diva retweeted
Kariakoo Derby Simba SC wataonesha Ubaya Ubwela dhidi ya mtani Yanga SC, Mchezo utakaochezwa Kesho Uwanja wa Mkapa.
Je, Simba Atafanikiwa kujitetea mbele ya Wananchi? Tabiri na Ushinde.
1. Follow @InfinixMobileTZ
2. Weka Utabiri wako kwenye comment section na watag marafiki zako watatu (Mfano; Simba SC 0 Vs. Yanga SC 0)
3. Re-tweet post hii
📌Washindi;
Wawili wa kwanza waliotabiri Kwa usahihi na kufuata vigezo na masharti
🎁Zawadi;
Mshindi wa kwanza - Infinix Towel Gift
Mshindi wa Pili - Infinix Towel Gift
📝NB; Utabiri wote utumwe kabla ya mchezo kuanza.
Vigezo na Masharti kuzingatiwa.
#Infinixtanzania #PredictAndWin
akaunti hii inanichanganya wazee nimelog in kwa Gmail naona eti hii akaunti inatumia Gmail yangu nimechanganyikiwa bora hata ingekua ya kiume
1
1
275
diva retweeted
KUTEKWA, KUPOTEA, KUTESWA, KUPATIKANA KWA SATIVA. 💔
Maelezo yote yametoka katika kinywa cha Edgar Edson Mwakabela, @Sativa255 ambaye alitekwa jumapili 23.06.2024 Darces Salaam na kupatikana 27.06.2024 Katavi.
Shughuli inaanza siku ya Jumapili, 23.06.2024, maeneo ya Ubungo. Edgar Edson Mwakabela aliagana na kaka yake Patrick, na akaanza safari ya kurudi Kimara.
Walitoka wote Coco Beach. Baada ya muda, Patrick alimuuliza kama amefika salama, hakujibiwa ujumbe wake, na simu za SATIVA baada ya hapo hazikupatikana tena.
SATIVA alikuwa anatafuta chumba, wakakubaliana na dalali kwamba hiyo sehemu ambayo anataka kuhamia, mpangaji katika nyumba hiyo anatoka mwezi wa (10) Oktoba.
Baada ya muda mfupi, dalali akarudi kumpigia simu SATIVA akimueleza kwamba jamaa katika nyumba ile ametoka hivyo anaweza kufanya malipo yake muda huo.
Wakati huo, SATIVA alikuwa amewaaga rafiki zake aliokuwa nao, akawa amechukua usafiri wa bodaboda, alipopigiwa simu na dalali, akabadilisha bodaboda yule.
Wakati akishuka na kutafuta bodaboda nyingine kueleka alipo huyo dalali, akawekwa mtu kati na watu watatu. Wakamfunga pingu na kumtupa katika gari waliyokuja nayo.
Watekaji hao walimpokonya simu zake zote tatu. Simu mbili walizima. Simu moja ikabaki hewani kwa muda mfupi, baadae simu zote za SATIVA zikawa hazipatikani.
Wakaondoka naye hadi kituo cha Polisi Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi - Kinondoni. Hapo wakamfikisha nyuma ya kituo cha Polisi Oysterbay, wanapaita 'karakana"
SATIVA akiwa karakana hapo majira ya saa 2 usiku, waliendelea kumuuliza, kosa lako ni lipi? Umewakosea jambo gani wakubwa hadi kuagiza ukamatwe na kuteswa?
Inavyoonekana, watekaji hao walikuwa na maelekezo ya kumteka SATIVA tu lakini hawakujua kwanini wametumwa kumteka. SATIVA aliwaambia hajui kitu yoyote.
Lakini katika maswali yao ya msingi waliendelea kumuuliza, rafiki zako ni akina Martin Maranja Masese na Boniface Jacob? Mnakutana wapi kupanga mambo yenu?
Akiwa hapo karakana ya magari ya kituo cha polisi Oysterbay, alifika mtu mmoja akiwa ndani ya gari aina ya VX V8 akashuka akiwa amevaa jezi ya timu ya Simba SC.
