SENIOR ADVOCATE | CHADEMA CC MEMBER 2019-2024 | CHADEMA DIRECTOR FOR LEGAL AND HUMAN RIGHT 2024-2029.

Dar es Salaam, Tanzania
Joined February 2019
Kazi nzuri ya Baraza la Wanawake CHADEMA. Chama hiki tutakilinda kwa wivu mkubwa.
43
201
1,406
Inaonekana kuna mkakati wa kukamata viongozi wa Baraza la Vijana Nchi hii. Tayari mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Kigoma Coletha Clavery Ntidyicha na Mwenyekiti wa vijananKanda ya victoria wamekamatwa. Tanzania ni moja ya nchi zilizoridhia mkataba wa haki za kiraia na kisiasa, ni bahati mbaya kwamba, sasa hivi matendo ya kisiasa yanageuzwa kuwa makosa ya jinai na washindani walioshindwa kwenye majukwaa ya kisiasa.
3
73
2
215
4,701
CHADEMA KICHEKO MAHAKAMA KUU DHIDI YA JAMHURI: Kuanzia tarehe 09 October 2026 hadi leo ijumaa ya tarehe 16 October 2026 jumla ya kesi 03, zinazowahusisha chadema zimetolewa uamuzi na Mahakama kuu ya Tanzania masijala mbalimbali huku chadema wakiibuka kidedea. 1. MHAKAMA KUU - MASIJALA YA MORORGORO. October 09, 2026 Mahakama kuu masijala ya Morogoro ilikubali maombi Criminal Revision No. 12322/2026 baina ya LUCIA SIMON SHAYO VRS REPUBLIC. Katika Maombi hayo, mawakili wa CHADEMA waliomba Mahakama kuu iangalie uhalali wa mwenendo na amri za Mahakama ya wilaya ya Morogoro iliyokubali taarifa ya mawakili wa Jamhuri kuongeza orodha ya mashahidi na vielelezo kwenye kesi inayomkabili mwanachama wa chadema , Lucia Simon Shayo. Katika uamuzi wake, Mhe Jaji Ebrahim Rose aliona maombi ya mawakili wa Lucia Simon Shayo yana mashiko na alikubali kuwa taarifa ya kutumia vielelezo vya Jamhuri havikufuata sheria na kwamba taarifa yake ilikuwa unreasonable na hivyo akatumia mamlaka yake kufuta taarifa (notice) hiyo. Kwa kufutwa taarifa hiyo, mashahidi na vielelezo hivyo havitakuwa sehemu ya ushahidi wa kesi Jamhuri dhidi ya Lucia Simon Shayo. 2. MAHAKAMA KUU - MUSOMA Tarehe 16/10/2026 Mahakama kuu Masijala ya Musoma imetoa uamuzi kufuatia Rufaa ya mawakili wa Chadema dhidi ya uamuazi wa Mahakama ya wilaya ya Bunda iliyomtia hatiani Mwanachama mmoja maarufu kama Tolu kupitia shauri “Criminal Appeal No. 13554/2026 GEORGE MAPULI BUKINGI VRS REPUBLIC”. Bukingi ni mwanachama pekee aliyepatikana na hatia kwenye kesi ya wananchi 30 walishitakiwa kufuatia vurugu za October 29, 2025. Hata hivyo Mawakiki wa Chadema walikata Rufaa mahakama kuu na leo, Mhe Jaji E Kakolaki amekubaliana na hoja za mawakili kwamba ushahidi uliotolewa na upande wa serikali wakati wa usikilizwaji wa kesi haukujitosgeleza kumtia hatiani ndugu Bukingi. Hivyo Mahakama imekubali rufaa na kuelekeza aachiwe mara moja, ameshaachiwa tayari, ameungana na familia yake Bunda Mjini. 3. DAR ES SALAAM Hatimaye uamuzi wa shauri namba 7300/2026 lililofunguliwa mawakili wa Mhe Tundu Lissu kupinga kitemdo cha uongozi wa Gereza la Ukonga kuwazuia mawakili kuongea na mteja wao Mhe Lissu bila kusikikizwa na Maafisa wa Magereza umetolewa. Jopo la Majaji watatu wamekubali kwamba kitendo kilichofanywa na Magereza Ukonga ni kinyume na sheria na Mahakama imeelekeza utaraibu ufuatwe. Ushindi huu ni ushindi mhimu dhidi ya uhuru wa mawakili katika kutekeleza majukumu yao ya uwakili lakini pia ushindi huu umeifahamisha dunia namna Mamlaka zinavyomtendea isivyo haki Mhe Tundu Lissu kwa kumnyika nafasi ya kuzungumzq na mawakili wake. Kwa upande wa Mahakama, Jamhuri wameshindwa katika mashauri yote matatu. Mapambano yanaendelea Mahakamani. Nawashukuru kwa dhati Mawakili waliojitolea nankupigania ushindi wa mashauri haya, taasisi za kiraia, wananchi ambao mumefuatilia na kuwapatia maneno ya faraja wapambanaji wetu Mahakamani, Mungu awabariki sana! Tumehitimisha week hii Mahakamani kwa kishindo kikubwa!
