OfficialBBTYIA (@BBTKilimo) header
OfficialBBTYIA (@BBTKilimo) profile picture

Updates on Building Better Tomorrow Project - YIA under @wizarakilimo

Joined April 2023
Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)Photo by OfficialBBTYIA (@BBTKilimo)
Asante sana kwa maswali ambayo naamini yanalenga kuhabarisha umma kuhusu maendeleo ya mradi. Awali ya yote nichukue nafasi hii kusisitiza tena, hata mradi huu ni jitihada za maksudi za Mhe Rais Dr. @SuluhuSamia katika kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Kilimo. Hili pia limedhihirika kupitia bajeti ya Wizara ya Kilimo Hadi kufikia trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na sote tunafahamu kilimo ni UWEKEZAJI. Kujibu maswali yako… Project ya BBT imefikia wapi? Kwanza ni muhimu tuelewe components za mradi wa BBT ni zaidi ya block farms. Ina components hizi 5 zote zinazolenga vijana na wanawake - 1) Mashamba Makubwa ya Pamoja (BBT Block Farms), 2) Utoaji wa Mitaji kwa Vijana na Wanawake 3) Uchimbaji wa Visima kwa Wakulima Wadogo 4) Huduma za Ugani, na 5)Uongezaji Thamani wa Mazao. Hadi kufikia Januari 2025 - Jumla ya ekari 340,244.98 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha vijana, kutoka ekari 300 zilizokuwa wakati wa uzinduzi wa programu. - Vijana 686 tayari wanazalisha kwenye mashamba ya Chamwino Dodoma (Chinangali na Ndogowe) mnakatibishwa kutembelea na hivi karibuni tutakua na site visits za kujionea kwa makundu mbali mbali na kujifunza - Programu imeendelea na uwekezaji wa umwagiliaji, usambazaji wa pembejeo, na utoaji wa mikopo. Ni vijana wangapi wameshafaidika na hii project mpaka sasa? - Hadi Desemba 2024, jumla ya vijana na wanawake 43,163 kupitia component zote 5 wamenufaika moja kwa moja kupitia programu ya BBT, ikiwa ni kupitia Wizara ya Kilimo, taasisi zake na Wadau wa Maendeleo. Awamu ya kwanza imeleta matokeo gani mpaka sasa? - Ingawa awamu ya 1 haijaisha- Vijana 686 wameanza uzalishaji katika mashamba ya Chamwino, Dodoma. - Shamba la Chinangali (ekari 1,772) limeanza kuzalisha mazao mbalimbali kama mbegu za alizeti, pilipili, mtama, maharagwe kunde, na mahindi. - Vijana 249 wamepata mafunzo ya usambazaji mbolea na uzalishaji mbegu. - Katika shamba la Ndogowe, vijana 418 wamekabidhiwa ekari 10 kila mmoja kwa ajili ya kilimo. - Kituo atamizi cha Mkonge Tanga na Zanzibar kimewezesha vijana 344 kuzalisha bidhaa za mkonge. Kuhusu Investment na Value for Money - Serikali na wadau wamewekeza jumla ya TZS 2.64 trilioni kwa kipindi cha 2022-2030, ambapo 24% ya bajeti inatoka serikalini na 76% kutoka kwa sekta binafsi na washirika wa maendeleo. Katika msimu wa 2024/2025, kipato tarajiwa ni faida ya TZS 1.94 bilioni baada ya gharama za uendeshaji. Kwa kiasi gani? Tunajivunia uwekezaji huu uliotengeneza ajira, kuimarisha uzalishaji wa kilimo, na kuwezesha vijana kumiliki mashamba na mitaji. Uwekezaji katika umwagiliaji, upatikanaji wa ardhi, na huduma za ugani umeleta tija kubwa katika uzalishaji wa mazao. Licha ya mafanikio haya, bado kuna changamoto za upatikanaji wa masoko na ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi ila hili najibu hapo chini Tumefika hatua gani na tunaelekea wapi? BBT inaendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha mashamba mapya kama Mapogoro-Chunya (ekari 51,528.5) na kuendelelea na Ujenzi wa miundombinu kama mabwawa ya umwagiliaji, barabara, na minara ya mawasiliano unaendelea. Mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa pembejeo inaendelea kutolewa, ambapo hadi Desemba 2024 maombi ya mikopo yenye thamani ya TZS 21.3 bilioni yalipokelewa, na TZS 5.24 bilioni ziko kwenye hatua za kutolewa. Tumefika ngazi ya halmashauri na ekari 148,563.91 zimetengwa kwa ajili ya programu ya BBT. Natumai nimejaribu kujibu maswali yako. Salaam Aleikum.
