Yesaya | Nafundisha programming na akili unde (AI) kwa Kiswahili ๐Ÿ’ป Majadiliano ya TEHAMA, livestreams & Yesaya Software Podcast ๐ŸŽ™๏ธ TEHAMA Awards ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Dar es Salaam, Tanzania
Joined March 2011
Kila requirement ina uthibitisho: MET au UNMET. Claude anakagua code dhidi ya acceptance criteria moja baada ya nyingine na kuonyesha ushahidi.
7
Somo: usiruhusu sehemu tofauti za code kuandika moja kwa moja kwenye stock tables. AI ikipewa njia moja tu, haiundi njia ya pembeni.
13
Wazo la usiku: stock reservations zinazuia kuuza kitu kimoja mara mbili. Order ikithibitishwa, stock inawekwa pembeni hadi itolewe.
12
Lot tracking: kila stock iliyopokelewa ina lot yake. Ukitoa mzigo, unajua ulitoka lot gani.
11
Kila kinachohamisha stock (receive, issue, transfer, adjust, reserve) kinapitia service moja. Njia moja ya kweli = makosa machache.
13
Siku ya 5: ERP sehemu ya 2. Inventory, testing, na jinsi tunavyohakikisha kazi ya AI ni sahihi kabla ya ku-release. #SoftwareEngineering #AI
18
Funzo la siku ya 4: ERP nzuri inaanza na kanuni zisizovunjika. AI inaharakisha, kanuni zinalinda ubora. Kesho: inventory, testing na phase gates. ๐ŸŒ™
32
Kwa wajenzi wa ERP Afrika: EFD na kodi za ndani ni lazima. Mifumo ya nje mara nyingi haizingatii haya. Hiyo ndiyo fursa yetu.
25
Maoni ni zawadi. Mtumiaji akisema 'menu ni nyingi', sikiliza tatizo, si suluhisho tu. Mara nyingi chanzo ni role: admin anaona kila kitu.
1
33
Maoni ya watumiaji wa pilot: RFQ kwa suppliers, logo kwenye documents, GRN na Delivery Note za kuchapisha, notifications za SMS/WhatsApp/Email. Zote zikawa requirements ndani ya saa moja.
2
64
Database migrations: kila mabadiliko ya schema ni faili jipya. Hakuna kuhariri migration iliyokwisha run. AI inafuata kanuni hii ikiwa imeandikwa kwenye skill.
1
37
Jioni njema. Skill ni kama playbook ya timu: badala ya kumweleza AI kanuni kila siku, unaziandika mara moja na anazisoma kabla ya kazi.
1
38
Tuliandika 'skills' kwa Claude: maelekezo ya jinsi ya kuandika ledger posting, stock movement, migrations na API endpoints kwa mtindo wa mradi wetu.
1
37
Somo kubwa: AI inafanya vizuri kwenye uhasibu ukiipa kanuni wazi. Bila kanuni, inaweza kubuni posting inayoonekana sahihi lakini si sahihi.
1
41
GRNI (Goods Received Not Invoiced) na COGS zina-post zenyewe. Hapa ndipo mifumo mingi midogo husahau, na hesabu zinaharibika.
2
68
Trial balance inathibitishwa na automated tests. Tests zikipita, debits na credits zinalingana daima. AI ilisaidia kuandika tests hizi.
34
Kanuni ya design: manual journals zisitumike kuziba feature iliyokosekana. Kama kitu kinahamisha fedha, ki-post kupitia ledger pamoja na document yake.
2
53
Mchana mwema. Sarafu: vitabu viko TZS, lakini document za USD zinahifadhi kiasi halisi na exchange rate. Usipoteze taarifa ya awali.
33
Kanuni #5: party tagging. Mistari ya receivable na payable inabeba mteja au supplier, hivyo ageing na statements zinatoka moja kwa moja kwenye ledger.
45
Kanuni #4: hakuna duplicate posting. Ukijaribu ku-post document mara mbili, mfumo unarudisha entry ya kwanza (idempotency).
1
37