6
34
1
139
5,337
Jana mahojiano hayakukamilika hivyo, Polisi walipanga leo kuendelea kumhoji Mhe John Pambalu, Mkurugenzi wa Organisation na Mafunzo. Yatakapokamilika tutawataarifu kilichojili.
5
46
276
3,591
MAHAKAMA KUU MUSOMA YAMWACHIA GEORGE MAPULI BUKINGI: Mahakama kuu ya Tanzania, masijala ya Musoma imekubali rufaa ya George Mapuli Bukingi aliyetiwa hatiani na mahakama ya wilaya ya Bunda. George Bukingi ni miongoni mwa vijana walioshitakiwa kutokana na vurugu za October 29, 2026 na kupewa kesi ya uhaini na baadaye ikabadilishwa na akashitakiwa kwa kosa la kumjeruhi Askari Polisi. Mahakama ya wilaya ya Bunda ilimhukumu Bukingi kifungo cha miaka 5, ikidai kwamva Mahakama iliridhika na ushahidi uliotolewa wakati wa usikilizwaji wa kesi . Hata hivyo, mawakili wa CHADEMA hawakuridhika na uamuzi wa Mahakama ya wilaya Bunda na wakaamua kukata rufaa Mahakama kuu - Musoma. Leo Mahakama kuu masijala ya Musoma, Mhe Jaji Kakolaki ametoa uamuzi. Katika uamuzi wake, Mhe Jaji Kakolaki amekubali hoja za warufani kwamba ushahidi haukijitosheleza kumtia hatiani na hivyo mahakama imemuachia rasmi leo. Kuachiwa kwa Bukingi, kumefanya watuhumiwa wote 30 walioshitakiwa kwa makosa ya uchaguzi wa october 29, Wilayani Bunda kuwa huru. Nawashukuru mawakili Alex Massaba nq Aloyce Kajitamusi kwa kuwa sehemu ya kutetea haki ya George Mapuli. Asanteni Bunda kwa ushirikiano kwa kipindi chote cha kushughulika na kesi ya Kaunya nanwenzake 29.
18
83
1
260
8,152
Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo @John_Pambalu amefikishwa Central Police Dar Es Salaam. Kwa sasa Mawakili wetu @Advocate_Jebra na @mwasipu_hekima wanakwenda Central Police ili aweze kuchykuliwa maelezo. Taarifa zaidi kuhusu amehojiwa kitu gani tutawataarifu baadaye! @MariaSTsehai @Liberatus80 @HecheJohn @JohnKitokavo08 @HildaNewton21 @jjmnyika @bavicha_taifa @BrendaRupia
3
55
3
184
5,556
UAMUZI KESI YA SAID ISSA UMESOGEZWA MBELE. Pokeeni taarifa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwamba, Mahakama imeahirisha kutoa Uamuzi juu ya Maombi ya zuio katika Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026 baina ya Said Issa Mohamed & Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Registered Trustees of Chama cha Demokrasia na Maendeleo & Secretary General of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)hadi tarehe 22/10/2026 saa 8 Mchana. Sababu za ahilisho hilo ni kutokana na Mhe Jaji aliyetarajiwa kutoa uamuzi huo kuwa na majukumu mengine nje ya kituo cha kazi. Tunawashukuru wanachama kwa utayari wao wa kufika Mahakamani, kwa taarifa hii, Tunaomba sasa tukutane Mahakamani tarehe 22/10/2026 saa nane mchana.
