Mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali,Ofisi ya Kanda ya ziwa,imehitimisha mafunzo kwa Wasimamizi wa kemikali ambayo yalilenga kukuza uelewa kuhusu usimamizi na Matumizi sahihi ya kemikali.Mafunzo hayo yamefanyika Novemba 18,2026.katika ukumbi wa TMDA,Jijini Mwanza.
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Ofisi ya Kanda ya Ziwa, imeendesha mafunzo kwa Wasimamizi wa Kemikali, yenye lengo la kuimarisha uelewa kuhusu usimamizi na matumizi sahihi ya kemikali.Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 17, Novemba, 2026, Jijini Mwanza.
1
50
Timu ya Riadha ya GCLA imeshiriki mashindano ya riadha na kukimbia na gunia kwenye michezo ya SHIMMUTA inayoendelea mkoani Morogoro Novemba 17,2026.GCLA imeibuka mshindi wa kwanza kwenye kukimbia na gunia na mshindi wa pili kwenye mbio za mita 800 kwa watu wazima kuanzia miaka 50
45
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali,ofisi ya Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo ili kuhamasisha matumizi salama ya kemikali.Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 16, Novemba ,2026,Jijini Mwanza
26
Timu ya Mpira wa Pete ya GCLA imefanikiwa kuingia 16 Bora baada ya kuifunga Timu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, kwenye mchezo wa mtoano ‘Round 32’ katika michezo ya SHIMMUTA, ambapo GCLA imeibuka na ushindi wa magoli 55 – 34 kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro leo.
36
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amefungua rasmi michezo ya SHIMMUTA 2026, katika kiwanja cha Jamhuri mkoani Morogoro Novemba 12, 2026.
20
Ofisi ya Kanda ya Kati, imeendesha Mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na biashara za matumizi ya kemikali yaliyofanyika katika ofisi za SIDO Mkoa wa Morogoro Novemba 9, 2026.
37
Timu ya Mpira wa Miguu ya Mamlaka ya @Gcla1895 imeibuka na ushindi wa magoli 2 : 0 kwenye mchezo wa leo dhidi ya Tengeru Institute of Community Development (TICD). mchezo huo wa Group J ulichezwa katika viwanja vya Ujenzi, jijini Morogoro Novemba 6, 2026.
1
29
Timu ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete za @Gcla1895 , zinaendelea na mazoezi kuelekea kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Kampuni Binafsi Tanzania (Shimmuta), yanayotarajia kuanza Novemba 6 hadi 21, 2026 mkoani Morogoro.
1
30
Ofisi ya Kanda ya Mashariki imetoa mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wafanyakazi wa kampuni ya uteketezaji wa kemikali taka iliyopo eneo la Fukayosi Bagamoyo, Pwani, Oktoba 30, 2026.
Aidha, Wafanyakazi hao wamejengewa uelewa kuhusu uteketezaji salama wa kemikali taka.
40
Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu katika maadhimisho ya Wiki ya Kujikinga na Sumu ya Madini ya Risasi,imeweza kutoa elimu kwa kutembelea viwanda vya Gravita na Balochistan vilivyopo Pwani kwa lengo la kuimarisha uelewa kuhusu usimamizi salama wa Madini ya Risasi.
37
Ofisi ya Kanda ya Mashariki, imetoa mafunzo ya Usimamizi na Usafirishaji salama wa Kemikali kwa madereva wanaosafirisha kemikali, mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mashariki, jijini Dar es Salaam
37
@Gcla1895 imefanya Kikao chake cha Nne cha Baraza la Nane la Wafanyakazi ambapo wamekutana kujadiliana utekelezaji wa mipango ya taasisi kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026 kilichofanyika Cate Hoteli mkoani Morogoro Oktoba 9, 2026.
38
Ofisi ya Kanda ya Mashariki, imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja kwa kujumuika pamoja na wateja katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam, Oktoba 8, 2026.




























































