Joe Allan (@JoeAllan_) profile picture

Jesus first : Thrilling since 80's👌

Joined September 2020
Photo by Joe Allan (@JoeAllan_)Photo by Joe Allan (@JoeAllan_)Photo by Joe Allan (@JoeAllan_)Photo by Joe Allan (@JoeAllan_)Photo by Joe Allan (@JoeAllan_)
Sisi wengine hatuna maisha mazuri ila mioyo yetu iko tayari kukosa kuliko kumdhulumu mtu🤔
7
16
37
900
Joe Allan retweeted
Send this to your Partner. 🧡
6
219
23
1,124
67,274
Law is about facts, evidence and the proper application of established legal principles, not personal beliefs, assumptions or opinions. A court that determines cases based on what it believes rather than what has been established through evidence and due process is a misguided court. Justice must be founded on facts, not beliefs. Tafsiri ya Kiswahili: Sheria inahusu ukweli, ushahidi na matumizi sahihi ya misingi ya kisheria, siyo imani binafsi, hisia au dhana za mtu. Mahakama inayoamua mashauri kwa kuongozwa na kile inachokiamini badala ya kile kilichothibitishwa kwa ushahidi na kufuata taratibu za kisheria, ni Mahakama iliyopotea katika misingi ya haki. Haki lazima ijengwe juu ya ukweli, siyo imani.
11
206
2
631
12,668
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 502 Mhe. Lissu anaendelea Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana. Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli. Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi. Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa. Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave. Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana. Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha. Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo. Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu. Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani. Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini. Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine. Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa. Majaji wanatoka. Naomba Repost yako.
154
482
28
1,352
80,926
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 501 Wakili wa Serikali kimsingi anasema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba 2025 yalitokana na kauli zangu kama nimemuelewa sawa sawa. Kwenye kesi hii sina hakika kama mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Chande wala yeye hajaja kutoa ushahidi hapa kuthibitisha hizo vurugu zilisababishwa na vurugu za wanasiasa gani. Mnaambiwa mnitolee adhabu kali kwa kosa ambalo kama lipo limefanyika kwazaidi ya miezi 6 limefanyika baadae mimi nikiwa gerezani, mkikubaliana na hoja hiyo huu utakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo. Watu kicheko😂😂😂😂😂 Wakili wa Serikali Mkuu anataka muamini projo za mitandaoni, mkikubali utakuwa ni uthibitisho kuwa ni maagizo. Wakili wa Serikali Mkuu amewaambia vile vile kwasasa hawana taarifa zozote kama hili ni kosa langu la kwanza, maana yake anaashiria kwamba kuna previous conviction, sasa kwavile hana uhakika mimi nitawaambia ukweli, sijawahi kutiwa hatiani na kosa lolote la jinai, wamenishtaki kwa zaidi ya miaka 24 tangu 2002 hawajawahi kunipata, I have never ever been convicted for a criminal offence, kwahiyo mnapofikiria adhabu lazima mjue kwamba mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia. Mhe. Lissu anaendelea Waheshimiwa majaji nafaham mnajua kwamba nina msiba mkubwa sana wa mtu aliyenilea, amenifanya mimi kuwa mwanasheria, kwasabu sikupata nafasi ya kumuuguza, nilikuwa natumaini kuwa Mahakama itaniacha niende nikamzike Mzee Alutte, I was hoping that, inaelekea kuwa hiyo haipo kwenye mahesabu yenu, mnapokuwa mnafikiria adhabu mfikirie na hilo, family obligationdls is a factor kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, Dunia nzima inajua, magazeti everywhere, I was hoping that nitapata nafasi ya kwenda kumzika huyu aliyenilea. Waheshimiwa majaji leo ni mwaka na miezi 7 niko gerezani, mnapofikiria adhabu kali muitoe msije mkasahau kwamba huyu mtu ameshakaa gerezani kwa kosa ambalo mmelisema wenyewe kuwa sio kosa, halijathibitishwa na wala msije mkasau walichokisema jopo la Majaji watatu wenzenu: Jaji Mruma, Dkt. Longopa na Jaji Rumisha kuhusiana na niliyotendewa gerezani. Wamesema nimenyimwa fursa ya kuwasiliana na mawakili wangu, Viongozi wenzangu wa chama halali cha Chadema, nimenyimwa fursa hata ya kuomba Mungu. Majaji wenzenu wamesema hayo yaliyotendeka nilinyimwa fursa na haki ya kujitetea, msije mkasau hayo mnapofikiria adhabu kali. Waheshimiwa Majaji mimi ni raia mwema wa nchi hii, mzalendo wa nchi hii, nimetumikia nchi hii kama Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi mara 2 nimekwenda Jeshini, nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa nchi hii, mimi sio mpiga kelele, I am a patriotic, ndio maana nimeona na mabalozi wako Mahakamani, wanajua mimi ni patriotic hivyo mnapofikiria adhabu msije mkasahau hoja hii. Waheshimiwa Majaji gerezani sio mahali pazuri sana, nasema hivyo kwasababu nimeishi kwa siku 577, nakaa kwenye chumba cha sita kwa sita, sio sheraton hotel, unaweza ukasema tu funga kama hujui Gereza ni nini? Nasema haya kwasababu mimi sio mzima sana, kwenye huu mwili wangu nina operesheni 25, visu vya madaktari, ninatembea na risasi mwilini. Katika risasi 16 zilizoingia mwilini moja walishindwa kuitoa, ninatakiwa niwe naenda Hospital Ubeligiji, Hospital ya chuo kikuu cha Luven nilikotibiwa baada ya yaliyonikuta miaka 9 iliyopita, nimeshamiss appointment 4 kwasababu ya kesi hii, juu ya yote hayo Majaji nina kisukari huu mwaka wa 6 sasa, kwahiyo mtakapokuwa mnatafakari hiyo adhabu kali, mkumbuke hilo kwamba hali yangu ya kiafya sio nzuri sana. Waheshimiwa majaji kosa la uchochezi mara ya mwisho nilipoangalia ni kosa lenye dhamana, kama itawapendeza Kwa vile hili kosa lina dhamana, mnipe dhamana ili nikatie uamuzi wenu huu rufaa nikiwa nje kwa dhamana lakini muhimu zaidi pia ili nikamzike huyu aliyelala (Mzee Alute), nilisema sina mpango wa kuomba ila dhamana naomba. Part 502 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
64
508
17
1,499
85,871