4
35
1
110
2,737
MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI KESHO KESI YA MAOMBI YA SAID ISSA MOHAMED DHIDI YA CHADEMA. Kesho tarehe 8 Oktoba 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam itatoa Uamuzi juu ya Maombi ya Zuio katika Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026 baina ya Said Issa Mohamed & Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Registered Trustees of Chama cha Demokrasia na Maendeleo & Secretary General of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mnamo saa 8 na Nusu Mchana. Wanachama na viongozi mnaombwa kufika kwa wingi kusikiliza uamuzi huo. Haya ni maombi mengine ambapo waombaji wanaomba Mahakama kuu kufungia Chama kwa Mara nyingine tena.
3
39
120
3,208
Leo viongozi na wanachama 17 wakiongozwa na Katibu wa Kanda ya Serengeti Jackson Rashid Mnyawami wamepandishwa kizimbani, Mahakama ya Hakimu mkazi wa Mkoa wa Shinyanga dhidi ya mashitaka ya Ugaidi yanayowakabili. Mashauri ya leo ni pamoja na Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Jackson Rashid Mnyawami, Mashauri mengine ni Economic Case No. 16503/2026, inayomkabili Jackson Venant Kabyeseleza, Economic Case No. 16504/2026 Inayomkabili Edwin Otieno Ongito na wenzake 8, Economic Case No. 16505/2026, inayomkabili Daniel Emanuel Athuman , Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Laurent na wenzake 4.
2
48
176
3,864
Makamu mwenyekiti Bara @HecheJohn aliwasili kwenye mkutano wa hadhara jana pale Bunda kwa hamasa hiyo. Kazi ya Bunda ilikuwa nzuri.
19
98
1,067
KESI ZA LEO SEPTEMBER 25, 2026 DHIDI YA WANACHAMA NA VIONGOZI WA CHADEMA NCHINI: September 25, viongozi wenzetu na wanachama watakuwa na mashauri yafuatayo kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini. 1. Dsm, criminal session No 19605/2026 shauri la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Lissu litaendelea ambapo Mhe Lissu anaendelea na kuwasilisha majumuisho ya hoja za mwisho. 2. Mkoani Morogoro, mwanachama Lucy simon shayo atakuwa mahakama kuu kwenye shauri la marejeo namba 12322/2026 ambalo litakuja kwa hatua ya kusomwa uamuzi. 3. Mkoani Shinyanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga itataja shauri namba 16506/2026, Jamhuri dhidi ya Jackson Rashid Mnyawami. (Ikumbukwe kuwa Jackson Mnyawami ni Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti ) Mashauri mengine (04) yatakayotajwa leo dhidi ya wanachama ni pamoja na shauri namba 16503/2926 Jamhuri dhidi ya Jackson Venant Kabyeseleza, Shauri Na. 16505 Jamhuri dhidi ya Daniel Emanuel Athuman, Shauri Na. 16504/2026 Edwin Otieno Ongito na wenzake 8 na shauri namba 16506/2026 Jamhuri dhidi ya Godwine Laurent na wenzake 4. Ukiacha Lucy Shayo, watuhumiwa wengine wote wanaletwa mahakamani wakitokea Magereza kwa kuwa makosa waliyopewa hayana dhamana kisheria. Viongozi na wanachama waliopandishwa kizimbani leo ni 19.
