2/2 Kwa hiyo, Tangazo lililotolewa hapo awali na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, kuwa nafasi tatu za udiwani jijini Tanga ziko wazi, limebatilishwa na Mahakama Kuu leo hii na hii ina maana wananchi wa Tanga hawatarudi kwenye uchaguzi wa kata zingine kwa sababu ya uhuni wa WASALITI.
Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha UHUNI wa Lipumba na Sakaya wa kuwafukuza uanachama madiwani watatu wa @CUFTanzania jijini Tanga. Mahakama imeamuru madiwani hao waendelee na udiwani na uanachama wao hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa. Uamuzi umetolewa leo.
4/4 - Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Taifa Mhe. Mbarala Maharagande kutokana na maamuzi ya Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa iliyoongozwa na Katibu Mkuu Seif Sharif Hamad jana jijini DSM.
3/4 - Katika kata 79 zilizotangazwa, @thecivicunitedfront ilipoteza Kata 4 ilizokuwa inaziongoza kwa Madiwani wake kuhamia CCM, Kata hizo mbili zipo Manispaa ya Tanga Mjini na Kata moja Mtwara Vijijini na Diwani mmoja kufariki wilayani Kwimba.
2/4 - kutokana na Mgogoro uliopandikizwa ndani ya CUF na Lipumba na washirika wake. Chama kinaona ni busara kwa sasa kuelekeza nguvu na rasilimali zake chache zilizopo katika kushughulikia na kuupatia ufumbuzi mgogoro huo uliopandikizwa. Katika kata 79 zilizotangazwa,
1/4 - @CUFTanzania haitashiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio katika Kata 79 na Majimbo mawili uliopangwa kufanyika nchini kote Agosti 12, 2018 Sababu kuu ya kutoshiriki Uchaguzi ni kutokana na mkanganyiko wa uongozi katika usimamizi wa uchaguzi huo uliojitokeza kutokana
2/2 - @CUFTanzania haiungimkono utumiaji huu wa kanuni ambao unawalazimisha wabunge kufikiria yale yanayohitajiwa na dola, Bunge limejigeuza kuwa idara ya serikali na linaongoza kwa kudhibiti uhuru wa wabunge kutoa maoni yanayotakiwa kikatiba, hali hii haikubaliki hata kidogo.
1/2 - Ndani ya siku tatu, wabunge 3 wa @CUFTanzania wametolewa bungeni kwa nyakati mbalimbali, Chama chetu kimejiridhisha kuwa wabunge hao wamepewa adhabu hiyo isiyokubalika kwa sababu ya kutoa maoni yao. Tunasikitishwa sana na tabia endelevu ya utumiaji mbaya wa kanuni za bunge.
Spika Job Ndugai amemtoa katika ukumbi wa Bunge, Mbunge wa jimbo la Mchinga (@CUFTanzania Mhe.Hamidu Bobali akidaiwa kutoheshimu kiti cha Spika, Bobali ametakiwa kutohudhuria hadi mkutano ujao wa Bunge #MwananchiUpdates xitter.cf/MwananchiNews/status/1…. @CUFTanzania inalaani uamuzi huo.
4/4 - Mhe. @Julius_Mtatiro amesisitiza yuko tayari kukamatwa na kushtakiwa kuliko kukimbia mapambano ya kuitetea @CUFTanzania dhidi ya vibaraka wa dola na wasaliti wa chama wanaoongozwa na Jaji Mutungi. Mtatiro ameweka bayana kuwa nafasi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa iko wazi.
3/4 - Sababu zingine zilizotajwa na Mhe. @Julius_Mtatiro zitakazomfanya aachane na wadhifa wa Uongozi wa Chama hicho ni ikiwa Baraza Kuu lililomteua litateua kamati nyingine ya uongozi au litakapoteua Mwenyekiti mwingine wa Kamati ya Uongozi, jambo ambalo halijafanyika.
2/4 - Mhe. @Julius_Mtatiro ameeleza kuwa kinachoweza kumfanya aachane na wadhifa huo wa Kamati ya Uongozi ni ikiwa Baraza Kuu halali la Taifa la @CUFTanzania litamwandikia barua na kumtaka afanye hivyo, au Baraza hilo likiitisha Mkutano Mkuu na kuchagua Mwenyekiti wa Taifa wa CUF
1/4 - Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya @CUFTanzania Mhe. @Julius_Mtatiro amemuonya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mutungi, dhidi ya njama za Msajili kuwashinikiza Polisi wamkamate na kumfungulia mashtaka kwa kile ambacho Msajili anakiita Mtatiro siyo kiongozi wa CUF.
Baadaye mchana tutawalatea kwa kina taarifa za Mkutano huu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya @@CUFTanzania Mhe. @Julius_Mtatiro na vyombo vya habari. Mkutano utakuwa MUBASHARA kwenye Ukurasa wa FB wa Mhe. Mtatiro pamoja na Instagram akaunti yake. xitter.cf/Julius_Mtatiro/status/…
2/2 - @Pia, @CUFTanzania imewataka kutopitisha marekebisho ya Sheria ya Korosho, kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018. (Amendement of The Cashewnut Industry Act, (Cap.203) 2018) kwani kufanya hivyo kutawakosesha Wakulima fedha asilimia 65% zilizomo kwenye sheria iliyopo.
1/2 - @CUFTanzania imetoa wito kwa wabunge wa vyama vyote kuungana na kuwatetea wakulima wa korosho hadi serikali iwalipe fedha zao, zaidi ya shilingi bilioni 200 ambazo (serikali) imezichukua na kuzitumia badala ya kuzirudisha kwa wakulima. @salimbimani2 @allysalehznz
Wiki hii inayokwisha kumekuwa na jaribio la tatu la Jaji Mutungi kuiba fedha za CUF na kumpa Lipumba, mara hii amejaribu kutumia Benki za Zanzibar, Chama kimendelea kuchukua hatua stahiki kumzuia. Ni Vita, ni mapambano. Nchi haina Utawala wa Sheria tena.
Mawakili wa @CUFTanzania wameanza mchakato wa kumfikisha Jaji Francis Mtungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kosa la kuidharau Mahakama (Contempt of the Court) baada ya kupuuza amri ya Mahakama Kuu na kujaribu kumpa Lipumba jumla ya Shilingi Milioni 600.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, ameiba Shilingi Milioni 600 na kumuwekea Lipumba na Genge lake, hata hivyo Katibu Mkuu @SeifSharifHamad na @JoranBashange wamezizuia fedha hizo benki, Benki imeamua kutii amri ya Mahakama Kuu.


