Mwachieni baba wa watu akamzike ndugu yake huu ukatili mnaomfanyia hamna mwanadam anaeustahili.
@SuluhuSamia @ccm_tanzania @jmkikwete
3
175
Buyobe chagua upande tujue wewe unasimama wapi xitter.cf/fbuyobe/status/2116896…
1
46
mkaruka retweeted
MARIDHIANO BILA UKWELI NA UWAJIBIKAJI NI USALITI.
Historia haina huruma kwa watawala katili. Historia inatunza kumbukumbu za sauti zilizopazwa mchana, lakini zikamezwa na giza totoro. Leo watawala wanazungumzia maridhiano, neno tamu vinywani, lakini lenye makovu makubwa moyoni
Humphrey POLEPOLE
Mwanachama mwandamizi wa CCM, alisimama, akanyoosha kidole hadharani akasema: “Tupatane kwanza kabla ya uchaguzi” Akatekwa, akapotezwa. Alipotea kwa hiari au alipotezwa kwa lazima? Sauti yake ikawa kama mwangwi uliopotea bondeni
Jaji Joseph Sinde WARIOBA
Mzee wetu wa heshima, akapaza sauti: “Tusikimbilie sanduku la kura bila maridhiano.” Badala ya kumsikiliza, mawe yakawa majibu yake. Mzee wa heshima akazuiwa, akawa mfungwa wa mawazo yake mwenyewe ndani ya kuta za nyumbani kwake
Askofu Josephat GWAJIMA,
Mtumishi wa Mungu akajitokeza, akashauri CCM na watawala, nchi inahitaji uponyaji, majadiliano kabla ya kwenda katika uchaguzi. Akashauri, uchaguzi huru na haki ni tunda la amani. Hakusikilizwa. Akapuuzwa. Akatukanwa. Akashambuliwa
Fr. Dr. Charles Hugo KITIMA,
Mwanatheolojia, alipojaribu kutoa ushauri wake wa busara kuelekea uchaguzi mkuu akiwa salama ndani ya makazi ya Maaskofu, alivamiwa na maharamia. Alishambuliwa. Akaonewa sana. Akayaona mauti moja kwa moja usoni kwake. Mbaya sana
Captain John Charles TESHA?
Askari wa JWTZ, alisema mengi, akataka maridhiano ya dhati. Akasema mifumo imeharibika na inahitaji marekebisho. Leo, sauti yake imekuwa kama redio iliyozimwa ghafla katikati ya msiba mzito. Tesha na wengine, walioona mvua kabla ya mawingu
Tundu Antiphas Mughwai LISSU
Mwanasheria mashuhuri, Mwanasiasa nguli, na Mwenyekiti wa CHADEMA, alizunguka kuwaeleza wananchi kuhusu umuhimu wa ‘NO REFORMS, NO ELECTION”, hakuvumiliwa, akakamatwa akiwa katika ziara za CHADEMA, ameshtakiwa kwa UHAINI
Na wengine wengi, waliotekwa na kupotezwa.
CHADEMA hatuwezi kusahau. Chini ya jua kali na mvua za EL NIÑO, ngurumo na radi, tulipita katika matope tukidai kitu kimoja: Mageuzi ya msingi kabla ya Uchaguzi. Lakini majibu yalikuwa ni kutekwa, magereza na kuzuiliwa kufanya siasa
Shingo za watawala zilijawa na kiburi, mioyo ikawa migumu, mkiamini ushindi ni kuiba kura na si kuchaguliwa na wananchi. Hamkutaka kuchaguliwa. Mkajitangaza washindi kwa ushindi wa kishindo. Watu milioni 32 walishiriki uchaguzi wapi?
Vongozi wa kiroho hawakubaki kimya. Walionya na walisema maridhiano si chaguo, ni hitaji la lazima ili taifa lipumue. Lakini, shingo za watawala zilikuwa ngumu sana. Mkajiona miungu watu msiohitaji ushauri wa ardhi wala mbingu. Mkasonga tu
Mdude Nyagali alivamiwa usiku, akatekwa na kupotezwa. Deusdedith Soka alitekwa na kupotezwa. Dioniz Kipanya alitekwa na kupotezwa. Mamia ya vijana wa CHADEMA, watoto wazalendo wa Tanzania, walitekwa na kupotezwa. Hii ni tabia mbaya
Baada ya kuitimiza azma yenu na kuwapoteza watu wenye sauti na kuwapiga mawe watu wenye hekima; baada ya kuvuna mlichokusudia kwa nguvu. Mmefikia kile mlichokusudia. Mlichokikinga, mlichokilinda, mlichokitimiza kwa nguvu zote
Mnataka maridhiano ya aina gani?