1
40
1
128
3,177
Orodha hii ni kesi kuanzisa kesho jumatatu tarehe 21 hadi Ijumaa tarehe 25/09/2026. Kila mwisho wa week nitakuwa naweka hapa orodha ya kesi dhidi ya viongozi ma wanachama wa CHADEMA zinazotarajiwa kuendelea Mahakamani nchini nzima. Ukiona kuna kesi dhidi ya kamanda wetu eneo lako, panga siku hiyo kuungana naye mahakamani, njoo Mahakamani uoneshe solidarity.
3
77
1
213
4,902
KESI DHIDI YA VIONGOZI NA WANACHAMA LEO TAREHE 16-09-2026: 1. Kesi ya uhaini dhidi ya Mhe Lissu, Criminal session no 19605/2026 inaendelea Mahakama kuu Dar es salaam. 2. Mahakma ya wilaya Ilala, kesi ya ugaidi inayomkabili Athumani Abdallah Muganda itatajwa. 3. Mbeya, kesi namba 16394/2026 Noah mwalwange na wenzake 3 itatajwa. 4. Kesi namba 16393/2026 Jamhuri dhidi ya Jasiri Robert Mwaisumbi nayo itatajwa.
3
36
127
2,456
KESI DHIDI YA VIONGOZI WA CHADEMA LEO SEPTEMBA 15: Mosi, Kesi ya uhaiji criminal session No. 19605/2026 inayomkabili Mwenyekiti Taifa, Mhe Tu du Lissu itaendelea leo kwa hatua ya utetezi, Mahakama kuu, masijala ya Dar Es Salaam. Pili, Criminal case No. 18445/2026 inayomkabili mwenyekiti wa Baraza la vijana, Maarifa Chagu na mwenzake John Joseph Ngolo, itatajwa mbele ya Mahakama ya wilaya Kahama. Wanashitakiwa kwa makosa mawili, kuchapisha taarifa za uongo na kuhamasisha umma kufanya vitendo vya uhalifu. Tatu, Shauri la Jinai namba 15461/2026 linalomkabili Katibu Mwenezi wa Jimbo la Busega, Athumani Joseph Kazinza inatajwa leo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu, huko Simiyu. Kamanda Kazinza anatuhumiwa kuhamasisha umma kufanya vitendo vya uhalifu. Hii mbinu ya kuhakikisha viongozi na wanachama wa Chadema wanashinda mahakamani kwa makosa yenye msukumo wa kisiasa nayo itashindwa kama zilivyoshindwa mbinu nyingine.
2
36
116
1,422
VIONGOZI NA WANACHAMA 41 WA CHADEMA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KESI ZA UGAIDI leo September 14, Mashauri saba dhidi ya viongozi na wanachama 40 wa chadema yametajwa huku shauri moja la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Lissu likiendelea kwa hatua ya utetezi. Mkoani Shinyanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga imeahirisha shauri namba 16506/2026, Jamhuri dhidi ya Jackson Rashid Mnyawami. (Ikumbukwe kuwa Jackson Mnyawami ni Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti ) Mashauri mengine dhidi ya wanachama yaliyoahirishwa mahakamani hapo ni pamoja na shauri namba 16503/2926 Jamhuri dhidi ya Jackson Venant Kabyeseleza, Shauri Na. 16505 Jamhuri dhidi ya Daniel Emanuel Athuman, Shauri Na. 16504/2026 Edwin Otieno Ongito na wenzake 8 na shauri namba 16506/2026 Jamhuri dhidi ya Godwine Laurent na wenzake 4. Mashauri yote haya yameahirishwa hadi tarehe 25/09/2026 huku viongozi na wanachama 17 wakirejeshwa rumande kwa kuwa makosa ya Ugaidi wanayotuhumiwa nayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria. Mkoani Mwanza, mashauri mawili yametajwa leo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanaza, ambapo jumla ya wanachama 23 walipandishwa Mahakamani. Shauri la kwanza ni Shauri namba 16375/2026 Jamhuri dhidi ya Deys E. Masalago na wenzake 09 na shauri la pili ni Shauri namba 16379/2026 Jamhuri dhidi ya Fantson Wilson Nyamwanga na wenzake 12. Mashauri yote mawili yameahirishwa hadi tarehe 28/09/2026 yatakapo tajwa tena huku watuhumiwa wote wakirejeshwa gerezani kwa kuwa makosa ya ugaidi hayana dhamana kisheria. Nawashukuru mawakili waliofika mahakamani kwa upande wa utetezi, Wakili Erick Mutta, Wakili Fellan Kweka, Wakili Sijaona Revocatus na wakili Gibson Ishengoma. Mkoani shinyanga pia wakili Aloyce Kajitamus nakushukuru kwa kusimama upande wa utetezi. Viongozi na wanachama waliopandishwa kizimbani leo jumla yao ni 41, ambao ni mwenyekiti Taifa Mhe Lissu (Uhaini) Shinyanga -17 (Ugaidi) na Mwanza (23) Ugaidi. Taarifa na mwendelezo wa shauri dhidi ya Mhe Lissu utawaajia baadaye, kwa sasa shauri linaendelea Mahakama kuu, Masijala ndogo ya Dar Es Salaam.