Mtu huyo chini alivaa pensi ya rangi ya kaki. Kwa muonekano wa nje alikuwa ni mtu wa mazoezi, mrefu wa wastani na siyo mweupe sana. Huo ni wajihi wake wa nje.
Mtu huyo aliposhuka kwenye gari akiwa pekee yake, wale waliokuwa pale walimpigia saluti, akamfuata moja kwa moja SATIVA pahali alipokuwa amefungwa pingu mikononi.
Akamuuliza, unaitwa nani? Katika mitandao ya kijamii unatumia jina gani? SATIVA akampa majibu. Baada ya hapo akawavuta pembeni wale watu waliokuwa na SATIVA pale.
Akatoa maelekezo kuwa kuna watu watakuja kumchukua SATIVA, afungwe katika Karakana ya Oysterbay. Akarudi katika gari aliyokuja nayo, ikawashwa, akasepa.
Usiku huo, SATIVA akafungwa pingu katika moja ya nguzo zilizopo katika hiyo karakana ya Polisi - Oysterbay. Wakiendelea kumuuliza SATIVA amekosa nini kikubwa hicho?
Wao walishangaa kiongozi mkubwa kufika hadi hapo Karakana ya Polisi - Oysterbay na kumuhoji SATIVA, jambo ambalo kwao siyo kawaida. Wakajiuliza, kosa lake nini?
Kwamba kiongozi mkubwa ameacha shughuli zake usiku hadi kumfuata hapo, kosa lake ni nini? SATIVA akawaambia kwa kweli hata mimi sijui gani nimefanya hadi sasa.
Kwa maelezo ya SATIVA anasema watu hao watatu waliomkamata awali, hawamkupiga isipokuwa waliendelea kumuuliza makosa yake hadi kuagizwa kuletwa hapo.
Tangu alipofikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay saa mbili na dakika 25 usiku, akafungwa pingu katika hizo bomba za karakana, amefuatwa alfajiri ya kesho yake.
Ilipofika saa 12 alfajiri ilimfuata gari ambayo haina 'playe number' za Tanzania. SATIVA akachukuliwa na kuwekwa katika gari hiyo, na huko ndani akakutana na sura mpya.
Hapo, wale waliomkamata tangu siku ya 23.06.2024 wakawa wamemaliza wajibu wao, akakutana na watu watu waliopewa kazi maalum ya kumtesa na kumuua.
Kitu cha kushangaza zaidi, ndugu na rafiki zake SATIVA walifika hadi kituo cha polisi Oysterbay, wakaelezwa mtu wa aina hiyo hajawahi kufikishwa kituo hicho cha polisi.
Polisi walipewa taarifa ya kupotea kwa SATIVA, na ikafunguliwa jalada katika kituo cha polisi Gogoni - Kimara, na polisi wakatoa Report Book (RB) Na.
Bado ndugu na rafiki zake waliendelea kumtafuta vituo vya Polisi vyote vikubwa na hospitali hadi mochwari, bado SATIVA hakuonekana na polisi walisema hawajui.
SATIVA anasema wakaanza safari ndefu sana, gari ikiwa mwendo, akiwa amefungwa kitambaa usoni. Lakini katika maongezi yao walisema uelekeo wao ni Arusha.
Tangu amekamatwa jana yake, hiyo ni siku nyingine, SATIVA hakuwa amekula au kunywa kitu chochote. Walipofika Mkoa wa Arusha, SATIVA akaomba apewe maji.
Lakini, wakiwa ndani ya gari kabla ya kumshusha walibadilisha aina ya matamshi yao ili SATIVA asiwasome. Mfano ugali wao waliisema ugaliwa. Wali walisema waliwa.
Wakiwa Arusha, walimshusha, akapelekwa katika moja ya mahabusu katika Mkoa wa Arusha lakini hakufanikiwa kufahamu ni mahabusu ya kituo gani cha Polisi.