Maridhiano ya kumsafisha mkosefu bila kutubu? Maridhiano ya kunyamazisha watu waliojeruhiwa kwa risasi za moto, ili msisikie sauti za maumivu yao? Maridhiano ya dhati yanayoanza na KUKIRI MAKOSA na KUWAJIBIKA? Sasa, tumekataa ulaghai
HAKI za watu wote waliouwawa, waliopotezwa, waliofungwa gerezani, na wote waliojeruhiwa. Maridhiano bila ya wahusika kukiri makosa yao ni kiini macho. CHADEMA hatuwezi kutumika katika safari ya wananchi kuelekea kusikojulikana
Maridhiano bila haki ni usaliti
Maridhiano ya kweli yanahitaji ujasiri kukiri makosa, si ujasiri wa kuficha yaliyopita. Yanahitaji haki, si hila. Yanahitaji sauti zisikike, si sauti za wapinzani kuzimwa ili zao pekee zisikike. Wapinzani waseme wapi panavuja. Watawala wakiri makosa
Kama mmetimiza mlichokusudia, angalau kuweni na ujasiri wa kusema: Tulikosea. Msione aibu. MLIUA.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila
mkaruka retweeted
🧵 Wewe unaesoma, ni mwaka toka wananchi wenzio walipouliwa, familia zao zilipobaki na simanzi ya kutowaona wapenzi wao tena katika maisha hapa duniani, na wengine kubaki na majeraha na makovu ya moja kwa moja. Wao walitangulia hivyo daima tutawakumbuka na kuwaenzi, 👇🏾
Hii video ilinifanya mwanaume nikalia @SuluhuSamia hii ilikua mbaya sana
Wakati tunamwomba Mungu mwisho mwema ndugu zetu wanauwawa kikatili sana
1
24
Wito na ombi kwa serikali ya @WilliamsRuto
Na wakenya wote,
Sisi waTanzania tunamhitaji ndugu yetu Twaha Serikali ya Kenya itusaidie kumpata ndugu yetu
#FreeTwahaMwaipaya @EricOmondikenya @edwinsifuna @AmnestyKenya @DCI_Kenya
Tusaidieni kupaza sauti
27
Thank you Edwin Sifuna
The @LindaMwananchi_ statement on the abduction of Tanzanian activist Twaha Mwaipaya .
32
mkaruka retweeted
The @LindaMwananchi_ statement on the abduction of Tanzanian activist Twaha Mwaipaya .
Tanzania where we heading as a country?
@SuluhuSamia na @ccm_tanzania mbona mmegeuka wakatili sana?
Mtatuteka hadi lini mtateka wangapi?
Mmeona huu mradi unamalipa? Mbona ni kama ndio mnazidisha khali ya watu kupambana?
Pls ndugu zangu sisi sote ni Watanzania tupendane
mkaruka retweeted
Dear Mate and Friend, Hon. Antiphas Tundu Lissu, as a D-Day gets closer, I am writing to you with profound sincerity to remind you that you are not alone. It is clear to so many of us - the patriots, that what you have been facing are unjust response to your dedication, 1/3
Jana nimerudia hotuba ya Mh. Ndejembi akiwa Arusha kwenye kongamano la CEOs wa mashirika ya umma. Hapa tena, nimerudia hotuba yake ya jana kwenye Tanzania Startup Week. Nikakumbuka pia maagizo yake akiwa kwenye banda la vijana Sumbawanga wakati wa Wiki ya Vijana, pamoja na hotuba zake kwenye ziara mbalimbali.
Kwa muda mfupi tu, jamaa muda mwingi ni hoja, mawazo mbadala, maendeleo na issues zinazohusu nchi, wananchi na vijana tu.
Composure yake, exposure yake, unaona kabisa jamaa anajua mambo.
So far, hashambulii watu au kutoa kauli za kejeli na dhihaka kwa wengine,yeye ni issues tu.
Hata ukiangalia comments nyingi kwenye page za Instagram, ni positive. Huoni uongo na maigizo ndani yake.
Ukiwa na akili timamu, kiongozi akiongea unajua kabisa hapa hakuna nia ya dhati, ni siasa tu. But huoni hilo kwa Mh. Ndejembi.
Binafsi, napata matumaini makubwa sana juu yake. Mungu amtangulie sana.
20
mkaruka retweeted
MWANGOZO WA MAOMBI/DUA YA KUMUOMBEA MHE. LISSU
Kwa wale ambao tulikubaliana jana kwamba tutafunga siku 21 kwa ajili ya Mhe. Lissu, maombi yetu yanaanza leo Oktoba 15.
Omba toba juu yako
Omba toba juu ya vizazi vya kwenu
Omba Toba juu ya Tundulissu na vizazi vya kwao
Omba toba kwajili ya wote wamtesao na achilia msamaha wako
Omba toba juu ya Tanzania
TOBA YA MOYO WA KWELI
1. Yoeli 2:12-13
"Hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, kwa kufunga, na kulia... Rarureni mioyo yenu, wala si mavazi yenu."
2. Zaburi 34:18
"BWANA yu karibu na wao waliovunjika moyo, na wale wenye roho iliyopondeka huwaponya."
3. Zaburi 51:10
"Ewe Mungu, uniumbie moyo safi, na roho imara uifanye upya ndani yangu."
4. Zaburi 51:17
"Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika na kupondeka, Ewe Mungu, hutaudharau."
MUNGU ANAPOITIKA TOBA
5. Isaya 30:15
"Kwa kurudi na kupumzika mtaokoka; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini."
6. Yeremia 29:13
"Mtaniitafuta, na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
7. Yakobo 4:8-10
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi... Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua."
8. Luka 15:7
"Kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye kuliko kwa wenye haki tisini na tisa."
MIFANO YA TOBA KATIKA BIBLIA
9. 2 Petro 3:9
"Bwana... huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba."
10. Matendo 2:38
"Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu."
11. Zaburi 32:5
"Naliungama dhambi yangu kwako, uovu wangu sikuuficha... Nawe ukanisamehe uovu wa dhambi yangu."
12. Luka 18:13-14
"Mtoza ushuru... alisema, Ewe Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki."
13. Isaya 44:22
"Nimezifuta dhambi zako kama wingu zito... nirudie mimi, maana nimekukomboa."
14. Hosea 14:1-2
"Ewe Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako... Semeni naye, Tuondolee uovu wote."
15. Ufunuo 3:19
"Wote nipendao nawakemea na kuwaadhibu; basi uwe na juhudi, ukatubu."
SIRI YA LEO: Soma Yoeli 2:12 kwa sauti, kisha lia mbele za Mungu dakika 10 bila kuomba kitu - tu toba. Mungu wa rehema atasikia.






