1. Project ya BBT imefikia wapi mheshimiwa Bashe? 2. Report ya utekelezaji wake tunaipata wapi na sisi tuipitie? 3. Ni vijana wangapi wameshafaidika na hii project mpaka sasa? 4. Awamu ya kwanza imeleta matokeo gani mpaka sasa? 5. Thamani ya fedha iliyowekezwa inaendana na matokeo yaliyopatikana? 6. Kwa kiasi gani? 7. Tumefika hatua gani na tunaelekea wapi? Umma wa watanzania ungetamani kufahamu haya Mheshimiwa.🙏🏿
105
67
16
271
53,772
#3rdG25AfricanCoffeeSummit 21-22 February 2025 Dar es Salaam Declaration 2025 - Tamko la Dar es Salaam linaweka mkazo kuwekeza kwa vijana na kahawa. Leo Nchi 10 zimetoa ahadi za kuungana na tamko hili linalolenga kuimarisha sekta yetu na kuwapa vijana ajira.
8
34
2
102
4,054
3rd G25 African Coffee Summit. 21-22 February, Dar es Salaam Tanzania.
8
22
2
71
4,082
Ni siku ya kuchambua makadirio ya mapato na matumizi ya @WizaraKilimo chini ya @bashe ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25. @BBTKilimo @TanzaniaTari @TPHPA_Official @SAGCOT #BajetiYaWakulima #Ajenda1030 #LishaTaifaLishaDunia – at Dar es Salaam, Tanzania
4
4
602
Napenda kuwashukuru wote tulioshiriki kwa pamoja kwenye mjadala huu wa kwetu wakulima uliolenga kwenye uchambuzi wa bajeti ya wizara ya kilimo @WizaraKilimo 2024/2025 , Zaidi sana Nimshukuru Waziri wetu wa Kilimo Mhe @HusseinBashe kwa kuungana nasi na kusikiliza maoni yetu , ni jambo la faraja sana kuwa kiongozi msikivu namna hii . Nimshukuru pia @MalemboLE Na @rutaraka kwa Moderation nzuri #BajetiYaWakulima xitter.cf/i/spaces/1eaKbgOXyraGX
6
7
1
39
4,941
OfficialBBTYIA retweeted
Waziri wa Kilimo, @HusseinBashe , amesema kuwa Wizara hiyo kupitia Bodi ya Mkonge Tanzania itahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji wa zao la mkonge kutoka tani 56,732.69 mwaka 2023/2024 hadi tani 80,000 mwaka 2024/2025. #WasafiDigital
6
40
2,097
Bajeti ya kimkakati, imelenga kutatua matatizo sugu na ya msingi kabisa Katika kuongeza tija kwenye kilimo, kama. 1. Kujenga bank ya mbegu (Gen Bank) 2. Kujenga kituo Cha Bioscience (Sayansi za kibailogia) 3. Kusomesha watafiti 4. Kukuza kilimo kwa 5% per year 5. Kuchangia 20% kwenye Pato la Taifa 6. Kujitosheleza kujilisha na kulisha wengine kibiashara. 7. Uuzaji mazao nje kufikia $bil 3 #BajetiYaWakulima Big up mzee @HusseinBashe
#BajetiYaWakulima Salaam Ndugu Zangu. Nimetoa hoja ya Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedha 2024-2025 Hotuba inapatikana hapa - kilimo.go.tz/resources/view/…
1
9
22
2,712
OfficialBBTYIA retweeted
Moja ya vipaumbele vya mpango na Bajeti katika Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 ni serikali itaanza kutoa Ruzuku ya kupima ardhi kwa wakulima wadogo na kuhakikisha hati za Hatimiliki. #BajetiYaWakulima #Agenda1030 #LishaTaifaLishaDunia
3
5
5
1,002
OfficialBBTYIA retweeted
Kipaumbele kingine katika mpango wa Bajeti ya Kilimo ni ; Kushirikiana na wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo na makazi , itaanza kupima ardhi ya wakulima wadogo 2000,na kuhakikisha wanapewa hati za umiliki bila gharama yeyote ikiwa ni sehemu ya urasimiahaji. #BajetiYaWakulima
1
4
4
749
#BajetiYaWakulima Tunatambua utafiti na teknolojia ni muhimu kwenye mapinduzi ya Kilimo nchini. Kwenye mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara itazidi kujikita kwenye utafiti kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji. #Agenda1030
6
31