SATIVA anasema katika hiyo mahabusu amewekwa kwa siku mbili. Kwa mantiki hiyo ni 25/06/2024 na 26/06/2024. Siku hiyo pili wakamtoa ndani ya mahabusu hiyo.
Wakaondoka naye kama wanampeleka katika moja ya mipaka ya Tanzania na kenya. Wakaendelea kumuhoji huko, saa saba mchana wakarudi naye Arusha Mjini.
Wakaanza safari ndefu, anasema walipofika katika moja ya mapori ambayo hajui ni wapi, gari ile ilisimama, wakatoa panga kubwa na kuanza kumpiga bapa za panga nyingi.
Katika mazungumzo yao yote wakati wakimpiga SATIVA mabapa ya panga, walikuwa wakimuuliza kama anatumwa na Boniface Jacob na Martin Maranja Masese.
SATIVA aliendele kusema hawajui watu hao na hajawahi kukutana nao pahali popote. Wao waliendelea kumtesa wakisisitiza kwamba awataje hao watu wanaomtuma.
Mgongo wa SATIVA umevia damu nyingi sana. Mabapa ya panga pia alipigwa sana kwenye kichwa, mapaja na miguu. Akapata maumivu makali sana kwenye miguu na kichwa.
Walimpiga mabapa ya panga zao mengi kwa muda mrefu wakiendelea kumuhoji SATIVA nani ambaye anamtuma kukosoa serikali ya CCM na kutukana viongozi wa nchi.
Mahojiano yao na SATIVA yalijikita katika kufahamu kama Martin maranja Masese na Boniface Jacob ndiyo wanaomtuma kufanya shughuli za kukosoa serikali yao?
Baada ya mateso makali sana, kiongozi wa msafara akaamuru waende wakamalizane naye haraka muda huo. Hapo imefika majira ya nne usiku wakiwa porini sana.
Wakamfunga kitambaa, wakamrudisha kwenye gari na safari ikaanza. Wakijadiliana kwamba, Katavi kuna wanayama wakali na misitu minene, waelekee huko.
Wakafika Katavi saa 10 kuelekea saa 11 alfajiri. Wakaingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, pembezoni ya mto Ikuu ambao unatajwa kuwa na viboko na mamba wengi.
Wakaegesha gari na kuanza kuingia naye msituni. Kuelekea ulipo huo mto Ikuu. Huko mahojiano yakendelea wakati huo akipigwa mabapa ya panga kila pahali. Noma.
Kwa maelezo yake SATIVA anasema alipigwa pingu na kitambaa usoni. Na wakamueleza kwamba biashara yake itakuwa imeishia katika msitu wa hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Kiongozi wa wauaji hao akatoa maelekezo kwa mmoja kati ya wauaji hao kwamba " mpige risasi huyo kibaka tumalizane naye twende zetu". Ikachapwa risasi kutoka kwa nyuma.
Risasi imepita kutoka kwenye upande wa kushoto wa kichwa, ikapita hadi kwenye shavu na kupasua taya mara mbili na kusaga taya. Damu zikamwagika nyingi akiwa chini.
Wakiwa hapo akasikia wakisema hapa kuna fisi wakali sana, ataliwa na fisi au mamba wakali kutoka katika mto huo au viboko wengi waliopo katika mto huo pembeni.0
Baada ya kama dakika mbili wakiwa hapo, akasikia wakiondoka, wakawasha gari. Akapoteza fahamu. Baadae akahisi mwili umepigwa baridi, akaanza kujivuta.
Akajivuta kwenda hadi ilipo barabara, na hapo ndipo akakutana na askari wa doria wa wanayamapori (TANAPA) na wakaanza kumuuliza maswali mengi ya ufahamu.
Sativa alipookotwa na hao watu wakiwepo askari wanyama pori Hifadhi ya Katavi, baada ya kumuhoji kidogo, akapelekwa kituo cha Afya Kibaoni njia ya kwenda Majimoto.
