JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE) header
JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE) profile picture

Kenyan Great Thinkers, We Dare to Talk Openly!

Nairobi
Joined June 2011
Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)Photo by JamiiForums Kenya (@JamiiForums_KE)
Kundi la waumini wanaohusishwa na huduma ya Ministry of Repentance and Holiness ya Nabii David Owuor limezua mjadala baada ya kuonekana mitaani wakiwa wamevalia mavazi yanayofanana na magunia Picha na video za kundi hilo zikitembea katika eneo la kibiashara zimesambaa mitandaoni, huku baadhi ya waumini wakiwa wamefunika vichwa. Muonekano huo umeibua maswali kuhusu maana na ujumbe wa mavazi hayo. More jamii.app/MavaziKanisaOwuor #JamiiForumsKE #KenyaNews
12
Wafanyakazi wa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) jijini Nairobi wamegoma wakilalamikia kutowasilishwa kwa makato ya kisheria kutoka kwenye mishahara yao pamoja na kushindwa kwa uongozi kutatua changamoto zinazohusu ustawi wao Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali wamekusanyika nje ya majengo ya hospitali wakitaka masuala yao yashughulikiwe. More jamii.app/KNHWagoma #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
1
99
Jamii ya wapenzi wa mchezo wa skating jijini Nairobi inaomboleza kifo cha Anita, maarufu kama Dimple, aliyefariki katika ajali ya barabarani eneo la Bulbul, barabara ya Ngong Hills Anita ni miongoni mwa wanawake wawili waliofariki baada ya pikipiki mbili kugongana na lori lililoripotiwa kufunga breki ghafla. Waendeshaji wa pikipiki hizo walinusurika na kupata majeraha. More jamii.app/SkaterDimpleAfarik… #JamiiForumsKE #KenyaNews
6
1,662
Baraza la Magavana limewaagiza wasimamizi wa hospitali za kaunti kupuuza agizo la serikali ya kitaifa la kuondoa nambari za malipo za Paybill katika hospitali za umma, likisema hatua hiyo inaweza kuvuruga huduma na kuingilia mamlaka ya serikali za kaunti Limesema agizo hilo linakiuka misingi ya ugatuzi, inayozipa kaunti mamlaka ya kusimamia hospitali na huduma za afya, na kuwa kaunti zina haki ya kutumia njia halali za kukusanya malipo ya huduma ambazo hazijajumuishwa katika bima ya SHA More jamii.app/MagavanaVsSerikali #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
13
Wanafunzi kadhaa wanailalamikia taasisi ya mafunzo ya Breakthrough International Training mjini Thika, kwa madai ya kuwasajili katika kozi ambazo hazipo au hazitambuliwi More jamii.app/ThikaStudents #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
50
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Erastus Ethekon, ameonya kuwa kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka vituo vyote 50,000 vya kupigia kura Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 kunaweza kuongeza gharama za uchaguzi Ni kutokana na ununuzi wa kamera, mafunzo ya waendeshaji na usambazaji wa vifaa na utekelezaji wa mpango huo utahitaji uwekezaji mkubwa na maandalizi ya kutosha More jamii.app/UchaguziMubasharaG… #JamiiForumsKE #KenyaNews
14
Mahakama Kuu imemuagiza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufika mahakamani Desemba 3, 2026, kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa kutoweka kwa mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Mwaipaya, anayedaiwa kutekwa Ruai, Nairobi, Oktoba 25, 2026 Jaji Alexander Muteti amesema DCI anatakiwa kueleza hatua zilizochukuliwa kumtafuta Mwaipaya, akibainisha kuwa ofisi ya DCIO Ruai inayoshughulikia kesi hiyo iko chini ya usimamizi wa DCI More jamii.app/DCIKizimbaniMwaipa… #JamiiForumsKE #KenyaNews
26
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Fred Matiang’i, amemshutumu Rais Ruto kwa kuwapotosha Wakenya kuhusu madai ya uchapishaji wa mitihani ya kitaifa ya mwaka 2026 nchini kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 65 Matiang’i amedai kuwa kumbukumbu za usafirishaji zinaonyesha vifaa vya mitihani vililetwa kutoka Ugiriki, jambo analolitumia kupinga kauli ya Serikali kwamba mitihani hiyo ilichapishwa nchini. More jamii.app/MatiangiMitihaniRu… #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
3
385
Video ya Morara kuhusu hali ya Shule ya Msingi ya Nyamkasi, iliyopo Borabu, Kaunti ya Nyamira, imeibua mjadala kuhusu uwajibikaji wa viongozi katika kuboresha miundombinu ya shule za umma Katika video hiyo, Morara anaonesha hali ya majengo na madarasa ya shule hiyo huku kiasi cha KSh 800,000 kikitajwa, jambo lililozua maswali kuhusu matumizi ya fedha hizo. More jamii.app/ShuleNyamkasiNyami… #JamiiForumsKE #KenyaNews
4
230
Video inayosambaa mitandaoni imezua wasiwasi kuhusu usalama wa chakula Kenya baada ya kuwaonyesha wanaume wakinyunyizia matikiti maji kemikali kwa kutumia kifaa cha kupulizia dawa Tukio hilo limeibua maswali kuhusu aina ya kemikali zinazotumika kwenye mazao na uzingatiaji wa taratibu za usalama wa chakula. More jamii.app/UsalamaChakula #JamiiForumsKE #KenyaNews