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 500 Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao. Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini. Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’ing’inia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu. Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini???? Maana yake ni nini waheshimiwa majaji? Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote. Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu. Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa. Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini. Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo. Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta. Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji. Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia. Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu, Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili. Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza. Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham. Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman. Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
83
654
14
1,767
97,836
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 499 Jaji Ndunguru anasema kwamba Mahakama inaamini kwamba mshtakiwa alikuwa na notice ya kosa dogo hivyo alikuwa na nafasi ya kujitetea na ushahidi wote uliotolewa umejikita kwenye uchochezi na alichochea umma kuzuia uchaguzi wa 2025 Kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu Mahakama imeridhika kwamba Lissu alitenda kosa la uchochezi kwa mujibu wa kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu. Hivyo Mahakama hii inamtia hatiani kwa kosa hili la Uchochezi. Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka Anasimama Katuga anasema Kamba kwa mujibu wa kifungu cha 339 cha CPA mahakama hii inaweza kupokea mpaka ushahidi kwenye kutoa proper sentence. Upande wa Jamhuri tunajua adhabu ina malengo mojawapo ni kutoa onyo kwa mtu aliyetenda kosa ili asirudie kosa hilo au makosa mengine na linakuwa onyo kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa hilo ambalo mshtakiwa ametiwa hatiani. Upande wa Jamhuri mbali na kutokuwa na previous records za mshtakiwa za makosa ya nyuma, kwa mujibu wa taarifa zilizopo polisi kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu wenye kutenda kosa la kuchochea umma wa watanzania kwa maslahi yao binafsi either ya kisiasa au ya kiuchumi. Vitendo ambavyo mara zote vinaharibu amani ya nchi, vinaathiri uchumi wa nchi kwa maana ama vinapelekea uharibifu wa mali za umma zikiwemo na mali binafsi. Hivi vitendo vya kichochezi vinaathiri uchumi wa nchi na vimepelekea umma wa watanzania kuwa na hofu kuwa kutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani hivyo wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi. Waheshimiwa vitendo vya kiuchochezi vinaathiri uchumi wa wananchi na hili ni kosa kisheria, wakati mnatoa adhabu tunawaalika katika hotuba halali ya Jaji Chande na Tume yake baada ya kufanya uchunguzi bila kuchagua upande wowote walisema sababu za vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa 2025 zilisababishwa na kauli za baadhi ya wanasiasa. Kifungu cha 35 kinatoa general punishment ambayo adhabu yake ni miaka 5 hivyo tunaomba mahakama hii iangalie athari ambazo zimetokea kutokana na kauli ambazo mshtakiwa ametiwa hatiani pamoja na hotuba ya jaji chande. Taarifa ya Chande inaonyesha hasara inayotokana na uchochezi uliotokana na kauli hizo. Tunaomba adhabu kali Waheshimiwa majaji ili iweze kukidhi nia ya adhabu kisheria. Waheshimiwa kifungu hiki kinasema adhabu kubwa ni miaka 5 au pamoja na faini. Ni faini kiasi gani ni Mahakama kuangalia athari kutokana na athari zilizotokea. Ni hayo tu. Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama analolote la kusema? Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina maneno ya kuzungumza ila naomba dakika 5 nifanye consultations na mawakili wangu ili niweze kuzungumza hayo ninayotaka kuzungumza. Jaji Ndunguru:Sawa Part 500 itaendea kwenye post inayofuata. Naomba Repost.
114
559
13
1,614
115,468
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 498 Jaji Ndunguru anasema katika kutafisiri hicho kifungu cha 319(1-2) cha CPA Mahakama ya Rufani ilielezea kwa marefu na mapana kwenye kesi ya DPP vs Zombe kuhusu kifungu hicho kuwa sio automatic. Kwakuwa mshtakiwa hakushtakiwa na kosa dogo, Mahakama pia haiwezi kutumia kifungu hicho bila kumpa mshtakiwa haki ya kusikilizwa au kumpa notice. Kwa mujibu wa ushahidi uliopo kuwa maneno hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma na video hizo video hazikutolewa mahakamani na kwa vile hajakanusha kutamka maneno hayo na upande wa jamhuri umesema kuwa alilenga kuchochea umma na mashahidi wa upande wa utetezi nao hawajakataa kuhusu mshtakiwa kutamka maneno hayo. Tumeridhika kwamba mshtakiwa kutamka maneno hayo hadharani mbele ya umma alilenga kuchochea umma ili kuvuruga uchaguzi wa 2025 kwa njia isiyo ya amani kutokana na maneno yake hivyo basi tukiongozwa na maamuzi mbalimbali na kwa muktadha wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu kosa lililotengenezwa na kifungu cha 390 ni kosa dogo la uhaini, kifungu cha 390 kinalengo la kuzuia crime katika hatua ya mwanzo before public harm. Kwa tafsiri yetu tunasema kifungu hiki kina prevent nia na present danger. Upande wa mashtaka wanapaswa kuthibitisha kuwa maneno ambayo mshtakiwa aliyatamka kufanya instigation yalikuwa communicated, pia mshtakiwa alilenga kuwa mtu au watu watende kosa. Tunaelewa kwamba kifungu cha 390 kinatumika kwenye kosa lolote hakijataja kosa lolote pale, tunaamini kwamba kufanya kosa la uchochezi kunaweza kupelekea present danger, tunaamini ni minor offence na ni cognate offence kwa mujibu wa 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Ni kwa mtazamo wetu sasa kwamba ni common sense kwamba incitement ni component ya offence ya treason hivyo sio lazima mtu awe charged independently. Kulingana na ushahidi uliotolewa mshtakiwa alichochea umma kuvuruga uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi na kukinukisha vibaya sana. Upande wa utetezi haujaonyesha ni kwa namna gani walipanga kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi, na mashahidi wa upande wa Jamhuri walieleza namna ambavyo walishawishika na maneno ya mshtakiwa mfano shahidi wa 4, 5,8 ,11, 13, 14 walishawishika na kujiunga na wale ambao walishawishika ili waweze kuvuruga uchaguzi. Part 499 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
