoka Nchini China na Mwanzilishi wa kampuni ya ZXMoto, Zhang Xue, ameweka historia katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness baada ya kufanikiwa kuendesha pikipiki umbali wa kilomita 40.74 juu ya maji katika Mkoa wa Hunan Nchini China. Zhang amefanya zoezi hilo kwa kutumia pikipiki maalumu aina ya MX450 iliyofanyiwa marekebisho ya kipekee ili iweze kusafiri juu ya uso wa maji badala ya barabara kama ilivyo kwa pikipiki za kawaida. Kupitia jaribio hilo, Zhang amevunja rekodi ya awali ya kilomita 31.8 iliyokuwa imewekwa na Mtu mwingine, na kuweka rekodi mpya ya kilomita 40.74, hatua inayodhihirisha ubunifu na uwezo wa teknolojia katika kupanua matumizi ya vyombo vya usafiri.#MillardAyoUPDATES
8
14
2
317
29,916
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kifo cha Benson Steven, maarufu kwa jina la Mkembo, aliyekuwa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Wanawake wawili ambao miili yao ilikutwa imefichwa uvunguni mwa kitanda katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Mtaa wa Makunguru, Kata ya Ruanda, Jijini Mbeya. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, tukio hilo liliripotiwa Oktoba 16, 2026, majira ya saa 11 alfajiri, baada ya mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala Wageni, Nice Kabuje, kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mbeya Mjini kuhusu kupatikana kwa miili hiyo ndani ya chumba kilichopewa jina la Uphilipino. Polisi wameeleza kuwa mmoja wa marehemu ametambuliwa kuwa Annastazia Mwakipesile (32), Mkazi wa Kabwe, Jijini Mbeya, huku mwili wa Mwanamke mwingine ambaye bado hajatambuliwa ukihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya. Oktoba 21, 2026, majira ya saa tisa alasiri, Polisi walimkamata Benson Steven, fundi sofa na Mkazi wa Iwambi, Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo alidai alifanya hivyo ili awe tajiri baada ya kupewa masharti na Mganga wa Jadi. Kwa mujibu wa Polisi, kuwa wakiwa njiani kuelekea kwa Mganga huyo, Mtuhumiwa aliruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia ambapo Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtaka asimame, lakini aliendelea kukimbia, ndipo risasi nyingine ilipofyatuliwa na kumpata kwenye paja la mguu wa kushoto ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali. #MillardAyoUPDATES
27
9
6
254
43,751
Upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo umesababisha mapaa ya nyumba 15 kuezuliwa huku baadhi ya nyumba zikibomoka katika Vijiji vya Kasana na Nyarugusu, Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma. Tukio hilo limetokea Oktoba 21 na 22, 2026, ambapo upepo huo pia umesababisha mti kuanguka juu ya nyaya za umeme na kuongeza athari kwa Wananchi wa maeneo hayo. Kufuatia maafa hayo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo imetembelea Vijiji vilivyoathirika kwa lengo la kuwapa pole na kuwafariji Wananchi waliokumbwa na maafa hayo. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya asili na kutoa taarifa kwa Mamlaka husika wanapokumbwa na majanga ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. #MillardAyoUPDATES
7
7
150
15,259
Tuyaite ni mahaba au mapenzi ? au ushabiki ? Kijana Abel Julius ambaye pia ni Mkazi wa Arusha, amesema ametumia takribani shilingi milioni sita kwa ajili ya kubandika picha za Mshindi wa Miss Grand International 2026, Jihan Dimack kwenye gari lake. Abel amesema ametumia kiasi hicho kupamba gari lake kwa picha za mrembo huyo, ikiwa ni njia ya kuonesha upendo na kumuunga mkono, pamoja na kutambua mchango wake katika kuitangaza Tanzania kupitia tasnia ya urembo. Abel ameeleza kuwa gari hilo hufanya safari katika Nchi mbalimbali, huku akiamini kuwa uwepo wa picha hizo unasaidia kumtangaza Jihan Dimack na Tanzania nje ya mipaka ya Nchi. #MillardAyoUPDATES
68
12
7
281
68,656
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MCC), Salim Abri Asas ametembelea Wanafunzi wa Shule ya Msingi Weru, iliyopo katika Jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa Vijijini na kupongeza mazingira ya kujifunzia kwa Wanafunzi shuleni hapo. Asas ameeleza kuridhishwa na mazingira hayo huku akitambua juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu Nchini. Amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM, unaendelea kuonekana kupitia maboresho ya miundombinu ya elimu na utoaji wa elimu bila malipo, hatua zinazolenga kuwawezesha Wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora. Aidha, amewahimiza Wanafunzi kusoma kwa bidii, kuzingatia nidhamu na kujituma katika masomo yao ili kunufaika na fursa za elimu na kupata matokeo mazuri katika mitihani huku akisisitiza juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia zinapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji wa Wanafunzi, Walimu na Wazazi katika kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta matokeo yanayotarajiwa. #MillardAyoUPDATES
2
5
163
14,910