90
5,122
OfficialBBTYIA retweeted
📍Bungeni,Dodoma VIDEO: #BajetiYaWakulima “Wizara ya Kilimo tumeamua badala ya kununua magari ya sisi viongozi tutaweka fedha kwa ajili ya kununua magari kwa Maafisa Kilimo.”-Waziri wa Kilimo Hussein Bashe 📹:W/Kilimo
2
4
3
734
OfficialBBTYIA retweeted
Serikali itaanza kutoa Ruzuku kwaajili ya kupima ardhi kwa wakulima wadogo na kuhakikisha wanapata hati za hakimiliki. #BajetiYaWakulima 2024/25
1
6
9
1,543
OfficialBBTYIA retweeted
Kuelekea Space ya Uchambuzi wa Bajeti ya Kilimo 2024/2025. Kipi unatamani kusikia na kupata ufafanuzi kutoka kwa @WizaraKilimo @HusseinBashe #BajetiYaWakulima #Ajenda1030 #LishaTaifaLishaDunia Shusha comment yako hapo 👇🏿👇🏿
5
15
2
21
3,802
#BajetiYaWakulima Wizara ya Kilimo tumeamua badala ya kununua magari ya sisi viongozi tutaweka fedha kwa ajili ya kununua magari kwa Maafisa Kilimo. #Agenda1030
42
58
5
262
15,981
Wakulima Ile siku yetu ni leo na Kesho , Kila la kheri mwamba Mhe @HusseinBashe Katika kuwasilisha mpango na makadirio ya bajeti ya wizara kilimo @WizaraKilimo kwa mwaka 2024/2025 #BajetiYaWakulima #agenda1030
5
22
1
42
3,262
Zoezi la kutoa mikopo kwa Vijana walio tayari kwenye Kilimo kupitia BBT-Financing chini ya Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) ni endelevu na unaweza kuomba mkopo muda wowote kwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu - Wizara ya Kilimo au Moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu - Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF). Muhimu ni kuwa na andiko (concept note na budget) la mradi/matumizi ya fedha unayoiombea, viambatishwe na barua. Kwa maelezo zaidi tembelea website ya Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) - agitf.go.tz/
This Post is from an account that no longer exists. Learn more
32
41
2
114
28,625
Ifikapo 2030 , ni dhahiri kwamba sekta ya kilimo itaweza kuchangia 10% ya pato la taifa endapo serikali na wizara ya Kilimo @WizaraKilimo chini ya Mhe @HusseinBashe itaendelea na spidi hii hii kama ilivyo sasa , kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2022/2023 , Upembuzi na usanifu wa miradi ya umwagiliaji umefanyika kama ifuatavyo •Skimu 42 zenye ukubwa wa hekta 91,357; •Mashamba sita (06) ya pamoja (Block farms) yenye hekta 79,518; na •Mabonde 22 ya kimkakati yenye ukubwa wa hekta 306,361 Hii hatua kubwa sana na tukiendelea namna hii basi #Agenda1030 Itakuwa na mafanikio makubwa huku wananchi wengi wakiwa na kipato kikubwa , ungana nasi kwenye space siku ya tarehe 2 May 2024 tujadili zaidi mafanikio, changamoto , maboresho katika kufikia malengo bora kwenye sekta yetu ya kilimo #BajetiYaWakulima #Ajenda1030
10
30
8
58
16,903
OfficialBBTYIA retweeted
Wadau wa Kilimo tutakuwa na Space ya Uchambuzi wa Hutuba ya Bajeti ya Kilimo. Link hii hapaa x.com/i/spaces/1rmxP… #BajetiYaWakulima
3
8
20
1,103
Moja ya hoja za vijana zinazotusumbua ni kuhusu mitaji katika kilimo,naamini ufafanuzi utatolewa kuhusu namna na sifa ya kupata mikopo kupitia mfuko wa pembejeo (AGTIF). #BajetiYaWakulima #Ajenda1030
Wanufaika wa mradi wa BBT-Financing unaoratibiwa na Mfuko wa Pembejeo (AGTIF) wanaendelea kutoa ushuhuda wa mikopo ya 4.5%. Unaweza kuomba mkopo muda wowote kwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu - Wizara ya Kilimo au Moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu - Mfuko wa Pembejeo za Kilimo.
1
4
244