116
567
27
1,580
149,011
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 497 Jaji Nduguru anasema, pia tunasukumwa hivyo na kifungu cha 10 cha Kanuni ya adhabu kuwa nia ya mtu lazima iambatane na matendo ya dhahiri ya mshtakiwa na sio maneno tu. Kwa mtazamo wetu dai kwamba upande wa utetezi walifanya kwa lengo la kushinikiza Serikali kufanya mabadiliko haimaanishi ni kuwa ni kuitishia Serikali ni msimamo wetu kuwa kesi ya upande wa mashtaka imeegemea zaidi katika maoni kuwa maneno ya mshtakiwa yalilenga kuitishia serikali. Mahakama inaamua kuwa sio lazima provocative speeches zinaweza to constitute kosa kwa maana zinalenga kuhamasiha mabadiliko hivyo sio lazima ziwe kosa la jinai. Hatujapata ushahidi wa moja kwa moja ukiachia ushahidi wa namba 1,2 na 16 ambao ni tafsiri zao, sisi tunaona kutokuwa na ushahidi tunasema kwamba maneno hayo sio kwamba yanapelekea uhaini. Tunajua kuwa Serikali ina wajibu wa kusimamia uchaguzi, sheria na hivyo maneno yanayo desrupt election yanaconstitute kosa la uhaini. Hoja ya tatu na ya mwisho ambayo ni ambayo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo ya kuchochea umma kuvuruga uchaguzo kwa lengo la kuitishia serikali. Tukiangalia ushahdi wa Jamhuri hasa namba 1,2 na 16 ambao waliegemea kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na walisema kusambazwa kwa maneno hayo kulifanywa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mshtakiwa na watu waliokuwepo kwenye mkutano huo, shahidi namba 17 alieleza kwamba matukio hayo yalirushwa live ili kuuhabarisha umma kuhusiana na msimamo wa No reforms, No election. Upande wa mashtaka wanaeleza kuwa kwa kuwa maneno hayo yalirushwa mubashara na mshtakiwa kukiri kuwa aliongea maneno hayo basi mahakama ione kuwa upande wa mashtaka umethibitisha publication hata kama hakuna picha mjongeo. Upande wa utetezi ulieleza kuwa sio Lissu aliyesambaza maneno hayo, na kukosekana kwa video hakuna uthibitisho kuwa Lissu alichapisha. Tunakubaliana na Lissu kuwa hakuna ushahidi kuwa yeye ndio alichapisha na kusambaza hayo maneno kwenye YouTube ya Jambo TV. Kitendo cha kuonekana tu kwenye Jambo TV sio lazima kuwa Tundu Lissu ndiye aliyepandisha kwenye Jambo TV. Tumeona kwamba upande wa mashtaka wamethibitisha kwamba kauli hiyo ilitolewa na mshtakiwa, na kuwa ilisambazwa na mshtakiwa alitoa hotuba hiyo katika umma sio kwa kificho hivyo kauli za mshtakiwa hazikuwa kauli za siri. Mahakama hii inaona kwamba kauli hizo kupandishwa kwenye mtandao wa Jambo TV haimaanishi kuwa Lissu ndiyo aliyepandisha. Hivyo basi kutothibitisha uhusika wa Lissu kuchapisha maneno hayo kwenye Jambo TV upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha element za kosa. Kwa kitendo cha kutokutolewa video clip does not defeat ushahidi wa mdomo ambao ulitolewa na shahidi wa 17 ambaye alikuwepo na mshtakuwa hapingi maneno hayo. Kutokana na ushahidi uliopo, upande wa mashtaka hawajatupa ushahid kuwa Lissu alilenga kutenda kosa la uhaini. Failure kuleta ushahidi hoja ya tatu inakuwa pia haina mashiko, treason per see kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) haijathibitishwa na kifungu hiki hakina minor offence lakini ni jukumu la ku evaluate ushahidi na kuona kama kuna kosa dogo. Kwa mujibu wa kifungu cha 319(1-2) cha CPA kinaelekeza mahakama kwamba inaweza to substitute kosa pale ushahidi unapoonyesha kwamba kunaweza kuwa na kosa dogo. Part 498 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
171
637
25
1,761
144,820
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 496 Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la! Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa. Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live. Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali. Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali. Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini. Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa. Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini. Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa. Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
167
634
28
1,736
149,195
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 495 Suala la uhalali wa hati ya mashtaka liliwahi kulalamikiwa mwanzoni mwa shauri hili na Mshtakiwa na katika uamuzi wake wa Sept 2025 ilieleza kuwa hati ya mashtaka ilikuwa sahihi. Mshtakiwa alisema kuwa Kifungu cha 39(2)(d) kinahitaji kushawishi kikundi cha watu na sio umma kama ilivyoandikwa hivyo alisema hati hiyo inakinzana na Ibara ya 13 ya Katiba ya Tanzania inayohusu uhalali wa kisheria (principal of legality) Katika pingamizi la pili alisema upande wa mashtaka haukueleza taasisi ya serikali ambayo anadaiwa kuitishia na katika hoja ya tatu mshtakiwa alisema haijasema nia au lengo la kufanya huo uhaini kwasababu pia maneno ambayo hayajatumika katika sheria hivyo alisema mahakama ione hati ina mapungufu Upande wa mashtaka walikiri kuwa ni kweli hati ya mashtaka imetumia neno public lakini tafsiri ya neno public kinajumuisha mtu yeyote au kikundi cha watu hivyo walikidhi matakwa ya sheria, katika hoja ya pili walisema hati ya mashtaka imetumia neno executive. Upande wa mashtaka walieleza kuwa majukumu ya Executive ni kutekeleza sheria hivyo mshtakiwa alikuwa anaelewa maana ya neno Serikali na hivyo aliweza kuelewa na kutoa utetezi wake. Mahakama inaona kwamba mapingamizi ya mshtakiwa kuhusu hati ya mashtaka hayana mashiko kwasababu ilishatolea uamuzi huko nyuma na inamaelezo ya kutosha. Neno public katika tafsiri ya kifungu cha 5 cha Kanuni ya Adhabu kinazumzia mtu yeyote au kikundi cha watu, tumeangalia pia kwa umakini ushahidi na utetezi hivyo mshtakiwa alielewa hati ya mashtaka. Maelezo katika hati ya mashtaka yanajitisheleza kabisa na kwa mujibu wa shauri la Nasibu Mahakama inatakiwa kutumia neno kama lilivyo hivyo neno executive linaeleweka kama lilivyotajwa kwenye hati ya mashtaka. Katika hoja ya tatu tunakubaliana kuwa upande wa mashtaka lazima waeleze nia mahususi kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), hivyo tunaona kwamba mapingamizi yote hayana mashiko kwasababu tulishayatolea uamuzi. Kinachofuata sasa ni kuangalia viini vitatu, viini hivyo ni-; 1. Endapo mshtakiwa yuko chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d). Ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha hili, pande zote mbili wanakubaliana kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT. Hata katika usikilizwaji wa hoja za awali mshtakiwa alikubali kuwa alikuwa na utii wa JMT ni mzaliwa wa Tanzania, ana pasipoti ya Tanzania na 3/4/2025 alitoa maneno hayo akiwa ndani ya JMT, Mahakama inaona kwamba mshtakiwa alikuwa na utii wa JMT. 2. Kiini cha pili ni endapo mshtakiwa alitenegeneza nia ya kuhamasisha umma kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali kinyume na kifungu cha 39(2)(d). Upande wa mashataka wana wajibu wa kuthibitisha nia hiyo tofauti na political criticism, nia ni internal state of mind na lazima kifafanuliwe na ushahidi, matendo ya mshtakiwa. Upande wa mashtaka waliegemea kwenye hoja kwamba 3/4/2025 mshtakiwa alisema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, tutauvuruga uchaguzi, upande wa mashtaka waliegemea kuwa mshtakiwa alikuwa na nia ya kuitishia Serikali na waliegemea kwa upande wa ushahidi wa mashahidi wao kuwa mshtakiwa ni mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya Tanzania. Upande wa Jamhuri waliegemea upande wa ushahidi wa shahidi wa kwanza ambaye aliona maneno hayo yanaviashiriia vya uhaini. Shahidi alieleza kuwa mshtakiwa kutoa maneno hayo mbele ya waandishi wa habari na kusambazwa maneno hayo, mshtakiwa alikusudia kuitishia serikali. Shahidi wa 16 upande wa mashtaka alieleza kuwa alipoona hayo maneno walipanga kuwapiga mawe wapiga kura, shahidi wa 17 alisema alikuwepo kwenye mkutano na kuwa ulirushwa live kwenye mitandao ya kijamii, alisena maneno aliyotamka Lissu hakuona kama yanashida yoyote ile. Part 496 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
58
537
10
1,470
102,214
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Leo November 6, 2026 Last time tuliishia part 493 so leo tunaendelea na -; Part 494. Karani amewasha kipaza sauti kutoa Tangazo kuwa watu wakae kwenye viti vyao na simu zao wahakikishe zinatolewa sauti na milio ya aina yote. Waandishi wa Habari na wao wako wakutosha sijawahi kuwaona Mahakamani kwenye kesi yoyote wakiwa wa idadi hii ni wengi sana sana. Hata waandishi ambao huwa hawajagi kabisa naona wamekuja, namuona yule Charles William wa Wasafi nae leo yupo kuna mtiti hapa unataka kutokea, wanataka kumnyayua Mzee Mpoki alienda kukaa viti vya Mawakili wa Serikali 😂😂😂 Wale watoto wa serikali ambao huwa wanakaa kwenye benchi la nyuma ya akina Katuga, leo wamekaa mawakili wa Mhe. wabishi hatari wamegoma kusimama. Ameingia Mheshimiwa Lissu akiwa na vibe na kusema TUTAFIKA! TUTAFIKA! TUTAFIKA! Wameingia Mawakili wa Serikali. MAJAJI walikwisha ingia hata kabla Mawakili wa Serikali hawajaingia. Muda huu wanawasha zile mic zao ili tuendelee. Jaji Ndunguru anasema karani tuendeleeee. Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasoma namba ya shauri karani. Anasimama Katuga anajitambulisha niko na wenzangu Job Mrema, Cathbert mbiringe ba Winniwa Kasala Tunaiwakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo. Shauri linakuja kwa ajili ya uamuzi na upande wa Jamhuri tuko tayari. Mshitakiwa vipi wewe? Mheshimiwa Lissu anasema niko tayari pia. Majaji Wanateta pale kabla hawajaanza kuusoma huo uamuzi. Jaji Ndunguru anasoma, naomba tusikilize Hukumu. Katika shauri hili Mshitakiwa Tundu Lissu anashitakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)d kanuni ya Adhabu 2023. Maelezo yanasema kwamba Tarehe 03/04/2025 Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam mshitakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Kudhihirisha nia hiyo kwa kitendo cha kutamka maneno ya wanasema kitu kimoja sahihi kwamba msimamo huu unaashiria uasi na tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kuleta mabadiliko na huu uchaguzi tutauvuruga. Mshitakiwa alikana hati ya mashitaka na shauri likaanza kusikilizwa. Kama ilivyo kawaida upande wa Mashitaka waliongozwa na Wakili Renatus Mkude na Ajuaye Zengeli na Nasoro Katuga na anawataja Mawakili wote wa Serikali. Upande wa Mashitaka walileta mashahidi 17 na ambao kati yao 17 walikuwa ni mashahidi wanaolindwa. Na mshitakiwa alijiwakilisha Mwenyewe na alileta Mashahidi wanne na yeye alikuwa watano na pia utetezi walitoa vielelezo anbavyo ni 16. Baada ya upande wa mashitaka kutoa ushahidi na mshitakiwa alijitetea na walileta hoja za majumuisho walileta hoja hizo. Mahakama hii iliongozwa na kanuni mbalimbali ni 1. Katika Mashauri ya Jinai mwenye jukumu la kuthibitisha ni Upande wa Mashitaka. 2. Kutiwa hatiani kwa mshitakiwa hakutazingatia udhaifu wa mshitakiwa. 3. Ushahidi utatazamwa kwa ujumla wake na sio vipande. 4. Mashaka yoyote hata kama yana uzito kiasi gani hayabadilishi burden ya kuthibitisha shitaka. Mahakama hii imechunguza kwa umakini hati ya mashtaka, ushahidi na mawasilisho ya pande zote mbili na kuja viini vitatu vya kuthibitisha Moja: Iwapo Mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT Mbili: Iwapo Mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali. Tatu: Iwapo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kusambaza maneno hayo. Mahakama imeona ni vyema ifafanue kwanza katika hoja ambazo zinaonekana kama mapingamizi wakati wa hoja za majumuisho ya mshtakiwa. Kwa kuwa hati ya mashtaka ndio inayoanzisha shauri la jinai ni vyema tuamue kwanza kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka. Mshtakiwa alisema hati ya mashtaka ina mapungufu katika maeneo matatu moja kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kinazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu, pili hati ya mashtaka haikutoa taarifa muhimu ambazo zilipelekea ashindwe kutoa utetezi kamili na tatu hakuna lengo lilioonyeshwa katika hati ya mashtaka. Part 495 itaendele kwenye post inayofuata Naomba Repost yako.
