Pinned Tweet
Mithali 9:11
Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Amina 🙏
Happy Birthday 🎂 To Me 🙏
Necto Kitiga retweeted
Tusambaze huu ujumbe kwa REPOST ZA KUTOSHA labda wakenya watatuelewa.
#FreeTwahaMwaipaya
Necto Kitiga retweeted
TAARIFA: Leo Jumapili polisi wameenda na Katibu wetu wa Nyasa @GraceShio03 nyumbani kwao Kimara, wamefanya upekuzi na kuondoka naye tena. Hawajaondoka na kitu chochote, maana yake hawajakuta kitu chochote!
NB: Tunaendelea kukemea haya mambo yakome, maybe kuna wanaofaidika nayo lakini kama NCHI tunaleta TAHARUKI tu na kusababisha nchi yetu kuonekana ni POLICE STATE.
Joseph Mbilinyi
Mkiti- CHADEMA Nyasa
#FREESHIO
Necto Kitiga retweeted
Dear #Kenyans, we earnestly appeal to you to join and amplify the #WhereIsTwahaMwaipaya campaign. Our Tanzanian brother, Twaha Mwaipaya, was abducted on Kenyan soil.
Please, #KOT, stand with us in demanding his safe return, well-being, and justice. We need voices from both sides to speak out loudly!
HELP! #FreeTwahaMwaipaya
Cc; @edwinsifuna @HEBabuOwino @GeorgeNatembeya @RobertAlai @MarthaKarua @OleItumbi @DrBKhalwale @MarthaKarua @bonifacemwangi
Necto Kitiga retweeted
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamepaza sauti wakitaka Mwanachama wa Chadema na Mwanaharakati Twaha Mwaipaya aachiwe huru, kufuatia taarifa za kutekwa kwake na watu wasiojulikana jijini Nairobi, Kenya.
Kupitia mitandao ya kijamii, watu mbalimbali wameeleza wasiwasi wao kuhusu usalama wa Mwaipaya, huku wakitumia alama ya reli ya **#FreeTwahaMwaipaya** kueneza ujumbe wa kutaka apatikane na kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambazwa, Mwaipaya anadaiwa kutekwa muda mfupi uliopita katika eneo la Kamulu Road, Nairobi, baada ya watu waliokuwa wamevaa kiraia na kufunika nyuso zao kwa barakoa kutumia magari matatu kuizuia gari aliyokuwa akisafiria.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa watu hao walimshusha Mwaipaya kutoka kwenye gari hilo na kuondoka naye, huku mazingira ya tukio hilo yakizua maswali kuhusu mahali alipo na usalama wake.
Baadhi ya watu waliosambaza taarifa hizo wameeleza kuwa namna tukio hilo lilivyotekelezwa ilionekana kama operesheni iliyopangwa.
Wanaopaza sauti kupitia mitandao ya kijamii wanataka kupatikana kwa taarifa za uhakika kuhusu alipo Mwaipaya, huku wakisisitiza umuhimu wa kulinda usalama wake na kuhakikisha haki zake zinaheshimiwa.
Necto Kitiga retweeted
Mpigania HAKI MWENZETU aliekuwa ukimbizini KENYA ametekwa akiwa "Makuru".
Twaha hakupenda kuwa MKIMBIZI hii ni baada ya KUTEKWA mara kadhaa akiwa Tanzania na kuteswa sana na WAKOLONI WEUSI.
Twaha amekaa jela muda mrefu kwa misimamo yake ya kudai haki.
Leo ANATEKWA AKIWA UKIMBIZI KENYA. WAKENYA TUSAIDIENI KUPAZA SAUTI KUMTAFUTA NDUGU YETU.
#FreeTwahaMwaipaya
REPOST 200
HABARI MBAYA.
@Twaha_Mwaipaya , Mwanaharakati kutoka Tanzania, ametekwa muda mfupi uliopita maeneo ya Kamulu, Kangundo road, Nairobi Kenya.
Wamemchukua na Gari aina ya Toyota HardTop nyeupe, na watu wenye silaha waliokuwa wamevaa nguo za kiraia muda mchache uliopita.
Necto Kitiga retweeted
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika ametoa wito kwa watanzania kufanya migomo mbalimbali ili kuunga mkono mgomo wa kula unaotarajiwa kufanywa na Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu, kuanzia Jumatatu ya Oktoba 26, 2026.
"Nitoe mwito kwa Watanzania kujiunga na ndugu yetu Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema kuanzia tarehe 26 mwezi wa kumi kwenye migomo mbalimbali kadri tutakavyoongozwa na roho wa Mungu. Chochote mtu anachoweza kugoma kwa njia ya amani kufikisha ujumbe kwamba tunataka haki ya Lissu, haki ya kuheshimiwa Katiba na sheria za Nchi, tunataka haki ya kuheshimiwa kwa amri za Mahakama." Amesema Mnyika.
Necto Kitiga retweeted
Mnataka nani atii Amri za mahakama kama nyie hamzitii?
Mnataka rule of the jungle?
Watanzania hawatakubali upuuzi huu.
Mwenyekiti wetu akipatwa na madhara yoyote lazima mjue kamba hatutakubali.
Necto Kitiga retweeted
Nimetoka Central police muda huu, niliambatana na Wakili @AdvMatata . Nimetaarifiwa na ZCO Msaidizi kuwa wanamshikilia Katibu wetu wa Kanda ya Nyasa @GraceShio03 na kwamba ‘taratibu za kipolisi’ zinaendelea. Hawajaturuhusu kumuona na wala kutuambia yuko kituo gani! Tunaendelea kufuatilia kwa usaidizi wa Wakili Matata.