Na kuanzia hapo, hadithi nyingine yote mnaifahamu. Hivyo ndivyo rafiki yetu, Edgar Edson Mwakabela, SATIVA alivyotekwa na maharamia na kuteswa na kunusurika kifo.
NB; Kumbuka, hifadhi ya Taifa ya Katavi katika kundi la wanyama wakali kuna viboko 5,400. Simba 190. Fisi 750. Mbwa mwitu na Mamba sensa haijafanyika. Noma.
Martin Maranja Masese, MMM.
diva retweeted
HII WANAIITA LAANA YA CARL PRUITT.
Mwaka 1938 wakati Carl anarejea nyumbani huko Pulaski, Kentucky US kutoka mihangaikoni akitarajia kumkuta mkewe jikoni akipika kama ilivyokuwa kawaida yake.
Siku hiyo mambo yalikua tofauti kwani alimkuta mkewe chumbani akiwa na mwanaume mwingine.
Jamaa baada ya kufumania akachukua mnyororo na kuwanyonga nao wote mkewe na mchepuko wake, baada ya kuwauwa nayeye akajiuwa.
Licha ya Carl nayeye kufa lakini familia yote ya mkewe ilikataa kumsamehe jamaa, na akazikwa mbali kabisa na alipozikwa mkewe, mji mwingine kabisa, ndugu wa mkewe walikasirika sana kwa kitendo cha Carl kumuuwa mkewe.
Baada ya miezi miwili katika kaburi la Carl kulianza kuonekana kitu ambacho hakikuwa cha kawaida, kulianza kuonekana kama vipande vya minyororo, lakini baadaye vikawa vinaungana na kuwa mnyororo kamili uliojiviringisha katika kaburi lake.
Watu walianza kutoka mbali kuja kutazama maajabu ya kaburi hilo, mvulana mmoja aliyefika hapo na baiskeli kushangaa akarusha jiwe kwenye kaburi hilo.
Aabu wakati anarudi kwao akapata ajali mbaya iliyosababisha mnyororo wa baiskeli yake kutoka na kujiviringisha shingoni, akafa.
Mama yake na kijana huyu alihuzunika sana kwani kila mmoja alifahamu sababu ya ajali hiyo na kosa alilolifanya, mama akabeba shoka na kwenda kukata mnyororo kwenye kaburi la Carl, alifanikiwa, lakini kesho yake akakutwa amejinyonga kwa moja ya nguo alizokuwa anafua.
Polisi waliona huo ni ujinga na hakuna laana yoyote hapo, wakaenda kulipiga picha kaburi kwaajili ya uchunguzi, wakati wanarudi kituoni wakiwa na gari wakapata ajali na kufa.
Miaka ya 1940 kila mmoja alikuwa hasogelei kaburi hilo, siku moja watu wakaanza kusikia mtu akigonga jiwe na nyundo, alikuwa anagonga kaburi hilo.
Ghafla akaskika anapiga kelele, dakika chache akawa kimya. Ilionyesha aliona kitu na akataka kukimbia lakini alishindwa, alikutwa kafa kaburini hapo.
Baadaye kulikuwa na mpango wa kuyaondoa makaburi yote katika eneo hilo kupisha ujenzi wa huduma za kijamii, ndipo kaburi hilo lilipo ondolewa.
MWISHO
Usisahau kunifollow @AMARYAMARY9
diva retweeted
Leo kuanzia saa 4 nitaanza kutag mtu mmoja mmoja apate followers
Shusha handle ili niwe wa kwanza kukutag
diva retweeted
Pengine tunaogopa kuchukua hatua kwasababu tunavyo vya kupoteza, tunahurumia watoto wetu na wazazi na familia zetu na kazi zetu tutavipoteza!! But kuna siku itafika hivyo vyote vitakuwa vimeshapotea vyenyewe automatically… watoto watakosa huduma bora za afya watapotea, wazazi watapata msongo wa mawazo kwa kukosa mafao yao na wao watatoweka, kazini tutakuwa hatuko tena tumesimamishwa hawana cha kutulipa na kuna ongezeko la ukosefu wa ajira…..Naam hapo tutakuwa hatuna tena cha kupoteza tumebaki sisi wenyewe kama sisi ONE MAN AAAAA!!