59
619
5
1,635
82,332
Hakika leo ni siku ngumu kwa wapenda haki
Leo ni siku nzito sana kwa mioyo ya watu wengi ila Huzuni ya leo isiue matumaini ya kesho. 🕊️🇹🇿 A new generation for TANZANIA will born again 👊👊👊👊👊👊👊👊👊✌️✌️✌️✌️✌️✌️✌️✌️
1
1
1
78
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 493 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Naomba nimalizie hoja ya mwisho ambayo ilikuwa ni maelezo yaliyoko kwenye witness statement na ushahidi uliotolewa mahakamani. Tutawaalika D1 hadi D16, what exactly kilichofanyika ni kuonyesha ommissions kwa asilimia kubwa na hata kama kulikuwa na contradictions zilikuwa minor which do not go to tje root of the case, kwa mfano aliyekosea dini, hiyo ni contradiction inayoenda kwenye root of the case kuliko aliyesema anagari 2 then baadae akagundulika ana gari 5 yeye ndio aaminiwe? Ushahidi wa hao mashahidi ulikuwa chini ya kiapo na wanapaswa kuaminika, maneno haya yapo kesi ya Abel Orua Matiku and others vs Republic criminal appeal no 441 of 2020. Kwenye maelezo yote hakukuwa na inconsistency isipokuwa ommissions na ushahidi wao haujahama kutoka kwenye msingi uliopo kwenye vielelezo hivyo ina defeat kifungu cha 163 cha CPA kuhusu contradictions, na kama zipo ni very minor, ni submission yetu kwamba kwa ushahidi wetu wa mashahidi 17 tumethibitisha pasipokuacha shaka na mtakapokuwa mnachambua ushahidi mshtakiwa awe convicted as charged. Waheshimiwa majaji naongea na wenzangu wanasema hawana cha kuongeza kwa kile ambacho nimefanya submission. Waheshimiwa Majaji kwa kumaliza kusema hayao tunaomba sekunde 5 tuweze kuwashukuru maana shauri hili lilianza mwaka jana septemba hadi mwishoni septemba 2026 kwa kusikiliza mashahidi wetu 17 na watano waliotusaidia. Tunawashukuru sana kwa jinsi Mahakama ilivyo to treat kama binadamu pale ambapo tulikosea. Tunamshukuru pia kaka yetu kwa umri na taaluma, mbali na maneno makali hayakuweza kujenga kitu kibaya isipokuwa tafsiri ya sheria na kwa upande wetu ilikuwa to discharge wajibu wetu katika kuthibitisha shtaka na kwa kifungu hiki ambacho kinakuwa tested kwa mara ha kwanza. Ni hayo tu kwa upande wa Jamhuri. Mara baada ya Wakili Katuga kusema kuwa amemamaliza kuwasilisha submission kwa upande wa Jamhuri. Jaji anamuuliza Mshitakiwa una rejoinder yoyote? Mhe. Lissu anamjibu huku anacheka, Waheshimiwa Majaji, mimi nilimaliza jana sina lingine. Majaji wanacheka. 😀😀😀 Jaji Ndunguru amemwambia kumchomekea akijua kabisa hawezi kuwa na la kusema kwasababu zamu yake ilishaisha. Jaji Ndunguru anasema basi tunashukuru shitaka lilikuwa refu sana, tunawashukuru pia hata Wananchi pamoja na kwamba walikuwa wanatuchochea kufanya fujo kidogo lakini hatukuchocheka. Kwa leo tunaishia hapa. Ngoja tupate muda ili tuweze kufanya kitu kwa ajili ya hukumu. Tutafakari neno kwa neno. Tarehe 06/11/2026 tutatoa hukumu. Naomba Repost yako.
43
239
8
686
36,470
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 492 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Katuga anasema kuna hoja ilitolewa kuwa mashahidi wa jamhuri sio competent and lack credibility kwasababu they were acting under their superior Ramadhan Kingai na IGP Wambura kuwa waliwahi kushiriki kumshtaki mshtakiwa mara kwa mara. Tunaalika Mahakama kuangalia ni sheria gani inasema hawa sio competent? Ni submission yetu kuwa hakuna sheria ya namna hiyo. Ni maneo ya Popart Emmanuel vs Republic criminal appeal no 200 of 2010 at page 5 as a regard to the reliance of witness from one office we know no law which states that they are not competent, police officers are competent to testfy, what is important is what they are saying is true. Mahakama ilisema walikuwa competent to testfy. Kesi inayotafsiri kuwa kila shahidi ni competent ni DDP vs Sharif Mohamed and 6 Others criminal appeal no 74 of 2016 CAT walisema kila mtu ni competent to testfy mwenye knowledge na matter at issue at the trial. Kulikuwa na hoja kuwa hawawezi kutestify sababu walijiandika maelezo yao wao wenyewe, utetezi huu haukuwa supported na kifungu chochote cha sheria rather rejea ya kifungu cha 11 cha CPA kinachosema Polisi anaweza kumuandika mtu yoyote maelezo. Kifungu hiki hakijaweka utaratibu wa je huyo polisi anayefanya investigation anaandikwa maelezo na nani? Kwakuwa hakuna kifungu mahususi kilicho restrict police anayepeleleza kuandika maelezo yake na declaration kuahidi kuandika maelezo kwa usahihi, kwahiyo hakuna kosa linalopelekea shahidi huyo kutokuwa competent. Waheshimiwa majaji hoja nyingine ilikuwa kwamba hao mashahidi ambao ni polisi officers na wale mashahidi ambao walichocheka wale wenye majina ya P ni mashahidi ambao wana interest to save. Tukianza na washtakiwa ambao walikuja kutoa ushahidi kifungu cha 151 cha Sheria ya Ushahidi kinasema an accomplice shall be a competent witness, kama walichocheka na maneno ya mshtakiwa ni washtakiwa wenza. Waheshimuwa majaji hoja kuwa mashahidi hawa wana interest to save wameiambia mahakama uongo, hoja ni kwamba waliona kideo au hawakukna,? Walichocheka au hawakuchocheka? Lalamiko kuwa wana interest to save yasichukuliwe kwa uzito, kesi ya Basil John Mlay vs Republic criminal appeal no 306 of 2018. Part 493 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
8
184
3
544
24,970