3
34
77
1,393
Orodha ya kesi zinazowakabili Viongozi na wanachama wa Chadema kwa week inayoanza tarehe 14 - 18/09/2026. Tuendelee kuunganisha nguvu kuoambania ndugu zetu wanaokabiliwa na mashitaka yenye msukumo wa kisiasa.
7
79
2
208
4,489
DAY - 5 GEREZA IRINGA Jana tarehe 10 September 2026 nimekamilisha ziara ya kuwatembelea wanachama wa CHADEMA wanaoshikikiwa magerezani baada ya kushitakiwa kwa makosa ya Ugaidi kwa kutembekea wanachama watatu Gereza la Mkoa wa Iringa. Wanachama hao, walioshitakiwa kwa Economic P. I No. 16453/2026 ni Ndugu Aqhudy Aqnay Qhyqhalay, Rahim Hussein na Helman Beatus Sambala wote wanatoka wilaya ya Mafinga. Wanachama hawa, kama ilivyokuwa kwa wanachama wengine walikamatwa na kuhojiwa kwa makosa ya uchochezi mtandaoni, baadaye wanadai kuletewa makaratasi mengi na kuambiwa wasaini ili ndugu zao wawadhamini bila kusoma kilichoandikwa. Baada ya kusign nyaraka hizo, wakashangaa hawadhaminiwi tena badala yake wakapelekwa Mahakamani ambako walipandishwa kizimbani. Wanachama hawa wanafanya ujasiliamali wa studio, wanarecord nyimbo , kupiga picha kwenye sherehe na matukio maalumu, kwenye ukamataji wao, nimeambiwa na vifaa vyao vyote vilichukuliwa. Leo kesi yao inatajwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa. Pamoja nao alishitakiwa mwanachama ambaye nimejulishwa ni GreenGuard anayejulikana kwa jina la Ambi Daudi Mwaisomba, kutoka Mafinga pia, naye eti kashitakiwa kwa makosa ya ugaidi.
2
24
69
1,956
DAY 4 GEREZA LA NJOMBE Nimefika Gereza la Njombe kumtembelea katibu mwenezi kata ya mavanga wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe. Augustino ambaye pia anajulikana kama Tinno alikamatwa kwa kosa la kuandika maoni yake kwenye ukurasa wa mtandao wa facebook wa @rose_mayemba maneno tunatoka. Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la ugaidi kama inavyoonekana kwenye hati ya mashitaka. Chaula ni miongoni mwa viongozi wa chadema 57 waliopewa mashitaka ya ugaidi nchi nzima. Ziara yangu leo imenifikisha Gereza la Njombe, kijana yuko imara, anawasalimia sana. Nimemhakikishia uwakilishi Mahakamani wakati wa usikilizwaji wa shauri hili. Ziara ya kuwatembelea wanachma wanaoshikiliwa magerezani inaendelea. Tuwafikie, tuwawakilishe Mahakamani, Tatizo la mwenzetu ni tatizo la jamii nzima.!!
2
37
1
94
2,737