Hapo sasa ndo’ tutachukua hatua…..💪
diva retweeted
Wakuu naona leo watu hawana Usingizi kabisa tuweke handles zetu tuongeze hata Followers..!🔥🔥✌👇
diva retweeted
KWANINI EDGER EDSON MWAKABELA (SATIVA ) ALIPELEKWA KUUWAWA MSITU WA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI?
Mwaka huu 2024 pekee yake binafsi nime’ ripoti taarifa za watu zaidi ya 50 waliotekwa na kupotezwa kabisa.
Hawa ni baadhi tu ya watu waliopotea kwa kutekwa na kisha taarifa zao kutopatikana mahala popote ikiwemo vituo vya Polisi na Hospitali katika vyumba vya kuhifadhia maiti.
1. Herman William
2. David Gasper Lema
3. Ridhiwani Hemed Msangi
4. Hamza Said
5. Paul Jerome Kisoka
6. Gidion Michael Mwihumbo
7. Kelvin Sebastian Mkabai
8. Benson Erasto Arbogast Ishungisa
9. Casian Mazambo
10. Charles Aden Mwampyate na wengine zaidi ya 40
Tofauti na tulivyozoea kuona matukio ya Jinai mengine ambapo mtu akiuwawa au Kutekwa baada ya muda ndugu na jamaa zake wanaweza kuokota mwili au mabaki ya mwili baada ya kuuwawa.
Miaka ya hivi karibuni imekuwa ni tofauti kidogo, ndugu au Jamaa yako akitekwa akapotea na kuuwawa
Basi uwezekano wa kupata taarifa juu ya kifo cha ndugu yenu ni mdogo sana
Na uwezekano hata wa kupatikana kwa mwili au mabaki ya mwili umekuwa ni mgumu sana.
Bila shaka wauaji wameacha ile mbinu ya zamani ya kuua na kupeleka maiti vyumba vya kuhifadhia maiti
Kuua na kuteleleza mwili barabarani, kuua na kutupa mwili ukiwa katika mifuko ya sandarusi au viroba.Kuua na Kutupa mwili katika bahari au mito
Kwa tukio hili la Edger Edson Mwakabela (Sativa) limetufundisha kuwa watekaji na wauwaji wana mbinu mpya ambayo inapoteza ushahidi kwa 100%.
Mbinu hii ni ya kupeleka watu matika mbuga za wanyama au hifadhi za taifa zenye wanyama wakali, ili baada ya kukuua mwili wako utafunwe na wanyama wa porini.
Edger Edson Mwakabela (SATIVA ) anasema watesi wake walio mteka siku ya tarehe 23 June 2024 walimchukua Dar es saalam kisha kumpaki katika karakana za Kituo cha polisi Oysterbay, Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni na baadae kuanza kuelekea naye mkoani Arusha.
Kwanini Arusha? Kwa akili za haraka utagundua walielekea mkoa wenye Mbuga nyingi za Jirani za Wanyama wakali wenye uwezo wa kula mwili na mifupa yake kama Serengeti, Ngorongoro,Manyara na Tarangire.
Lakini huenda kwa sababu ya msimu wa watalii na ubize wa wageni katika mbuga hizi,Wauwaji wa Edger Edson Mwakabela waliamua kuchagua eneo lingine mbali kabisa baada yabkuona mbuga za Arusha hazina utulivu nyakati hizi
Wakaanza safari ya masaa 15 yenye umbali wa Kilomita 1091 ya kutoka Arusha kuelekea huko hifadhi ya ya Taifa ya Katavi wilaya ya Mlele
Sababu ni moja tu.Walifuata Fisi wenye madoa madoa (Spotted hyena) ambao wanasifa ya kunusa mzoga kuutafuna wote hadi mifupa ikaisha
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ina ukubwa wa kilomita za mraba 4,471 (maili za mraba 1,727) ipo Kusini Magharibi mwa Tanzania,kaskazini mwa ziwa Tanganyika, Kilomita 40 kutoka Mji wa mpanda.