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 491 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Jaji Ndunguru anamwambia Katuga, hebu rudia tena hapo. Kutokuwepo kwa video haimaanishi kwamba mashahidi wa Jamhuri hawawezi kuthibitisha hoja ya kwamba walisikia maneno hayo ya uchochezi iliyoko kwenye YouTube channel ya Jambo. Video ya Jambo matumizi yake ilikuwa just to back up ushahidi wa mashahidi waliosikia na sio kwamba kutokuwepo kwa video maana yake mashahidi hawa hawaaminiki. Kila shahidi anastahili kuaminiwa unless mahakama iwe na sababu za kutokumwamini shahidi huyo. Maneno hayo yapo kwenye kesi ya Goodluck Kyanda versus Jamhuri (2006) TLR ikieleza haki ya mashahidi kuaminiwa. Kama ambavyo tumesema mashahidi waliona na wakachocheka na mshtakiwa anasema alitamka hayo maneno hivyo mtaona jinsi gani ushahidi wa defense una carry forward kesi ya Jamhuri. Suala kwamba oral testmony inaweza kuthibitisha documentary evidence inaelezwa kwenye kesi ya Abbas Kondo Gede vs Republic criminal appeal no 472 of 2017 CAT ilisema therefore, oral evidence if worth of credit is sufficient without documentary evidence to prove a fact or title. Thus where a fact may be proved by oral evidence it has not neccessary that documentary evidence must substitute oral evidence. Hivyo inaweza kuthibitishwa without even kutoa documentary evidenve ambayo ni video Ni hitimisho kuwa manifestation imethibitishwa pasipokuacha shaka regardless ya kutokuwepo kwa hiyo video. Tunajua kwamba ni jukumu letu kuthibitisha shtaka pasipokuacha shaka, ila tumewarejesha kwenye ushahidi wa Jamhuri, mahakama inapotoa uamuzi inalazimishwa to consider utetezi wa mshtakiwa, ni rai ya Jamhuri kuwa mahakama ni muhimu kuangalia theory ya defense na ni wazi kwamba ushahidi wa utetetzi umeshindwa kabisa kuonyesha doubt ushahidi wa Jamhuri. Katika kujaribu kuweka matundu kwenye prosecution case, upande wa utetezi ulisema kulikuwa na mikanganyiko na mapungufu katika ushahidi. Waheshimiwa majaji mapungufu ambayo yalionyeshwa na upande wa utetezi ni minor na hayana madhara kwa maana hayaendi to the root of the case. Minor contradictions ni vitu ambavyo haviepukiki wakati wa trial kwasababu kila shahidi anatoa ushahidi jinsi alivyoona, alivyosokia yaani zile sense za ushahidi. Minor contradictions na discrepancies ni msimamo wa kisheria kwamba zinaithibitishia mahakama kuwa sio mashahidi waliokuwa coached before testfying rather wanatoa ushahidi kulingana na nature ya ushahidi wao. Ni msimamao wa kisheria kwamba contradiction ambayo haiendi to the root of the matter ichukuliwe kawaida tu. Kuna neno la kilatini linasema De minimis non curat lex , meaning “The law does not concern itself with trifles.” Waheshimiwa majaji haya maneno yanatoka kwenye kesi ya Mussa Mbelechamo vs Republic criminal appeal no 912 of 2023 katika ukurasa wa 8 wanasema minor contradictions do not affect conviction. Ni submission yetu hizo minor contradictions does not affect the root of the case.. Part 492 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
15
186
3
573
25,264
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 490 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Waheshimiwa majaji kwanini mashahidi watatu kati ya 17 wa Jamhuri wameeleza maneno ya law and order? Kifungu cha 132 cha Cap 6 kinasema hakuna namba mahsusi ya mashahidi inayotumika kuthibitisha existence ya hoja fulani, hata mmoja anatosha, mbali na namba hii ya mashahidi wa jamhuri kuthibitisha na kufafanua kwanini maneno ya mshtakiwa ni uhaini inatosha kuthibitisha. Naomba niende sasa hoja ya tatu kama nia ya mshtakiwa ilidhihirishwa. Tumeomba mahakama ku note kwamba hakuna dispute kuwa mshtakiwa alitamka hayo maneno, hoja mnayotakiwa kuitolea uamuzi kuwa aliisambaza? Ambapo kwenye Oxford Dictionary publication is to make something known to the public. Ukiangalisha ushahidi, manifestation ilifanyika by deed of uttering and publishing alleged words (kwa kitendo Chake cha kutoa na kusambaza, kutoa maneno hayo kwa umma). Kuhusu kusambaza hapa kuna aina mbili ya publication ya haya maneno. Maneno haya kwanza yalisambazwa kwa mara ya kwanza tarehe 3/4/2025 kwa watu walioko kwenye mkutano, ikiwemo PW17 katika ukurasa wa 491 anasema alisikia mshtakiwa akisema tutazuia uchaguzi na tutakinukisha, kwahiyo tayari kwa shahidi huyu hiyo nia ilikuwa known, ilikuwa communicated kwa huyu shahidi lakini ni ushahidi pia kuwa DW2 anakiri kuyasikia hayo maneno na DW3, DW4 Publication ni to make it known kwahiyo haya maneno yalikuwa communicated kwa watu waliokuwepo kwenye mkutano. Maneno haya pia yalisambazwa kwa umma kwenye social media specifically YouTube. PW17 alisema kwamba walikuwa wanafanya livebroadcasting ya mkutano huo, ushahidi ambao umeungwa mkono na upande wa utetezi na ililetwa hoja kuwa mshtakiwa sio yeye aliyealika mkutano wala kuwaalika waandishi wa habari. Ukisoma ushahidi wa PW17 katika ukurasa wa 497 anasema, we livestreamed the video through you. Kuhusiana na ushahidi wa mshtakiwa kwamba sisi mimi niliyefanya mkutano, is immaterial, suala la mahakama kujiuliza ni kwamba mshtakiwa alisambaza au hakusambaza? Aliandaliwa speech au hakuandaliwa? Majibu ya utetezi ni kuwa hakuandaliw speech, ni ushahdii wa mshtakiwa katika ukurasa