31
Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET) kimepinga mpango wa Rais William Ruto wa kuunganisha usimamizi wa shule za ECDE, msingi na Junior Secondary School chini ya mkuu mmoja wa shule Ruto alitoa agizo hilo Novemba 13, 2026, jijini Mombasa, akielekeza Wizara ya Elimu kuandaa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Elimu ya Msingi ndani ya siku 90, kwa lengo la kuanzisha mfumo wa Comprehensive Schools utakaounganisha usimamizi wa ngazi hizo za elimu More jamii.app/KUPPETMpango #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
1
138
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen, amepinga wito wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nyeri, Anthony Muheria, wa kuyataka makanisa kukataa michango ya fedha kutoka kwa wanasiasa Akizungumza katika ibada ya madhehebu mbalimbali iliyofanyika Marioshoni, Molo, Kaunti ya Nakuru, Murkomen alihoji kwa nini wanasiasa wanapaswa kuzuiwa kuchangia miradi ya makanisa ilhali watu wa taaluma nyingine, wakiwemo madaktari, wahandisi, wafanyabiashara na wakulima, hawapingwi wanapofanya hivyo More jamii.app/WanasiasaKanisani #JamiiForumsKE #KenyaNews
4
486
Wateja wa umeme Kenya wanatarajiwa kulipa zaidi katika bili za mwezi huu baada ya EPRA kutangaza ongezeko la jumla ya KSh4.56 kwa kila uniti (kWh) ya umeme Ongezeko hilo linajumuisha KSh3.54 za gharama ya mafuta ya kuzalisha umeme, KSh1.0031 za marekebisho ya ubadilishaji fedha za kigeni na KSh0.0136 za ushuru wa maendeleo ya maji More jamii.app/GharamaUmemeKupand… #JamiiForumsKE #KenyaNews
2
48
Aliyekuwa Mbunge wa North Horr, Francis Chachu Ganya, ameripotiwa kupatikana akiwa hai kando ya Barabara ya Ngong jijini Nairobi baada ya kutoweka kwa siku kadhaa katika mazingira yasiyoeleweka Ganya aliripotiwa kutoweka Novemba 21, 2026, hali iliyozua wasiwasi kwa familia na viongozi wa eneo hilo, huku Mbunge wa sasa, Adhe Wario, akizitaka mamlaka za usalama kuingilia kati kumtafuta. More jamii.app/MbungeNorthHorrHai #JamiiForumsKE #KenyaNews
2
113
Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimekubaliana kurejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia baada ya takribani miaka minne ya mvutano Makubaliano hayo yalifikiwa Novemba 22, 2026, katika mkutano wa viongozi wanne uliofanyika Oyo, Jamhuri ya Congo, ukihudhuriwa na Rais William Ruto, Felix Tshisekedi, Denis Sassou Nguesso na Faure Gnassingbé. More jamii.app/DRCUhusianoKE #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
2
95
Wakazi wa Syokimau-Katani, Kaunti ya Machakos, wameandamana kupinga hali mbaya ya barabara na kuitaka Mamlaka ya Barabara za Mijini Kenya (KURA) pamoja na Serikali ya Kaunti kuchukua hatua za haraka kuzirekebisha Wakazi hao wanasema uharibifu wa barabara umekuwa ukikwamisha usafiri, biashara na shughuli za kiuchumi, huku madereva na waendesha bodaboda wakikabiliwa na changamoto za mashimo na vumbi More jamii.app/MaandamanoShidaBar… #JamiiForumsKE #KenyaNews
4
287
Mvutano umeibuka kati ya Afisa wa Trafiki na mmiliki wa gari baada ya Afisa huyo kutaka kuliendesha gari hilo hadi kituo cha polisi, lakini mmiliki akakataa kumpa usukani Katika video inayosambaa mitandaoni, wawili hao wanaonekana wakibishana huku mmiliki akisisitiza kuwa hatamruhusu afisa huyo kuendesha gari lake. More jamii.app/MmilikiGariPolisi #JamiiForumsKE #KenyaNews
9
9
137
22,129
MCA wa Watamu, Ibrahim Matumbo, amezua mjadala baada ya video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha akiwagawia wakazi fedha taslimu za KSh 5,000 kila mmoja Tukio hilo limeibua maswali kuhusu chanzo na matumizi ya fedha hizo, pamoja na uwazi na uendelevu wa misaada inayotolewa na viongozi kwa wananchi. More jamii.app/MatumboHela #JamiiForumsKE #KenyaNews
2
236
Lugha ya Kiswahili imepata hadhi mpya katika soka la Afrika baada ya CAF kupitisha pendekezo la kuitambua kuwa mojawapo ya lugha rasmi za shirikisho hilo Pendekezo hilo lilitolewa na TFF katika Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika Abuja, Nigeria, Novemba 21, 2026, likiungwa mkono na FKF ya Kenya na FUFA ya Uganda. More jamii.app/KiswahiliRasmiCAF #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
1
134
Mashabiki wa soka Kenya wamepata pigo baada ya mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane, kutarajiwa kuukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ajax utakaofanyika Nairobi Januari 5, 2027 Ni kutokana na jeraha la kifundo cha mguu wa kushoto alilopata wakati wa mchezo dhidi ya FC Köln, Novemba 20, 2026. More jamii.app/KaneKuikosaNyayo #JamiiForumsKE #KenyaNews
1
1
145