"an estimated 4,000 elephants might converge on the area,together with several herds of 1,000-plus buffalo, while an abundance of giraffe, zebra,impala and reedbuck provide easy pickings for the numerous lion prides and spotted hyena clans."
Spotted hyena ndiyo siri ya wauaji ya Edger Edson Mwakabela kutembea umbali wa Kilomita 1,091 kutafuta hifadhi ya Taifa ya Katavi wanakopatika Fisi wa aina hiyo.
Walikuwa wana uhakika wa kuua na kupoteza ushahidi kwa haraka sana, ndani ya masaa 12 tu pasingebaki mabaki ya mwili.
Na ili wasibahatishe kazi yao wakahakikisha wanatekeleza mauaji pembeni ya Mto Ikuu unaosifika kwa Mamba wakali sana pamoja viboko wengi.
Kwa mujibu wa wenyeji wanaoishi pembezoni mwa msitu wa hifadhi wa Katavi wanashangaa imekuwaje mtu huyo ameweza kupatikana akiwa hai bila kutafunwa na fisi au Mamba
Wenyeji wanasema Jamaa ana bahati sana,aende akatoe sadaka,ule msitu nusu saa tu ni nyingi sana sana kuishi,wanyama wanakutafuna
Sasa nimejiridhisha kwa mbinu hii miili ya watu waliopotea kwa miaka ya hivi karibuni tusiwe na matumaini ya kuja kupatikana.
Au kupata ushahidi wa mabaki yao, kama wauaji wanatumia mbinu ya Kuua ndani ya hifadhi na kutelekeza mwili wako ili utafunwe na wanyama.
diva retweeted
Msiwe watu wa kupuuzia hisia zenu sometimes zina maana kubwa.
Baada ya kuona video ya Sativa akihojiwa na kudai alikuwa Oysterbay nikakumbuka Jumatatu nilipelekwa na gari ya @millardayo Oysterbay nikakutana na Brother Patrick baada ya kupata majibu yasiyo na matumaini nilimuuliza Patrick @PatrickMnyama96 kuwa saizi kituo wapi akaniambia twende makumbusho. Nikamwambia hapana tusubiri hapa hapa Oysterbay mimi ntakuwa naangalia magari yanayoingia kituoni nione kama kuna mtu anafanania na Sativa atashuka mpaka tutakapopata taarifa za wakina Aunt huko walipo wamepata nini kwenye kituo walichoenda wao.
Huwezi amini mpaka Patrick ana request Bolt kuondoka mimi aliniacha pale pale ingawa sielewi nilikuwa nasubiri nini. Waandishi waliokuwa kwenye gari ya @millardayo akiwemo @BecaTZA waliniuliza whats next nikawaambia kama mnaenda nendeni mimi nabaki ila nawaomba mkamuhoji Kamanda Murilo kama ataweza kutusaidia kwa chochote . Niliendelea kubaki pale Mpaka akatokea Jamaa mmoja wa kuitwa @Aboucontrolla akachukua Bolt toka Oysterbay akanipeleka mpaka Home.
Vituo vyote nilivopita nilikuwa nikipata majibu mabovu tu naondoka ila hapa Oysterbay niliamua kupiga mpaka hizi picha.
Then leo naona Sativa anasema ametolewa Oysterbay saa mbili asubuhi pale.
Anyway nashindwa kuiweka hii Vizuri lakini nawaomba msiwe watu wa kupuuzia Hisia zenu hasa kipindi cha matatizo.🙏🙏🙏

