wa 590 anasema we held the meeting which is the subject of this case na through huo mkutano ndio alisambaza hayo maneno. PW17 nae alisema kuna muda alisema waliambiwa waondoke kwaajili ya mambo yao mengine ya ndani Mshtakiwa alisema pale ambapo tunataka kupublish matter zetu kwa umma tunaalika waandishi wa habari. Mkutano ulikuwa livestreamed, alitaka umma ujue, umma umejua anasema tena yeye hajasambaza. Waheshimiwa majaji tunatafsiri sheria kiupande upande, kwa ushahidi huu ni wazi mstakiwa alikusudia na amesambaza nia yake kwa umma , hivyo tunasema jamhuri imethibitishwa pasipo na shaka. DW3 anasema mshtakiwa alitaka taarifa yake iufikie umma wa watanzania, mshtakiwa mwenyewe anasema kuwa ukiona waandishi wa habari ni kwamba wanataka taarifa yao iwafikie umma. Utetezi wao ni best evidence kwasababu mshtakiwa alitaka taarifa yake iwafikie umma waweze kuchocheka, baada ya kuchocheka walikamatwa, wakatoa ushahidi mahakamani. Waheshimiwa majaji mnaweza kuambiwa kwamba hao mashahidi wanaosema waliiona video, video iko wapi? Video ni moja ya electronic evidence, ushahidi wa ki elektroniki ni document kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Ushahidi. Ikiwa document inamaanisha ni moja ya admissible document, kuna oral testmony, kuna real evidence (ushahidi wa exhibits), hizi aina sa ushahdii kisheria hakuna kubwa zaidi ya mwenzie. Absence ya documentary evidence haimaanishi kwamba it can be proved by oral testmony. Part 491 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
8
186
2
532
20,176
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 489 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Katuga anasema Treasonable intention ya mshtakiwa pia inathibitishwa kwa kauli aliyoitoa tarehe 03/04/2025 hapa pia upande wa Jamhuri unabebwa na upande wa defense, DW4 Brenda Rupia yeye anasema alikuwepo tarehe 03/04 na alimsikia mshtakiwa akisema kwani tukikinukisha watatuua? Si watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini? Hivyo mshtakiwa alitamka akiamini kuwa atafunguliwa kesi ya uhaini. Ni kitu gani ambacho Waheshimiwa majaji mtakitafuta kuthibitisha nia ya uhaini?? Waheshimiwa Majaji kwenye shauri nililolitaja ushahidi wa mshtakiwa ni the best evidence dhidi yake alivolunteer kuyasema hayo. Waheshimiwa majaji mahakama yenu sasa itajiuliza kweli zile kauli zilichochea umma? Upande wa mashtaka umeleta mashahidi waliochocheka na maneno ya mshtakiwa na wanatoka sehemu tofauti tofauti ya umma wa watanzania ambao ni named kama P. Mashahidi hao wote waliiambia mahakama ni kwa jinsi gani walichocheka na maneno ya mshtakiwa, wanachama, wafuasi, wengine wapenzi wa mwenyekiti ambaye hapa ni mshtakiwa. Kwenye ukurasa wa 397 wa records unaonyesha kwamba alichocheka kwa kiwango ambacho kinamleta chuki na alipanga kumsapoti mwenye kwa kuungana kupinga kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa kuwapiga na kuwarushia mawe. Ushahidi wa mashahidi hawa unaungwa mkono na DW2,3,4 waliunga mkono kuwa mshtakiwa hakufafanua alipotamka maneno tutazuia uchaguzi, au tutahamasisha uasi, tutavuruga uchaguzi au kukinukisha. Ushahidi wa utetezi ni kwamba watu waliosikia hotuba ya Mwenyekiti wana haki na kutafsiri kwa kadri wanavyoona inafaa. Point hiyo tunasema hao watu wana haki ya kuamini na kufanyia kazi uchochezi uliofanywa na mshtakiwa tukikopa ushahidi kutoka kwa mshtakiwa mwenyewe akiiambia Mahakama kuwa yeye ni mtu wa kuheshimika na kuaminika na watu, huu ushahdii nao pia una carryforward kesi ya Jamhuri kwani anaaminika na kuheshimika. Ni submission yetu kwamba kupitia haya maneno kwenye hati ya mashtaka na ushahidi wa Jamhuri ulioungwa mkono na upande wa utetezi ni wazi kwamba mshtakiwa aliform intention to isntigate the public to intimidate the public na kwamba maneno hayo yalilenga Serikali yenye wajibu wa kusimamia sheria na kuvuruga uchaguzi ni kuitisha mamlaka inayosimamia sheria ambayo ni serikali. Maelezo kuwa maneno hayo yalitolewa kwa nia ya kuitishia serikali yaliungwa mkono na ushahidi wa PW16 kwenye ukurasa wa 445, kuwa kuzuia uchaguzi, kuhamasisha uasi yalilenga kuvuruga amani ya nchi. Maneno ya shahidi huyu yanaungwa mkono na ushahidi wa DW1, ukurasa wa 619 anasema serikali ina wajibu wa ku administer na kuenforce sheria zilizotungwa na Bunge na ukurasa wa 622 kuwa Police ndio wana maingain law and order na ukuraswa wa 813 DW4 Brenda alisema ni Police ndio wanawajibu wa maintain peace and security na DW5 alisema executive ndio ina wajibu wa to maintain peace and ordee. Waheshimiwa ni rahisi sasa kuona kumbe kuchochea umma, kuvunja amani ni as good as good ni kumtisha yule mwenye majukumu hayo ambaye ni executive regardless kama ametishika au hajatishika, hivyo maneno hayakulenga Mahakama au Bunge. Waheshimiwa Majaji Ibara ya 147(2) ya Katiba ya JMT inaelekeza kwamba serikali itakuza na kuimarisha majeshi ya aina mbalimbali kwaajili ya usalama na ulinzi wa watu wa Tanzania. Ushahidi wa PW16 unaungwa mkono na kifungu cha 5(a)(b) cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Wasaidizi wake Cap 322 kwamba ni jukumu la serikali kulinda amani. Hapa pia tunakopa ushahidi wa DW1 kwamba Polisi inafanya kazi chini ya Serikali na iia jukumu la to maintain law and order ukijumuisha na kesi ya Hamisi chuma supra hivyo unavyotishia jeshi la polisi unatishia walinzi wa amani ambao ushahidi huo umeungwa mkono na DW1-DW4. Part 490 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