Joseph Mbilinyi
Mkiti- CHADEMA Nyasa
#FREESHIO
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amewataka vijana na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kuongoza mapambano ya kudai mabadiliko pamoja na Katiba Mpya, akisisitiza kuwa kundi hilo ndilo lenye kila sababu ya kupigania mfumo bora wa nchi.
Akizungumza Oktoba 23, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Nzega mkoani Tabora, Heche ameeleza kuwa mabadiliko mengi ya kihistoria duniani yamekuwa yakisukumwa na vijana na watu wa tabaka la chini kwasababu wao ndio wanaokumbana moja kwa moja na athari za kile alichokiita uongozi mbovu na huduma duni katika jamii.
“Ndugu zangu vijana mabadiliko duniani hapa yameletwa na vijana na watu masikini kwa sababu nyie hamna cha kupoteza…kijana na mtu maskini. Kijana mabadiliko yanakuhusu kwasababu utatoka kwenye hali ya umasikini utaenda kwenye hali bora zaidi”, ameeleza Heche na kuongeza,
“Wanaoogopa mabadiliko kama alivyosema Mwalimu Nyerere ni wanyonyaji. Sisi tuna kila kitu cha kupigania ili tupate mabadiliko”.
Heche amesisitiza kuwa mapambano ya kudai Katiba Mpya ni takwa la msingi la mfumo na wananchi wote ili kuinusuru nchi iliyobarikiwa na rasilimali nyingi kama dhahabu, bandari na madini lakini wananchi wake wakiendelea kuteseka na tozo pamoja na umasikini.
Necto Kitiga retweeted
Mama awasihi ‘watekaji wa Landcruiser nyeupe’ kumrudisha mwanaye. Watekaji walivaa jezi za Simba: ‘Mrudisheni mwanangu, mpelekeni Mahakamani’
Mama wa Juma Kijazi (30), mfanyabiashara wa chips amewasihi watekaji waliomchukua mwanaye toka Oktoba 21, 2026, na kutokomea naye kumrudisha kijana wake, ambaye ndiye mtoto wake wa kwanza.
"Toka tarehe 21 Oktoba mpaka leo, sijaweka hata maji mdomoni. Siwezi kujua mwanangu yupo kwenye hali gani: anakula, analala, au amekufa. Nyinyi wakina baba mliomchukua mwanangu, mrudisheni; mpelekeni hata polisi. Naombeni mnirudishie mwanangu, popote pale alipo. Mimi ndiye mama yake. Nawaombeni sana mnirudishie mwanangu," Mama huyo amewasihi watekaji.
Watekaji hao ambao hawakujitambulisha walifika katika eneo lake la kazi Kinondoni Manyanya na kupaki gari lao Landcruiser nyeupe, baada ya muda walishuka na kumkamata kijana huyo akiwa anafanya usafi, pamoja na kijana mwingine waliyemuachia.
Tukio hilo limeripotiwa Polisi na kusajiliwa kwa OYB|RB|7259|2026
Necto Kitiga retweeted
TAARIFA:
Nimepokea taarifa kutoka kwa familia ya Katibu wangu wa Kanda ya Nyasa, Ms Grece Shio kuwa amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi, jana usiku akiwa nyumbani kwao Kimara, Dar.
Mpaka sasa haijulikani yuko kituo gani na amekamatwa kwa kosa gani!
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na nimeshawasiliana na Mawakili wetu Dickson Matata na Hekima Mwasipu ili watusaidie kufuatilia kwa karibu pia.
Joseph Mbilinyi
Mkiti- CHADEMA Nyasa
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Bara John Heche @HecheJohn amesema ataendelea kukagua na kuonyesha changamoto zilizopo katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa na ambayo bado haijatekelezwa na serikali nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Oktoba 23, 2026 Heche amechapisha video akieleza ubovu wa barabara ya Katesh-Singida ambayo imekuwa na mashimo mengi yanayotokana na lami kumeguka jambo ambalo linaathiri muda wa usafiri na usafirishaji lakini kuharibu vyombo hivyo.
Amehoji serikali kutenga zaidi ya shilingi bilioni 700(zimetengwa Shilingi bilioni 730) kwa ajili ya kujiandaa na kuikabili El Niño, huku hatma ya barabara hiyo ikiwa bado na maswali pamoja na kuwa na umuhimu mkubwa katika uchumi wa Taifa letu kupitia usafirishaji wa bidhaa kuelekea nje ya nchi.
Oktoba 14, 2026 Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa alichapisha video ya Msikilize Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohammed Besta akieleza kuwa ukarabati wa barabara hiyo unaendelea huku akionyesha vifaa vikiwa vinaendelea na uwekaji wa lami katika barabara hiyo.
Necto Kitiga retweeted
Makamu Mwenyekiti Mhe. @HecheJohn jana ameweka jiwe msingi la ujenzi wa Ofisi ya Chama Wilaya ya Igunga kabla ya kwenda kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Nzega mjini.
Necto Kitiga retweeted
"Nimepokea taarifa kutoka kwa familia ya Katibu wangu wa Kanda ya Nyasa, Ms Grece Shio kuwa amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi, jana usiku akiwa nyumbani kwao Kimara, Dar.
Mpaka sasa haijulikani yuko kituo gani na amekamatwa kwa kosa gani!
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na nimeshawasiliana na Mawakili wetu Dickson Matata na Hekima Mwasipu ili watusaidie kufuatilia kwa karibu pia." Mhe. @TheRealJongwe



