17
209
3
576
24,282
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 488 Upande wa Jamhuri wanaendelea kufanya Mawasilisho yao ya mwisho yani Final Submission. Katuga anasema Mashahidi wote wa Jamhuri waliyosikia hayo maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, walisema waliyasikia kupitia YouTube ya Jambo Tv na PW17 mtumishi wa Jambo Tv aliyasikia na kuyarusha moja kwa moja. Wakati wa maswali ya dodosa kuhusu kutamka maneno hayo, mshtakiwa hakudodosa ila tu alisema maneno hayo yanatengeneza kosa? Hivyo ushahidi huo haukudodoswa na uliungwa mkono na mashahidi wote wa utetezi, mshtakiwa mwenyewe alisema ni kweli alitamka hayo maneno lakini anachokipinga yeye ni kuyasambaza kwa umma, DW2 alisema pia mshtakiwa alitamka hayo matamshi. Kwahiyo kupitia ushahidi wa jamhuri ulioungwa mkono kuwa hakuna dispute mshtakiwa kutamka maneno haya tarehe 03/04/2025 Hivyo hayo maneno yaliyotokana na hotuba ndefu ya mshtakiwa ni maneno yenye sentensi timilifu na zenye kueleweka. Ushahidi uliotolewa na jamhuri umeelezea jinsi ulivyoyapokea na kuyaelewa hayo maneno na yalieleweka kwa mashahidi wa upande wa jamhuri, PW1 alieleza kuwa maneno hayo yalilenga kuitishia serikali. Mbali na mashahidi kusema kuwa waliyaelewa na kuyatafsiri, bado ushahidi wao unaungwa mkono na ushahidi wa DW3 ambaye nae anaunga mkono kwamba maneno yalikuwa quoted kwenye hati ya mashtaka ni maneno yaliyotimilika na yenye kuleta maana, vilevile DW4 Waheshimiwa majaji sasa tuyatafsiri basi maneno yenyewe tuone kama yana maana au hayana maana, neno uasi limetafsiriwa kwenye kamusi kuu ya kiswahili kwa kumaanisha kwamba uasi ni kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu kwa lengo la kujaribu kubadili mfumo wa kisiasa wa nchi yao. Tafsiri ya pili uasi ni kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka au kupinga sheria na taratibu zilizopo kama vile katika taasisi, shirika au chama (kisawe chake yaani synonymous yake ni uhalifu. Kwa mazingira ya kesi tafsiri ya kwanza ndio ina fiti. Ni ushahidi wa DW3 katika ukurasa wa 819 slogan ya no reforms no election ililenga kuleta mabadiliko kwenye siasa za nchi. Kwenye ukurasa wa 829 DW3. Tunajua sio jukumu la utetezi kuthibitisha kesi lakini ni msimamo wa kisheria kwamba ushahdii wa defense unaweza kuibeba mbele kesi ya Jamhuri. Msimamo huu upo katika kesi ya Hamisi Chuma Hando Muhoja versus Republic criminal appeap no 36 of 2018 citing with approval case ya Haruna mtopeni vs R CAT ilisema accused person akitoa ushaidi unaoipeleka kesi ya jamhuri mbele mahakama itatumia ushahidi huo katika kuamua kuhusu hatia yake. Nimeleta hii kesi japo ushahidi tunaoutumia ni wa Brenda Rupia shahidi wa defense tunaomba mahakama hii iutumie na tafsiri ya kwanza ya neno uasi. Tafsiri ya neno uasi lilikuwa ni kuhamasisha uvunjaji wa sheria ili kuleta mabadiliko. Part 489 itaendelea kwenye post inayofuata, Naomba Repost yako.
15
216
1
604
24,051
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 487 Tumerejea mchana huu baada ya mapumnziko. Anasimama Katuga anasema quorum iko kama asubuhi na wako tayari kuendelea. Anasema naomba kuendelea na kiini cha shitaka namba 2 baada ya kile cha kwanza kwamba mshitakiwa ana duty ya utii. Upande wa Jamhuri unasema kwamba mshitakiwa kwa ushahidi uliotolewa imethibitika kwamba alitengeneza nia ya kuchochea umma kwa nia ya kuitisha serikali ili ifanye yale anayoyataka. Na hiyo ni kutokana na sentensi au maneno yakiyotamkwa na mshitakiwa na upande wa mashitaka kuyanukuu kwenye hati ya mashitaka. Maneno hayo utaona mshitakiwa akieleza umma kwamba kuhamasisha uasi ni namna ya kupata mabadiliko. Utaona anasema kukinukisha ni namna ya kupata mabadiliko. Kwahiyo maneno yenyewe yaliyotumika kwenye mashitaka yakithibitishwa yametamkwa na mshitakiwa tafsiri yake vile yakivyokaa yalilenga ku compel kuitishia serikali iweze kufanya anayoyaamini mshitakiwa yanatakiwa kufanywa. Waheshimiwa Majaji neno uchochezi au instigation kwenye hati ya mashitaka kabla ya kwenda kutengeneza nia ya ku instigate ni busara tunaona Jamhuri tupate tafsiri ya neno to instigate. Katika Mahakama Supreme Court ya India katika kesi ya Mahendra KC vs State of Karnataka and another Criminal Appeal No. 1238/2021 walidefine to instigate Is to provoke, insight, .... Katuga kingereza chake kina matege sana haeleweki anatakamka nini? Mdomo mzito unaweza kudhan anaongea kisukuma. Kwa tafsiri hiyo unaweza kuwa uchochezi maneno au conduct lakini uchochezi huo labda u suggest madhara au unajitosheleza na uchochezi huo uwe capable kuwekwa hadharani. Sasa Mahakama tunaialika iyapime maneno yakiyopo kwenye hati ya mashitaka kwamba yalichochea umma kwa nia ya kuitisha Serikali. Tunaomba Mahakama i note kitu muhimu kuhususiana na maneno haya. Maneno haya hayajakubalika katika kipindi cha PH lakini wakati wa usikilizwaji upande wa Jamhuri kupitia mashahidi wake 16 isipokuwa PW 3 walieleza kumsikia mshitakiwa akitamka maneno haya yaliyotamkwa kwenye hati ya mashitaka. Part 488 itaendelea kwenye post inayofuata. Naomba Repost yako.
18
222
2
615
25,245